Maswali ya Biblia Toka 2 Petro

 

S: Muhtasari wa kitabu hiki cha 2 Pet ukoje?

J: Kitabu hiki kinajigawa kirahisi kabisa kwenye sehemu tatu:

2 Petro 1 Ufahamu wokovu wako

2 Petro 2 Mfahamu adui yako

2 Petro 3 Ufahamu unabii wako

 

S: Kwenye 2 Petro, kwa nini kuna mambo yanayofanana kati ya vitabu vya 2 Petro na Yuda? (Kwa mfano, 2 Pet 2:17 na Yuda 13; 2 Pet 2:1-18 na Yud 4-16)

J: Vitabu hivi vinaongelea mada zinazofanana, na huenda mitume Yuda na Petro waliwahi kuyaongelea mambo haya. Pia, Roho Mtakatifu aliweka mioyoni mwao mzigo unaofanana. Inawezekana pia kuwa Mtume Yuda alisoma 2 Petro au Mtume Petro alisoma Waraka wa Yuda. Wakati mwingine tofauti husistizia zaidi kufanana; kwa mfano, 2 Petro 1 inaongelea wokovu wetu, wakati Yuda haiongelei, lakini Mtume Yuda anasema angependa kuongelea wokovu ambao ni wetu sisi sote, lakini mambo anayoyaongelea yanahitajika zaidi.

Jambo kubwa zaidi ni namna gani Biblia ilivuviwa? Wazo lingeweza kuwa Mungu alitumia imla kuwaambia waandishi wanadamu kila herufi na kila neno la kuandika. Biblia haisemi kuwa ilitolewa kwa njia ya imla. Badala yake, Mungu alichagua watu ambao waliandika Bibilia, na aliwapa ufahamu na fursa ya kupitia mambo mbalimbali. Katika sehemu zingine, Mungu aliwapa maneno bayana ya kutumia. Katika sehemu zote, watu wanaoamini kuwa Biblia haina makosa huamini kuwa hakuna maneno yaliyoingia kwenye nakala za awali za Maandiko ambayo Mungu hakupenda yawemo. Tazama swali kuhusu 2 Pet 1:21 kwa maelezo zaidi kuhusu kuvuviwa kwa Maandiko.

 

S: Kwenye 2 Petro, kwa nini mitindo ya uandishi ya 1 Petro na 2 Petro inatofautiana?

J: Kuna sababu mbili.

1 Petro iliandikwa na mwandishi mtaalamu: Kwenye 1 Pet 5:12 inaonyesha kuwa Mtume Petro alimwelekeza mwandishi mtaalamu aliyeitwa Silwano (Sila), ambaye anaelekea kuwa na ufahamu mkubwa zaidi wa sarufi ya Kigiriki. Yerome (karibu mwaka 404 BK) aliliongelea jambo hili kwa mara ya kabisa na alisema kuwa 1 Petro iliandikwa na mwandishi mtaalamu Silwano.

Mada tofauti: Kimsingi 1 Petro inazungumza kuhusu kustahimili shinikizo kama watu watakatifu wa Mungu, na 2 Petro inaonya dhidi ya waalimu wa uongo. Hata hivyo, ingawa mada za nyaraka hizi mbili ni tofauti mambo yaliyomo yana ufanano usiokuwa dhahiri. Kwa mfano, kwenye Biblia nzima ni nyaraka za Petro tu (1 Pet 3:20 na 2 Pet 2:5) zenye kueleza kuwa ni watu nane tu waliookolewa kwenye safina ya Nuhu.

 

S: Kwenye 2 Pet 1:2 imani yetu ni ya thamani kwa jinsi gani?

J: Imani yetu ni ya thamani kwetu sasa, kwani ndio chimbuko la tumaini na furaha vyetu, na nguvu za kuishi maisha ya leo, na kufanya yale tunayojua kuwa tunapaswa kuyafanya, na kujiepusha na yale tunayojua kuwa hatupaswi kuyafanya. Imani yetu ni ya thamani kwetu siku zijazo kwani wokovu wetu uliopatikana kwa imani (Efe 2:6) hutupa uzima wa milele. Imani ya waumini wengine ni ya thamani kwetu, kwani inatuonyesha mwenendo wao na kutufanya tifurahi ndani ya Mungu kwa ajili ya maisha na wokovu vyao. Imani yetu ni ya thamani kwa Mungu kwani inampa utukufu na Ebr 11:5 inasema kuwa ni kigezo cha kumpendeza Mungu.

 

S: Kwenye 2 Pet 1:2 mtu mmoja asiyeamini uwepo wa Mungu aliona kuwa ni jambo la ajabu kuwa kitu kikubwa zaidi ambacho Mungu anakitaka kwetu ni kumwamini Yeye. Kwa nini Mungu anatilia maanani jambo hili? Ni kitu gani ambacho mtu huyu asiyeamini uwepo wa Mungu hakukielewa?

J: Imani ni zaidi ya kuafiki mambo kadhaa kuhusu jambo au nadharia fulani. Imani ni kuweka tumaini kwa Mungu kuhusu mambo yote ya maisha yetu. Kwa kiasi kidogo, huwa tunaamini kuwa wenzi wetu wa ndoa wanatupenda, hata tunapokuwa hatuwaoni, na imani yenye kutuwezesha kuendelea kuwapenda wenzi wetu, kwenye nyakati nzuri na mbaya, ndiyo tunayotaka kufanya.

S: Kwenye 2 Pet 1:3, je Mungu anatupaje vitu vyote tunavyohitaji kwa ajili ya kuishi na kuwa watauwa?

J: Mungu ametupa ufahamu wote tunaohitaji ili tuweze kuja kwa Kristo, na kuishi maisha ya utiifu yenye kumpendeza Bwana wetu. Lakini Mungu ametupa pia Roho wake Mtakatifu, anayeishi ndani mwetu, ili atuongoze kwenye kweli yote. Roho Mtakatifu hututia nguvu, na kutufariji, kama Yesu alivyosema kuwa (Roho) atafanya kwenye Yoh 14:15-16; 25-26.

Si tu kwamba Mungu anaweza kuwa hakutupa vitu vyote tunavyotaka, ni karibu mara zote huwa hatupi kila kitu tunachokitaka. Kama mtu mmoja alivyowahi kusema, uzi kwenye chombo cha muziki chenye kutumia nyuzi hutoa sauti nzuri zaidi ukiwa umekazwa. Uzi uliolegea kabisa hauwezi kutoa sauti ya wimbo wowote ule. Vivyo hivyo, tunaweza tusiridhike kabisa na maisha hapa duniani, - wala hatupaswi kuwa hivyo. Sisi ni wapitaji tu, tumo safarini kuelekea mbinguni.

 

S: Kwenye 2 Pet 1:4, je unafikiri ni ahadi gani zenye thamani zaidi ambazo Mungu ametupa?

J: Waumini wengi wanasema kuwa ni wokovu kupitia kifo cha Yesu msalabani kwa ajili ya dhambi zetu, kwani bila hicho tutaangamia hakika na hatutakuwa na tumaini la uzima wa milele. Lakini uzima wa milele ni kitu gani! Wokovu wetu sit u kuishi vema milele hapa duniani, au peke yetu mahali pengine, bali ni kuishi kwa furaha pamoja na Mungu milele. Kwa hiyo watu wengine wanaweza kusema kuwa wokovu ni hatua ya kwanza ya uzima wa milele. Kwa hiyo ahadi kubwa zaidi ni vyote: kuanza kwa furaha isiyoisha, na ukubwa wa furaha yenyewe isiyoisha.

 

S: Kwenye 2 Pet 1:4, kwa vile tu washiriki wa tabia ya uungu, je tumefanyika miungu?

J: Hapana. Hatufanyiki kuwa na nguvu zote, hatuumbi malaika, hatuabudiwi, au tuna tabia nyingine nyingi za Mungu. Aya hii inamaanisha kuwa Mungu anatoa na ataendelea kutunza baadhi ya tabia za kiungu, kama vile uzima wa milele, utakatifu, na kuweza kuishi naye.

 

S: Kwenye 2 Pet 1:4, je tunashiriki vipi tabia ya uungu?

S: Yesu alituita sisi kaka na dada (Mak 3:35), na tumekalishwa pamoja na Kristo kwenye enzi yake (Efe 2:6). Hatufanyiki kuwa ama miungu wadogo, au Mungu mwenyewe wa Kweli na wa Pekee, lakini tunashiriki tabia ya uungu kwa sababu Kristo anaishi ndani yetu kupitia Roho wake Mtakatifu (Yoh 14:23; 1 Yoh 4:12,15; Rum 9:10-18; 1 Kor 6:19).

 

S: Kwenye 2 Pet 1:4, je ulimwegu unawaharibu watu kwa namna gani?

J: Ulimwengu huharibu mawazo yetu kwa njia ya kutufanya tuamini uongo hata kushindwa kuona kilicho cha kweli na kilicho cha uongo. Sote tuna dhamiri iliyo mwongozo wa msingi wa mambo mema na mabaya, na ulimwengu hupunguza nguvu ya dhamiri za watu. Ulimwengi huharibu mioyo yetu, kwa kutufanya tuache kutaka yaliyo mema, na kuacha kutaka njia iliyo bora zaidi.

Kama mfano, fikiria mtumia madawa ya kulevya aliye athirika kiwango kikubwa zaidi. Mwanzoni alifikiri kuwa madawa yanafurahisha, kisha akajipa moyo kuwa hayamdhuru kabisa, na mwishoni, ingawa anaweza kuona wazi kuwa yamemharibia maisha yake, hajali tena.

 

S: Kwenye 2 Pet 1:6, siri moja ya kuwa na kiasi ni kuwa inakuja kwa kiwango fulani kupitia ufahamu. Je kiasi kinakujaje kupitia ufahamu?

J: Ni kweli kuwa ufahamu hutuelekeza mambo ya kufanya na kutokufanya, lakini si kitu kinachoongelewa hapa, kwa sababu kiasi si kujua kitu cha kufanya lakini kuchagua kuwa na kuwa na nidhamu na kufanya jambo unalojua kuwa ni jema. Ufahamu huleta maono. Kwa kuwa na ufahamu unaweza kuona matokeo ya kuwa na kiasi, na mara nyingi kuona mambo yenye uwezo wa kutokea kwa sababu ya kutokuwa na kiasi. Wakati mwingine unapojaribiwa kutokuwa mwaminifu, au kufanya dhambi nyingine, unaweza kuchagua kutokufanya dhambi kwa sababu tu hupendi kufanya hivyo. Hupendi kwa sababu unajua matokeo ya kufanya hivyo, kwenye maisha ya watu wengine na wewe mwenyewe.

 

S: Kwenye 2 Pet 1:6, je ustahimilivu unahusianaje na kuwa na kiasi?

J: Kama tukiyalinganisha maisha ya Kikristo na mbio, yanafanana zaidi na mbio ndefu kuliko mbio fupi. Kiasi hakiwi na maana sana kama hakidumu kwa muda mrefu. Ni vema kusema "Sitafanya dhambi leo", lakini kama unamaanisha kweli "Nitaliangalia jambo hili tena kesho", kusema hivyo si vema sana kama kusema "Sipendi kufanya dhambi tena." Kuahirisha anguko lenye uwezo wa kutokea si jambo jema kama kupata ushindi dhidi ya dhambi.

 

S: Kwenye 2 Pet 1:6, je utauwa unawezaje kuletwa na ustahimilivu?

J: Utauwa unahitaji uthabiti. Endapo mtu atakuwa mwaminifu, ataweza kuwa safi, au ataweza kujiepusha na baadhi ya dhambi, hivi havifanani hata kwa kiasi kidogo na kuwa mtu anayetegemewa kufanya mambo haya.

 

S: Kwenye 2 Pet 1:7 je upendo wa kindugu unaletwaje na utauwa wa kweli? Kwa nini aina nyingine za ushika dini hazileti kabisa upole wa kindugu?

J: Mungu anapenda tuwapende watu wengine kama tunavyojipenda sisi wenyewe. Tunapaswa kuwa makini kuhusu kuwa wacha Mungu, yaani kutii amri za Mungu, na Mungu anatuagiza kuwapenda watu wengine. Sisi wenyewe tunaweza tusiwe na upendo wa kutuwezesha kufanya hivyo. Lakini tunao upendo wa Mungu unaotenda kupitia kwetu, tunaweza kuwapenda watu wengine.

 

S: Kwenye 2 Pet 1:8 inawezekana kuona jinsi upendo unavyoleta upendo wa kindugu, lakini ni kwa jinsi gani upendo wa kindigu unaleta upendo?

J: Tukiwa makini kuonyesha upendo wa kindugu kwa watu wengine, inakuwa wahisi kwetu kuwapenda. Kwa namna fulani, kuchagua kuwa mwema kwa watu wengine ni sawa na kuchagua kuwapenda.

 

S: Kwenye 2 Pet 1:9, watu wanawezaje kusahau kuwa walitakaswa kutoka kwenye dhambi zao za zamani?

J: Watoto wadogo wanawezaje kusahau kuwa wametoka kuogeshwa muda mfupi tu uliopita na kwenda kucheza tena kwenye uchafu? Wanaweza kufanya hivyo. Kwa bahati mbaya, kama watoto wa Mungu, tunaweza pia kuwa wajinga kama watoto wadogo.

 

S: Kwenye 2 Pet 1:10, tunawezaje kuufanya kuitwa kwetu imara?

J: Kuitwa (au kutoitwa) hakuwezi kuthibitishwa zaidi machoni pa Mungu asiyefungwa na muda. Hata hivyo kunaweza kuthibitishwa machoni petu.

Kwa kuwa kumtii Yesu ni kielelezo cha mtu aliyeokolewa, kama muumini haishi maisha ya utiifu kwa Kristo, kielelezo hakiwepo (angalau kwa muda huo), na kuna swali halali la kuuliza endapo mtu huyu ameokolewa kweli au la. Anaweza kuwa hayumo kwenye safari ya kwenda mbinguni, kama 2 Pet 2:19-22 inavyoonyesha. Au, wanaweza kuwa Wakristo wasio watiifu. Hakuna utata wa jinsi hii kwa mtu anayeishi kwa utiifu kwa Kristo.

 

S: Kwenye 2 Pet 1:11, je mapokezi makubwa yanatofautianaje na mateso ya moto yenye uchungu ya Wakristo huko toharani/pagatori?

J: Mapokezi haya hayafanani sana. Toharani/pagatori ni mafundisho ya Kikatoliki ambayo hayapo kabisa kwenye Biblia, na hatuja haja ya kuyaamini. Tazama maelezo kwenye 1 Kor 3:13-15 kwa ufafanuzu zaidi.

 

S: Kwenye 2 Pet 1:12-15, kwa nini tunahitaji kukumbushwa katika maisha yetu ya Kikristo?

J: Petro aliona haja ya kutumia muda mwingi kulikumbusha kundi lake wakati ule mambo waliyokuwa wameyasikia kabla. Tunahitaji kukumbushwa kwa jinsi hii leo. Tunahitaji kukumbushwa kwa sababu mbalimbali. Mawazo yetu yanaweza kuwa masahaulifu ya baadhi ya mambo tuliyojifunza, lakini hii siyo sababu kubwa. Mara nyingi, ingawa tunaweza kukumbuka, tunatakiwa kufikiria tena na kwa uangalifu umuhimu na matokeo ya mambo tuliyofundishwa. Hatutaki kuuacha upendo wetu wa kwanza, kama kanisa la Efeso lilivyofanya kwenye Ufu 2:4-5. Mwisho, tunahitaji kukumbushwa lengo letu ili kutiwa nguvu katika udhati wetu wa kutenda mema.

 

S: Kwenye 2 Pet 1:16 na 1 Yoh 1:1-2, kwa nini ni muhimu sana kwa mitume kuwa mashahidi?

J: Mitume na manabii ni msingi wa imani yetu, kwa mujibu wa Efe 2:20, Yesu Kristo akiwa jiwe kuu la pembeni. Ni muhimu kuwa wawe walimwona Yesu wao wenyewe.

 

S: Kwenye 2 Pet 1:17, lini Mungu Baba alisema maneno haya kwa Yesu huku Petro akiwa anasikia?

J: Maneno haya yalisemwa wakati wa kubatizwa kwa Yesu kwenye Mat 3:17. Inawezekana pia kuwa Petro alisikia maneno haya wakati wa kugeuzwa kwa sura ya Yesu au wakati mwingine ambao haujarekodiwa kwenye Maandiko.

 

S: Je 2 Pet 1:19 inamaanisha kuwa baadhi ya vifungu vya Maandiko vina uhakika zaidi kuliko vingine?

J: Hapana. Kitu ambacho ni cha kweli hakiwezi kufanywa kuwa cha kweli zaidi. Hata hivyo, mashahidi zaidi wanaweza kufanya jambo liwe na uhakika zaidi kwa kutoa ushahidi zaidi. Hii ni nahau ya Kigiriki yenye kumaanisha "Tunaweka tegemeo lenye uhakika (zaidi) kwenye . . .".

 

S: Kwenye 2 Pet 1:20-21, kwa kuwa Maandiko hayapo kwa ajili ya tafsiri ya mtu fulani tu, kwa nini watu wanapenda kuitafsiri ya mtu fulani?

J: Kuna mambo matatu ambayo yanafaa kuyaangali katika kujibu swali hili.

1. Tafsiri binafsi haipaswi kuchanganywa na kujisomea binafsi kwa Maandiko. Waumini wote wanapaswa kuwa wanajisomea Neno la Mungu wao binafsi pia. Tunapaswa kupima mambo tunayosikia toka kwenya Maandiko kama Wakristo wa Berea waliokuwa tayari kupokea mawazo mapya walivyofanya kwenye Mdo 17:11-12.

2. Hata hivyo, kila mmoja wetu anawahitaji waumini wengine kanisani kujifunza na kujirekebisha toka kwao. Mit 27:17 inasema kuwa kama chuma kinoavyo chuma ndivyo mtu amunoavyo rafiki yake.

3. Wale wanaojitenga na watu wengine kwa makusudi mara nyingine huingia hasara ya kuikataa maana dhahiri ya Maandiko na kuchukua maana za kipumbavu ambazo hazikufahamika kabisa na Wakristo wote wenye asili Kigiriki. Kama theolojia yako inakulazimisha udai kuwa Mungu anaonekana kushindwa kuwasilisha maana ya msingi kwa Mkriso yeyote kabla ya mwaka 400 BK, huenda maana hiyo ya msingi haijawahi kabisa kuwa ya msingi.

 

S: Je 2 Pet 1:20-21 inaonyesha kuwa kanisa zima liwe linatafsiri?

J: Hapana. Kwa kuzingatia uzoefu wa kanisa Katoliki, yafuatayo ni baadhi ya mafundisho yao.

Walihalalisha mateso, hata ya Wakristo wa kweli.

Mahusiano yote ya karibu, hata ya kwenye ndoa, ni dhambi.

Waue watu wote wasiolitii kanisa.

Lilipa kanisa hela unapokuwa umefanya dhambi (misamaha ya pagatori)

Wakati wa kushiriki Meza ya Bwana, Wakristo wa kawaida (walei) wasishike kikombe, wachungaji na mapadri tu.

Watu wanatakiwa kuuawa endapo wanamiliki Biblia wakati wao si wachungaji au mapadri.

Wachungaji au mapadri wanaooa wanapaswa kuuawa.

Wachungaji au mapadri wenye marafiki wa kike na watoto wanatakiwa kulipa kodi, kisha itakuwa shwari kwao.

Kwenye 2 Pet 1:20-21, Biblia inaongelea mada mbili: manabii na Roho Mtakatifu. Imeongelea kutoa unabii, siyo kusoma au kutafsiri Biblia.

 

S: Kwenye 2 Pet 1:21, je waandishi wa Biblia waliongozwa kwa namna gani hasa na Roho Mtakatifu?

J: Neno ‘kuongozwa' limetumiwa tena kwenye Mdo 27:15,17 kwa maana ya meli kuchuliwa na upepo. Yafuatayo ni mambo manne yahusuyo kuvuviwa kwa Biblia.

1. Neno la Mungu kupitia kwa watu

1a. Sehemu kubwa zaidi ya kufunuliwa ilihusisha mawazo ya na fikra za watu ambao Mungu aliwachagua kipekee. Ufu 1:19 inatoa mfano mmojawapo. Lakini hakuna neno lolote lililokuwa la mwanadamu tu (2 Pet 1:19-21).

1b. Baadhi ya ufunuo ulikuwa ni maneno ya moja kwa moja, kama kwenye 1 Yoh 12:28, Isa 6; Kut 3:4, 5 na kadhalika.

1c. Mungu alitumia mtindo wa waandishi wanadamu katika kuandika. Hakuna kitu kilichoandikwa kama Neno la Mungu ambacho ama Mungu hakupenda kiandikwe ama hakikuwa sahihi.

1d. Biblia si kitabu chenye maandishi ya siri. Maana za maneno si ufafanuzi wowote wa sasa ambao tunaweza kupenda kuyapa, lakini ni maana za kawaida ambazo wazungumzaji wa wakti ule wa lugha hii waliielewa.

2. Uwezo wa Mungu wa kuwasiliana nasi

2a. Hatuwezi kufahamu vitu vyote kuhusu Mungu asiye na ukomo na mwenye kupita mipaka ya kibinadamu na "aliyetofauti" na sisi. Hata hivyo, tunao wajibu wa kujfunza na kuelewa mambo ambayo Mungu ametufunulia.

2b. Mungu huwasiliana nasi kwa njia ambazo tunaelewa. Ana uhuru wa kututembeza kwa kutumia mashairi, kueleza mambo kwa kutumia vielelezo, na kurahisisha mambo kwa maelezo yenye kutumia umbo la kibinadamu (anthropomofisimu). Munga anaweza kutumia nahau, kama "machweo", na Mungu anaweza kutumia migawanyo yetu ya vitu, kama kumuweka sungura kwenye makundi ya Kiebrania ya wanyama wenye kucheua kwa sababu sungura hufanya hivyo.

2c. Neno la Mungu lina tamko kuhusu kwelie na linamwakilisha Mungu mwenyewe. Lina lugha chanya kuhusu mambo yaliyo ya kweli, na lugha hasi kuhusu mambo yasiyo ya kweli.

2d. Waandishi wanadamu wangeweza kunukuu maandiko mengine yasiyokuwa ya Kibiblia, kama vitabu vya historia ya Kiyahudi (Kitabu cha Yashari kwenye Yos 10:13; 2 Sam 1:18, n.k.), na hata mashairi ya Kigiriki yaliposema vitu vilivyokuwa kweli (Mdo 17:23,28; Tit 1:12).

3. Neno la Mungu ni kweli yote

3a. Maandiko Matakatifu yote (Biblia nzima) yametoka kwa Mungu. Neno la Mungu ni kweli kwenye mambo yote linayoongelea. Kweli haijipingi yenyewe. Maandiko si tu kuwa yana maneno ya Mungu, bali ni Neno la Mungu (Rum 3:1-2; Yoh 10:35; Mit 30:5-6; 2 Tim 3:15; 2 Sam 22:31; Zab 33:4; 119:151).

3b. Maandiko si tu kwamba yako sahihi, yana ufasaha unaotakiwa kwa ajili ya kutufanya tuielewe maana iliyokusudiwa na Mungu. Ufasaha huu huenea hata kwenye nyakati na idadi ya maneno, kama Zab 82:6 na Mat 22:32. Hata hivyo, Maandiko mara nyingi hutumia makadirio, hasa ya muda na kiasi.

3c. Mungu hadanganyi. Hata hivyo, kutokutuambia kila kitu kihusocho mada fulani si kudanganya. Kwa mfano, ikiwa angalau wanawake watatu walikuwa kenye kaburi la Yesu kwenye Mak 16:1 na Mat 28:1, Biblia iko sahihi inapowataja wanawake wawili tu miongoni mwao. Agano Jipya lina ujumbe wenyewe kabisa wa mafundisho ya Yesu, lakini si maneno yenyewe kabisa ya Yesu (Mat 22:37; 13:22; Mak 12:30; 4:19).

3d. Maandiko yamekamilika katika kutuambia mambo yote tunayohitaji kujua kwa ajili ya wokovu na kukua katika imani. Maandiko si ensaiklopidia: kitabu au seti ya vitabu vinavyotoa taarifa kuhusu mambo mengi, wala hayadai kutuambia kuhusu kila kitu.

3e. Mungu aliruhusu baadhi ya makosa wakati wa kuenezwa kwake, lakini Neno lake linadumu milele. Isa 59:21; 40:8; Zab 119:89. Neno lake limehifadhiwa bila makosa (bila makosa ya kiasi kikubwa) hadi wakati wakati huu (Isa 55:11; 1 Pet 1:23-25; Zab 119:89, 91, 144, 160).

4. Itikio letu

4a. Tunapaswa kuyapenda na kuyatunza Maandiko kama kitu cha thamani kwetu (Zab 56:10; 119:72, 97, 105, 120). Hatupaswi kuyaabudu Maandiko, lakini kumshukuru Mungu aliyetupa Maandiko (Zab 119:12). Tunapaswa kupendezwa na sheria ya Mungu (Zab 119:16, 35, 47) na "kutetemeka" tunaposikia Neno la Mungu (Isa 66:5). Tumaini letu limo kwenye Neno la Mungu (Zab119:74, 81).

4b. Tunatambua kuwa tumeokolewa na Yesu, si kwa kusoma Maandiko (Yoh 5:39-40; Yak 1:22-25; 1 Kor 13:2).

4c. Yathamini Maandiko (Mdo 13:48; Kol 3:16) kwa kufundisha, kukaripia, kusahihisha, kurekebisha, na kufunza kwenye haki (2 Tim 3:16-17) na kusaidia kwenye majaribu (Zab 119:10).

4d. Tunapaswa kusoma na kujfunza Maandiko kwa bidii (Mdo 17:11; Ufu 1:3). Tunapaswa kuyatafsiri kwa uaminifu na usahihi, siyo kuyabadilisha au kuyatafsiri isivyo sahihi (2 Pet 3:16). Hatupaswi kuongeza au kwenda mbali zaidi ya Neno la Mungu (Mit 30:5-6; 1 Kor 4:6-7; Kumb 4:2; Ufu 22:18-19; Wim 12:12; Mak 7:13).

4e. Baadhi ya amri za Agano la Kale zimetimizwa na hazipaswi kutekelezwa tena, kama vile kula nyama ya nguruwe, kutoa kafara, n.k. (Mdo 10:9-16; 15:1, 5-29; Mak 7:19; Gal 5:2-4; Ebr 9:9-10; 10:18).

4f. Maandiko si mapendekezo tu kwa ajili ya maisha, lakini yana mamlaka katika maisha yetu (Zab 119:33-34; Yoh 8:37; 12:48-50; 14:23). Tunapaswa kuyaamini mambo yote ambayo Mungu anafundisha na kuzitii amri zote za Mungu (Jn 14:23-24).

Kwa wasomaji wa maandiko ya Kimomoni, jambo hili linatofautiana na mafundisho ya Kimomoni kuhusu kuvuviwa kwa Kitabu cha Momoni. Joseph Smith anadaiwa kutafsiri kimiujiza Kitabu cha Momoni neno kwa neno na herufi kwa herufi, kwa kuangalia jiwe la mwonaji kwenye kofia nyeusi.

Kwa wasomaji wa Kiislamu, maoni ya Kikristo ya kuvuviwa kwa Biblia yanatofautiana na maoni ya Waislamu ya kuvuviwa kwa Kurani. Waislamu walio wengi wanaamini Kurani iliyopo dunniani ni nakala halisi iliyotolewa kwa imla ya mbao za Kurani zilizoko mbinguni.

Tazama maelezo kuhusu Biblia kuona tofauti kati ya kutokosewa na tafsiri sisisi iliyovuka mpaka.

;Ps119:74,81,89, 92,105

S: Kwenye 2 Pet 2:1, ni aina gani ya waalimu wa uongo ambao Mtume Petro alikuwa anatahadharishi dhidi yao? Je walikuwa ni watu waliokuwa wameokolewa (2 Pet 2:1b, 3b)?

J: Petro anawaelezea watu hawa kwa undani zaidi kwenye 2 Pet 2:10-22. Anasema "walizaliwa kama wanyama tu wa kukamatwa na kupotezwa" (m.12, "weusi wa giza ni akiba waliyowekewa" (m.17), na "ingekuwa heri kwao kama wasingaliijua njia ya haki,kuliko kuijua, kisha kuiacha ile amri takatifu waliyopewa" (m.21). Kwa hiyo ni dhahiri kuwa waalimu wa uongo ambao Petro alikuwa anawaongelea wamo njiani kuelekea jehanamu. Wakristo wanaoamini kuwa muumini anaweza kupoteza wokovu wake wanafikiri kuwa watu hawa walikuwa wameokolewa kwanza kisha wakapoteza wokovu wao na sasa wanakwenda jehanamu (kama hawatatubu). Wakristo wanaoamini kuwa mtu akiokolewa hudumu katika wokovu milele wanasema kuwa ingawa waalimu hawa wa uongo waliijua njia ya kweli (m.21) lakini hawakuwa wameokolewa wakati wowote ule.

 

S: Kwenye 2 Pet 2:1, je Mtume Petro anasema kuwa tunapaswa kustaajabishwa na waalimu hawa wa uongo?

J: 2 Petro 2 inatupa mifano mingi sana toka kwenye historia ili kutufahamisha kuwa tusishangazwe na mifano inayoweza kuwa ya ziada tu. Kwa jinsi ulivyokuwa na watenda maovu miongoni mwa waumini wakati ule, ndivyo watakavyokuwepo miongoni mwa wacha Mungu sasa. Kwa kweli, baadhi yao bado wamo kanisani wakifundisha mambo maovu.

 

S: Kwenye 2 Pet 2:1, je "Bwana" aliyewanunua ni nani?

J: Neno la Kigiriki despotes limetumiwa mara kumi tu kwenye Biblia. Mara tano likimwongelea mkuu wa nyumba, mara tatu Mungu Baba (Luk 2:29; Mdo 4:24 (despota); Ufu 6:10) na maara moja Yesu Kristo kwenye Yuda 4, aya ambayo inasema "humkana yeye aliye peke yake Mola, [Mungu] na Bwana wetu Yesu Kristo."

Wakalvanisti walivuka mpaka (kama vile John Gill), na Wakalvinisti wengine wanasistiza kuwa "Bwana" hapa si Yesu tu, lakini ama Baba ama Mungu wa Utatu. Maneno haya hayaongelei kitu chochote kuhusu kazi ya kuwafia wanadamu msalabani bali Mungu "kuwanunua" Waisraeli wakati wa kutoka Misri kupitia kuangamizwa kwa jeshi la Farao. Clark ni mmoja wa wafafanuaji mwenye maoni haya.

Watu wasiokuwa Wakalvanisti, na baadhi ya Wakalvanisti wanasema kuwa "Bwana" hapa inamaanisha Kristo, kama ilivyo kwenye Yuda 4. Mtoa ufafanuzi wa Maandiko aitwaye Blum anasema maneno haya yanamwongelea Kristo kwa sababu utambulisho wa pronomino "wale" na nomino "watu" uko mbali sana kulinganisha na nomino inayotangulia "waalimu wa uongo."

Toleo la Biblia lenye mlengo wa Kikalvanisti liitwalo New Geneva Study Bible uk.1981, lina mtazamo unaofurahisha ulio tofauti kabisa na wa Alford. Linaafiki kuwa maneno haya yanamwongelea Kristo, lakini linasema kuwa "Kitu ambacho Mtume Petro alikuwawa amekusudia kusema hapa ni kusistiza namna ambayo waalimu wa uongo wanahusika kuliko kuelezea dhana ya upatanisho wa Mungu na wanadamu uliofanywa kifo cha Yesu. Matendo yao yenye kuharibu pamoja na kudai kwao kuwa wamekombolewa na Kristo (m.2) husababisha Kristo na kafara yake aliyoitoa kwa ajili ya dhambi vitukanwe."

Hata hivyo, watu wote wanapaswa kuafiki kuwa, angalau kwa kiasi fulani, Mungu "aliwanunua" baadhi ya wenye dhambi waliopangiwa hukumu waliokuwa wanakwenda motoni. Kwa hiyo swali si kuwa endapo Mungu aliwanunua wenye dhambi waliopangiwa hukumu, bali ni kuwa aliwanunuaje.

 

S: Kwenye 2 Pet 2:1, na Yuda 5, je Yesu aliwafia wenye dhambi waliopangiwa hukumu? Kama ni hivyo, ni kwa vipi basi?

J: Yesu alikufa msalabani kwa kwa neema yake ili awape watu wote fursa ya kuokolewa. "Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu . . ." (Efe 2:8). Hata hivyo, si watu wote watakaokuwa na imani. Ebr 4:2 inasema, "Sisi nasi tumehubiriwa habari njema vile vile kama hao. Lakini neno lile lililosikiwa halikuwafaa hao, kwa sababu halikuchanganyika na imani ndani yao waliosikia."

Wakalvinisti wenye msimamo mkali hawaafiki maoni haya wakisema kuwa Yesu hakufa kwa ajili ya watu ambao wasingeipokea injili, na hawakuwa na nafasi ya kuepuka kwenda jehanamu. Kwa nini Mungu mwenye nguvu zote na mamlaka juu ya vitu vyote, afanye mambo ambayo hayana uwezekano wa kufanikiwa, au ajaribu kuwaleta watu kwake bila mafanikio?

Jibu limo kwenye kilio chenye kusikitisha cha Yesu, "Ee Yerusalemu, Yerusalemu, uwauaye manabii, na kuwapiga kwa mawe wale waliotumwa kwako! Ni mara ngapi nimetaka kuwakusanya pamoja watoto wako, kama vile kuku avikusanyavyo pamoja vifaranga vyake chini ya mbawa yake, lakini hamkutaka" (Mat 23:37).

Mungu ana mamlaka juu ya vitu vyote; anaweza kuamua hata kujidhibiti Yeye mwenyewe. Hili ni jambo la kushukuru, kwani isingekuwa hivyo mambo yenye dhambi yangeangamizwa mara moja. Wakalvinisti wanaweza kusema kuwa hakuna mambo aliyoyafanya Mungu ambayo hayakufanikiwa, lakini kwa mujibu wa mtu asiyekuwa Wakalvinisti aitwaye Yona, "Watu waangaliao mambo ya ubatili na uongo hujitenga na rehema zao wenyewe." (Yon 2:8). Ni lazima kuna kitu kilichipotezwa hapa.

Mtu anawezaje kukataa kusudi la Mungu, na kusudi la Mungu lisifanikiwe? Hakuna mtu anayeweza kupingana na kusudi la Mungu mwenye nguvu zote – isipokuwa Mungu ameruhusu hivyo. Mtu mwingine asiyekuwa Mkalvinisti, Luka, aliandika, "Lakini, Mafarisayo na wana-sheria walilipinga shauri la Mungu juu yao, kwa kuwa hawakubatizwa naye [Yohana]" (Luk 7:30).

Si kwamba Mungu alitaka watu wamkatae ili waangamie, lakini Mungu anao uwezo wa kuruhusu, ikiwa anataka kufanya hivyo – na ndivyo alivyofanya. Ezel 33:11 inasema, "Waambie, Kama mimi niishivyo, asema Bwana Mungu, sikufurahii kufa kwake mtu mwovu; bali aghairi mtu mwovu, na kuiacha njia yake mbaya, akaishi . . ."

"Hili ni zuri, nalo lakubalika mbele za Mungu Mwokozi wetu, ambaye hutaka watu wote waokolewe, na kupata kujua yaliyo kweli. Kwa sababu Mungu ni mmoja, na mpatanishi kati ya Mungu na wanadamu ni mmoja, Mwanadamu Kristo Yesu; ambaye alijitoa mwenyewe kuwa ukombozi kwa ajili wote, utakaoshuhudiwa kwa majira yake" (1 Tim 2:3-6).

Yesu hakuwafia baadhi ya watu tu ulimwenguni kwa mujibu wa 1 Yoh 2:2, lakini ama aya hii iliwapotosha Wakristo wa awali wenye asili ya Kigiriki au Yesu aliufia ulimwengu wote. Pia kuna jambo maalumu kuhusiana na Atonement – Malipo ya dhambi, upatanisho wa Mungu na wanadamu uliofanywa kifo cha Yesu, lakini tunapaswa kuyachukua mambo haya kwa pamoja, kwani Yesu ni "Mwokozi wa watu wote, hasa wamwaminio" (1Tim 4:10).

1 Yoh 2:2 "Naye ndiye kipatanisho kwa dhambi zetu; wala si kwa dhambi zetu tu, bali na kwa dhambi za ulimwengu wote."

Rum 5:18 "Basi tena, kama kwa kosa moja watu wote walihukumiwa adhabu, kadhalika kwa tendo moja la haki watu wote walihesabiwa haki yenye uzima." Sasa kama ‘wote' ya pili haimaanishi watu wote, kwa nini ‘wote' ya kwanza imaanishe watu wote? Maneno ni yale yale kwenye Kigiriki na katika ufahamu wa Wakristo wa awali.

 

S: Kwenye 2 Pet 2:2, kwa kuwa baadhi ya watu wanaojaribu kuitafuta kweli, kwa nini Mungu ameruhusu njia ya kweli itukanwe?

J: Mungu hutupa uhuru wa kutosha hata kuweza kuutumia vibaya na kujiumiza sisi wenyewe. Mungu hata hutupa uhuru hata wa kuwaumiza watu wengine pia.

1. Kuna kiasi cha kweli ya Mungu kinachoweza kupatikana (Rum 1:19-20; Zab 19:1-3).

2. Mungu ana nia ya kuifunua kweli zaidi kwa wale wamtafutao (Mat 7:11; Rum 2:7).

3. Mungu ni mwenye haki, na anahukumu watu kufuatana na kiasi wanachojua (Rum 4:15; 5:13, Kumb 1:39).

4. Hata hivyo, kwa wale wasiomtafuta Mungu, Mungu hasiti kuwaruhusu waamini uongo na kuchanganyikiwa kwenye ujinga wa hali ya juu (Rum 11:8-10).

 

S: Kwenye 2 Pet 2:3, kwa nini watu wanafurahishwa na hadithi za kutungwa?

J: Watu wanapenda kusikia hadithi zenye kufurahisha, na hadithi hufurahisha zaidi inapokuwa ya kweli. Kwa hiyo, kwa kuamua kwa haraka haraka, inaonekama kuwa kweli kwa asili ya kibinadamu kwamba mara nyingine watu hupenda hadithi zenye kufurahisha ziwe kweli, hivyo wana uwezekano mkubwa wa kuziona kuwa za kweli. Endapo hadithi za zamani za Wahindu na Wanostisia, au Wamomoni au Sayantolojia (dini yenye kutafuta ufahamu wa mtu mwenyewe na kujitosheleza kiroho kupitia masomo yaliyowekewa viwango vya kufaulu na mafunzo) wa leo, watu wamebuni hadithi za kufurahisha ambazo watu wengi wameziamini.

 

S: Kwenye 2 Pet 2:4 na Yuda 6, je malaika walioasi wamefungwa, au wako huru kama Ufu 16:14 na aya nyingine zinavyosema?

J: Kuna mambo matatu ya kuzingatia kabla ya kujibu swali hili.

1. Kuna baadhi ya mapepo yaliyofungwa.

2. Yako mengine yaliyo huru, kwa mujibu wa Mat 12:22; 17:14-18 na Mdo 16:16-18.

3. Kuna baadhi ya mapepo yaliyokuwa huru, lakini yaliogopa kufungwa na maneno ya Yesu kwenye Luk 8:28-32.

 

S: Kwenye 2 Pet 2:5, kwa kuwa Mungu aliokoa "nafsi" saba tu kwenye safina ya Nuhu, vipi kuhusu wanyama wa baharini wenye "nafsi" kwenye Ufu 16:3?

J: Ingawa neno la Kigiriki ni lile lile, muktadha ni tofauti. Kwenye 2 Pet 2:5, muktadha ni nafsi za wanadamu. Neno hili la Kigiriki linaweza pia kumaanisha maisha, kama kwenye Ufu 16:3. Kwa hiyo, ni binadamu tu ndio wenye nafsi zenye kuhitaji kuokolewa kama kwenye 2 Pet 2:5, lakini wanyama wana uhai pia, kama kwenye Ufu 16:3.

 

S: Kwenye 2 Pet 2:7-8, je Lutu aliwezaje kuwa mwenye haki, tukizingatia mambo aliyofanya kwenye Mwa 19:30-38?

J: Kuna mambo matatu ya kuzingatia katika kujibu swali hili.

1. Lutu alifanyiwa hadaa kwa kufanywa alewe hata kujamihiana na binti zake muda mfupi tu baada ya kufiwa na mke wake.

2. Ikiwa mapendekezo na majaribu ya mtu asiye haki yataendelea yanaweza kumwangusha hata mwenye haki.

3. Dhambi ya Lutu ilikuwa ni baada ya maelezo ya matukio yanayoongelewa kwenye 2 Pet 2:7-8.

 

S: Kwenye 2 Pet 2:8, kuna usahihi gani kwa nafsi ya mwenye haki kuteswa na matendo maovu ya watu wengine? Je jambo hilo linawezaje kuacha kuwa hivyo?

J: Lutu alijaribu kuishi maisha ya haki miongoni mwa watu waliokuwa waovu kupita kiasi. Jambo hili halikumtesa kwa nje tu, lakini lilimtia kwenye hatari ya kimwili wakati wageni watatu walipokuja. Kibaya zaidi, kutokutii kwa mkewe kulisababisha kifo chake (mkewe). Lakini kibaya zaidi, watu waovu waliokuwa wamemzunguka waliuathiri mwenendo wake, kumfanya alewe. Na kitu kibaya zaidi, jambo hili halikuathiri mwenendo wake tu bali pia mwenendo wa watoto wake. Wakati unafika ambapo inampasa mtu kumuuliza Mungu ikiwa anataka aishi sehemu fulani.

 

S: Kwenye 2 Pet 2:9, kwa kuwa Lutu alijamihiana na binti zake, aliwezaje kuwa mfano wa namna Mungu alivyowaokoa wasio haki kutoka kwenye majaribu?

J: Lutu ni mfano wa mambo ambayo Mungu anayafanya na mambo ambayo Mungu hayafanyi. Lutu alimcha Mungu maishani mwake. Mungu alimwokoa kila mtu na familia yake, isipokuwa mke wa Lutu aligeuka nyuma akawa nguzo ya chumvi. Hata hivyo, mabinti wa Lutu, baada ya kumlewesha baba yao, walijamihiana naye. Mungu alimwokoa Lutu, lakini hakumuondolea wajibu wa kuchunga maisha yake na kujibidisha kumcha yeye maishani mwake.

Mfano mwingine usiokuwa mzuri wa mtu mwenye kumcha Mungu, wokovu wa Mungu, na kuanguka kwa mtu baadaye maishani mwake ni Gideoni kwenye Amu 8:24-28.

 

S: Kwenye 2 Pet 2:9-10, kuna tofauti gani kati ya "wasio haki" na wale waufuatao mwili katika tama ya mambo machafu na kudharau mamlaka?

J: Kuufuata mwili katika tamaa ya mambo machafu, na kudharau mamlaka, ni namna mbili za kutokuwa na haki kulikozidi kiasi.

Kuna tofauti kati ya kukosa haki kusikoonyeshwa kwa vitendo na kukosa haki kwenye kuonyeshwa kwa vitendo. Kuna tofauti kati ya watu wanaoanguka mara kwa mara mara wanapojaribiwa, na watu wanaotafuta njia za kuanguka. Wakati mwingine watu wanaonekana "kujuta mara kwa mara" kwa ajili ya makosa yao, lakini wanaendelea kuyafanya. Watu wengine hawajifanyi kujuta lakini wanafanya kama wanavyojisikia kikweli. Na bado wengine wanaonekana kujivunia kwa wazi kabisa dhambi zao. Kuna uzuri gani kuwa "mlevi mkubwa zaidi" kwenye mashindano ya kunywa, kupata ushindi mkubwa zaidi wa idadi ya watu uliolala nao (na kisha kuwaacha). Kuna sinema zenye kuwasifia watu wngine kwa kuwa wezi wazuri, au wauaji wazuri. Huenda kungekuwa na watu wachache "wenye kujisifia" kwa ajili ya dhambi zao wenyewe kama kungekuwa na watu wachache "wenye kuwasifia" kwa ajili ya matendo yao ya dhambi.

 

S: Kwenye 2 Pet 2:10 na Yuda 8-10, watu wanawadharauje malaika?

J: Kuna namna tatu za kudharau. Kudharau kunaweza kumaanisha kuzua uongo kuhusiana na jambo fulani. Je malaika wanaonekana kama watoto watoto wapendazao walio na mbawa? Vipi kuhusu Mikaeli, na malaika aliyeliangamiza jeshi la Waashuri? Je mapepo yote yana pembe na uma wa nyasi? Kwa kweli Biblia inasema kuwa Lucifer alikuwa na sura nzuri sana. Baadaye Wanostisia walikuwa na hadithi zisizo kweli zenye maelezo mengi sana walizozitunga kuhusu malaika na viumbe wengine ambao ni nusu miungu. Hatupaswi kutunga mambo kuhusu malaika au mapepo.

Dharau inaweza ikamaanisha kudhalilisha au kushusha hadhi ya kitu fulani. Sidhani kuwa Ayubu angeweza thubutu kumshushia hadhi yake shetani.

Dharau kwenye 2 Pet 2:10 na Yuda 8-10 inamaanisha kumshitaki mtu kwa kutumia mamlaka yako mwenyewe. Hivyo hata Mikaeli hakumkemea shetani moja kwa moja bali alisema, "Bwana akukemee."

 

S: Kwenye 2 Pet 2:10, ni mamlaka gani inayoongelewa hapa?

J: Neno lilitumiwa kwa ‘mamlaka' linaweza kumaanisha mamlaka ya Mungu, kanisa, serikali, watawala wa serikali, wazazi, au mamlaka kwa jumla. Mara nyingi watu wanaodharau mamlaka ya aina fulani wanakuwa na shida ya kutii mamlaka nyingine kwa ujumla. Hakuna kitu chenye kuonyesha kuwa Petro anaongelea mamlaka ya aina moja tu na si nyingine.

Kama 2 Pet 2:10 inavyo pendekeza, kudharau mamlaka na tamaa za uharibifu vinaweza kwenda pamoja. Believer's Bible Commentary uk.2297 inasema, "Siyo siri kuwa viongozi wa kidini, wanaposimama kama watumishi wa Kristo, mara nyingi wamekuwa na viwangu duni vya uadilifu. Si tu kuwa wanajihusisha na vitendo vya zinaa viliyokatazwa, lakini huunga mkono uasherati kwa wazi kabisa. Mchungaji wa wanafunzi wa dhehebu la Kianglikana anayehudumu kwenye shule ya wasichana huko Baltimore, Maryland, alisema: "Tunapaswa kutulia na kuacha kujihisia hatia kwa ajili ya vitendo mawazo na matakea vyetu vya ngono. Na ninamaanisha hivi, mawazo hayo kama yatakuwa ya mahusiano ya watu wa jinsi tofauti, jinsia moja, au kujipiga punyeto . . kujamihiana kunafurahisha . . . na hii inamaanisha kuwa hakuna sheria zilizofunganishwa nako ambazo unatakiwa kuzifanya au kutokuzifanya. Hakuna sheria za mchezo huu, tunaweza kusema hivyo" (imenukuliwa kutoka Pageant Magazine, Oktoba, 1965).

 

S: Kwenye 2 Pet 2:10-11, neno la Kigiriki lenye kumaanisha wenye utukufu/mamlaka limetumika sehemu gani nyingine?

J: Limetumiwa kwenye mandhari za aina tofauti. Zifuatazo ni baadhi ya mandhari hizo.

Utukufu wa Mungu uitwao Shekinah: Luk 2:9; Mdo 7:55

Utukufu wa Mungu, au sisi kumtukuza Mungu: Mat 24:30; Mak 13:26; Luk 2:14; 19:38; 21:27; Yoh 7:18; 11:4; Rum 1:23; 3:7, 23; 4:20; 15:7; 16:27; 1 Kor 10:31; 2 Kor 1:20; 4:6; 4:15; 8:19; Gal 1:5; Efe 3:21; Fil 1:11; 4:19; Kol 1:17; 1 Tim 1:17; Tt 2:13; Ebr 1:3; 1 Pet 4:13, 14; 2 Pet 1:17; Ufu 4:9, 11; 19:7 Yer 13:16 (Septuajinti); 1 Sam 6:5 (Septuajinti)

Utukufu apewe Bwana: 2 Tim 4:18

Kumtukuza Mungu: Ufu 11:13; 14:7; aina tofauti za utukufu (doxa) kwa mtoto wa Miriamu kwenye Kut 15:1-6 katika toleo la Septuajinti Mpe Mungu utukufu [kwa kusema ukweli]: Yoh 9:24; Yos 7:19 kwenye Septuajinti

Mheshimu Mungu: Kitabu cha Kiapokrifa (cha kubuniwa cha dini ya Kiyahudi) 4 Wamakadia 1:12

Kushindwa kumpa Mungu utukufu: Mdo 12:23; Ufu 16:9

Uadhama wa neema ya Mungu: Rum 9:23; Efe 1:12, 14, 18; 3:16; 1 Tim 1:11; 2 Pet 1:3; Efe 1:6

Matendo ya nguvu: Yoh 11:40; Rum 6:4 (inafanana na Isa 12:2; 45:24 Sept.)

Baba: Yoh 8:49; Efe 1:17; Fil 2:11; 4:20

Baba anamtukuza Kristo: Yoh 8:54

Uadhama wa Kristo: Mak 10:37; Mat 16:27; Mak 8:38; Luk 9:26; 24:26; Yoh 17:5, 22, 24; 1 Tim 3:16; Ebr 2:7, 9; 13:21; 1 Pet 1:11, 21 Fil 3:21; Ufu 5:12

Mungu Baba amemtukuza Mungu Mwana: Yoh 11:4; 2 Pet 1:17

Yesu ana heshima kubwa kuliko Musa: Ebr 3:3

Kristo alipobadilika sura: Luk 9:32

Malaikaa walipotokea: Luk 9:31; Ufu18:1

Watu ni utukufu wa Kristo: 2 Kor 8:23

Tunapaswa kumtukuza Kristo: 2 Pet 3:18

Mungu anatusifia: Yoh 5:44

Mtu mmoja anamheshimu/sifia mwingine: Luk 14:10; Yoh 5:44

Si kutafuta kusifiwa na wanadamu: 1 The 2:6

Sura ya Musa: 2 Kor 3:7

Kwa utukufu wetu: 1 Kor 2:7; 2 Kor 6:8; Efe 3:13

Wakristo wa Thesalonika walikuwa ni utukufu wa Paulo: 1 The 2:20

Tutapokea taji ya utukufu: 1 Pet 5:4

Utukufu wao ni aibu: Fil 3:19

Kupata utukufu kwa ajili yako mwenyewe: Yoh 7:18; 8:50, 54

Mambo yote mawili kwa pamoja: Walipenda utukufu wa watu kuliko wa Mungu: Yoh 12:43

Jua, mwezi, na nyota: Mdo 22:11; 1 Kor 15:40

Sehemu nyingine: 1 Pet 1:17

Kwa mujibu wa kamusi ya Thayer ya Kigiriki cha zamani neno doxa lina mlolongo wa maana unaoanzia maoni/mawazo binafsi ya mtu hadi umaarufu.

Kwenye kitabu cha Kiapokrifa cha 4 Wamakabia 5:17 linamaanisha maoni, uamuzi, kwa mujibu wa kamusi ya Thayer iitwayo Greek Lexicon of the New Testament uk.155.

Kamusi ya Thayer inaendelea kusema kuwa ingawa haimaanishi utukufu, au wangavu, au mng'ao kwenye maandiko ya Kigiriki, lilitumika hivyo kwenye Biblia kama tafsiri ya neno la Kiebrania.

Kama unavyoweza kuona, utukufu ni dhana muhimu sana kwenye Biblia. Kwenye 2 Kor 3:18, tunaagizwa kuuakisi utukufu wa Bwana. Unaweza kuwa unajishughulisha sana na kuwapenda watu wengine kwa ajili ya Mungu, kujifunza, kufanya mambo mbalimbali lakini unajishughulisha pia na kuuakisi utukufu wa Mungu?

 

S: Kwenye 2 Pet 2:10-11 je malaika wakuu sana kwa nguvu na uwezo ni kina nani?

J: Neno la Kigiriki doxas linamaanisha "utukufu" (wingi), tazama itifaki ya Strong 1391. Kwenye Kigiriki za zamani lilimaanisha kuwa na maoni, mtazamo mzuri kuhusu mtu au kitu fulani, au heshima. Kwa mujibu wa Vocabulary of the Greek New Testament ya ya Moulton and Milligan, uk.168, ilimaanisha jua katika kuwaelezea wanawake na meli, na kwenye makaratasi ya mafunjo ya kinajimu. Wakristo wenye asili ya Kigiriki walilitumia neno hili kwa utukufu au uadhama wa Mungu, na malaika, na kututukuza sisi kwenye Agono Jipya na tafsiri ya Kigiriki ya Agano la Kale (Septuajinti).

Mara nyingi unapoona neno "utukufu" kwenye Agano Jipya huwa ni neno hili. Kwa kuwa neno "utukufu" lina mlolongo wa maana, limetafsiriwa kumaanisha vitu vifuatavyo:

Mamlaka ya kiserikali/kifalme (John Calvin),

Viongozi wa kanisa

Malaika wema

Huenda malaika waasi (mapepo)

"uadhama wa malaika" au "malaika"

"viumbe vya mbinguni" [yaani ama malaika wema na/au malaika waasi (mapepo)]

"Waheshimiwa" (hii ni maana pana zaidi) "Wenye hadhi" "wenye nyadhifa za juu" "waliotukuka"

Nyaraka za 2 Petro na Yuda zinafanana. Yuda 8 inasema watu hawa waovu wanayakana mamlaka na kuwatukana viumbe wa mbinguni (doxa, neno lile lile la Kigiriki). Yuda 9 inaendelea kutoa mfano wa Mikaeli ambaye hakumshitaki shetani kwa kumlaumu bali alisema "Bwana na akukemee."

Mahitimisho mawili: Kwa kuufanana kwake na Yuda maneno haya yanaonyesha kuwa yanaongelea kuwatukana viumbe wa mbinguni. Hata hivyo, hakuna kitu chochote kwenye neno hili kinachozuia lisimaanishe pia kuwatukana "waheshimiwa", ama viongozi wa serikali au wa kanisa.

 

S: Kwenye 2 Pet 2:12, watu wanafananaje na wanyama wasio na akili?

J: Baashi ya wanyama wanaweza kufikiria tu kula, kupandana, starehe, na kupigana na kutawala. Kuna watu wanaofanana nao kabisa.

 

S: Kwenye 2 Pet 2:13, unawezaje kumweleza mtu asiyeamini ni kwa sababu gani si vema kuendekeza karamu za anasa?

J: Kama Yer 5:31b inavyosema, "Mtafanya nini mwisho wake?" Inakuwaje endapo ulikwenda kwenye karamu "nzuri zaidi" miaka kadhaa iliyopita. Je, jambo hilo litawezaje kukufanya ufurahi leo? Tafuta furahi isiyokuwa na mwisho, si ya muda mfupi ambayo inageuka kuwa uchungu.

 

S: Kwenye 2 Pet 2:14, Biblia inasema kitu gani kingine kuhusu macho na uzinzi? Mambo haya yanahusianaje?

J: Mara nyingi majaribu yanayotokana na uzinzi yanakuja kupitia kwenye macho. Huenda hii ndiyo sababu Yesu alisema kwenye Mat 5:27-30 akitumia lugha ya picha kuwa inafaa kuling'oa jicho lako kuliko kuzini. Ayubu alisema kwenye Ayu 31:1, "Nilifanya agano na macho yangu; basi nawezaje kumwangalia msichana [kwa tamaa]."

 

S: Kwenye 2 Pet 2:15, je watu, hata waumini leo hii, wanawezaje kupotea na kuifuata njia ya Balaamu mwana wa Beori?

J: Balaamu hakumkana Mungu moja kwa moja; bali alikiuka kanuni kwa kusudi la pesa. Pesa si mbayo, na kutafuta pesa siyo kitu kibaya. Lakini kwa sababu ya kuzitafuta, inakuwa rahisi sana mara nyingi kuhalalisha na kukiuka kanuni za Mungu, kama alivyofanya Balaamu.

 

S: Kwenye 2 Pet 2:16, ni kwa namna gani nabii wa kweli wa Mungu kama Balaamu mwana wa Beori alikuwa na wazimu?

J: Balaamu hakuwa wazimu kwa maana ya kuwa kichaa, bali alikuwa na wazimu kwa maana ya kufanya mambo ya kijinga na kujaribu kubadilisha maagizo ya Mungu ili kupata pesa. Ni wazimu kujaribu kugeuza matakwa ya Mungu kwa lengo la kupata pesa, anasa, au usalama, lakini watu wanafanya jambo hili hata leo hii.

 

S: Kwenye 2 Pet 2:17-19, waalimu wengine wanakuwaje kama vijito visivyokuwa na maji? Je maneno haya yanahusiana na Mit 25:14?

J: Kijito hupendeza na huwa na maji ya kutumia. Lakini kwa kutoa kwake maji kijito hutoa mazigazi ya kuwa na maana ingawa hakiko hivyo. Wakati mwingine waalimu huonekana kwa baadhi ya watu kuwa wazuri, lakini hawafundhishi kweli ila maoni yao tu. Waalimu wengine wanaweza kuwa na ufahamu, lakini mafundisho yao yasiwe na uhai, kwa sababu hawana sehemu katika maji yaliyo hai ya Yesu.

 

S: Je 2 Pet 2:19-22 inasema kuwa watu wanaweza kupoteza wokovu?

J: Neno la Kigiriki lenye kumaanisha "kujua" hapa linamaanisha "kutambua" au "kuafiki." Kuna baadhi ya Wakristo wanaolitumia neno hili kudai kuwa waumini wanaweza kupoteza wokovu. Wakristo wengine hawakubali kwa sababu nguruwe na mbwa wanawakilisha wanyama najisi. Kumbuka kuwa nguruwe alioshwa nje tu, na nguruwe na mbwa hawakuwahi kugeuzwa kutoka kuwa nguruwe na mbwa.

Wakristo wote wanakubali kuwa wako watu kanisani wanaonekana kwa watu wengine, japo kwa kipindi fulani, kuwa Wakristo, lakini watakwenda jehanamu watakapokufa. Hili ni onyo kubwa kwa watu wanaoijua njia ya wokovu lakini wanaikataa. Tazama maelezo kwenye Ebr 6:4-8.

Watu wanaweza kuasi na kuwa wabaya kuliko walivyokuwa awali na kwenda jahanamu, na watu hawa "waliongoka", ingawa kusema hivi hakumaanishi kuwa walizaliwa mara ya pili.

 

S: Kwenye 2 Pet 2:19-22, tuzungumzie maoni yasiyoafikiwa ili kuufanikisha mjadala, endapo nguruwe ni mzinzi, au mbwa anawaua mbwa wengine, lakini jambo hili halimuudhi Mungu, inakuwaje basi Mungu anaudhiwa wanadamu wanapofanya hivyo hivyo?

J: Hata nguruwe au mbwa huwa hasahau kuwa yeye ni nani, lakini binadamu wengine wanaelekea kusahau kuwa waliumbwa kwa kitu kizuri zaidi kuliko kuishi tu kama mnyama.

 

S: Kwenye 2 Pet 3:1, nini ni malengo hasa ya Mungu ya kutupa unabii?

J: Tunaweza kuona sababu angalau tatu za Mungu kutubariki na maneno yake ya unabii.

a) Nyakati nyingine huwa panakuwa na mambo bayana tunayotakiwa kufanya tunapoona hali ya kinabii. Kwa mfano, kwa habari ya Babeli iliyoongelewa kwenye Kitabu cha Ufunuo tumeamriwa "Kuikimbia Babeli." Masihi alipokuja, Wayahudi walitakiwa kumtambua na kumfuata.

b) Tunapokuwa tumevunjika moyo, mambo maovu hutokea, mara nyingi Mungu hutuambia mapema ili tuweze kujua kuwa Mungu alilifahamu jambo hili, na hata mambo haya hayata kwamisha mpango wa Mungu. Mifano kadhaa ya jambo hili ipo kwenye Dan 7:28 na Daniel 11.

c) Kuimarisha imani pale tunapomwona Mungu akitimiza ahadi zake alizozitoa huko nyuma.

 

S: Nini ujumbe wa 2 Pet 3:1-2?

J: Petro anasema kuwa maneno yake na maneno ya mitume wengine yana kiwango sawa cha mamlaka na Agano la Kale. Petro pia anathibitisha bayana kuwa nyaraka za Mtume Paulo ni Maandiko matakatifu kwenye 2 Pet 3:15-16.

 

S: Kwenye 2 Pet 3:3 watu wenye kudhihaki ni kina nani hasa?

J: Kwanza kabisa mtu mwenye kudhihaki si nani, kisha ni nani.

Kila mtu anatilia shaka mambo fulani – ama anapaswa kuwa hivyo. Si vema kuwa mwepesi kuamini kila kitu; badala yake tunapaswa kushuku vitu ambavyo ama havina ushahidi ama vina ushahidi mwingi sana unaoonyesha kuwa si vya kweli.

Lakini mtu mwenye kudhihaki hutilia shaka kwa wazi kabisa vitu ambavyo ama hajautathmini ushahidi wake, au hajauangalia ushahidi wa kitu fulani. Mara nyingi mtu mwenye kudhihaki huonekana kuwa mjinga kwa sababu anakidharau kwa wazi kabisa kitu ambacho watu wengine wanajua kuwa ni cha kweli.

 

S: Kwenye 2 Pet 3:3, ni kwa vipi kudhihaki na kufuata matakwa mabaya ya mtu huenda pamoja?

J: Mara nyingi sababu ya msingi, ingawa haisemwi kuwa ndio lengo la kudhihaki, ni kuhalalisha kufuata matakwa yao wenyewe badala ya Mungu. Kama hawamwamini Mungu, hawawezi kujisikia hatia kwa kutokumfuata.

 

S: Je 2 Pet 3:4-7 inaongelea yunifomianizim?

J: Huenda ikawa hivyo. Yunifomianizim (nadharia kuwa mabadiliko kwenye umbo/uso wa dunia wakati wa historia ya kijiolojia yametokana na vitendo vinavyoendelea kutokea na vyenye kufanana.) ni mtazamo maarufu sana wa kijiolojia kuwa michakato iliyopo sasa na pamoja na muda ndivyo vitu pekee vinavyotakiwa kuelezea maukio yote yaliyopita kwenye historia ya dunia.

Hata hivyo, mtazamo wa kiyunifomia unapungua umaarufu wake siku hizi. Wanajiolojia wengi zaidi wanafuata mtazamo tofauti, unaoungwa mkono na Stephen Jay Gould, uitwao ‘punctuated equilibrium' (muingilio mlinganifu), kwa sababu ushahidi wa kijiolojia unaunga mkono zaidi nadharia hii. Ingawa Gould alithibitishwa kuwa mtu asiyeamini uwepo wa Mungu, kuna ushahidi wenye kuunga mkono muingilio mlinganifu dhidi ya yunifomianizim ambao pia unaunga mkono imani kuwa ulimwengu na vimube vilivyopo ndani yake viliumbwa na Mungu (ama yenye kuona kuwa ulimwengu uliumbwa mamilioni ya miaka iliyopita [the Old Earth] au miaka elfu kadhaa tu [a Younger Earth]).

Kama nyongeza, watu wamekuwa wakisema kuwa kila kitu kiko vile vile na wanakosa matukio makubwa. Kwa mfano, kwenye kitabu cha kumbukumbu za kila siku cha Mfalme George III wa Uingereza aliandika Julai 4, 1776: "Hakuna jambo muhimu lililotokea leo." Julai 4, 1776 ni siku ambayo Marekani ilijitangazia uhuru toka kwa Waingereza.

 

S: Kwenye 2 Pet 3:5-8, unafikiri ni kwa nini ulimwengu uliangamizwa kwa maji na moto?

J: Uliangamizwa kwa mafuriko yaliyotokea wakati wa Nuhu kwenye Mwanzo 6-8. Lakini Mungu aliahidi kwenye Mwa 9:11 kuwa hatauangamiza tena ulimwengu kwa mafuriko tena. Kwa hiyo Mungu aliahidi kutokutumia tena mafuriko kuuangamiza ulimengu.

 

S: Kwenye 2 Pet 3:7, je "kuangamia kabisa" kunamaanisha kuwa watu wasiomcha Mungu wataangamizwa kabisa mara moja?

J: Hapana. Kuna mambo matatu ya kuzingatia katika kujibu swali hili.

1. Jehanamu ni mateso ya milele kwenye Mat 25:41, 46. Shetani na watu wengine watateswa milele kwa mujibu wa Ufu 20:10.

2. Ni kuangamizwa kwenye Luk 13:3; Yoh 3:15, 16; 10:28 na aya nyinginezo. Ni kuangamizwa milele kwenye 2 Thes 1:9, na wasioamini watangamizwa kwenye 1 Kor 6:13; 2 Thes 2:8; Ufu 11:18 na aya nyingine.

3. Hakuna aya kwenye Biblia inayosema kuwa watu wataangamizwa kabisa.

Je majibu 1 na 2 hapo juu yanawezaje kuwa ya kweli? Yanaweza kuwa hivy kwa njia mbili, au yanaweza kuwa yote mawili.

1. Magofu/mahame: Kwa kuwa vitu vingi vya hapa duniani vinaweza kuangamizwa nab ado vikaendelea kuwepo. Vitu hivi hutoa mifano isiyorekebishwa ya namna watu wanavyoweza kuangamizwa na bado wakaishi milele. Magari yanaweza kuharibiwa kisha yakapelekwa kwenye sehemu ya kuhifadhiwa. Nyumba inaweza kuharibiwa na moto kisha mabaki yake yalionguwza kwa kiasi na moto yakazombwa na kupelekwa sehemu nyingine. Mwisho, watu wasiomcha Mungu wangali wanaishi hata baada ya miili yao kuangamizwa.

2. Asimptote (Asymptotes), yaani mstari unaousogelea mchirizo lakini hauukuti mahali popote halisi (panapofahamika): Kitu kingine kinaweza kuwa kwenye mchakato wa kufanywa kama hakipo lakini bado kinaweza kuwa cha milele kwa sababu mchakato wenyewe haumaliziki milele. Kwa mfano, kitu kinapungua nusu ya ukubwa wake kila mwaka. Itachukua miaka mingapi kwa kitu hicho kuisha kabisa (yaani, kufikia ukubwa sifuri)? Jibu ni miaka isiyoweza kuelezeka. Sijaona kitu chochote kwenye Biblia chenye kuunga mkono au kupinga kisio hili la asimptote.

Kuna watu wanaofundisha maoni ambayo ni asimptote kana kwamba ni mbadala wa maoni asilia (magofu). Hata hivyo, maoni haya yanayanakamilishana, na kuonyesha umantiki wa maoni ya asimptote hayapingani na maoni asilia.

Tazama When Critics Ask, uk.493-494, When Cultists Ask, uk.297, na swali linalofuata.

 

S: Kwenye 2 Pet 3:7, 10-12; Ufu 21:1 na Zef 1:2-3, dunia itawezaje kuangamizwa wakati Muh 1:4 inasema kuwa dunia itadumu milele?

J: Ili kujibu swali hili, natuangalie jinsi dunia ilivyoangamizwa na mafuriku. Mwa 9:11 inasema mafuriko hayataiangamiza nchi tena. Ikumbukwe kuwa msingi na miamba vilikuwa bado vipo, lakini vitu vyote vyenye uhai, na vitu vingine vyote vilifutiliwa mbali na mafuriko kutoka kwenye uso wa nchi. Hivyo dunia ilipoangamizwa wakati wa Nuhu haikuacha kuwepo bali vitu vyote vilivyokuwepo usoni pake viliondolewa.

Neno ‘nchi' lina mlolongo wa maana kwenye Kiebrania, kama lilivyo kwenye Kiingereza. Nchi inaweza kumaanisha udongo, nchi, ulimwengu huu, au vitu vilivyo kwenye ulimwengu huu. Mungu amechagua kuvifanya vitu vilivyo chini ya nchi kudumu milele lakini atavifutilia mbali vitu vilivyo juu ya uso wa nchi kama anavyosema kwenye Zef 1:2-3. Nchi mpya kwenye Ufu 21:1 itatokana na vitu vitakavyobakia baada ya nchi za zamani kuondolewa.

 

S: Kwenye 2 Pet 3:8, miaka 1,000 inamaanisha nini?

J: Wakristo wa kweli hawakubaliani na hili.

1. Kuna wanaofikiri kuwa msemo huu ni kama mlinganyo: Siku 1 kwenye Kitabu cha Mwanzo = miaka yetu 1,000. Epistle of Barnabas (ulioandikwa mwaka 100-150 BK) sura ya 15, uk.146 unasema, "Wahudumie watoto wangu, kuhusiana na msemo huu, ‘Alimaliza kwa muda wa siku sita.' Jambo hili linamaanisha kuwa Bwana atamaliza vitu vyote kwa muda wa miaka elfu sita, kwani siku moja kwake ni miaka elfu moja. Na yeye mwenyewe anashuhudia akisema, "Tazama, leo itakuwa kama miaka elfu moja." Kwa hiyo, watoto wangu, kwa muda wa siku sita, yaani miaka sita, mambo yote yatakuwa yamekamilika. Na alipumzika siku ya saba."

2. Kuna wanaolichukulia neno "kama" na ukweli kuwa 1 ni kama 1,000 na 1,000 ni kama 1 vinamaanisha kuwa muda ambao Mungu anauita siku moja kwake unaweza kuwa mrefu sana mfupi sana kuliko muda wetu. Mfano mmojawapo ni neno la Kiebrania yom lenye kumaanisha zaidi ya masaa 24 ni wakati walipotabiriwa kuuvuka Mto Yordani kwenye Kum 7:1. Pia kwenye Agano la Kale na Agano Jipya, "Siku ya Bwana" ni kipindi kinachozidi masaa 24.

 

S: Kwenye 2 Pet 3:8-9, unafikiri ni kwa nini Mungu alimtuma Yesu duniani kwa mara ya kwanza muda mrefu sana baada ya kuumbwa kwa dunia?

J: Jibu fupi ni kwamba Yesu alikuja wakati ule ule aliokuja kwa sababu kwenye Dan 9:20-27 ndio wakati ambao Mungu alitabiri kuwa Yesu angekuja. Hata hivyo, jambo hili linaleta swali kuwa kwa nini Mung hakutabiri muda mwingine, na amfanye Yesu aje wakati huo?

Rum 5:6 inasema, "Kwa maana . . . wakati ulipotimia, Kristo alikufa kwa ajili ya waovu." Maandiko hayajibu swali hili moja kwa moja kuwa kwa nini muda huu ulikuwa ndi sahihi, lakini inafurahisha kukisia.

Baada ya 90% ya watu: Tunakisia kuwa kumekuwepo watu karibu bilioni 32 (uwezekano wa kukosea wa karibu bilioni 6) ambao wamewahi kuishi hapa ulimwengu. Zaidi ya 90% kati ya hao wameishi baada ya kuja kwa Kristo.

Ni haki kwa wale waliotangulia: Mungu huwapima watu kwa kuzingatia ufahamu walio nao kuhusu kweli; dhambi haihesabiwi mahali ambapo hakuna sheria (Rum 4:15; 5:13). Kwa hiyo watu walioishi kabla ya Kristo, kama vile Abraham, Daudi, n.k. waliokolewa kupitia kwa Yesu ingawa Yesu alikuwa bado kuja duniani.

Muda mrefu zaidi wa amani: Wakati Yesu alipokuwepo duniani palikuwa na kipindi cha amani kuliko vipindi vilivyotangulia kabla ya ushindi wa Warumi, na vipindi vilivyofuatia vya vita vya Warumi na Waparthia (ufalme wa zamani ulikuwepo kusini mashariki mwa Bahari ya Kaspian (Caspian Sea) kwenye Irani ya sasa), na kuvamiwa kwa Himaya ya Rumi na watu wasiostaarabika na makatili wa Ulaya. Tazama www.BibleQuery.org/History/Calamities/Wars.html kwa maelezo ya vita zaidi za wakati huo endapo unapenda.

Muda mzuri zaida wa kuenea: Wakati wa kushamiri kwa Himaya ya Rumi, moja ya sababu kubwa ya kuenea kwa haraka kwa ukristo ilikuwa ni barabara bora zilizojengwa na Warumi zilizowezesha usafiri wa haraka na wenye kufikisha maeneo mengi. Kama Yesu angekuja kabla ya muda huu, ingekuwa vigumu zaidi kueneza injili kwenye nchi nyingine.

Kuhifadhiwa kwa Maandiko: Kama Yesu angekuja muda mrefu sana kabla ya wakati aliokuja duniani, tungeweza kuwa na hata chache sana zenye maandiko ya kazi za kale ambazo hazipo tena zenye kuonyesha kuaminika kwa Agano la Kale. Kama ingekuwa karne kadhaa baada ya wakati Yesu alipokuja duniani, tungeweza kuwa na hati nyingi zaidi za maandiko ya kazi za kale, lakini hata hivyo tunazo hati za kazi za kale za Kigiriki na vipande vya Agano Jipya zaidi ya 10,000. Hati ya zamani zaidi ni karatasi ya mafunjo ya John Rylands papyrus, iliyoandikwa mwaka 110-138 BK. Zifuatazo ni hati za kazi za kale zilizopo:

Mwaka 110/117- 125/138 BK

p52 (= karatasi ya mafunjo ya John Rylands)

Yoh 18:31-33, upande wa pili 18:37-38 - aya 4

Mwaka 100-150 BK

p104

Mat 21:34-37, 43, 45(?) - aya 5.5

Mwaka 100-150 BK

p46 (=Chester Beatty II)

70% ya nyaraka za Paulo na Waebrania - aya 1,680

Karibu mwaka 125 BK

p87 -imeandikwa kwa mkono kama p46

Flm 13-15, 24 (sehemu), 25b na mapengo - aya 4

Karne ya 2

Makaratasi ya mafunjo ya Magdalen

Mat 26:7-8, 10, 14-15, 22-23, 31-33 - aya 10

Mwaaka 100/125-150/175 BK

p66(=Bodmer II) p14/15, p75

92% ya Injili ya Yohana - aya 808.5

Mwaka 125-150 BK

p64, p67 (hati hiyo hiyo)

(p67) Mat 3:9, 15; 5:20-22, 25-28 - aya 19

(p64) Mat 26:7-8, 10, 14-15, 22-23, 31-33

Mwanzo hadi katikati ya karne ya 2

p4 - imeandikwa kwa mkono kama p64, p67

Luk 1:58-59; 1:62-2:1, 6-7, n.k. - aya 95

Karibu mwaka 170 BK

Uncial 0212

Vipande vya Diatessaron: Mat 27; Mak15; Luk 23; Yoh 19

Karibu mwaka 175 BK

p90

Yoh 18:36-19:7 - aya 12

Mwaka 177BK- 97% (855/878) ya Injili ya Yohana, 70% ya nyaraka za Paulo na Waebrania (mateso ya Aurelius)

Kwa kutumia hati za maandiko ya kale tuliyonayo zilizoandikwa kabla ya mateso ya Marcus Aurelius kwenye 177 BK tuna 97% ya Injili ya Yohana (aya 855/878) na 70% ya nyaraka za Paulo na Waebrania.

Eusebius kwenye Ecclesiastical History (mwaka 323-326 BK) kitabu cha 1 sura ya 2, uk.84 kinatoa jibu tofauti lakini lenye kukamilisha. Anasema tu kuwa injili haikuhubiriwa kabla ya hapo kwa sababu wanadamu wenye dhambi hawakuwa tayari kuipokea (Nicene and Post-Nicene Fathers Second Series juzuu ya 1, uk.84).

 

S: Kwenye 2 Pet 3:8-9, kwa nini Mungu alichukua muda mrefu sana kabla ya kumtuma Yesu mara ya pili?

J: Mungu huchelewesha mambo mengine kwa neema. Hatufahamu vigezo vyote ambavyo Mungu alivitumia alipopanga ratiba. Mdo 1:7 inasema kuwa si kazi yetu kujua nyakati au majira, Baba alivyoweka katika mamlaka yake mwenyewe. Lakini 2 Pet 3:8-9 inasema kuwa Bwana hapendi mtu yeyote apotee bali wote wafikie toba; kwa hiyo kuchelewesha anakokufanya Mungu ni neema.

 

S: Kwenye 2 Pet 3:10, je mwizi huja kwa kutegemewa au bila kutegemewa? Je mwizi anapokuja huwa anaonekana au haonekani?

J: Mwizi huja bila kutegemewa, na kuja kwa Yesu hakuonekani. Hata hivyo, baada ya mwizi kuondoka matokeo yake yanaonekana dhahiri. Siku ya Bwana pia haitafahamika kabla, lakini Yesu atakapokuja kila jicho litamwona (Ufu 1:7). Kuja kwake kutakuwa kama alivyoondoka, kwenye mawingu (Mdo 1:9-11).

 

S: Kwenye 2 Pet 3:11, ni kwa jinsi gani ufahamu wa unabii unapaswa kutuhimiza kuishi kwa utakatifu na kumcha Mungu?

J: Tunajua kuwa Mungu anaona na kujua kila kitu. Tunajua kuwa watu watatakiwa kutoa hesabu ya kila neno ovu walilolisema (Mat 12:36-37). Kama waumini tutatakiwa kutoa hesabu mbele ya kiti cha bema cha Kristo (2 Kor 5:10). Tunajua kuwa anasa zozote za dhambi tunazoweza kuzifanya kwa kipindi kifupi hazilingani na furaha ya milele pamoja na Mungu.

 

S: Kwenye 2 Pet 3:11-12, waumini wanawezaje "kukuhimiza" kuja kwa Kristo?

J: Wakristo wameagizwa kuombea kuja kwa ufalme wa Mungu tokea wakti Yesu alipofundusha Sala ya Bwana, (ambayo pia inaitwa "Baba Yetu" na watu wengine). Yesu hakutuagiza kufanya sala kidogo tu "kwa ajili ya kujifurahisha", bali maombi yetu hutenda kazi.

Ni vema kuzingatia kuwa Mwenyezi Mungu amechagua maombi yetu kuwa moja ya vyombo anavyovitumia kutimiza mapenzi yake.

Pia kwa kuwa 2 Pet 3:9 inasema kuwa Mungu anachelesha kwa makusudi kabisa ili kwamba mtu yeyote ambaye angependa kuokolewa asiangamie, kuueleza kwetu ulimwegnu mzima habari njema za Yesu Kristo ni njia mojawapo ya kukuhimiza kuja kwa Yesu.

 

S: Kwenye 2 Pet 3:16, ni kwa jinsi gani watu wasio na elimu na wasio imara wanayapotosha Maandiko? Kuna mifano gani ya watu wasioamini na waasi wa kidini kupotosha Maandiko?

J: Kwanza kabisa tambua kuwa Mtume Petro hakutumia neno wajinga, au wasio na akili hapa. Mtu anaweza kuwa na akili nyingi tu, lakini bado akawa hana ujuzi. Jambo hili linaishia kwenye eksigesisi (ufafanuzi au tafsiri ya kihakiki ya maandishi) dhidi ya eisegesisi (kutafsiri matini au maandishi kwa namna inayolazimisha fikra, maoni, mtazamo au agenda ya mwenye kutafsiri kwenye maandishi). Eksigesisi inatafuta kupata maana ambayo kifungu cha Maandiko kinaitoa. Eisegesisi ni kukifanya kifungu cha Maandiko kitoe maana unayoipenda wewe. Shetani anataka kukana Maandiko, lakini kama hawezi kutimiza azma hiyo, anataka kutiashaka kwenye Maandiko. Na kama hataweza kufanya hivyo, anataka kuyapindisha Maandiko. Kupindisha Maandiko kunaweza kuwa ni kuthibitisha kitu kisichokuwa sahihi, au kutilia mashaka kuwa tunaweza kufahama maana yake halisi.

Mit 30:5-6 inatuagiza kuwa waangalifu tusiongeze neno kwenye Maandiko. Tunapoweka mawazo yetu kwenye kiwango kimoja na Maandiko tunaacha kuitii Mit 30:4-5. Agizo hili linapaswa kufuatwa hata kama mawazo yetu na kutafsiri kwetu Maandiko ni sahihi.

Mifano ya kupindisha Maandiko ni kama ifuatavyo:

Mch. Moon, anayekana kuwa Kristo atatokea mawingu hasa, anatafsiri vifungu vyote vyenye kuongelea jambo hili kuwa mawingu ni makundi ya watu kwani Ebr 12:1 inasema sisi [siyo Yesu] tumezungukwa na kundi kubwa la mashahidi [siyo wingu].

Mashahidi wa Yehova, wanaokana uwezo wa mtu kujitambua baada ya kufa, wanatafsiri mateso ya tajiri aliyempuuzia maskini Lazaro (Luk 16:19-31) kuwa "kuaibishwa kwa kundi la Mafarisayo na kundi la mtumwa mwaminifu."

The Divine Light Mission inafundisha kuwa kwa kuwa Yesu atakuja tena mawinguni na Guru Maharajah alikwenda Marekani kwa ndege iliyopita mawinguni, hivyo alitimiza aya hii.

WaMomoni ambao wanaamini kuwa Mungu ni mtu aliyetukuzwa, mara nyingine hutafsiri Hes 23:19: "Mungu si mtu aseme uongo" kuwa "Mungu si aina ya mtu aseme uongo.

Tafsiri hizi zilizotangulia zina "mantiki ngeni." Inapotokea kuwa maana ya wazi ya neno la Mungu inapingana na theolojia yao wanataka kuweka maana nyingine badala ya maana ya wazi kabisa.

Aina nyingine ya kupindisha Maandiko ni kusema kuwa hatuwezi kuijua maana ya kifungu fulani, ingawa ukweli ni kwamba tunaweza na tunaijua. Hatupaswi kusita kuthibitisha jambo tunalolijua kuwa kweli. Huwezi kuwa unachukua aya kadhaa na kuziach nyingine. Kwa mfano, Waprotestanti wa kiinjili (wenye kusistiza mamlaka ya Biblia, kuokolewa kwa mtu binafsi, na mafundisho kuhusu wokovu unaopatikana kwa imani katika kifo cha Yesu msalabani kwa ajili ya dhambi za wanadamu), Mch. Moon, Mashahidi wa Yehova, Waisalamu, wafuasi wa New Age (harakati pana inayotafuta namna tofauti na zile za Kimagharibi yenye kukazia mambo ya kiroho, miujiza, kuchukulia vitu kiujumla na utunzaji wa mazingira), na watu wenye kutilia shaka/kutoafiki msimamo wa asili, asilia au mapokeo, na wengine wengi wametoa maoni yanayotofautina sana kuhusu kufufuka kwa Yesu kiasi kwamba, "kwa hiyo" hatuwezi kujua kitu ambacho Biblia inamaanisha inaposema kuwa Yesu alifufuka kutoka kwa wafu. Hivyo, badala ya kuamini kitu kisichokuwa sahihi, tusiamini kitu chochote kuhusu jambo hili. Njia nyingine ya kuliangalia jambo hili hili ni kuuliza, je ni mambo mangapi ya uongo ambayo Shetani anatakiwa kukueleza kabla huamwambia, "HAYA, nimejisalimisha na kuafikiana na wewe. Sitamwamini Mungu tena kwa kitu chochote atakachosema kuhuhu jambo hili." Wakristo hawatakiwi kumsikiliza shetani, na tusijali ni mambo mangapi ya uongo yaliyosemwa kuhusu kifungu che Maandiko, au ni mashaka ya kiasi gani ambacho hukileta. Maana ya "kufufuka" ilikuwa wazi na dhahiri kwa waandishi wa Biblia na Wakristo wa awali, na kwa mujibu wa 1 Korinto 15, wale wanaokana kufufuka kwa Yesu kimwili wako nje ya kundi, na ni pale tu watakapookolewa, hawatakuwa na sehemu kwenye wokovu wa Mungu.

Baadhi ya dalili za kupinduliwa kwa Maandiko ni pamoja na:

1) Kama unataka aya iwe na "maana ya ndani" inayokwenda kinyume na maana wa wazi ambayo mtu yeyote angeielewa ambayo mwandishi aliikusudia. Kama jambo hili lingevumiliwa basi kila yenye kusema jambo ambalo mtu halitaki, lingeweza vivyo hivyo kuwa na maana inayodaiwa kuwa "halisi" iliyo tofauti na Mungu anavyosema wazi. Mtu anapoitafuta maana ya ndani kwa nguvu sana, na maana hiyo inapingana na maana iliy wazi basi maana hiyo inayodaiwa kuwa ya ndani si sahihi.

2) Kwa jinsi hiyo hiyo, kutoa tafsiri ya kiistiari (kiishara) ya Maandiko kunakovuka mpaka: Kuna baadhi ya vifungu vya Maandiko vinavyochukuliwa kuwa vya kiistiari, lakini vingi ya vifungu vya Maandiko haviko hivyo.

3) Unatakiwa kusema kuwa kwenye Kigiriki au Kiebrania neno lina maana maalumu ambayo hakuna mzungumzaji wa Kigiriki au Kiebrania ambaye angeweza kuitambua. Kama unalazimika kutoa maana tofauti au isiyo ya kawaida ya maneno ambayo msomaji wa kawaida asingeiona kabisa basi utakuwa unayapindua Maandiko kuwa kuyapa maana mpya.

4) Kama maana ya neno unayotaka kuitoa inapingana na Maandiko mengine na mtazamo wa jumla wa Biblia nzima.

5) Kama makusuduo yako ni kupunguza umuhimu wa Maandiko kuliko kuyafafanua Maandiko. Kinyume cha hapo, ni vema endapo thiolojia yako haitapunguza umuhimu wa Maandiko tu bali pia itatafuta ukweli wa neno/maneno hayo ya Biblia. Kama ufafanuzi wako unavifanya baadhi ya vifungu vya Maandiko visiwe na maana basi ufafanuzi huo una makosa.

6) Kwa upande uliovuka mpaka zaidi, ufafanuzi wako unamaanisha kuwa Mungu aliificha kutoka kwa kila muumini kwa miaka karibu 2,000 maana maalumu ya siri ambayo sasa ameifunua kwako.

Hata Wakristo wa kweli wanaweza kupindua Maandiko kwa kutokujua. Tunapaswa kumwomba Roho Mtakatifu atuongoze tunaposoma Maandiko.

 

S: Kwenye 2 Pet 3:16, kuna mifano gani ya waumini wa kweli waliowahi kupidua Maandiko?

J: Ifuatayo ni mifano kutoka kwenye historia ya kanisa ambayo Wakristo wote wa leo wanaafiki kuwa yalikuwa mambo mabaya. Lengo la kuielezea hapa si kuwaaibisha watu waliofanya mambo haya bali kuhakikisha kuwa hatufanyi makosa mengine kwa sababu hizo hizo.

Kutokuangalia maelezo yote: Justin Martyr (mwaka 138-165 BK) alisema kuwa kuhani mkuu alikuwa na kengel 12 chini ya kanzu lake. Ukweli ni kwamba kulikuwa na mawe ya thamani 12 kwenye naivera yake, na idadi isiyoelezwa ya kengele chini ya kanzu lake (Dialogue with Trypho the Jew sura ya 42, uk.215)

Kuchanganya majina: John Chrysostom (aliyekufa mwama 407 BK) anaongelea kuuawa kwa Mefiboshethi wakati alitakiwa aeme Ishiboshi (Commentary on Philippians Mahubiri ya 5 aya ya 3, uk.206).

Kuchanganya maneno ambayo Biblia inasema mtu asiyekuwa muumini amesema na maneno ambayo Mungu anasema: Irenaeus (mwaka 182-188 BK) inasema kuwa Yesu alikuwa na miaka karibu 50 alipoanza huduma yake (Irenaeus Against Heresies kitabu cha 2 sura ya 22.6, uk.392).

Kutokuzingatia sehemu nyingine za Maandiko: Shepherd of Hermas (karibu mwaka 160 BK) kwenye kitabu cha 2 amri ya 10 sura ya 2, uk.27 anasema huzuni humwondoa Roho Mtakatifu kwani Roho Mtakatifu ni mwenye furaha. Vipi kuhusu kutubu, na Kitabu cha Maombolezo? Je Roho Mtakatifu huondolewa kwa Wakristo kila wakati tunapokuwa na huzuni?

Kutoa maana ya Maandiko ya kiistiari (kiishara) kunakovuka mpaka: Novatian (mwaka 250/4-256/7 BK) anasema kuwa amri ya kwenye Agano la Kale ya kutokula nyama ya ngamia inamaanisha kuwa inakataza maisha yaliyopotoshwa na uhalifu (On the Jewish Meats sura ya 3, uk.647).

Kutoa maana ya Maandiko ya kiistiari kunakovuka mpaka kweli kweli: Clement wa Alexandria (mwaka 193-202 BK), "Kanzu la kuhani mkuu ni kielelezo cha ulimwengu wenye busara. Sayari saba zimewakilishwa bam awe matano na vito vyekundu viwili, kwa ajili ya sayari ya sayari ya Zohali (Saturn) na mwezi. Kito cha kwanza kipo kusini magharibi, na ni kibichi na chenye udongo (kama dunia) na ni kizito; kito cha pili kina sura ya anga, kutona na hivyo, watu wengine wanakiita Artemis, kana kwamba Aerotomos (kukatisha anga); na anga lina mawingu" (Stromata kitabu cha 4 sura ya 6, uk.453).

Kusoma vibaya maneno yaliyotafsiriwa: Theodotus, ambaye anaelekea kuwa alikuwa Mmontani (karibu mwaka 240 BK), "‘Mungu ameweka hema lake kwenye jua' ifahamike hivyo? Mungu ‘ameweka jua,' yaani, kwa Mungu aliye pamoja naye, kama kwenye Injili, Eloi, Eloi, badala ya Mungu wangu, Mungu wangu." Maelezo chini ya ukurasa yanasema kuwa Theodotus alichanganya Eloi, Eloi na Helios, Helios ambayo inamaanisha jua kwenye Kigiriki (Excerpts of Theodotus sura ya 57, uk.50 5:2, 8).

Kuzuia kuliko Biblia inavyosema: Muanabaptisti Conrad Grebel (mwaka 1498-1526 BK) aliamini kuwa kuimba hakuruhusiwi kanisani. Kol 3:16 inasema, ". . . kwa zaburi, na nyimbo, na tenzi za rohoni; huku mkimwimbia Mungu kwa neema mioyoni mwenu." Lakini Conrad alitafsiei maneno "mioyoni mwenu" kumaanisha hampaswi kuimba kwa sauti inayosikika.

Kuongeza matumizi ya maneno zaidi ya kiasi ambacho Biblia inasema: Athanasius (mwaka 326-373 BK) alifundisha kuwa Yeremia na Yohana Mbatizaji walizaliwa bila asili ya dhambi.

Kuzifanya hisia zako kuwa hisia za Mungu: Mungu hana ghadhabu hata kidogo, kwa mujbu wa Clement wa Roma [mwaka 96-98 BK] (1 Clement sura ya 19, uk.10) na To Diognetus (mwaka 130-150 BK) sura ya 8, uk.28.

Kuyapa maoni yako mamlaka sawa na Maandiko: Cyprian wa Carthage [karibu mwaka 248-256 BK] (Letters of Cyprian Barua ya 58.2, uk.353), Ambrose wa Milan (mwaka 370-390 BK), Augustine wa Hippo (mwaka 388-430 BK), na Prosper wa Aquitaine [karibu mwaka 390-455] (On Forgiveness of Sin 5:25, 26-28-29, na Baptism sura ya 26-30, 33-35) wote hawa walifundihsa kuwa watoto wadogo waliobatizwa wanapokufa wanakwenda mbinguni kwa uhakika, na watoto ambao hawajabatizwa wanapokufa wanakwenda jehanamu kwa uhakika.

Kuongezea maoni yako ya kiroho kwenye Biblia: Origen (mwaka 225-254 BK) aliamini kuwa nafsi za wanadamu zilikuwepo hata kabla ya wanadamu hao kuzaliwa kwenye de Principiis. Hata hivyo hakuamini kuwa nafsi huzaliwa upya kwenye mwili mwingine.

Kuweka kwenye Biblia maoni yako kuhusu asili: Lactantius (c.303-c.325 BK) alifundisha kuwa dunia ina umbo bapa. Ni ujinga kufikiri kuwa ina umbo la duara na kwamba kuna watu upande mwingine wa mduara wanaotembea kichwa chini miguu juu (The Divine Institutes kitabu cha 3 sura ya 24, uk.94).

Kuweka imani za kishirikina kwenye maneno ya Mungu: Mlutheri Philip Melanchthon (mwaka 1497-1560) aliamini kuwa unajimu na kusoma viganja vya mikono ni muhimu katika maisha. Hata hivyo, Martin Luther aliyapinga mambo hayo.

Kuweka hisia zako za upendo au chuki bila sababu kwenya Neno la Mungu: Lactantius (mwaka c.303-c.325 BK) anawataja wanaume kuwa wenye nguvu na afya kuliko wanawake ambao anasema kuwa ni wadhaifu na wanyonge (The Divine Institutes kitabu cha 1 sura ya 16 uk.29. Athanasius (mwaka 318 BK) aliandika: "Kwani hata wanawake, ambao si salama kuwaingiza kwenye maazimio yahusuyo mambo ya umma, wanaabudu na kutumika kwa heshima anayostahili Mungu kama watu waliofundishwa na Theseus kama ilivyoelezwa hapo juu" (Athanasius Against the Heathen sura ya 10.2, uk.9. John Chrysostom (aliyekufa mwaka 407 BK) alikuwa anawachukia sana Wayahudi; aliandika kitabu kizima chenye kuwapinga Wayahudi. Kitabu hiki hakikuipinga dini yao tu bali pia Wayahudu wenyewe.

Kutokusamehe: Novatian (mwaka 250/254-256/257 BK) alianzisha utengano kwenye kanisa. Wanovatia walikuwa wanamini kama Wakristo wengine tu, isipokuwa walifundisha kuwa mtu akiikana imani, hata kama atakuwa ametishiwa, atakuwa amepoteza wokovu wake milele na hataweza kuupata tena.

Kutokuwa na upendo: Martin Luther aliamini kuwa Waanabaptisti wote wanatakiwa kuuawa. Lakini alibadilisha maoni yake kwenye mahubiri yake ya mwisho. Augustine aliunga mkono kutswa kwa waasi wa ukristo kama vile Priscillian.

Lakini Wakristo wa kweli wanaweza kufanya makosa ya kiasi kinachofanana na haya hapa juu. Tunapaswa kuwa na mafundisho sahihi na kuenenda na Roho. Kama ambavyo Mkristo mmoja wa miaka hii alivyosema kwa kejeli: "Ukiwa na mafundisho bila kuwa na Roho utakauka, ukiwa na Roho bila kuwa na mafundisho utapasuka, na ukiwa na vyote viwili utakua."

 

S: Kwenye 2 Pet 3:17, ni kwa jinsi gani waumini wa kweli wanaweza kupotoshwa na makosa ya watu wa uasi?

J: Inasikitisha kusema hivi, lakini inaweza kutokea. Binafsi namjua Mkristo ambaye alibadili imani na kuwa Mmomoni (watakatifu wa Siku za Mwisho). Kisha aliacha tena akaurudia ukristo.

Pia nimewahikusoma habari ya mwanamke aliyeuacha ukristo na kuugeukia uislamu. Baada kuwemo kwenye uislamu kwa miaka 15 alisema, "Jana nitambua kuwa nimekuwa nikijaribu kupuuzia hasa kutokana na kiburi. Nimekuwa Mkristo wakati wote, ingawa niligeuka kuwa Muislamu. Wakai wote huu kumekuwa na sehemu yangu ambayo haikuamini kama Waislamu wengine wanavyoamini. Sauti ndogo iliyokuwa inasema: Je, Mungu anapenda watu wapondwe kwa mawe hadi kufa?", je, Mungu anapenda wanawake watengwe kwa kuvaa hijabu kichwani?", "ikiwa uislamu ni bora zaidi, kwanini wanatendeana vibaya namna hii?" Jana nilihisi uhitaji wa ukombozi na rehema ya kweli ya ukristo.

Kwa hiyo 2 Petro inawapa waumini wa kweli onyo kali la kuwa macho; inaweza kututokea hata sisi. Kuanguka kutoka kwenye nafasi zao salama kunaweza kumaanisha si tu kupoteza tuzo, lakini pia kupoteza hakika ya wokovu. Hata hivyo, ikiwa tuna imani yenye ustahimilivu tutarudi kwa Mungu.

 

S: Kwenye 2 Pet 3:17, kwanini waumini wa kweli, ambao wamekwishaokolewa, wanapaswa kuwa macho?

J: Mungu anatuamuru tujitathimini wenyewe kwenye 2 Kor 13:5-7 kuhakikisha kuwa tumeokoka hakika. Pia tunahitaji kumwomba Mungu atuchunguze ili atuonyeshe ikiwa tunafanya jambo lolote linalomwuudhi kama Zab 139:24 isemavyo.

 

S: Kwenye 2 Pet 3:17, ni kwa jinsi gani waumini wanaweza kuanguka kutoka kwenye nafasi yao salama?

J: Kuna Wakristo wanaofikiri kuwa waumini wa kweli wanaweza kupoteza wokovu wao; Wakristo wengine hawafikiri hivyo. Lakini licha ya hayo, Mat 7:22-23 itatokea, ikiwa unakuita unasema kuwa huku ni kupoteza wokovu au wokovu wa kugushi. Tumeamuriwa kujitathimini wenyewe, kuona kuwa tumo kwenye imani katika 2 Kor 13:5-7.

Hata waumini halisi wanaweza kuhadaiwa kwa kipindi fulani. Ninamfahamu Mmomoni aliyeuacha umormoni na kuja kwa Kristo. Baadaye alirudi kwenye umomoni. Kisha Wakristo kadhaa waliowahikuwa Wamomoni waliongea naye, na akauacha tena na kurudi tena kwa Kristo.

Hata Wakristo wanaweza kuanguka dhambini. Lakini wanaweza kurudi, na 1 Kor 5:1-5 na 2 Kor 2:5-11 zinaonyesha.

Kwa kuongezea, Wakristo wanaweza kupoteza tuzo zao kama 1 Kor 3:5-15 na 2 Yoh 8 zinavyoonyesha. Hatutaki kuja kuaibishwa mbele ya Kristo kwa ajili ya mambo tuliyotenda (1 Yoh 2:28).

 

S: Kwenye 2 Pet 3:18, kwa kuwa neema ilikwishatolewa kwetu kupitia kwa Yesu msalabani, tunawezaje kukua katika neema?

J: Tunaweza kukua katika neema kwa njia mbalimbali, na hapa ni chache kati ya hizo.

1. Kila mmoja anaweza kukua kwa kuonyesha neema ya Mungu maishani mwetu. Matoleo yetu ya kifedha ni matendo ya neema (2 Kor 8:6), na tunapaswa kuufanyia kazi wokovu uliomo ndani mwetu kwenye Flp 2:12-13.

2. Kila mmoja wetu anaweza kukua katika ufahamu na tumaini la neema ya Mungu. Kwenye 2 Tim 2:1, Timotheo anatakiwa kuwa hodari katika neema iliyo ndani mwa Kristo Yesu.

3. Neema ya Mungu inaweza kuwafikia watu wengi zaidi na zaidi kwenye eneo letu (2 Kor 4:15).

4. Tutapokea utajiri usiolingana na kitu chochote wa neema ya Mungu kwa mujibu wa Efe 2:6-7

 

S: Je Waraka wa 2 Petro uliandikwa lini?

J: Kwa kuwa 2 Pet 1:13-15 inasema kuwa Mungu alimwonyesha Petro kuwa kifo chake kilikuwa kimekaribia, maelezo rahisi ni kuwa uliandikwa muda mfupi kabla ya kifo chake mwaka 67-68 BK.

Firmilian (mwaka 256 BK) anaongelea maonyo ya Petro dhidi ya walimu wa uongo.

Methodius wa Olympus na Patara (mwaka 260-312 BK) alinukuu 2 Petro 3:8 kama inatoka kwa Petro kwenye On the Resurrection.

Kwa mtizamo usiokuwa wa Kikristo, Asimov's

Guide to the Bible (uk.1165) inasema, "kuna uwezekano kuwa 2 Petro, kama 1 Petro na Yakobo, zinaweza kuwa ziliandikwa wakati wa mateso ya Dominitia" (yalianza mwaka 90 BK). Watoa maoni mbalimbali wanasema hivi kwa sababu,

a. Hutaja nyaraka za Paulo kana kwamba zilikuwa zimeshakusanywa, au angalau zilikuwa zimeandikwa.

b. Inatia mkazo wenye kuashiria kuwa Wakristo walikuwa wanateswa.

c. Waraka huu unafanana na Yuda, kwa hiyo kuna uwezekano kuwa zote ziliandikwa karibu muda mmoja.

Hata hivyo, kwa kuwa nyaraka za Paulo ziliandikwa kabla ya kifo cha Petro, mateso makubwa yalianza miaka mitatu hadi mnne kabla ya kifo cha Petro, na Yuda ingeweza kuandikwa kirahisi kabla ya kifo cha Petro, hapana tatizo hapa la kusema kuwa 2 Petro iliandikwa kabla ya mwaka 67-68 BK. Angalia pia maelezo ya muda 1 Petro ilipoandikwa.

 

S: Kwenye 2 Petro, tunajuaje kuwa kitabu cha 2 Petro kiliandikwa na Mtume Petro, hasa kwa sababu mtindo wa uandishi Kigiriki cha 1 Petro na 2 Petro vinatofautiana?

A: Kuna sababu zisizopungua tatu.

1. 2 Petro 1:1 inasema hivyo, na kanisa la awali lilikubaliana na maneno haya. Mtu pekee aliyekuwa na maoni tofauti ni Origen, aliyesema kuwa Waraka wa Pili wa Petro hauna uhakika. Baada ya baraza la kanisa la Nikea Eusebius alisema kuwa 2 Petro haina uhakika.

2. Mtindo (si sarufi ya Kigiriki) wa nyaraka hizi mbili ni tofauti kwa sababu mada zake ni tofauti. Kama Gleason Archer (Encyclopedia of Bible Difficulties uk.425-426) anavyoeleza, kulinganisha orodha za maneno hakuthibitishi zaidi kuwa nyaraka zimeandikwa na watu tofauti kuliko ambavyo orodha ya maneno ingeweza "kuthibitisha" mashairi ya John Milton yaliandikwa na mtu tofauti na Paradise Lost, na kila mtu anakubali kuwa Milton aliandika kazi zote hizi mbili.

3. Sarufi ya Kiyunani ya 2 Petro haijakamilika, kwa sababu, kama 1 Pet 5:12 inavyooonyesha, Silwano alimsaidia Mtume Petro kuandika 1 Petro. Hata hivyo, hatujui kama Petro alimwambia Silwano aandike kwa Kiaramuau Kiyunani.

 

S: Kwenye 2 Petro, Mtume angewezaje kuandika kitabu hiki kwa kuwa [anadaiwa] kutokufahamu Kigiriki (Bart Ehrman atoa madai haya)

J: Ehrman adhani kuwa Petro hakujua Kigiriki kwa sababu kimbari na kitamaduni alikuwa Myahudi aliyekuwa anaishi Palestina na kuufuata utamaduni wa Kiyahudi. Hata hivyo, wazazi wake wenyewe walimpa mtoto wao wa kiume jina la Kigiriki! Ingawa jina alilopewa Petro wakati wa kuzaliwa lilikuwa Simoni (ambalo ni la Kiebrania na Kiaramu) mdogo/kaka yake aliitwa Andrea, jina lenye kumaanisha "ya kiume" kwenye Kigiriki. Zaidi ya hayo, walitokea Bethsaida, ambako kulikuwa karibu na mpaka wa Nazareti na mikoa iliyokuwa ikiongea Kigiriki ya kwenye nusu ya mashariki ya mwambao wa Bahari ya Galilaya. Filipo, ambalo ni jina lingine la Kigiriki, naye pia alitoka Bethsaida. Jambo hili linaweza kueleweka zaidi kwa kudhania kuwa raia wa Marekani aliyezaliwa na kukulia Texas kwenye mji wa mpakani wa El Paso, akiwa na kaka yake anayeitwa Manuel au Jose, wasijue Kihispania hata kidogo kwa sababu wao ni Wamarekani.

 

S: Kwenye 2 Petro, tunawezaje kujua endapo waraka tulionao leo ni nakala yenye kuaminika ya kile kilichoandikwa hapo mwanzo?

J: Kuna sababu zisizopungua tatu.

1. Mungu ameahidi kulitunza neno lake kwenye Isa 55:10-11; 59:21; 40:6-8; 1 Pet 1:24-25; na Mat 24:35.

2. Ushahidi wa kanisa la awali. Wafuatao ni waandishi walioiongelea 2 Petro au aya zilizomo ndani yake.

Clement wa Roma (mwaka 96-98 BK) anadokezea 2 Pet 2:5 kwenye 1 Clement sura ya 7 juzuu ya 1, uk.7; juzuu ya 9 uk.231.

Justin Martyr ananukuu Zab 90:4 na 2 Pet 3:8 anaposema, "Siku moja ya Bwana ni kama miaka elfu."

Letter of Barnabas sura ya 15, uk.146 (mwaka 70-130 BK), Justin Martyr (karibu mwaka 138-165 BK) na Irenaeus (mwaka 182-188 BK) wanasema siku moja ya Bwana ni kama miaka elfu (2 Pet 3:8). Hata hivyo, maneno haya yanaweza kuwa yananukuu Zab 90:4 na 2 Pet 3:8.Waraka wa 2 Petro ni kitabu chenye ushahidi kidogo zaidi kwenye Agano Jipya.

2 Clement (karibu mwaka 120-140 BK) sura ya 2, uk.517 inadokeza 2 Pet 3:9 "Ni jambo zuri na lenye kupendeza kulithibitisha, si vitu vinavyosimama, bali vile vinavyoanguka. Hivyo Kristo alivyotamani kuokoa vitu vilivyokuwa vinapotea . . ."

2 Clement (karibu mwaka 120-140 BK) sura ya 16, uk.522 anadokeza 2 Petro, "Lakini unajua kuwa siku ya hukumu ‘inakuja kama tanuru liwakalo' hata sasa na sehemu ‘ya mbingu itayeyuka', na dunia yote itakuwa kama risasi iyeyukavyo kwenye moto, na kisha mambo yote yaliyojificha ya wanadamu yataonyeshwa."

Irenaeus (mwaka 182-188 BK) anukuu theluthi ya 2 Pet 3:8m "Siku moja kwa Bwana ni kama miaka elfu." Maneno haya yanapatikana hivi yalivyo kwenye 2 Pet 3:8m na Zab 90:4 tu (Irenaeus Against Heresies, uk.551 ). Ananukuu maneno hay ohayo tena kwenye Irenaeus Against Heresies, uk.557.

Kama wazo la nyongeza, Muratorian Canon (karibu mwaka 170 BK) haikuviweka vitabu vya Yakobo, Waebrania, 1 na 2 Petro, wala 3 Yohana kwenye orodha ya vitabu vya Agano Jipya.

Clement wa Alexandria anukuu sehemu ya katikati ya 2 Pet 2:5 kwenye Stromata (mwaka 193-202 BK) kitabu cha 1 sura ya 21, uk.331, "Nuhu alihubiri toba." Wazo hili hili, ambalo Clement alichukulia kuwa wasomaji wake walikuwa wameshalisikia, halimo kwenye Maandiko isipokuwa 2 Pet 2:5. (maneno 3 likiwemo moja refu) kati ya maneno 15)

Hippolytus (mwaka 222-235/246 BK) anukuu robo ya 2 Pet 2:22, "lakini baada ya muda mfupi, kjigaagaza tena matope yale yale" (The Refutation of All Heresies kitabu cha 9 sura ya 1, uk.125).

Hippolytus (225-235/246 B.K.) asemea juu ya 2 Petro 1:18,19 Kanusho la Mafundisho Yote Potofu kitabu cha 10 sura ya 24 uk.151

Hippolytus (222-235/246 B.K.) asemea 2 Peter 1:21. Andiko juu ya Kristo na Mpinga Kristo sura ya 2 uk.204

Hippolytus (mwaka 225-235/246 BK) anadokeza 2 Pet 1:18, 19 (The Refutation of All Heresies kitabu cha 10 sura ya 24, uk.151).

X Origen (mwaka 225-254 BK) anasema kuwa Petro aliacha "waraka mmoja ambao uhalali wake unakubaliwa. Fikiria kuwa tunaafiki kwamba aliacha waraka wa pili; kuna mashaka kuhusu jambo hili" (Origen's Commentary on John kutoka kitabu cha Tano sura ya 3, uk.346).

Origen (mwaka 225-254 BK) anasema "Bwana wetu Yesu Kristo, ambaye ni ‘nuru ya kweli' na "azukaye mioyoni mwetu.'" Azukaye mioyoni mwetu ni dokezo la 2 Pet 1:19.

Cyprian wa Carthage (karibu mwaka 246-258 BK) anautaja "Waraka wa Petro: na anukuu 2 Pet 2:11, 12 kwenye Treatises of Cyprian makala ya 12- kitabu cha tatu Testimonies sura ya 11, uk.536.

Firmilian (mwaka 256 BK) anaongelea onyo la Petro dhidi ya walimu wa uongo, ambayo ni dokezo la 2 Petro.

Adamantius (mwaka 300 BK) anukuu 2 Pet 3:15b kama kazi ya Petro. "kisha kwa mkono wa Mtume Petro alipoandika, ‘kufuatana na hekima, aliyopewa ndugu yangu Paulo.'"

Adamantius (karibu mwaka 300 BK) anukuu 2 Pet 2:19b kwa mamlaka ya Maandiko. Anasema kuwa ananukuu kifungu cha maandiko anaposema, ‘kila mtu ni mtumwa wa yule aliyemshinda.'"

Methodius wa Olympus na Patara (karibu mwaka 260-312 BK) anukuu 2 Pet 3:8 kama kazi ya Petro kwenye On the Resurrection.

Lactantius (karibu mwaka 303 hadi karibu mwaka 325 BK) anadokeza 2 Pet 2:22, "Wakirenaiki (watu wanaofuata filosofia ya Kihedoni yenye kusistiza starehe kuwa ni kitu kizuri zaidi na kwamba maadili yanapaswa kufanywa kuwa sawa na kuona raha) wanasema kuwa uadilifu unapaswa kusifiwa kwa msingi huu, kwa sababu unaleta raha. Kweli, yasema mbwa mchafu au nguruwe mwenye kugaagaa kwenye matopeni" (The Divine Institutes kitabu cha 3 sura ya 8, uk.75).

Lactantius (karibu mwaka 303 hadi karibu mwaka 325 BK) anadokeza 2 Petro 2:22 "wamejiingiza wenyewe kwenye tamaa zenye kuchukiza, kama nguruwe jike mwenye kugaagaa kwenye matope; kwa kuwa hujipaka matope wanaoabudu miungu, yaani, wanaoabudu matope na udongo" (The Divine Institutes kitabu cha 4 sura ya 17, uk.119).

Lactantius (karibu mwaka 303 hadi karibu mwaka 325 BK) anadokeza 2 Pet 2:11 ambayo pia ni Zab 90:4 (The Divine Institutes kitabu cha 7 sura ya 14, uk.211).

Watu wengi wameiongelea siku ya Bwana kuwa miaka elfu.

Baada ya Nikea

Baraza Nikea (mwaka 325 BK) linadokeza 2 Pet 2:22 (mbwa na nguruwe) kwenye canon 12, uk.27.

? Kitabu cha Eusebius kiitwacho Ecclesiastical History (mwaka 323-326 BK) kitabu cha 3 sura ya 3, uk.133-135 kinaelezea vitabu vya Agano Jipya. Anasema 1 Petro ni ya kweli. Anasema nyaraka 14 za Paulo zinajulikana sana, ingawa kanisa la Roma lilitia shaka kuwa Paulo aliandika Kitabu cha Waebrania. Anasema kuwa 2 Petro ina mashaka. Kitabu kilichoitwa Matendo ya Paulo, [Shepherd of] Hermas, Matendo ya Petro, na Injili ya Petro na Kuhubiri kwa Petro na Ufunuo si halali (Nicene and Post-Nicene Fathers Second Series juzuu ya 1, uk.1233-145).

Firmicus (karne ya 4) anaongelea 2 Pet 2:11

Athanasius (mwaka 367 BK) haongelei aya yeyote maalumu ya 2 Petro, lakini anaorodhesha vitabu vya Agano Jipya kwenye Festal Letter 39, uk.552.

Synopsis Scripturae Sacrae (mwaka 350-370 BK au karne ya 5) inavitaja vitabu viwili vya Petro kama sehemu ya Agano Jipya. Inanukuru 2 Petro 1:1 yote. Hilary wa Poitiers (mwaka 355-367/368 BK) "Na tena, japokuwa anajua kuwa mshiriki wa asili ya kimungu, kama mtume mtakatifu Petro anavyosema kwenye waraka wake wa pili, hapaswi kupima asili ya kimungu kwa ukomo wake mwenyewe . . ." (On the Trinity kitabu cha 1 sura ya18, uk.45).

Ephraem Mshamu (mwaka 373 BK)

Cyril wa Yerusalemu (karibu mwaka 349-386 BK) anadokeza 2 Pet 1:19 kwenye Lecture 10.15, uk.61.

Ambrose wa Milani (mwaka 370-390 BK) anadokeza 2 Pet 1:21, "hivyo Roho Mtakatifu naye ni mmoja anayewatia nguvu manabii"

Baraza la Tatu la Carthage (mwaka 397 BK)

Lucifer wa Cagliari mwenye kuleta utengano (mwaka 370/371 BK)

Didymus Kipofu (mwaka 398 BK)

Julius Firmicus Maternus (karne ya 4) The Error of Pagan Religions

Jerome (mwaka 404 BK) anaongelea 2 Pet 1:4; 2:13; 3:10

Jerome anasema, "Mitume Yakobo, Petro, Yohana na Yuda walichapisha nyaraka saba ambazo kwa pamoja ni za kiroho, na fasaha, fupi na ndefu, fupi kwa maneno lakini ndefu kwa umuhimu na matokeo yake ni kuwa kuna watu wachache ambao wanapokuwa wanazisoma hawajikuti wamepotea" (Letter 53 [To Paulinus] juzuu ya 6, uk.102).

Hata hivyo, Jerome aliona kuwa mtindo wa 1 Petro na 2 Petro ni tofauti. Alisema ilikuwa ni kwa sababu Silwano aliandika 1 Petro kama mwandishi.

Augustine wa Hippo (mwaka 416-430 BK) anaitaja 2 Pet 1:4 kama kazi ya Mtume Petro kwenye On the Proceedings of Pelagius juzuu ya 5 sura ya 42, uk.202. Pia anaiongelea 2 Pet 1:2, 17, 21; 2:4, 15, 20; 3:9, 11, 18.

John Cassian (mwaka 419-430 BK) anadokeza 2 Pet 2:19 kwenye Institutes of John Cassian kitabu cha 5.8, uk.238.

Cyril wa Alexandria (mwaka 444 BK) anaongelea 2 Pet 2:4; 3:11.

Speculum (karne ya tano) anaongelea 2 Pet 1:2 (3), 5; 2:11, 13; 3:9, 10, 11.

Quodvultdeus (karibu mwaka 453 BK) anaongelea 2 Pet 1:21; 2:4.

Varimadum (mwaka 445/480 BK) anaongelea 2 Pet 1:21.

Ushahidi wa vitabu vya uongo na vya waasi

Muasi Priscillian anaongelea 2 Pet 2:2

Pseudo-Hippolytus (baada ya mwaka 235/246 BK) inaongele 2 Pet 3:3 kama kazi ya Petro. Sehemu ya 10 uk.244.

Pseudo-Cyprian (baada ya mwaka 358 BK) inaongelea 2 Pet 2:13.

Pseudo-Methodius (baada ya mwaka 312 BK) ina nukuyu inayoweza kuwa nusu ya 1 Pet 2:6, Zab 118:22; au Isa 28:16. Oration Concerning Simeon and Anna sura ya 6, uk.387.

Muasi Pelagius (mwaka 416-418 BK) aanaongelea 2 Pet 2:20; 3:9, 10, 11.

Julian wa Eclanum (karibu mwaka 454 BK) anaongelea 2 Pet 3:11.

3. Hati za awali zaidi zenye maandiko ya kazi za kale ambao nakala zake za awali hazipo za 2 Petro tulizo nazo zinaonyesha kuwa kuna tofauti ndogo za maandishi lakini hakuna makosa makubwa ya kitheolojia.

p72 Bodmer 7 na 8 Papyrii 1 Pet 1:1-5:14, 2 Pet 1:1-3:18 na Yuda 1-25. Karibu mwaka 300 BK picha ya sehemu ya hati hii (yenye kuonyesha 2 Pet 1:16-2:2) imo kwenye The Complete Text of the Earliest New Testament Manuscripts, uk.468. Inasema maandishi haya yameandikwa "katika mfumo wa kuandika hati kwa mkono."

p74 (=Bodmer 17) Mdo 1:2-5, 7-11, 13-15, 18-19, 22-25; 2:2-4; 2:6-3:26; 4:2-6, 8-27; 4:29-27:25; 27:27-28:31; Yak 1:1-6, 8-19, 21-23, 25, 27; 2:1-3, 5-15; 18-22, 25-26; 3:1, 5-6, 10-12, 14, 17-18; 4:8, 11-14; 5:1-3, 7-9, 12-14, 19-20; 1 Pet 1:1-2, 7-8, 13, 19-20, 25; 2:6-7, 11-12, 18, 24; 3:4-5; 2 Pet 2:21; 3:4, 11, 16; 1 Yoh 1:1, 6; 2:1-2, 7, 13-14, 18-19, 25-26; 3:1-2, 8, 14, 19-20; 4:1, 6-7, 12, 16-17; 5:3-4, 9-10, 17; 2 Yoh 1, 6-7, 13; 3 Yoh 6, 12; Yud 3, 7, 12, 18, 24 (karne ya 7)

Karne ya 7 - 1968 - The Text of the New Testament lina Yak 2:4 na 1 Pet 1:12

Karne ya 7 - 1975 - Aland et al. toleo la tatu

Karne ya 6 - 1998 - Aland et al. toleo la nne lililorekebishwa

Vaticanus [B] (mwaka 325-350 BK), Sinaiticus [Si] (mwaka 340-350 BK), na Alexandrinus [A] (karibu mwaka 450 BK) ina 2 Petro yote. Clementine Vulgate karne ya 4 hadi ya 5 ina 2 Pet 1:1; 2:14.

Wordsworth-White Vulgate karne za 4 na 5 ina 2 Pet 1:1-2; 3:9.

Stuttgart Vulgate karne za 4 hadi ya 5 ina 2 Pet 1:1-2; 3:9.

048 karne ya 5

0209 (karne ya 7)

Italic (h) karne ya 5

Italic (j) karne ya 5

Italic (q) karne ya 6/7

Bohairic Coptic [Boh] karne ya 3/4

Sahidic Coptic [Sah] karne ya 3/4

Ephraemi Rescriptus [C] karne ya 5

Peshitta Syriac [SyrP] hati zaidi ya 350, za zamani zaidi zikiwa mwaka 411-435 BK (2 Pet 3:18 kwenye A Textual Commentary on the New Testament ya Bruce Metzger, uk.633).

Harclean Syriac [SyrH] karne ya 3/4 au mwaka 616 BK ina 2 Pet 1:3-5, 10, 17, 19, 21; 2:4, 6, 9-13, 15, 20; 3:9-11, 18.

Philoxenian Syriac [SyrPh] mwaka 507/508 BK ina 2 Pet 1:3, 10, 14, 17; 2:4, 6, 11-13, 15, 17, 20; 3:9-11, 18.

Palestinian Syriac [SyrPal] karne ya 6 ina 2 Pet 1:1-5, 10; 3:10-11, 18.

Armenian [Arm] kutoka karne ya 5

Georgian [Geo] kutoka ya 5

Gothic mwaka 493-555 BK

 

Angalia www.BibleQuery.org/2petMss.html kuangalia hati zaidi za awali za 2 Petro.