Maswali ya Biblia Waraka kwa Warumi


S: Kwenye Warumi, ni kwa nini Paulo aliandika waraka huu?

J: Kwa jula, Paulo alikutana na (au alianzisha) makanisa aliyokuwa anayaandikia lakini sivyo ilivyokuwa kwa kanisa la Roma. Hapana shaka kuwa Paulo aliwafahamu watu kadhaa, lakini hakuwa amewahi kufika Roma. Jambo la msingi ni kuwa Paulo aliandika Waraka kwa Warumi kwa sababu Mungu alitaka aandike. Lakini Paulo alikuwa mtume si tu kwa makanisa aliyoyaanzisha lakini mtume wa Kristo kwa waumini wote. Waraka kwa Warumi unachukuliwa kuwa ni kitabu chenye mantiki na mpangilio bora zaidi kilichoandikwa na mtunzi aliyekuwa anaandika kimantiki.
Paulo alitaka kuwaandikia kabla ya kuwatembelea, na kuweka wazi kinaganaga maana ya injili, kwa nini tunaihitaji, na na jinsi inavyofanya kazi. Pia alitaka kuelezea wokovu katika muktadha wa Wayahudi na watu wa mataifa mengine.

S: Kwenye Warumi, muhtasari wa waraku huu ukoje?

J: Ufuatao ndio muhtasari:
Rum 1:1-17 Ujumbe wa muhimu wa Paulo
Rum 1:18-3:20 Hukumu yetu

- Rum 1:18 Ghadhabu ya Mungu dhidi ya dhambi zetu zilizo za hatari, zenye kuongezeka, na kuleta mauti
- Rum 2-3:20 Watu wote Wayahudi na wasio Wayahudi hawana kitu cha kujitetea, na wanawajibika kwa hatia yao
Rum 3:21-5 Kuhesabiwa haki kwetu

- Rum 3:21-31 Kristo ndiye aliyetuhesabia haki, si matendo yetu
- Rum 4:1-25 Ibrahimu: alihesabiwa haki kwa imani
- Rum 5:1-21 Kifo cha Yesu kilitupa kuhesabiwa haki
Rum 6:18:39 Kutakaswa kwetu

- Rum 6:1-23 Tumehesabiwa wafu kwa ajili ya dhambi
- Rum 7:1-25 Jukumu letu lisilokwisha la kujitakasa
- Rum 8:1-39 Roho Mtakatifu: Nguvu ya kutuwezesha kuishi maisha matakatifu
Rum 9:1–11:36 Uchaguzi wa Mungu wenye mamlaka ya mwisho wa Waisraeli na watu wa mataifa mengine

- Rum 9:1-33 Uchaguzi wa Mungu wa muda mrefu wa Israeli
- Rum 10:1-21 Uchaguzi wa Mungu wa leo
- Rum 11:1-36 Uchaguzi wa Mungu wa siku zijazo wa Israeli watimizwa
Rum 12:1–16:27 Kuuishia wokovu

- Rum 12:1-1-21 Maisha ya kujitoa yenye kumtumikia Mungu na watu wengine
- Rum 13:1-14 Maisha ya unyenyekevu
- Rum 14:1-23 Kuwapenda waumini wengine
- - Bila kuwahukumu au kuwakwaza, bali kama ambavyo Kristo angefanya
- Rum 15:14–16:27 Mipango ya baadaye ya Paulo na shukrani zake kwa watu wengine

S: Kwenye Warumi, Paulo alikufa lini?

J: Inakubalika kwa jumla kuwa Paulo alikufa wakati wa utawala wa Nero, unaoweza kuwa kipindi cha mateso cha mwaka 67 BK. Kwa hiyo aliandika vitu vyote kwenye kipindi cha miaka karibu 34 baada ya kufa kwa Yesu.
Hatuujui umri halisi wa Paulo, lakini kwenye Mdo 7:58 Sauli wa Tarso alikuwa kijana, na kwenye Filemoni 9 Paulo alikuwa mzee.

S: Kwenye Rum 1:4, kwa kuwa Yesu alidhihirishwa kuwa Mwana wa Mungu, je alikuwa Mwana wa Mungu kabla ya hapo?

J: Ndiyo. Mtu anaweza kuwa kitu fulani kabla ya kudhihirishwa kwa ulimwengu. Hakuna muda wowote kabla ya Yesu kuwa Mwana wa Mungu, lakini Mungu azaliwe duniani ndipo adhihirishwe namna hii kwa wanadamu.

S: Kwenye Rum 1:7 na 1 Kor 1:3, kwa kuwa neno la Kigiriki kai linaweza kumaanisha "hata" pia "moja", je jambo hili linamaanisha Yesu ni Mungu Baba, kama Wasabelia na baadhi (si wote) ya Wapentekosti wa nafsi moja wanavyofundisha?

J: Hapana. Hebu na tuliangalie jambo hili kwa uhalisia wake.
1.
Watu wote wanakubali kuwa "na" ni maana ya msingi ya neno la Kigiriki kai, lakini mara nyingine linamaanisha "hata."
2.
Huwezi kuuthibitisha Upentekosti wa nafsi moja, Utatu Mtakatifu, au mafundisho yoyote kwa kutumia neno ambalo linaweza kuwa na maana yoyote kati ya mbili.
3.
Kwenye sura hii ya Warumi, Yesu anatofautishwa na Mungu Baba kwenye Rum 1:9. Yesu si yatima, wala mtoto asiyekuwa na Baba.
4.
Yesu pia anatofautishwa na Baba kwenye sehemu mbalimbali za Biblia ikiwemo Efe 1:3, 17; Mat 3:16-17; 12:18; Mak 10:38-40; Luk 3:21-22; Yoh 1:1, 33; 6:38; 14:16, 26, 28, 31; 5:26; 6:28; 7:5; Mdo 5:31-32; 1 Kor 11:3; 15:25-28; Ebr 1:9; 5:7-8. Wakati wa kubatizwa kwa Yesu, Yesu hakuwa anatoa sauti kama ya mtu mwingine.
Haielekei kuwa Usabelia ulikuwa na wafuasi wengi, isipokuwa kwa kipindi kifupi huko Roma. Yafuatayo ni baadhi ya mambo ambayo Wakristo waliokuwepo kabla ya baraza la kanisa la Nikea walifundisha kuwa Baba na Mwana ni nafsi tofauti, ingawa hawakusema kuwa hawako pamoja.
Athenagoras
(mwaka 177 BK) alisema kuwa Baba, Mwana na Roho Mtakatifu wana utofauti katika umoja wao (A Plea for Christians sura ya 12, uk.134).
Athenagoras (mwaka 177 BK) "Roho Mtakatifu mwenyewe pia, anayetenda ndani ya manabii, tunamchukulia kuwa kijito cha Mungu chenye kutiririka kutoka kwake, na kumrudia tena kama mwanga wa jua. Ambaye tena, haitashangaza kusikia watu wanaomwongelea Mungu Baba, na Mungu Mwana, na Roho Mtakatifu, na wanaotaja nguvu za wawili hawa kwenye umoja na utofauti wao kwa mfuatano, wanaitwa wakana Mungu? Pia mafundisho yetu yanayohusiana na uungu hayaishii kwenye mambo haya tu; bali tunatambua pia umati wa malaika na watumishi . . . ." (A Plea for Christians sura ya 10, uk.133).
Theophilus
(mwaka 168-181/188 BK) [kwa sehemu] "Kisha Mungu, akiwa na Neno lake ndani yake mwenyewe, alimtoa pamoja na hekima yake mwenyewe kabla ya vitu vyote kuweko. Neno alikuwa ndiye msaidizi wake kwenye vitu vyote vilivyoumbwa naye" (Theophilus to Autolycus kitabu cha 2 sura ya 10, uk.98).
Irenaeus
(mwaka 182-188 BK) alisema, "Neno, yaani Mwana, alikuwa na Baba wakati wote; na kwamba Hekima pia, ambaye ni Roho, alikuwa naye, kabla ya viumbe vyote." Kisha anaendelea kunukuu Mit 3:19, 20 na kuendelea, akonyesha kuwa Roho Mtakatifu ni nafsi ya tatu (Irenaeus Against Heresies kitabu cha 4 sura ya 20.3, uk.488).
Tertullian
(karibu mwaka 213 BK) "Na kama, kwa kunukuu kifungu kingine, "Asema Bwana kwa Bwana wangu Kristo", Bwana anayeongea na Baba wa Kristo atakuwa ni nafsi tofauti. Isitoshe, wakati mtume anaomba kwenye nyaraka zake, "Kuwa Mungu wa Bwana wetu Yesu Kristo awape nyinyi roho ya hekima, na ufahamu", atakuwa mbali (tofauti) na Kristo, ndiye Mungu wa Yesu Kristo, mwenye kutoa karama za Roho. Na tokea sasa, tusingukezunguke kwenye kila kifungu, Yeye "aliyemfufua Kristo kutoka kwa wafu, na ataifufua miili yetu isiyokuwa ya milele", ni lazima awe mwenye kuhuisha, aliye tofauti na Baba, au hata atokaye kwa Baba aliyehuishwa, kama Kristo aliyekufa ni Baba" (Against Praxeas sura ya 28, uk.625).
Hippolytus
(mwaka 222-235/6 BK) aliandika kazi nzima akipingana na Noetus ambaye "alidai kuwa Kristo alikuwa ndio Baba mwenyewe, na kwamba Baba mwenyewe alizaliwa, kusulubiwa, na kufa" (Against the Heresy of One Noetus sura ya 1, uk.223).
Hippolytus (mwaka 222-235/236 BK) "Yeye [Yesu] hakusema, ‘Mimi na Baba tu nafsi moja, bali kuwa tu wamoja.' Kwa kuwa kitenzi tu hakiongelei nafso moja, bali nafsi mbili, na nguvu moja", na ananukuu 1 Kor 15:23-28 (Against the Heresy of One Noetus sura ya 7, uk.226).
Origen
(mwaka 225-254 BK) "Sasa kuna watu wengi wanaichukulia dini kwa uzito, na wanaoanguka hapa katika mkanganyiko mkubwa. Wanahofia kuwa wanaweza kuwa wanatangaza miungu miwili, na hofu yao inawapeleka kwenye mafundisho maovu na ya uongo. Ama wanakana kuwa Mwana ana asili yake mwenyewe mbali na ile ya Baba, na inamfanya yeye anayeitwa Mwana wa Mungu awe ni jina tu, au wanaukana uungu wa Mwana, wakimchukulia kuwa na maisha yake tofauti, na kuyafanya wigo wa asili yake kuwa tofauti na ule wa Baba, hivyo walikuwa tofauti" (Commentary on John kitabu cha 2 sura ya 2, uk.323).
Novatian
(mwaka 250/4-256/7 BK) (imeonyeshwa bila kutaja) aliongea kuhusu uasi wa Sabellius kuwa ni kufuru kwa kuamini kuwa Kristo si Mwana, lakini Baba (Treatise on the Trinity sura ya 12, uk.621-622).
Dionysius wa Alexandria
(mwaka 246-265 BK) "Mmea unaochipuka kutoka kwenye mzizi ni kitu tofauti na ule ambao kutoka kwake umemea; lakini una asili moja nao. Na mto unaotiririka kutoka kwenye chemchemi ni tofauti na chemchemi. Kwa kuwa hatuwezi ama tukauita mto chemchemi, au chemchemi mto. Hata hivyo tunaruhusu kuwa vyote ni umoja kwa mujibu wa asili, pia katika mambo yote ya msingi; na tunakubali kuwa chemchemi inaweza kuchukuliwa kuwa kama baba, na kwamba mto ni ndio uliotokana na chemchemi" (On the One Substance, uk.120).
Lucian wa Antioch
(karibu mwaka 300-311 BK) "??? la Baba aliye Baba kweli, na la Mwana aliye Mwana kweli, na la Roho Mtakatifu aliye Roho Mtakatifu kweli; majina haya hayajatolewa kiholela au kiuzembe, bali yanaonyesha kwa usahihi nafsi maalumu, mpangilio, na utukufu wa hawa waliotajwa ili kwamba katika nafsi wako watatu, lakini katika ulinganifu wao ni mmoja" (Creed of Lucian of Antioch kwenye The Creeds of Christendom iliyoandikwa na Philip Schaff juzuu ya 2, uk.27.
Methodius
(karibu mwaka 260-312 BK) "Kwa kuwa ufalme wa Baba, wa Mwana, na wa Roho Mtakatifu ni mmoja, kama kiini cha asili yao na utawala wao ni kimoja. Kwa ajili hiyo pia, tunamtukuza na kumwabudu Mungu mmoja aliye na nafsi tatu, aliyepo pasipokuwa na mwanzo, hakuumbwa, hana mwisho, na hana mtu atakayekuja kumbadili. Kwani Baba hataacha kuwa Baba, wala Mwana kuwa Mwana na Mfalme, wala Roho Mtakatifu kuwa na asili na nafsi alivyonavyo. Kwani hakuna kitu chochote katika Utatu Mtakatifu ambacho kitapungua, ama katika umilele wake, ama ushirika, ama enzi. Kwani Mwana haitwi Mungu kwa sababu hiyo, kwa kuwa alifanywa mtu kwa ajili yetu" (Oration on Psalms sura ya 5, uk.397; pia The Banquet of the Ten Virgins hotuba ya 8 sura ya 10, uk.338 na sura ya 11, uk.339).

S: Kwenye Rum 1:8, ni kwa namna gani imani ya Wakristo waliokuwa Roma ilifahamika ulimwenguni mwote?

J: Maneno haya yana maana ileile kama 1 Thes 1:8. Tokana na ukubwa na umuhimu wa jiji la Roma, kusema kuwa kanisa la Roma lilikuwa ndio kielelezo kikuu cha ukristo kwa watu wengi hakuwezi kuwa kutia chumvi.

S: Kwenye Rum 1:11 na Rum 15:29, je Paulo hakuwa amejiinua kiasi alipowaambia Wakristo wa Roma kuwa anataka kwenda kuwapa karama ya rohoni?

J: Kama Paulo angekuwa mtu wa kawaida, huenda ingekuwa hivyo. Lakini kwa kuwa Paulo alikuwa mtume wa Kristo, alikuwa muwazi na mkweli bila kusema maneno kupita kiasi. Ni sahihi kumweleza mtu kuwa unaweza kunufaika naye, kama ni kweli.

S: Kwenye Rum 1:18, watu wanawezaje kuishika kweli pasipokuwa na haki?

J: Ni jambo rahisi sana watu kukubaliana walau kwa sehemu ukweli kuhusu jambo la haki na lenye manufaa kwa watu wengine, na kutokuyafanya wao wenyewe.

S: Kwenye Rum 1:18, watu wanaipingaje kweli?

J: Kuna njia nyingi, lakini iko moja iliyo wazi kabisa. Waroma walikuwa na taasisi nyingi za kidini za kipagani ambazo waliamini kuwa walikuwa nazo kwa sababu mbalimbali za kidini na kimiujiza. Nying zake zilikuwa zimeanzishwa na mfalme wa Waroma Numa Pompilius. Mwana historia wa Kiroma Varro aliandika kuwa mkulima wa Kiroma Terentius, akiwa analima karibu na kaburi la Pompilius, alivumbua vitabu vya Pompilius, ambavyo vilikuwa vimeandikwa sababu ya taasisi za kidini. Alivipeleka kwenye bunge, ambalo baada ya kuiona sababu halisi ya taasisi hizo, lilimwamuru hakimu avichome vitabu hivyo. Unaweza kusoma kuhusu jambo hili kwenye kazi ya Augustine wa Hippo iitwayo City of God (mwaka 413-426 BK) kitabu cha 7 sura ya 34, uk.141-141. Wakati watu walikuwa wakichoma nakala za awali za vitabu vya dini zao wenyewe ambavyo walidai kuviamini, unaweza kushangazwa na udhati wao katika kushika kweli.

S: Kwenye Rum 1:19-20, inawezekanaje watu wote wakamjua Mungu kupitia uumbaji?

J: Kuna mambo matano ya kuzingatia katika kujibu swali hili.
1.
Tunaweza kujua vitu vingi kuhusu Mungu kupitia vitu alivyoviumba. Kwa mfano, hakuna kiumbe kilichojiumba chenyewe. Kuna Muumbaji, ambaye ni mkubwa kuliko vitu vilivyoumbwa. Tunaweza pia kuona ukuu wa enzi, nguvu, na uzuri wa Mungu kwenye viumbe, ingawa viumbe vimeanguka dhambini.
2.
Watu wanaweza kutafsiri maneno kwa njia nyingi za ajabu ajabu. Kwa mfano, nadharia tete yenye kudai kuwa viumbe hai vinatokana na vitu visivyokuwa na uhai, nadharia ambayo ilichukuliwa kuwa ni "ukweli wa kisayansi" wakati wa miaka ya kati ya historia ya Ulaya, ilisema kuwa nzi wanaweza kutokana na nyama inayooza, na kuwa maisha yanaweza kutokea mara moja kutoka kwenye vitu visivyo na uhai.
3.
Vitu vingi muhimu kuhusu Mungu hatuwezi kuvifahamu kupitia uumbaji, kama vile Utatu Mtakatifu, Yesu kufa msalabani, na kurudi tena kwa Yesu.
4.
Ingawa viumbe haviwezi kutufundisha kikamilifu kuhusu injili ya wokovu, vinaweza kuwafundisha watu kuwa Mungu yuko na kuwaelekeza wamtafute.
5.
Ikiwa mtu ataukataa ukweli anaoufahamu kuhusu Mungu Mwenyezi, Mungu halazimiki kumpa mtu huyu ukweli zaidi.

S: Kwenye Rum 1:19-20, je watu wote wasiokuwa Wakristo watakwenda jehanamu?

J: Kuna jibu moja tu sahihi, lakini lina vitu viwili: hapana na ndiyo.
Hapana, kwa sababu nne
H1.
Hapana, kwa sababu baadhi ya watu ambao bado hawajawa Wakristo watakuja kuwa Wakristo baadaye na kwenda mbinguni. Msemo wa kibiblia wa watu ambao hatimaye watakwenda mbinguni ni "wateule."
H2.
Hapana, kwa sababu kwenye Agano la Kale, Wayahudi wengi wacha Mungu, walioitii sheria, walikufa wakitarajia kuja kwa Masiha, bila kumjua Masiha (Efe 3:4-6; 1 Pet 1:10-11; 2 Pet 1:19; huenda pia Ebr 11:39-40). Walikufa kabla ya Kristo kuja, lakini wako mbinguni.
H3
. Hapana, kwa sababu Mungu alijidhihirisha kupitia kwa Ibrahimu, ingawa hakuijua sheria. Mungu anaweza kutenda "nje ya sanduku" la mambo tuliyowaza kabla, na kuwaleta watu kwake kama anavyopenda kupitia kwa Kristo. Tunaweza kuwa na uhakika kuwa watu wote waliokufa bila ya kusikia injili ya Kristo leo hii, ikiwa ni watoto wadogo, wenye ulemavu wa akili, au watu waliopungukiwa ufahamu kwa kiasi kikubwa sana, watahukumiwa na Mungu mwenye rehema kwa haki. Tazama Rum 4:15; 5:12; huenda pia Yoh 9:41.
H4.
Kuna Wakristo wanaofikiri kuwa Kristo aliwahubiria watu waliokuwa wamekwisha kufa kulingana na 1 Pet 3:19-20 na 4:6. Clement wa Alexandria kwenye Stromata (mwaka 193-202 BK) kitabu cha 6 sura ya 6, uk.490, watu waliokuwa wenye haki kwa mujibu wa sheria ya Mungu, walitakiwa kuwa na imani tu. Kwa sababu watu waliokuwa hawana sheria, lakini walikuwa wenye haki kwa mujibu wa falsafa yao, walihitaji imani na toba dhidi ya ibada ya sanamu. "Moja kwa moja, kwenye ufunuo wa kweli, pia walitubu mwenendo wao wa zamani [wa kuabudu sanamu]." Tazama pia Stromata kitabu cha 6 sura ya 6, uk.492. Irenaeus (Irenaeus Against Heresies kitabu cha 4 sura ya 27.1, uk.499), Hippolytus (Fragment from Commentary on Psalm 19 or 20, uk.170. Pia sura ya 7.14, uk.189), na Origen (Origen Against Celsus kitabu cha 2 sura ya 43, uk.448) pia alifundusha kuwa Kristo alihubiri kwa watu waliokuwa wamekufa ili awaokoe baadhi yao.
Hata hivyo, Wakristo wengine hawakubaliani na maoni haya.
Ndiyo, kwa sababu nne
N1.
Watu wote waliookolewa, wanaookolewa, na watakaookolewa, wanaokolewa kupitia kwa Mpatanishi na Mwokozi mmoja tu, Yesu Kristo (Mdo 4:12; Yoh 10:7-8; 10:26-28).
N2.
Watu wote wanamhitaji Yesu. Yesu aliwaambia hata Mafarisayo waliokuwa Wayahudi washika dini, kuwa kama hawatamwamini watakufa katika dhambi zao (Yoh 8:24). Yesu aliwaonya kuwa kumkataa kwao Mungu kutawapeleka jehanamu (Mat 23:33-36).
N3.
Hata watoto wachanga waliokufa kabla ya kufanya dhambi yoyote huku wakijua bado wanamhitaji Yesu kuwatakasa na kuwasafisha asili yao ya dhambi. Ingawa hawajafanya dhambi yoyote kwa kuchagua wao wenyewe, na hawakuwa na nia ya kufanya jambo loloteovu, bado wana asili ya dhambi yenye ubinafsi na wanahitaji kubadilishwa kupitia kwa Yesu ndipo waende mbinguni.
N4.
Kwa kuwa Yesu alimwokoa mtu yoyote aliyetaka kuokolewa, basi kila mtu anayekwenda mbinguni, sasa au baadaye, atamwamini Kristo (Rum 14:10-11; Fil 2:9-11; Yoh 6:37,45).
Kwenye maelezo N3, kuna Mkristo mmoja aliyewahi kutokukubalina nami juu ya wazo hili, na alisema kuwa kama (watoto wachanga) hawawezi kufanya uamuzi wa kumwamini Yesu, hawawezi kwenda mbinguni. Hata hivyo, tunapaswa kuangalia jambo la msingi kabisa, ni "kitu gani" kinachotuokoa? Hatima ya yote kitu chenye kutupa wokovu si uamuzi wetu, kwa kuwa siyo "sisi" tunaojiokoa. Kimsingi, Mungu ndiye anayetuokoa. Anaokoa watu wote waliookolewa kupitia Yesu, lakini hatujui jinsi atakavyowaokoa watoto wachanga kupitia kwa Yesu. Kitu tunachokijua ni kuwa yeye ni Mungu! 

S: Kwenye Rum 1:20, ni kwa kiasi gani watu wanaweza kujifunza kweli ya Mungu na injili kwa kuuangalia uumbaji?

J: Tunaweza kujifunza mambo matatu, lakini hatuwezi kujifunza jambo la nne.
1.
Uwepo wa Muunbaji wa aina fulani (nafsi iliyo hai vinginevyo) kutokana na uwepo wa viumbe.
2.
Sifa za Mungu zisizoonekana, nguvu zake za milele na asili yake ya kiungu (Rum 1:20).
3.
Ufahamu kwa kiasi fulani wa sheria za Mungu za mwenendo (Rum 2:14-16).
Kutoka kwenye viumbe, watu hawawezi kujifunza kuhusu siri ya Kristo (Efe 3:4-6, 9; 6:19; Kol 1:26-27; 2:2; 4:3; Rum 16:25-26; 1 Pet 1:10-12). Tazama pia swali linalofuata kwa maelezo zaidi.

S: Kwenye Rum 1:20, je inawezekana kuamini kwa kujifunza kutoka kwenye uumbaji tu?

J: Kwa uhalisia wa mambo, haiwezekani. Bila ya Mungu, hakuna mtu anayemtafuta, kama Rum 3:9-20 inavyosema.
Kinadharia,
swali hili limejengwa kwenye msingi usiokuwa sahihi. Swali hili linadhania kuwa Mungu hafanyi kitu chochote, na kama mtu anamtafuta, Mungu atakaa tu bila kukusudia kumleta kwenye kweli. Kwa ukweli, Mungu anataka watu waiamini kweli kuliko watu wenyewe wanavyotaka kuiamini kweli.

S: Kwenye Rum 1:24, 26, 28, kwa kuwa Mungu hapendi uovu, kwa nini basi anataka kuwaachilia watu uovu zaidi?

J: Mungu hapendi uovu, lakini kama mtu anapenda kwa mwovu, humwachilia aende kwenye uelekeo anaopenda kuufuata. Warumi 1 inaonyesha kuwa moja ya matokeo ya dhambi ni haja ya dhambi mbaya zaidi. Ama una haja ya kufanya dhambi zaidi, ama una njaa na kiu ya haki kama Yesu alivyoamuru kwenye Mat 5:6. Ikumbukwe kuwa Wakristo hawatakiwi kuacha kuwa na njaa na kiu ya haki zaidi.

S: Je Rum 1:26-27 inamaanisha tu kuwa hairuhusiwi kubadilika na kutaka uhusiano wa kimwili na mtu wa jinsia moja na wewe, lakini kama umezaliwa na haja hiyo ni sawa kutimiza haja hiyo?

J: Hapana. Rum 1:26-27 inasema kuwa watu wote wanaume na wanawake wanafanya dhanbi kubwa sana wanapobadilisha mahusiano yao ya asili na kuhusiana kimwili na watu wa jinsia moja na wao. Kuna watu wanaodai kuwa "kubadilisha" tu ndiko kuliko dhambi, na ni sawa kuhusiana kimwili na watu wa jinsia moja na wewe kama umezaliwa na haja hiyo. Lakini jambo hili haliwezi kuwa hivyo. Si tu kuwa aya hii inakazia mahusiano yenyewe kuwa ya "aibu", neno "kubadili", metallaso, ni neno hilohilo la Kigiriki lililotumika kuelezea kubadili kweli ya Mungu kuwa uongo. Kwa hiyo shida si "kubadili" tu bali kutenda mambo "yasiyopasa" na wanaume wengine kama Rum 1:27 inavyosema. Kwa kuwa Law 18:22, 24; 20:13 na 1 Kor 6:9-10 zinasema kuwa mahusiano kimwili ya watu wa jinsia moja ni dhambi, ni dhahiri kuwa si vema kuwa kwenye hali ya dhambi. Jambo hili ni kweli bila kujali mtenda uovu ni mtu mwenye mahusiano kimwili ya jinsia moja au jinsia tofauti. Kitu cha muhimu kuzingatia ni kuwa sisi sote tumezaliwa na asli ya dhambi na kuwa tunapaswa kuzaliwa upya ili tuwe watakatifu. Tazama pia maelezo kuhusu Law 18:22, 24; 20:13, na 1 Kor 6:9-10.
Tertullian kwenye de Corona sura ya 6, uk.96 anatafsiri Rum 1:26 kuwa wanaume na wanawake wanabadili matumizi ya asili na kufanya matumizi yasiyokuwa ya asili "kama adhabu inayostahili makosa yao."

S: Kwenye Rum 1:26-27, mwandishi mwenye kushuku Bart Ehrman anasema, "Katika kufikiria sehemu za Biblia zenye kuongelea mambo yanayohusu mandhari ya sasa, ni vema kuzingatia maoni kuwa wandishi wa Biblia waliishi kwenye ulimwengu ulio tofauti na wetu na waliwakilisha mawazo na imani za watu wa ulimwengu wao. Tukichukua mfano rahisi, ulimwengu wao haukuwa na dhana tuliyonayo sasa ya mahusiano ya kimwili ya watu wa jinsia moja. Kwa kuelezea kwa njia tofauti, mahusiano ya kimwili ya watu wa jinsia moja hayakuwepo katika ulimwengu ule. Kwa nini? Si kwa sababu wanaume hawakuwa wanalala na wanaume wenzao (walifanya hivyo) au wanawake na wanawake wenzao (walifanya hivyo), lakini ni kwa sababu hapakuwa na fikra za mwelekeo wa kijinsia katika ulimwengu ule, au ulimwengu wowote hadi dhana ua mwelekeo wa kijinsia ilipotokea miongoni mwa watu wenye akili sana wa magharibi kwenye karne za kumi na tisa na ishirini" (Jesus, Interrupted, uk.280).
Ehrman anatumia mifano miwili iliyotangulia kuelezea kwa jumla. "Pia hivyo, kuhusiana na mafundisho mengine ya Biblia – kuhusu wanawake, kuhusu mahusiano ya kimwili ya watu wa jinsia moja, kuhusu zinaa, kuhusu adhabu ya kifo, kuhusu vita, kuhusu mali, kuhusu utumwa, kuhusu magonjwa, kuhusu . . . kila kitu" (Jesus, Interrupted, uk.281).

J: Ajabu! Inaonekana kuwa Ehrman hajasoma Agano la Kale kwa muda mrefu sana, hasa Law 21:22, 29. Kwa hakika hafikirii kuwa Mambo ya Walawi 21 "iliandikwa na watu wenye akili sana wa magharibi kwenye karne za kumi na tisa na ishirini"!
Mambo yoyote ambayo wapagani walifanya karne nyingi baadaye hayabadilishi dhana ya uhusiano wa kimwili wa watu wa jinsia moja kuwa ni uovu kwa Wayahudi (kama vile Sauli wa tarso au hata Yesu), kwa sababu walikuwa wanasoma Agano Jipya. Licha ya hayo, muda mrefu kabla ya kuwako watu wenye akili sana, waandishi wa kikristo wasiopungua 11 waliandika bayana dhidi ya mahusiano ya kimwili ya watu wa jinsia moja kabla ya mwaka 325 BK. Unaweza kuona mambo haya waliyoandika kwenye tovuti hii www.BibleQuery.org/History/ChurchHistory/WhatEarlyChristiansTaught.html. Kwa maoni yangu, Ehrman "anashangaza" sana hapa.

S: Kwenye Rum 1:26-27, Mungu anawaachiliaje watu kwenye tamaa za mioyo yao?

J: Moja ya adhabu za dhambi ni kutaka kufanya dhambi. Matokeo ya dhambi ni kuwa ni mzunguko unaoashiria mkwamo. Unaweza kufikiri kuwa dhambi isiyotubiwa inafanana na lindi kuu la angani linalofyonza kila kitu kinachofika karibu yake. Ufu 22:11 na Dan 12:10 pia zinamaanisha kuwa wema na uovu utajizidisha.

S: Kwenye Rum 2:6-7, je matendo mema yanatakiwa ili kupata wokovu?

J: Hapana. Kuna mambo matatu ya kuzingatia katika kujibu swali hili.
1.
Watu wote wanakubaliana kuwa matendo mema yanahusiana na uzima wa milele; mambo haya mawili yanatakiwa kwenda pamoja.
2.
Jambo ambalo haliongelewi kwenye kifungu hiki ni dhana ya kafara ya Kristo kutokuwa kamilifu au kutokutosheleza. Jambo lingine lisiloongelewa ni dhana ya kuwa watu wanapata uzima wa milele kama malipo ya mambo mazuri waliyoyafanya.
3.
Kwa kuwa matendo mema si kigezo cha wokovu, na yanahusiana na wokovu, ni kwa jinsi gani basi mambo haya mawili yanahusiana? Matendo mema yanahusika kama matokeo ya wokovu, kama Efe 2:9-10 na Yako 2:18-26 zinavyoonyesha. Matendo mema ni ishara ya wokovu, kama ambavyo mapigo ya moyo yalivyo ishara kuwa mtu yupo hai.

S: Kwenye Rum 2:6, je hukumu itakuwa tofauti kwa watu tofauti?

J: Ndiyo, kwa namna nyingi.
Kwa watu wasioamini,
adhabu za baadhi ya watu zitakuwa kubwa zaidi kuliko za wengine, kama ambavyo Mat 10:15; 11:22-24 na Mak 12:40 zinavyoonyesha.
Kwa waumini,
kutakuwa na zawadi tofauti mbinguni, kama vile Mat 5:12; 10:42; 6:19-21; Luk 6:23; 1 Kor 3:12-15; na Ufu 22:12 zinzvyosema.
Kwa jumla,
Yesu kwenye Mat 5:7 anasema kuwa watu wenye rehema watapata rehema.

S: Kwenye Rum 2:7, je tunapata maisha yasiyokuwa na mwisho sasa, au baadaye?

J: Tutapata ukamilifu wa uzima wa milele baadaye, lakini tunapata ahadi yenye uhakika ya uzima huo sasa. Tazama ufafanuzi wa 1 Tim 6:16 kwa maelezo zaidi. Mkristo ana maisha yasiyokuwa na mwisho kuanzia wakati anapoamini.

S: Kwenye Rum 2:11, kwa kuwa Mungu hana upendeleo, kwa nini alitofautisha kati ya Wayahudi na watu wa mataifa mengine (Rum 3:1-2), hasa wa Moabu?

J: Kwanza kabisa tunapaswa kuofautisha kati ya haki ya milele na hali za kidunia na laana. Biblia inatufundihsa kuwa Mungu hapendelei mtu mmoja dhidi ya mwingine kwa namna nyingi (kama vile wokovu), lakini Mungu hupendelea baadhi ya watu na mataifa yao kwa namna nyingine. Kumbuka kuwa mifano ya pande zote mbili za jambo hili kwenye vitabu hivyo hivyo vya Biblia, hivyo ukinzani huu haukuwa "kosa" la bahati mbaya la waandishi mbalimbali, bali jambo ambalo Paulo alilikusudia kabisa.
Mungu hapendelei watu kwenye hukumu na kwa wale wanaomtafuta au kumkataa:

Kwa sababu Mungu hapendelei watu (au Mungu haonyeshi upendeleo) kwenye Rum 2:11 na Mdo 10:34-35 (Petro alisema). Watu wote wana thamani sawa mbele ya Mungu (Gal 3:28). Mungu anawaokoa watu wote wanaomwita (Rum 10:11-12). Wokovu ni uleule kwa Wayahudi na watu wa mataifa mengine (Mdo17:26-27).
Mungu hupendelea baadhi ya watu:
Maandiko hayasemi mahali popote kuwa watu wote watazaliwa kwenye mazingira yanayofanana. Ukiangalia maisha utaona uthibitisho wa jambo hili. Haruni alipangiwa tangia awali kuwa kuhani, na matendo yake kwenye Mlima Sinai hayanaonyeshi sana kuwa alistahili kuliko watu wengine. Mtu yoyote mahali popote anayo nafasi ya kujua mambo yenye kutosha kuhusu Mungu kupitia uumbaji hata aweze kuhitaji kujua zaidi. Yesu aliahidi kwenye Mat 7:7-12 kuwa watu wanaoomba, tafuta, na kubisha watapata, na kufunguliwa mlango.
Kwa ufupi,

1. Kwenye maisha haya, kuna watu wenye mazingira mazuri kuliko wengine.
2. Mungu humhukumu kila mtu kwa haki, na anazingatia mambo yote yanayohusika.
3. Bila kujali mazingira ya mtu, hakuna aliye na sababu ya kujitetea kwa kutokuyafanyia kazi mambo ambayo alikwisha kuyajua.

S: Kwenye Rum 2:12, je watu wote ambao hawajaisikia sheria ya Agano la Kale au Kristo, watakwenda jehanamu bila kuwa na nafasi ya kuokolewa?

J: Hapana. Kuna uwezekano kuwa Ayubu hakuwa Myahudi, na Mungu alijifunua kwake. Vivyo hivyo Ibrahimu na watu wengine wote hadi Musa, ambao hawakuwa na sheria ya Agano la Kale. Hatima ya yote ni kwamba, siyo utiifu wa injili unaookoa, au hata injili yenyewe yenye kuokoa. Ni Mungu anayeokoa kupitia kwa Yesu, na anaweza kufanya jambo lolote kwa namna yoyote anayopenda.

S: Kwenye Rum 2:14, je watu wa mataifa mengine wanaruhusiwaje kuwa sheria kwa nafsi zao wenyewe?

J: Maneno haya hayamaanishi kuwa watu wanaweza kujifanyia sheria na kanuni za maadili kwa kadri wanavyopenda wao wenyewe kuzifuata. Pia maneno haya hayamaanishi:
1)
Watu wote wanaelewa kweli kwa kiasi fulani, kupitia uumbaji na dhamiri zaoa (Rum 1:19-20; 2:14-16).
2)
Watu wote wanapaswa kuifuata kweli wanayoijua (Rum 2:15).
3)
Watu wote wanaoifuata kweli wanajua kuwa watapungukiwa (Rum 3:23) na kuelewa jambo hili.
4)
Mungu ni mwenye haki; dhambi haihesabiwi mahali ambapo hakuna sheria (Rum 4:15; 5:13).
5)
Hata hivyo, kutokujua kwa aina fulani si hakumwondolei mtu hatia (Rum 1:21-22, 25).

S: Kwenye Rum 2:16, je Paulo alikuwa na "injili yake mwenyewe" aliyokuwa anaihubiri?

J: Kuna injili moja tu ya kweli (Gal 1:8), lakini pia ilikuwa ya Paulo, kama ilivyokuwa yetu.

S: Kwenye Rum 2:24, ni kwa jinsi gani jina la Mungu lilitukanwa kwa ajili ya Wayahudi?

J: Wayahudi walikuwa wateule wa Mungu, lakini kwa ajili ya kutokutii kwao, uovu na kumkataa Masiha hawakutenda kama watu wa Mungu. Matendo maovu ya watu walichukuliwa kuwa watu wa Mungu yalilichafua jina la Mungu machoni pa watu wengine.
Leo hii, Wakristo wote wanaofahamika na watu wengine ni mashahidi wa Mungu. Suala si tena kwamba wewe u shahidi au la, bali kwamba u shahidi mzuri au mbaya.

S: Kwenye Rum 2:24, kutukanwa kwa jina la Mungu kuna umuhimu gani? Kwa maneno mengine, ni nani anayeona na kusikia kutukanwa huku?

J: Rum 2:24 inasema kuwa watu wa mataifa mengine (wasiokuwa Wayahudi) wanawaona Wayahudi wakitukana. Jambo hili lina umuhimu kwa njia mbili:
1.
Linawazuia watu wasije kwa Mungu wanapoona watu wanaoitwa ‘watu wa Mungu' wakilifanya jina la Mungu litukanwe.
2.
Mungu alisema yeye ni Mungu mwenye wivu. Maana mojawapo ya maneno hayo ni kuwa hapendi jina lake na sifa yake ikashfiwe na ikose kuheshimiwa.

S: Kwenye Rum 3:4, je maneno haya, "Mungu aonekane kuwa amini na kila mtu mwongo" yanamaanisha nini?

J: Maneno haya hayaruhusu watu kusema uongo. Badala yake, yanamaanisha kuwa Mungu anaendelea kuwa amini hata kama watu wengine wote duniani hawatafikiri hivyo. Ni jambo lisilohitaji mjadala kuwa Mungu ni kweli. Efe 4:25 inatuagiza kuvua uongo na kusema kweli.

S: Kwenye Rum 3:5, ni kwa jinsi gani udhalimu wa watu unaithibitisha haki ya Mungu?

J: Haki na udhalimu si vitu vyenye ukubwa sawa ila muelekeo tofauti. Badala yake, udhalimu ni upungufu au uharibifu wa haki ya Mungu. Ushahidi wa jambo hili ni kuwa, hata kwenye udhalimu wao, mara nyingi watu hutambua kuwa ni wadhalimu, na hependelea haki – japo kwa watu wngine.

S: Kwenye Rum 3:7, je uongo wa watu humpa Mungu utukufu?

J: Uongo wa watu haumpu Mungu utukufu kwa njia ya moja kwa moja. Hata hivyo, Rum 3:7 inaelezea ukweli unaoshangaza kuwa licha ya uongo na udanganyifu wa watu, kwa ujumla watu bado wanamkiri Mungu na sheria yake ya mwenendo.

S: Kwenye Rum 3:8, kwa nini tufanya maovu ili memaa yaje? (Dhehebu la Kirusi lenye mafundisho yanayochukuliwa na Wakristo wengine kuwa mapotofu na mwasherati Grigori Rasputin walifundisha hivi).

J: Kama jambo hili lingekuwa kweli, basi shetani angekuwa ameleta mambo mengi mema kuliko mtu yoyote. Mara nyingi Mungu hutumia mambo mabaya kuleta mema. Lakini jambo hil halihalalishi watu kufanya maovu, au kuwaepusha watu walioishi kama Rasputin kupata malipo ya maovu yao kwenye ziwa la moto. Tazama ufafanuzi wa Rum 6:1,15 kwa maelezo zaidi.
Alipolizwa sababu ya kusema kuwa dhambi ni lazima mbele za Mungu, Rasputin alijibu kuwa "‘Hasa, baba uliye mdogo' alisema, ‘Mwokozi wetu na baba zetu watakatifu walikemea dhambi, kwa sababu ni kazi ya mwovu. Lakini unawezaje kuuondoa uovu, baba uliye mdogo, isipokuwa kwa toba ya kweli? Na unaweza kutubu kweli endapo hujafanya dhambi? . . . Ondoka na Maandiko yako!' alisema kwa sauti kubwa. ‘Maandiko! Hakika nakuonya, baba uliye mdogo, achana na jambo hili la ovyo na lisilokuwa na maana ili uweze kusimama mbele za Bwana. Yachukulie maisha kama yalivyo, kwani hicho ni kitu pekee ulichopewa na Mungu. Na ngoja nikuambie hivi. Usiwe unafikiria sana kuhusu chanzo cha dhambi, kuhusu sala ngapi mtu anatakiwa kufanya kwa siku, na ni kwa muda gani mtu anatakiwa kufunga ili kujiepusha na dhambi! Dhambi, kama bado imejificha kwako; ni kwa njia hii tu ndio utaweza kuishinda! Fanya dhambi, kisha utatubu na kuuondoa uovu. Kwa kadri unavyokuwa na dhambi kisiri ndani mwako, na kwa ajili ya uoga unaificha kwa kufunga, maombi, na mjadala usiokwisha wa Maandiko, kwa kadri unavyoendelea kuwa mnafiki na usiye na thamani, na mambo kama hayo ni chukizo kwa Mungu. Uchafu lazima uondolewe, unasikia ewe baba uliye mdogo? Ni hapo tu ndipo mwokozi wako atampendeza Bwana?'" (Rasputin : The Holy Devil, uk.54-55).
Angalia mantiki hii potofu:
1) Kwa kuwa dhambi ni mbaya, unapaswa kutubu.
2) Huwezi kutubu dhambi usiyoitenda.
3) Kwa hiyo, ili kushinda dhambi, unatakiwa kuitenda kwanza!
Watu wana maarifa sana hata wanaweza kutoa visingizio vya kuhalalisha kitu chochote kiovu, angalau katika mawazo yao wenyewe, wakifanya bidii sana.

S: Kwenye Rum 3:11; Zab 14:2-3; 53:3, kwa kuwa hakuna mtu anayemtafuta Mungu, Daudi aliwezaje kumtafuta kwenye Zab 27:8; 105:4; 31:1; 34:4; 28:1-2; 42:1-2; 120:1?

J: Rum 3:11 inanukuu Zab 14:2. Kuna mambo matano ya kuzingatia katika kujibu swali hili.
1.
Watu wengi, akiwemo Daudi, wanamtafuta Mungu kwa kweli.
2.
Hakuna mtu, akiwemo Daudi, anayemtafuta Mungu kwa uwezo wao wenyewe.
3.
Mungu alitupenda hata kabla hatujampenda yeye (1 Yoh 4:19), na Mungu alitutafuta kabla hatujamtafuta yeye. Hakuna mtu awezaye kuja kwa Yesu isipokuwa amevutwa na Baba (Yoh 6:44).
4.
Hata imani yetu, na kumtafuta kwetu Mungu, ni zawadi tunayopewa na Mungu.
5.
Jukumu kubwa la Roho Mtakatifu ni kuuhakikisha ulimwengu hatia itokanayo na dhambi, haki, na hukumu (Yoh 16:8-11). Hivyo, Mungu amemshuhudia kila mtu kwa kiasi fulani. Tunaweza kusema kuwa kila mtu amepewa zawadi ya uwezo wa kiasi fulani wa kumtafuta Mungu. Hata hivyo, kuna Wakristo kadhaa wa kweli wanaokataa wazo hili.
John Chrysostom (mwaka 392-407 BK) alisema hivi kwenye Commentary on Galatians sura ya 2 mstari wa 23, uk.23 alipokuwa anaongelea Zab 63:1: "Isitoshe, maneno haya yanatufundisha kuwa kila mtu anawiwa deni kubwa ka kumshukuru Kristo, kana kwamba alimjia yeye peke yake, kwani hakuruhusu ukuu wake umzuie kumfikia mtu yoyote, ili kwamba kipimo cha upendo wake kwa kila mtu kina ukubwa sawa na kipimo cha upendo wake kwa ulimwengu wote. Hakika kafara ilitolewa kwa watu wote, na ilitosha kuwaokoa wate, lakini wale wanaofurahia baraka ni waumini tu." John Chrysostom anasema kuwa karamu iliandaliwa kwa ajili ya watu wote kwenye Luk 14:16, lakini baada ya wageni kutokuja, watu wengine waliitwa.

S: Kwenye Rum 3:13-19, je vifungu hivi vya Agano la Kale vinaongelea baadhi ya watu ambao ni waovu, au watu wote kabisa?

J: Vinatuongelea sisi sote, kwa kiasi kimoja au kingine. Moja ya vifungu vilivyonukuliwa ni Zab 14:1-3 ambacho kinaeleza wazi kabisa kuwa kinawaongelea watu wote. Isitoshe, Yak 2:10 inasema kuwa yoyote anayetimiza amri zote isipokuwa moja atakuwa na hatia ya kuvunja sheria yote.

S: Kwenye Rum 3:23-24, endapo watu wote wanaohesabiwa haki ni walewale waliofanya dhambi, je watu wote watakwenda mbinguni kama Wayunivesalist wanavyosema?

J: Hapana, Wayunivesalist ni dhehebu la kizushi. Tazama ufafanuzi wa Kol 1:20 ili kupata jibu.

S: Kwenye Rum 3:25, kwa kuwa kifo cha Yesu ni kwa ajili ya kutuliza ghadhabu ya Mungu itokanayo na dhambi zetu zote za zamani, endapo Mkristo atafanya dhambi kwa makusudi, atakwenda jehanamu, kama Ebr 10:26-31 inavyoweza kuwa inamaanisha?

J: Hapana. Mungu siyo tu kuwa alitupa wokovu, bali pia huulinda wokovu wetu, kama 1 Yoh 1:8-10 na 2:2 zinavyosema.

S: Kwenye RUM 3:27-28, je Paulo anaongelea kazi za sheria ya Musa, au au matendo mema kwa jumla?

J: Kwanza kabisa, kuna sheria moja tu, sheria ya Mungu. Ingawa Paulo anaongelea amri ambazo Wayahudi walijfunza (Rum 3:21), hakuwa amesahau sehemu za sheria ya Mungu walizokuwa nazo watu wa mataifa mengine, kwani anazitaja bayana kwenye Rum 3:29-30.
Hebu natufikiri kwa sekunde moja kuwa ni kweli, jambo ambalo watu wengine wamesema kwa uongo, kuwa Paulo anaongelea tu sheria ya Musa kushindwa kuwafanya watu wastahili kupata wokovu, na kwa hiyo inawezekana kuwa matendo mema kwa kiasi fulan yanaweza kuwafanya watu wastahili kupata wokovu. Sasa sheria ya Musa haikusema tu mambo mabaya ambayo watu hawapaswi kuyafanya, lakini pia imeeleza kibayana mambo mazuri ambayo watu wanapaswa kuyafanya. Kama maneno ambayo baadhi ya watu wameyasema ni kweli, basi amri ambazo Mungu Mungu alizitoa hazitaweza kuwafanya wastahili kupata wokovu, lakini amri nyingine ambazo Mungu hakuzitoa (kutokana na kusahau, uchoyo, au sababu nyingine) zingeweza kufanya hivyo.
Jambo la msingi hapa ki kuwa kuna Mungu mmoja tu, na watu ama wanajaribu kumtii au kutokumtii. Mstari huu si tu kuwa unatuonyesha kwamba matendo mema hayawezi kutufanya tustahili kuupata wokovu, lakini Efe 2:8-9 inathibitisha kuwa hayawezi.
Ili kuona vizuri uhusiano kati ya imani inayojionyesha kwa matendo, na kutohesabiwa haki kwa njia ya matendo, angalia sura inayofuata kwenye Biblia, Warumi 4.

S: Kwenye Rum 3:28, mwanadamu anahesabiwaje "haki kwa imani pasipo matendo ya sheria", wakati Yak 2:24 inasema "mwanadamu husebiwa kuwa ana haki kwa matendo yake; si kwa imani peke yake"?

J: Tunaokolewa kwa neema kwa njia ya imani tu, lakini imani ya kweli haiwi peke yake, bali inakwenda pamoja na matendo. Jibu limeonyeshwa kwenye kifanani: "Haiwezekani kutenganisha imani na matendo, kama isivyowezekana kutenganisha joto na mwanga kutoka kwenye moto." Dondoo hii ilitoka kwa Martin Luther. Ikiwa wewe na rafiki zako mliuzunguka moto wa kambi mkipika chakula chenu, "mpiga kambi mmoja" aliyeitwa Paulo angeweza kusema kuwa si mwanga utokao kwenye moto unaofanya chakula kiive bali ni joto. Na angeweza kuongeza kusema kuwa kuelekeza mwanga wa tochiyako kwenye moto wa kambi hakusaidii kitu chochote pia. "Mpiga kambi" mwingine anayeitwa Yakobo angeweza kusema kuwa huwezi kutambua iwapo kuna moto wa kupika chakula isipokuwa kwa mwanga. Angeweza kusema, kama hakuna mwanga, basi hakuna kitu kinachoweza kupikwa.
Tazama ufafanuzi wa Yak 2:14-25 kwa jibu la undani zaidi.

S: Kwenye Rum 4:1, ni kwa namna gani Ibrahimu alikuwa baba wa Paulo kwa jinsi ya kimwili?

J: Neno lenye kumaanisha baba lilitumika pia kumaanisha mhenga, na kwa kuwa Paulo alikuwa Myahudi, Ibrahimu alikuwa mhenga (babu wa zamani) wake.

S: Kwenye Rum 4:4-5:15, kuna tofauti gani zilizotajwa kati ya anguko la Adamu na kafara ya Kristo?

J: Kuna tofauti tatu:
1.
Moja ni matokeo, na nyingine ni zawadi (Rum 4:4-5).
2.
Zawadi inatofautiana kwa kiwango na kosa (Rum 5:15). Kitu ambacho zawadi ilikifanya ni zaidi ya kurekebisha anguko lililotokana na uovu.
3.
Zawadi na anguko vilitofautiana kwa aina. Zawadi ilileta kuhesabiwa haki na uzima, uovu ulileta hukumu na mauti (Rum 5:16-17).

S: Kwenye Rum 4:8,22, kama Mungu hakumchukulia Ibrahimu kuwa na dhambi, je Mungu alitenda haki alipowachukulia watu wengine kuwa na dhambi?

J: Ndiyo. Rum 4:23-24 inasema kuwa kumchukulia Ibrahimu kuwa na haki badala ya dhambi halikuwa tukio la kipekee. Jambo hilihili ni kweli kwetu pia, endapo tunamwamini Mungu. Hata hivyo, kwa watu wanaoamini haki yao wenyewe badala ya haki ya Mungu, watahukumiwa kwa ajili ya mambo waliyotenda na wasiyotenda kama Ufu 20:12 na Mat 25:32-46 zinavyosema.

S: Kwenye Rum 4:16, kwa nini tunapaswa kuwa na imani siyo uhakika?

J: Hebu fikiria jambo hili: Malaika hawana imani kama sisi, wana ufahamu. Malaika walioasi hawawezi kupata wokovu upitia kwa Kristo, aliyejua vitu ambavyo walikuwa wanavikosa kwa mujibu wa Ebr 2:16.
Sisi hatuna hiari ya moyo kwa namna inayofanana na malaika na mapepo. Wana ufahamu wa aina fulani, sisi tuna imani. Mungu angeweza kuchagua kuja dunia kila mwaka, kuhakikisha bila shaka yoyote kuwa atawahukumu watu wote, na kisha atawaambia wachague kwa hiari yao wenyewe kumkubali au kumkataa. Haitaonekana kuwa kama uchaguzi halisi. Lakini, ni rahisi kwa mtu kuchagua kutokuangalia mambo haya, kubaki katika hali ya mashaka na kutokuwa na uhakika, na kuendelea na njia yao wenyewe.
Mungu angeweza kuumba viumbe ambao wanachagua kumfuata kwa sababu wanajua kwa hakika jinsi vitu vyote vilivyokuwa. Mungu alifanya hivyo, na viumbe hao wanaitwa malaika. Mungu alituumba, watu tulioanguka. Licha ya asili yetu ya dhambi, na licha ya kutokuwa kwetu na ufahamu wa uhakika, Mungu ametuwezesha kuchagua kwenda kwake.

S: Kwenye Rum 4:17, 18, ni kwa namna gani Ibrahimu alikuwa baba wa mataifa meengi?

J: Ibrahimu alikuwa mhenga wa Waisraeli, Waedomu, na Wamidiani, lakini hili sio lengo kuu la mstari huu. Badala yake, Ibrahimu alikuwa baba wa watu wote wanaoamini (Rum 4:11) bWayahudi na watu wa mataifa mengine.

S: Ni kwa vipi Rum 5:1-10 inasema kuwa mabadilishano ya wokovu yanatokea?

J: Kuna mambo nane.
1.
Kuhesabiwa haki kwa njia ya imani (5:1).
2.
Kupata njia kwa imani (5:2) ya kuifikia neema hii (5:2).
3.
Upendo wa Mungu umemiminwa mioyoni mwetu na Roho Mtakatifu (5:5).
4.
Tulipokuwa hatuwezi, Kristo alikufa kwa ajili ya wenye dhambi (5:6).
5.
Mungu alionyesha upendo wake (5:8).
6.
Tulipokuwa tungali wenye dhambi, Kristo alikufa kwa ajili yetu (5:8).
7.
Kuhesabiwa haki kupitia damu ya Yesu (5:9).
8.
Kupatanishwa kupitia mauti ya Mwana wa Mungu, Yesu (5:10).

S: Kwenye Rum 5:2, 9-10, je wokovu unapatikana kwa neema, au kwa imani?

J: Mwanzo, nguvu, uwezo wa kutosha, na matokeo yanawezeshwa na neema ya Mungu iliyomtuma Yesu kufa kwa ajili ya dhambi zetu. Tazama Efe 2:5, 8, 9.
Mungu alichagua kupatanisha zawadi hii kupitia imani yetu kwa Yesu.

S: Kwenye Rum 5:6, je ni kweli kuwa kabla ya Yesu kufa kwa ajili yetu hatukuwa na nguvu zozote?

J: Kwa namna zote zinazotakiwa, ndiyo. Tazama ufafanuzi wa Rum 3:9-20 kwa maelezo ya kina ya Paulo.

S: Kwenye Rum 5:9, tunaokolewa na ghadhabu ya Mungu?

J: Kuna mambo matatu ya kuzingatia katika kujibu swali hili.
1.
Tulikuwa huru na ghadhabu ya Mungu tokea kuzaliwa kwetu, kwani wakati fulani hata wateule (wanaokwenda mbinguni) walikuwa chini ya ghadhabu ya Mungu kwenye Efe 2:3.
2.
Tuko huru na ghadhabu ya Mungu wakati wa hukumu ya mwisho.
3.
Hata hivyo, Mungu anaweza kutuadhibu (Ebr 12:5-11), na tunaweza kupata ghadhabu ya wanadamu wengine (Rum 8:36).

S: Kwenye Rum 5:9-21, ni mambo gani yaliyoelezwa kutokea kutokana na Kristo?

J: Mada hii ni ngumu kufahamika kwa kweli. Yafuatayo ni matokeo yaliyoelezwa.
1.
Kuhesabiwa haki kwa damu yake. Kuokolewa na ghadhabu ya Mungu kupitia kwake (Yesu) [Rum 5:9].
2.
Kupatanishwa na Mungu kupitia kifo cha Mwanawe (Rum 5:10).
3.
Kuokolewa kupitia maisha yake (Rum5:10).
4.
Karama ya Mungu na neema yake ilizidi kwa watu wengi (Rum 5:15).
5.
Kuhesabiwa haki (Rum 5:16).
6.
Kutolewa kwa neema na kipaji cha haki kutawala katika maisha (Rum 5:17).
7.
Neema inatawala kupitia haki na inaleta uzima wa milele (Rum 5:21).
8.
Kuhesabiwa haki kunakoleta uzima kwa watu wote (Rum 5:18).
9.
Wengi watahesabiwa haki (Rum 5:19).

S: Kwenye Rum 5:10, je Wakristo walipatanishwa kwa njia ya kifo cha Yesu, au maisha yake, na Paulo anataka kuonyesha tofauti gani?

J: Paulo anataka kuonyesha kuwa Yesu alifanya vitu vingi kwetu. Kwa kufa kwake, alilipa deni la dhambi zetu. Kwa kufufuka, anatupa uzima na amekuwa uzima wetu. Mwisho, ikiwa tumehesabiwa haki kwa neema kwa njia ya imani, matendo yetu mema yatashuhudia jambo hili.

S: Je Rum 5:12 inaonyesha kuwa kabla ya kuzaliwa watu wanakuwa viumbe wenye uwezo wa kuwa wanadamu, na si wanadamu halisi? (Kwa ajili hiyo, kutoa mimba ni jambo zuri tu).

J: Hapana. Mstari huu hauongelei wakati kati ya kutungwa mimba na kuzaliwa kwa watu, bali wakati wa Adamu kabla ya kutungwa mimba kwetu. Tazama pia ufafanuzi wa Ebr 7:9-10.

S: Kwenye Rum 5:12-19, je laana ya Adamu inakuwaje "aina" ya Kristo kuwachukulia waumini kuwa wenye haki?

J: Wakristo wote wanakubaliana na mambo yafuatayo.
1.
Kifo, uharibifu, asili ya dhambi, na laana zimewapata watu kutona na dhambi ya Adamu.
2.
Yesu alichukua adhabu ya dhambi zetu.
3.
Wateule wamepata uzima wa milele, haki, utakaso, na baraka kutoka kwa Kristo.
Wakristo hawakubaliani katika mambo yafuatayo:
Baadhi ya Wakristo wa kweli
wanasema kuwa asili ya kuhukuliwa kuwa wenye dhambi au wenye haki ni ile ile kutoka kwa Adamu kuja kwetu, kutoka kwetu kwenda kwa Kristo, na kutoka kwa Kristo kuja kwa waumini (Charles Hodge kwenye Systematic Theology, uk.194 na Commentary on the Epistle to the Romans, uk.142-190). Wako wengine wanaoenda mbali zaidi na kusema kuwa kama Mungu hajasema kuwa watu wote, wakiwemo watoto wachanga, wana hatia na wanastahili ghadhabu ya Mungu tokana na dhambi ya Adamu, basi hatakuwa na "haki" ya kuwachulia wateule wote kuwa wenye haki. Wote wanakufa, hata watoto, hivyo wanathibitisha kuwa wanayo laana na hatia ya Adamu.
Hata hivyo, kuna mambo yasiyopungua matatu ambayo hayakubaliani katika maoni haya.
1.
Ikiwa watu wote "wanastahili kupata hatia" kwa sababu ya dhambi ya Adamu, basi ikiwa kuchukuliwa kuwa wenye dhambi au wenye haki ni kule kule kama Hodges anavyosema, Kristo "alistahili kuchukua" hatia yetu. Na je Yesu alistahilishwa hatia ya Hawa?
2.
Ikiwa mpotovu alichukua hatia ya Adamu, basi Adamu hakuwa na hatia tena, au vinginevyo Mungu anatoa adhabu halisi kwa ajili ya hatia hiyo hiyo mara mbili.
3.
Watoto wa wanyama hufa pia. Viumbe vimebeba laana itokanayo na dhambi ya Adamu, lakini kifo hakithibitishi tena kuwa watoto wa wanadamu wana hatia ya dhambi ya Adamu, kuliko watoto wa mbwa walivyo na hatia ya dhambi ya Adamu.
Wakristo wengi wa kweli
wanakataa kabisa kuwa tuna hatia ya Adamu. Yesu hakuwa na hatia yoyote ya dhambi, hata yetu sisi. Badala yake, Yesu alichagua kuchukua adhabu ya hatia yetu kwa kufa msalabani na kwenda kaburini. Ingawa Yesu alichukua dhambi zetu (Ebr 9:28), na yeye ambaye hakuwa na dhambi alifanyika dhambi kwa ajili yetu (2 Kor 5:21), Yesu aliendelea kuwa bila dhambi (Ebr 4:15, 1 Pet 2:22), na ndani yake hakuna dhambi (1 Yoh 3:5).
Huenda
katika kukuba kutokukubali, Wakristo wote wanaweza kukubaliana na jambo hili: Tunasimama kama wenye dhambi wenye hatia ya dhambi zetu wenyewe. Tuna hatia kwa ajili ya dhambi ya Adamu kama ambavyo Kristo alivyokuwa na hatia kwa ajili ya dhambi zetu.

S: Kwenye Rum 5:12-21, ni kwa jinsi gani laana na kuchukuliwa kuwa na haki vinatofautiana?

J: Maoni ya Charles Hodge kuwa namna kuchukuliwa kuwa mwenye dhambi au mwenye haki kunafanana kwa Adamu na Kristo na hakuko sahihi kwa sababu nane:
1.
Kristo alichukua adhabu yetu na tunapokea haki yake kwa kubadilishana naye kwenye njia mbili kubwa, lakini katika njia moja tu ya kubadilishana na Adamu, Adamu hakuchukua kitu chochote kutoka kwetu.
2.
Hatia yetu iliondolewa na Kristo, lakini hatia ya Adamu haikupunguzwa nasi kwa namna yoyote ile.
3.
Uovu ulikuja kwetu, lakini uovu haukwenda kwa Yesu.
4.
Tulipokea uharibifu na asili ya dhambi kutoka kwa Adamu, lakini Kristo hakupokea uharibifu, asili ya dhambi, hatia, au lawama.
5.
Kuchukuliwa kwetu kuwa wenye haki kulifanikishwa na imani yetu, lakini si imani wala upungufu wake vilivyohusika na dhambi ya Adamu (Douglas Moo Commentary on Romans 1-8, uk.338-339).
6.
Kristo alichagua kutoa uhai wake kwa ajili yetu; Adamu hakuchagua kwa hiari yake kuhamishia kitu chochote kile kwa wazao wake.
7.
Haki ya Kristo ilitolewa kwetu pale tulipomkubali. Laana ya Adamu (na watu wengine wanaamini hatia) havikuhususha hiari yetu.
8.
Haki ya Kristo "haikuhamishwa" kupitia wazazi. Baadhi ya Wakristo wanafuata mafundisho ya Kitradusia; wanaamini kuwa hatia ya Adamu inahamishwa kupitia kwa wazazi au kupitia kwa baba.
Ni pale tu mtu anapokana tofauti hizi nane (na nafikiri Charles Hodge hafanyi hivyo), basi kusema kuwa asili ya kuchukuliwa kuwa mwenye dhambi na mwenye haki ni ile ile.

S: Kwenye Rum 5:12-21, kufa kwa Yesu kwa ajili ya dhambi za ulimwengu kunahusiana vipi na kuanguka kwa Adamu?

J: Wakristo wote wanakubali kuwa kufa kwa Yesu kwa ajili ya dhambi za ulimwengu kunahusiana na kunguka kwa Adamu katika dhambi kwa njia mbili zifuatazo:
1.
"Kama tulivyopokea asili ya dhambi kutoka kwa Adamu, tunatakaswa ili tuwe kama Kristo.
2.
Isitoshe, kama tulivyozaliwa tukiwa tumetengwa na Mungu kwa ajili ya Adamu, ndani ya Yesu tunazaliwa upya kama watoto wa Mungu.
Si Wakristo wote wanaokubaliana na njia hizi tatu.
3.
The NIV Study Bible, uk.1713 inasema kuwa Rum 5:18 "haimaanishi kuwa mwisho wa siku watu wote wataokolewa, lakini inasema kuwa wokovu upo kwa watu wote. Ili karama ya neema ya Mung iwe na maana, ni lazima ipokelewe (tazama mstari wa 17)."
4.
Tulipata laana kutoka kwa Adamu na neema kutoka kwa Yesu, lakini Yesu hana hatia yoyote tokana na dhambi zetu kama tulivyo na hatia kwa ajili ya dhambi ya Adamu.
5.
Kama Mungu hakutuchukulia kuwa na hatia tokana na dhambi ya Adamu, Mungu asingeweza kutuchukulia kuwa tuna haki kutokana na Kristo.
6.
Kama Mungu hawaadhibu waovu kwa kuwapa mateso zaidi jehanamu, Yesu asingeweza kuchagua kuchukua adhabu yetu.

S: Kwenye Rum 5:12, msemo "Kwa hiyo" unaongelea nini?

J: Unaongelea moja kwa moja jambo ambalo lilikuwa kabla kuhusu kuhesabiwa haki kwenye Rum 5:1-22. Kwa kuwa kila sura ya Warumi imejengwa kwenye sehemu zilizotangulia. Mtu mwingine anaweza kuona kuwa mstari huu unaongelea kwa njia isiyokuwa dhahiri sehemu zote zilizotangulia za Waraka wa Warumi.

S: Kwenye Rum 5:12-19, upeo wa kuanguka kwa Adamu na kafara ya Kristo vimeelezwaje kuwa ni nini?

J: Wakati mwingine Wakristo hulumbana kuwa ama kafara ya Kristo imewanufaisha watu wote (Wayunivesalisti), au imewanufaisha baadhi ya watu tu (Ukombozi wa watu maalumu). Wakristo wa pande zote mbili wanaweza kuona mambo wanayoyapendelea hapa.
Dhambi ya Adamu:
Wote (Rum 5:12, 18), na wengi (Rum 5:15,19).
Kuhesabiwa haki na Yesu:
upeo ule ule. Wote (Rum 5:18), na wengi (Rum 5:15, 19).
Adamu alikuwa mfano (aina), wenye ukunzani (Rum 5:14); hukumu na kuhesabiwa haki vina ulinganifu katika kifungu hiki.
Tazama pia 1 Kor 15:21-22, 45-49.

S: Kwenye Rum 5:12-21, ni vitu gani vinavyotuunganisha na sisi na Adamu?

J: Maandiko hayasemi, lakini yafuatayo ni maoni yanayoweza kuwa ndio vitu vyenye kutuunganisha. Kila maoni yanahusisha hayo yaliyotangulia.
1. Watu wanateseka katika maisha kwa sababu ya dhambi aliyofanya Adamu.
2. Sisi sote tulifanya kitu hicho hicho. Adamu ni mfano wetu.
3. Tumerithi, yaani, asili ya dhambi.
4. Mungu aliamua kuwa turithi hatia ya mtu ambaye alimchagua (Adamu) kuwa mwakilishi wetu.
5. Watoto (wakiwemo Wayahudi na Wakroashia) wamerithi hatia ya makosa ya wahenga wao. (Theluthi moja ya maoni ya Tradusia).

S: Kwenye Rum 5:12, ni kwa jinsi gani watu wote walifanya dhambi kwa Adamu?

J: Adamu na Hawa walifanya dhambi kabla ya kuwa na asili ya dhambi. Sisi sote tunafanya dhambi, kwa sababu tuna asili ya dhambi kutoka kwa Adamu. Zaidi ya hapa, Wakristo hawakubaliani na jambo hili. Yafuatayo ni baadhi ya maoni.
Matokeo yaliyodhihirishwa:
Kwa sababu sisi sote tunafanya dhambi, matokeo hayo yanaonyesha kuwa kifo na dhambi vinakuja kwa watu wote waliozaliwa kupitia Adamu. Tazama kitabu cha Douglas Moo, Wycliffe Exegetical Commentary on Romans 1-8, uk.339.
Kushiriki kwenye laana tu:
Kwa sababu ya kusababisha (Adamu), matokeo yake ni kwamba sisi (wanadamu) wote tuna laana ya kifo na asili ya dhambi (Rum 5:14).
Kushiriki kwenye hatia na laana:
Kwa sababu ya kusababisha (Adamu), matokeo ni kwamba sisi (wanadamu) wote tumefanya dhambi kwa kushiriki katika pamoja na Adamu, na pia tuna laana ya kifo na asili ya dhambi.

S: Kwenye Rum 5:12-14, kama Mungu alituhukumu pamoja na hatia ya Adamu, ni kwa nini basi?

J: Wakristo wa kweli hawakubali, wanatoa maoni matatu:
1.
Hatia ya Adamu haikuchukuliwa kuwa yetu, ni asili yake tu na laana.
2.
Kama ambavyo Mungu katika asili yake analazimika kuadhibu dhambi kuwa kuhitaji haki na utakatifu hata akatuchukulia kuwa na hatia.
3.
Mungu hakulazimika kutuchukulia kuwa na hatia ili kutimiza matakwa ya haki, bali alifanya hivyo kwa sababu nyingine.
3a.
Kama Mungu hakuwa ametufanya kwa ajili ya hatia ya Adamu, basi asingeweza "kumfanya" Kristo kuwa kafara ya dhambi zetu.

S: Kwenye Rum 5:12-18, dhambi ya asili ni nini?

J: Dhambi ya asili ni dhanailiyo na sehemu mbili:
1. Sisi sote tumeirithi asili ya dhambi, na tumetengwa na Mungu kutoka kuzaliwa kwetu.
2. Sisi sote tuna hatia, si tu ya dhambi zetu wenyewe, lakini pia ya dhambi ya Adamu.
Wakristo wanakubaliana kuhusu jambo la kwanza, lakini Wakristo walio wengi wanaamini kuwa jambo la pili si sahihi. Miongoni mwa watu wa kwanza kufundisha jambo la pili walikuwa Ambrose wa Milan (mwaka 370-390 BK) na Augustine wa Hippo. Wawili hawa walikuwa miongoni mwa Wakristo wa kwanzo kuunga mkono mateso ya watu wasiokuwa Wakristo. The New Dictionary of Christian Ethics and Pastoral Theology, uk.641-643 inaongelea dhambi ya asili kuwa "Jambo la muhimu zaidi ni kuwa dhana ya hatia na ile ya urithi havipingani. Lugha yetu ya wanadamu kutokuwa na hatia inakuwa na maana tu kwenye mandhari ya maamuzi na matendo ambayo sisi wenyewe tunahusika kwa namna moja au nyingine."

S: Kwenye Rum 5:12-18, je tulichukuliwaje kuwa na hatia ya Adamu (kama ndivyo hivyo)?

J: Rum 5:12-18 haisemi bayana ni kwa jinsi gani. Wakristo wanatofautiana sana katika jibu la swali hili. Yafuatayo ni baadhi ya maelezo, na watu wanaweza kuamini zaidi ya moja ya haya.
1.
Tumerithi asili ya Adamu, lakini hatujawahi kuchukuliwa kuwa na hatia ya dhambi ya Adamu kwa namna yoyote ile.
2.
Watu wote wana hatia ya Adamu, lakini ndani ya Kristo, hatia ya Adamu ilisamehewa na iliondolewa kabisa (100%) kwa watu wote (nadharia ya neema iliyokuwepo kabla, yaani Prevenient Grace theory).
3.
Hatia ya Adamu imesamehewa na kuondolewa kutoka kwa watu wote, kama wakati uliopita, lakini imewekwa upya kwa watu wanaomkataa Kristo (maoni ya Millard Erickson).
4.
Watu wote walikuwa na hatia ya Adamu, lakini ndani ya Kristo, hatia ya Adamu imesamehewa na imeondolewa kwa wateule.
5.
Watoto wadogo wanaweza kuwa kwenye ziwa la moto kwa sababu tu ya hatia ya dhambi ya Adamu, bila hatia ya dhambi zao wenyewe.
6.
Watu watakaokwenda kwenye ziwa la moto wanaweza wakaishutumu dhambi ya Adamu kwa sehemu ya mateso yao.
7.
Kwa sababu ya kuchukuliwa kwetu kuwa wenye dhanbi, hatia ya Adamu ilipungua.
8.
Hatia ya Adamu haikupungua, na Mungu alituhesabu kuwa wenye dhambi mara mbili.
9.
Hatia ya Adamu imechukuliwa kuwa yetu, lakini si kwa namna yoyote kubwa.
Wakalvanisti na watu wasiokuwa Wakalvanisti wanaweza kukubaliana na toleo la Biblia la Kikalvanisti, New Geneva Study Bible uk.1775 katika jambo hili. Toleo hili linasema watu wote walifanya dhambi kupitia Adamu lakini inasema kuwa Rum 5:12-21 haisemi ni kwa namna gani.

S: Kwenye Rum 5:12-19, ni Wakristo gani wanaoamini kuwa hatukuchukuliwa hata kidogo kuwa na hatia ya dhambi ya Adamu?

J: Waandishi wote wa kikristo wa awali walioandika kabla ya baraza la kanisa la Nikea hawakuongelea kuhusu kuwa kwetu na hatia ya dhambi ya Adamu, ingawa walinukuu Warumi 5.

Justin Martyr (aliandika karibu mwaka 138-165 BK)

Athenagoras (karibu mwaka 177 BK)

Clement wa Alexandria (aliandika karibu mwaka 193- 217/220 BK)

Arnobius? (mwaka 297-303 BK)

Athanasius, kiongozi wa Nikea (mwaka 326-373 BK)

Gregory wa Nyssa (mwaka 335-394 BK)

Basil wa Cappadocia (mwaka 357-379 BK)

Gregory wa Nazianzus/Nanzianzus (mwaka 330-391 BK) [alidokeza kwenye On the Theophnay sura ya 13, uk.349]

John Chrysostom (mwaka 392-407 BK) [Matthew Homily 28:3]

Kanisa la Greek Orthodox (maoni ya kitradusia kuwa nafsi hairithi hatia)

Mkutano wa Society of Friends (Wakweka) mwaka 1675

Ulrich Zwingli (mwaka 1454-1531) na Zwinglians (kwa mujibu wa Menschreck , uk.198)

Andreas Karlstadt, mwana matengenezo ya kanisa, (mwaka 1480-1541)

Menno Simons, mwanzilishi wa kanisa la Mennonite (mwaka 1495/6-1561)

Dirk Philips, Mmennonite (mwaka 1504-1568)

John Smyth, Mbaptisti (mwaka 1570-1612)

Thomas Helwys, Mbaptisti (mwaka 1575-1616)

Johannes Wollebius (mwaka 1626-1629)

John Wesley, aliwahi kufanya kazi na Whitfield (mwaka 1703-1791)

Wamethodisti wenye kutunza mapokeo

Thomas Coke, Mmethodisti (mwaka 1747-1814)

Dan Taylor, Mbaptisti (mwaka 1738-1816)

Francis Asbury, Mmethodisti (mwaka 1745-1816)

Lyman Beecher (mwaka 1775-1863)

D.L. Moody? (mwaka 1837-1899)

Charles W. Carter

Wolfgang Pannenberg, mtheolojia mwenye kutilia shaka mapokeo

Stuart Denney

Gore Sanday-Headlam

Cranfield

Dhehebu la Wanazareti

Dhehebu la Assemblies of God

Wengi wa Wapentekosti na Wakarismatiki

Walter Connor, mwalimu mashuhuri wa Southwest Baptist Theological Seminary)

Dhehebu la Christian and Missionary Alliance

The New dictionary of Christian Ethics and Pastoral Theology
(IVP)


Athanasius aliamini kuwa tumerithi asili ya dhambi, "Lakini Athanasius hadokezi kuwa tunashiriki kwenye hatia halisi ya Adamu, yaani, kulstahili kwake kulaumiwa kimwenendo . . ." (Kelly Early Christian Doctrines, uk.346-347).
"Namna ambayo Helwys anaielewa nadharia ya kwamba Mungu ameamua kuwa watu wengine waende mbinguni na wengine waende motoni, isipokuwa mafundisho kuhusu kuanguka kwa wanadamu kupitia Adamu, inapingana na Ukalvanisti - kwa kweli, maoni haya ni ya kawaida kwa Wabaptisti wa Uholanzi. Kuchukuliwa kokote kwa wanadamu kuwa wenye dhambi, au matokeo ya kawaida ya kuanguka kwa Adamu, kumebatilishwa na wokovu, kwani neema imetolewa kwa watu wote ili wamchague au wamkatae Mungu "(Calvin Augustine Pater kwenye Karlstadt as the Father of Baptist Movements, the Resurgence of Lay Protestantism, uk.267-268).
Watu wote wamepewa fursa ya kumchagua Mungu au kumkataa kuhusiana na wokovu? Jibu la swali hili ni moja ya njia kuu ya kumtenganisha Mkalvanisti na mtu asiye Mkalvanisti.

S: Kwenye Rum 5:12-19, ni Wakristo gani walioamini kuwa wanadamu walichukuliwa kuwa na hatia ya dhambi ya Adamu?

J: Augustine wa Hippo (mwaka 388-430 BK). Augustine aliamini pia kuwa watoto wachanga wasiobatizwa wanakwenda jehanamu.

Ambrose wa Milan (karibu mwaka 370-390 BK) Alisema kuwa hatia ya Adamu inaondolewa baada ya ubatizo kwa kuosha miguu (On the Mysteries 6, uk.321).

Prosper wa Aquitaine (mwaka 390-463 BK)

Vincent wa Lérins (karibu mwaka 434 BK, maoni ya Kipelagia nusu)

Thomas Aquinas (mwaka 1224-1274 BK)

John Wycliffe? (mwaka 1331-1384)

Baraza la kanisa lililifanyika Trent (mwaka 1546 BK)

Martin Bucer (karibu mwaka 1491-1551)

John Calvin (mwaka 1509-1564) na Guillaume Farel (mwaka 1489-1565)

John Knox (karibu mwaka 1546-1572)

Heinrich Bullinger (mwaka 1504-1575)

Theodore Beza (mwaka 1519-1605)

Ukiri wa imani wa Westminster (mwaka 1646)

John Owen (1mwaka 616-1683)

John Bunyan (mwaka 1628-1688)

Johannes Cocceius (karibu mwaka 1669-1699) mpinzani mkubwa wa theolojia ya agano)

George Whitfield (mwaka 1714-1770) Mkalvinisti aliyeshirikiana na Wesley

John Gill (mwaka 1697-1771) Mkalvinisti mkereketwa

Augustus Toplady (mwaka 1740-1778) mpinzani wa Wesley

Charles Hodge (mwaka 1797-1878)

A.A. Hodge (mwaka 1823-1886)

C.H. Spurgeon (mwaka 1834-1892)

B.B. Warfield (mwaka 1851-1921)

A.W. Pink (mwaka 1886-1952) Mkalvinisti mkereketwa

John Murray (mwaka 1989-1975)

J. Vernon McGee (mwaka 1904-1988)

Loraine Boettner (mwaka 1929-1990)

Katekisimu ya kanisa Katoliki (mwaka 1994)

Wabaptisti (Wabaptisti wa mwanzoni na baadhi wa leo)

R.C. Sproul (mwaka 1939-)

Douglas Moo (mwaka 1950-) (hakuna uhakika, baada ya majadiliano ya kurasa 42)

Believers Bible Commentary

Wycliffe Bible Dictionary
(p.589)

The Bible Knowledge Commentary
(Federal Headship au Utradisia)

Ambrose wa Milan (karibu mwaka 370-390 BK) Alisema kuwa hatia ya Adamu inaondolewa baada ya ubatizo kwa kuosha miguu (On the Mysteries 6, uk.321).

Prosper wa Aquitaine (mwaka 390-463 BK)

Vincent wa Lérins (karibu mwaka 434 BK, maoni ya Kipelagia nusu)

Thomas Aquinas (mwaka 1224-1274 BK)

John Wycliffe? (mwaka 1331-1384)

Baraza la kanisa lililifanyika Trent (mwaka 1546 BK)

Martin Bucer (karibu mwaka 1491-1551)

John Calvin (mwaka 1509-1564) na Guillaume Farel (mwaka 1489-1565)

John Knox (karibu mwaka 1546-1572)

Heinrich Bullinger (mwaka 1504-1575)

Theodore Beza (mwaka 1519-1605)

Ukiri wa imani wa Westminster (mwaka 1646)

John Owen (1mwaka 616-1683)

John Bunyan (mwaka 1628-1688)

Johannes Cocceius (karibu mwaka 1669-1699) mpinzani mkubwa wa theolojia ya agano)

George Whitfield (mwaka 1714-1770) Mkalvinisti aliyeshirikiana na Wesley

John Gill (mwaka 1697-1771) Mkalvinisti mkereketwa

Augustus Toplady (mwaka 1740-1778) mpinzani wa Wesley

Charles Hodge (mwaka 1797-1878)

A.A. Hodge (mwaka 1823-1886)

C.H. Spurgeon (mwaka 1834-1892)

B.B. Warfield (mwaka 1851-1921)

A.W. Pink (mwaka 1886-1952) Mkalvinisti mkereketwa

John Murray (mwaka 1989-1975)

J. Vernon McGee (mwaka 1904-1988)

Loraine Boettner (mwaka 1929-1990)

Katekisimu ya kanisa Katoliki (mwaka 1994)

Wabaptisti (Wabaptisti wa mwanzoni na baadhi wa leo)

R.C. Sproul (mwaka 1939-)

Douglas Moo (mwaka 1950-) (hakuna uhakika, baada ya majadiliano ya kurasa 42)

Believers Bible Commentary

Wycliffe Bible Dictionary
(p.589)

The Bible Knowledge Commentary
(Federal Headship au Utradisia)



S: Kwenye Rum 5:12-19, kuna maoni mengine waliyonayo Wakristo wa kweli kuwa tunayo hatia ya dhambi ya Adamu au hatunayo?

J: Kuna maoni matatu.
1. Watu wote wana hatia ya dhambi ya Adamu, lakini Yesu ametoa "neema iliyokuwepo kabla", inayobatilisha hatia ya Adamu kwa watu wote.

H. Orton Wiley (mwaka 1877-1961)

Norman L. Geisler and Thomas Howe (When Critics Ask, uk.441)


2. Tunachukuliwa kuwa na hatia ya Adamu pale tu tunapochagua kufanya dhambi

Millard Erickson (Christian Theology, uk.639)

Dr. Honer, Dave Geisler, James P. Boyce (mwaka 1827-1888) mwanathiolojia Mbaptisti


3. Tumepata hatia kwa ajili ya dhambi ya Adamu, pia tumepata hatia ya dhambi za wahenga wetu.

Anselm (mwaka 1033-1109)

Martin Luther (mwaka 1483-1546)

Philip Melanchthon (mwaka 1497-1562) alipendekeza kuuawa kwa watu wenye maoni tofauti

Jonathan Edwards (mwaka 1703-1758)

William G.T. Shedd (mwaka 1820-1894)

A.H. Strong (mwaka 1836-1921)


S: Kwenye Rum 5:12, kuna maandiko yoyote ya Kiyahudi mbali ya Biblia yanayofanana na kifungu hiki?

J: Ndiyo. Maandiko ya Kiyahudi yanayofanana na Rum 5:12 ni 4 Ezra 7:118 (=2 Esdras 7:118), Sirach 25:25, na 2 Baruch 23:4; 48:42; 54:19.
Kwa mujibu wa Hard Sayings of the Bible, uk.548, hivi ndivyo 2 Esdras inavyosema,
"[Adam] Alifanya dhambi . . . Uliamuru kifo kwake na kizazi chake . . .
Kwa kuwa Adamu wa kwanza, akiwa na moyo mwovu, alifanya dhambi na alishindwa, vivyo hivyo watu wote waliotokana naye. Kwa hiyo ugonjwa umekuja kuwa wa kudumu" (2 Esdras 3:7, 21-22).
"Oh Adamu, umefanya nini? Kwani ingawa ni wewe uliyetanda dhambi, angko hili si lako wewe peke yako, bali letu pia sisi tulio watoto wako" (2 Esdras 7:118).
Tazama kuwa kifungu hiki kinaongelea madhara yaliyotupata sisi: tumeanguka, tunaugua, na tunakabiliwa na kifo. Hakisemi kuwa tuna hatia ya dhambi ya Adamu.

S: Kwenye Rum 5:12, ni kwa jinsi gani Augustine wa Hippo na toleo la Kilatini la Agano la Kale (Vulgate) walitafsiri kifungu hiki kimakosa?

J: Rum 5:12 ilieleweka vibaya na Augustine (mstari wa 5, uk.302), kwa mujibu wa M. Erickson (uk.636), C. Daniel (uk.242), na J.N.D. Kelly (uk.354), kwa sababu Vulgate inasema "ndani mwake" (in quo) wakati Kigiriki kinasema "kwa sababu."

S: Kwenye Rum 5:12, je Mungu aliwalaumu au "aliwasingizia" watu wote kwa ajili ya hatia ya Adamu au yao wenyewe?

J: Kuanzia mwanzo wa Enzi ya Kati, makanisa mengi ya Katoliki, Reformed, Kilutheri yamekuwa yakifundisha kuwa wanadamu tuna hatia ya dhambi ya Adamu kama yetu wenyewe. Kama baadhi ya Wakristo wa Reformed walivyothibitisha nilipowauliza, watu watateswa jehanamu kwa sehemu tu ya dhambi walizofanya. Sehamu nyingine ya mateso ni kwa ajili ya mambo ambayo hawakuyafanya, bali wataadhibiwa na Mungu tokana na dhambi ya Adamu.
Hata hivyo, dhana hii haikuwepo kwenye kanisa la awali (mpaka wakati wa Ambrose na Augustine), na haikuwepo miongoni mwao walioongea lahaja ya Kikoine ya Kigiriki ambacho kilikuwa lugha ya Agano Jipya.
Justin Martyr
(karibu mwaka 150 BK) "Na tena, isipokuwa wanadamu wana uwezo wa kuepuka maovu na kuchagua mema kwa hiari yao wenyewe, hawawajibiki kwa matendo yao . . ." (First Apology of Justin Martyr sura ya 43, uk.177). "Daudi aliyasema maneno yaliyonukuliwa hapo juu miaka 1500 kabla ya Kristo . . . Lakini ilikuepusha baadhi ya watu wasidhani kuwa, kutokana na maneno tuliyoysema, tunasema kwamba jambo lolote litakalotokea bila kuepukika, kwa sababu lilitabiriwa kama ilivyojulikana kabla, hili pia tunalielezea" (The First Apology of Justin Martyr sura ya 43, 44, uk.177).
Athenagoras
(mwaka 177 BK) "Kama ilivyo kwa wanadamu, ambao wana uhuru wa kuchagua mema au mabaya (kwani ama huwezi kutukuza mwenendo mwema au kuadhibu mwenendo mbaya, isipokuwa mwenendo mzuri na mbaya vilikuwa ndani ya uwezo wao" (A Plea for Christians sura ya 24, uk.142).
Basil wa Cappadocia
(mwaka 357-379 BK) Prolegomena "Kwa upande mwingine, maovu yanayoleta adhabu ya jehanamu hayasababishwi na Mungu, bali sisi wenyewe. Chanzo na msingi wa dhambi vimo ndani ya uwezo na hiari yetu wenyewe" (Prolegomena kwenye Nicene & Post-Nicene Church Fathers Second Series juzuu ya 8, uk.lviii).

S: Kwenye Rum 5:15, je kifo cha kimwili kinachowakuta watu wote kinamaanisha kuwa sisi sote, wakiwemo watoto wadogo, tuna hatia ya dhambi ya Adamu?

J: Hapana. Kama kifo cha kimwili kingekuwa ni kithibitisho cha hatia toka kwa Adamu, basi wanyama nao wangekuwa na hatia ya dhambi ya Adamu, kwani wao nao hufa kimwili. Kifo cha kimwili cha wazao wa Adamu ni laana na matokeo ya dhambi ya Adamu na hawa, lakini hakithibitishi kuwa Mungu anatuhesanu kuwa na hatia kwa ajili ya dhambi ya mtu mwingine. Ezekieli 18 na Kum 24:16 zinaonyesha kuwa mtu hafi kwa sababu ya dhambi ya baba yake, bali dhambi yake tu.

S: Kwenye Rum 5:16, 18, ni kwa njia gani hukumu ilikuwa matokeo ya dhambi moja?

J: Wakristo hawakubaliani na jambo hili. Yafuatayo ni mambo sita yanayowezekana, na mtu mwingine anaweza kuchukua mchanganyiko wa mambo kadhaa kati yake.
1.
Haijaelezwa bayana (New Geneva Study Bible maelezo chini ya ukurasa wa 1775 yanasema, "Paulo haelezi ni kwa jinsi gani watu wote wanahusishwa na Adamu na dhambi yake, lakini analitaja tu jambo hili. Watu wote wamefanya dhambi kwenye dhambi ya Adamu."
2.
Watoto (mfano: wanaozaliwa na AIDS) wanaweza kurithi, katika maisha haya, matokeo ya dhambi, hata kama hatia haikuwa yao.
3.
Jambo la muhimu zaidi kuliko 2, Mungu alimhukumu kila mmoja wetu (sisi na Adamu) kwa sababu ya dhambi ambazo amezifanya.
4.
Kwa kuongezea 2-3, tumerithi asili ya dhambi ya Adamu iliyoanguka na ktengwa, na asili hii inatuhakikishia kuwa tutafanya dhambi na kuhukumiwa.
5.
Kwa nyongeza ya 2-4, kwa kuwa Mungu aliwatangaza kuwa na hatia ya mambo ambayo hawakuyafanya. (Hivyo, jambo hili linaendana na haki ya Mungu inayomfanya awapeleke kwenye mateso ya milele watoto wadogo wasiobatizwa na mimba zilizoharibika hata kama hawakufanya dhambi yoyote au kuvunja sheria yoyote. Hata kama hawakujua kitu chochote kuhusu dhambi, na kusingiziwa kwa ajili ya makosa ya watu wengine, Mungu bado ni mwenye haki kwani anayo haki isiyoweza kueleweka (Maoni ya Federal Headship view)
6.
Pamoja na hoja 2-5, watoto wanahukumiwa mbele ya watu na Mungu kwa ajili ya makosa ya wazazi na wahenga wao, kwa kuwa nafsi zao ziliumbwa kutokana na nafsi za wazazi wao (theluthi ya maoni ya Kitatrusia).

S: Kwenye Rum 5:19, ni kwa jinsi gani watu wengi walifanywa kuwa wenye dhambi?

J: Kama ilivyokuwa kwenye swali lililotangulia, Wakristo hawakubaliani kuhusiana na suala hili. Yafuatayo ni mambo sita ambayo yanawezekana, pia unaweza kuchagua jambo zaidi la moja.
1.
Maandiko haya hayasemi bayana ni namna gani.
2.
Tuliumbwa na uwezekano wa kufa na dhambi ilipewa nafasi.
3.
Jambo muhimu kuliko la 2, kama ambavyo Mungu alimhukumu Adamu kwa kosa alilofanya, Mungu humhukumu kila mmoja wetu kwa makosa tunayofanya kwa njia ileile.
4.
Pamoja na hoja 2-3, sisi tu wenye dhambi siyo tu kwa sababu tunafanya dhambi, lakini pia tunafanya dhambi kwa sababu tu wenye dhambi, kwa maneno mengine, tuna asili ya dhambi.
5.
Pamoja na hoja 2-4, tunawiwa kwa mambo ambayo si hatia yetu wenyewe (Boettner uk.77-78), au dhambi ambazo hatukuzifanya sisi wenyewe (Boettner uk.238).
6.
Pamoja na hoja 2-5, mtu yoyote aliyezaliwa na msaliti, mzinzi, au mtenda dhambi, anapaswa kuadhibiwa kama msaliti, mzinzi, au mtenda dhambi (theluthi ya maoni ya Kitatrusia, yanayopoingana na Ezekieli 18 na Kumb 24:16).

S: Kwenye Rum 5:19, ikiwa watu wote wanafanyika kuwa wenye dhambi kupitia Adamu, na wanahesabiwa haki kupitia Kristo, je jambo hili linamaanisha kuwa kila mtu ataokolewa, kama falsafa ya kizushi ya yuniveso (Universalism) inavyofundisha?

J: Kikundi kidogo cha kikristo chenye mafundisho ambayo Wakristo wengine wanayachukuliwa kuwa potofu kiitwacho ‘Watoto wa Mungu (The Children of God) kinafundisha hivi. Wakristo wa kweli (angalau baada ya Rufinus) wanakubaliana kuwa falsafa ya yuniveso si sahihi, lakini Wakalvanisti na wasio Wakalvanisti wanatoa sababu tofauti za maoni hayo.
Wasio Wakalvinisti
wakiwemo "Warimiraldi au Wakalnisti wa wastani," Walutheri, "Wakalminia," (watu wanaofuata mafundisho yaliyo kati ya Ukalvinisti na Uarminia, na wengineo. Wanasema kuwa Yesu alilipa deni la dhambi za kila mtu. Mfano unaotolewa mara kwa mara kuhusiana na mafundisho haya ni huu: Chukulia kuwa kuna mtu mwenye deni la dola milioni moja ambalo hawezi kulilipa. Rafiki yake tajiri na mkarimu amefungua akaunti ya benki yenye dola milioni moja kwa jina lake, na akamweleza kutoa dola milioni moja na kulipa deni analodaiwa. Fikiria kuwa mtu huyu hakumwamini rafiki yake tajiri, au pengine alitoa hela na kuzitumia vibaya. Mtu huyu atakuwa bado anadaiwa kiasi hicho cha hela, licha ya ukarimu wa rafiki yake tajiri.
Kwa mujibu wa Maandiko, hili ni hitimisho la mafundisho matatu ya Maandiko.
N1.
Yesu alikufa kwa ajili ya watu wote (1 Tim 2:5-6; 1 Yoh 2:2; Rum 11:32; 1 Tim 4:10), na Mungu anatoa na kuagiza watu wote kuitii injili (2 Thes 1:8; Tito 2:11).
N2.
Kuna baadhi ya watu watakaokwenda kwenye ziwa la moto (Ufu 19:20; 20:10-15; 21:8; Mat 13:24-43; 25:31-46).
N3.
Watu wakuwa jehanamu milele (Mat 18:8; 25:41, 46; 3:12; Yuda 7; 2 Thes 1:9; Ufu 20:10; 14:9-11).
Wakalvinisti,
labda isipokuwa Waarimiradi au Wakalvinisti wa wastani Waamiradia, wanasema kuwa neno "wote" la kwanza kwenye Rum 5:18 lina upeo tofauti na neno "wote" la pili kwenye Rum 5:18, na neno "wengi" la kwanza kwenye Rum 5:19 lina upeo tofauti na neno "wengi" la pili kwenye Rum 5:19. Kiini cha mafundisho ya ya Wakalvinisti halisi si malipo bayana ya dhambi za watu kupitia kifo cha Yesu msalabani, lakini kuikana dhana ya kuwa malipo ya dhambi za watu wote, kuwa Yesu hakufa kwa ajili ya watu wote. Watu wengi waliumbwa bila ya fursa ya kuchagua kuepuka miale ye moto ya mauti ya pili.
Kwa nini Wakristo wengine wanafikiri hivi? Ninaamini kuwa moja ya sababu kubwa mbili za kufikiri hivi ni kutokuelewa enzi kuu ya Mungu. Sababu ya pili ni kutakufafanua kwa usahihi upotovu wa binadamu kwa namna ambayo inamwekea Mungu mipaka kwa kufanya kama hawezi au hapendi kutenda katika maisha ya mtu yoyote.
Kutokuielewa enzi kuu ya Mungu:
Baadhi ya Wakalvinisti wana maoni ambayo nadhani ni sahihi kuhusu enzi kuu ya Mungu. Mungu, aliye na uwezo wa kufanya jambo lolote lile kama apendavyo, anaweza kuchagua kunaibisha sehemu ya mamlaka yake kwa muda kiasi. Mungu anaweza kuruhusu mambo yafanyike, kama vile dhambi ambazo zinauhuzunisha moyo wake. Hata hivyo, Wakalvinisti wengi hawajafikia kiwango hiki cha ufahamu. Isipokuwa wanafikiria mambo yafuatayo:
#1.
Aya nyingi za Biblia zinaongelea upendo maalumu wa Mungu na neema yake kwa watu aliowateua, na watu wengi wasiokuwa Wakalvinisti hawazingatii aya hizi. (Mifano mikubwa ni Rum 9:6-23 na Rum 11:3-23).
#2.
Aya nyingi za Biblia zinaongelea kuhusu mpango wa Mungu uliofahamika tangu asili, na usioweza kuzuiliwa, wenye kuhusisha vitu vyote na watu wote, hata waovu. (Mifano ya mpango huo ni Efe 1:11; Mit 16:4).
#3.
Kwa sababu ya kutazama kwa undani mambo mawili yaliyotoka kabla, Wakalvinisti wengi (si wote) wanazipuuzia aya hizi ambapo Mungu anaonyesha kuwa watu wana fursa ya kweli ya kuchagua (Yos 24:22-23), na kuwa Mungu amewapa watu uhuru kuvunja moyo wake (Yer 9:1; Mat 23:37-39, n.k.).
Kwa nini Wakalvinisti wanafikiri hivi? Naamini kuwa wanaamini hivi kwa sababu mbili kubwa.
Kosa la 1 la Wakalvinisti (Uhakika mkamilifu wa hali ya baadaye unaondoa fursa za kweli za kufanya uchaguzi).
Ni vigumu kwa watu kuelewa kuwa Mungu ni mkubwa kuliko muda. Watu wanaposhindwa kufahamu jambo hili, kuwataka waelewe kabisa kwamba kuwa na uwezo wa kweli wa kufanya uchaguzi, na kuwa Mungu anafahamu kwa uhakika mkamilifu jambo ambalo sisi tunaliita hali ya baadaye, ni kama kutaka mwanafunzi wa darasa la saba aelewe kalkulasi; haja hii inaelekea itamchanganya sana mwanafunzi huyu.
Wakristo wengi wazuri wameridhika kuaini mambo haya mawili sambamba, wameshindwa kuelewa jinsi yanavyohusiana, lakini bado wanaamini kuwa yote ni kweli. Watu wengine wanaingia kwenye shida za kitheolojia, sawa na falsafa ya majaliwa, kwa kutokushikilia ukweli kuwa tunayo fursa ya kuchagua, na kutufanya tuwe kama roboti. Pia kuna wengine wanaoingia kwenye shada ya kitheolojia ya fikra kuwa Mungu ana mipaka kwa kutoshikilia ukweli kuwa Mungu anafahamu hali ya baadaye kwa uhakika mkamilifu.
Kosa la 2 la Wakalvinisti (hakuna jambo ambalo halitafanikiwa).
Sababu ya pili inayowafanya Wakalvinisti waone kuwa Ukalvinisti ni wa kweli imewasilishwa vema kwenye kitabu cha Kikalvinisti kiitwacho, Putting Amazing Back into Grace, kilichoandikwa na Michael Horton. Kuna sura yenye kichwa "Hakuna Jambo ambalo Halitafanikiwa." Kwa sababu Mungu ana uwezo wote, anajua yote, ni mwenye enzi kuu, na hakuna kitu kinachotokea isipokuwa kile kilichoruhusiwa naye, Horton anasema kuwa Mungu hawezi kufanya jambo lolote lile kwa kujisumbua tu, au hakuna jambo ambalo lingeweza kutokea ambalo Mungu hajalikusudia.
Hata hivyo, kwa sababu ya ??? ??? ??? Wayahudi Yesu alilalamika kwa ajili ya kumkataa kwao kwenye Mat 23:37-39.
Mafarisayo walilikataa "kusudi la Mungu kwao" kwenye Luk 7:30.
Paulo aliwasihi watu wenye mazoea ya kwenda kanisa kutokupokea neema ya Mungu bure kwenye 2 Kor 6:1.
Yesu alilia kwa ajili ya watu wake. Kwa nini alilia endapo mambo aliyofanyiwa ndiyo ambayo Mungu alikusudia afanyiwe?
Mwishoni, ni muhimu kusema kuwa si Waklvinisti wote wanaoamini kuwa "hakuna vitu ambavyo havitafanikiwa." Mkalvinisti Mswisi, hayati Francis Schaeffer, alisema kwenye kitabu kiitwacho The Church at the End of the Twentieth Century: "Tunaweza kumtukuza Mungu, na Agano la Kale na Jipya vyote vinasema kuwa tunaweza pia kumhuzunisha Mungu. Jambo hili ni zuri sana" (Hymns for the People of God, wimbo namba 364). Kama watu wengine wanaweza kutambua, kama Francis Schaeffer alivyofanya, jambo lilelile ambalo Mungu alilifanya alipowazuia watu kumhuzunisha, kicho chetu kwa neema ya ajabu ya Mungu kitakuwa kikubwa zaidi.

S: Kwenye Rum 5:19, kwa kuwa uyuniveso (mafundusho kuwa hatima ya yote watu wote wataokolewa) umekanushwa kwenye mistari mingine, ni kwa namna gani watu waliofanywa kuwa wenye dhambi watahesabiwa haki?

J: Wakristo hawakubaliani kuhusu jambo hili. Yafuatayo ni baadhi ya maoni:
1.
Msingi wa kuhesabiwa haki kwa watu wote.
2.
Wateule wote wanahesabiwa haki kiuhalisi, na neno ‘wote' linamaanisha wenye dhambi.
3.
Maneno yasiyokuwa fasaha yaney kuonyesha uhusiano sambamba: Kristo anafanya kwa walio wake kwa uhakika kama Adamu anavyofanya kwa walio wake.

S: Kwenye Rum 5:19, je dhambi hutufanya kuwa wenye dhambi, au kuwa wenye dhambo kunatufanya tutende dhambi?

J: Mara nyingine Wakristo hubishana kuhusiana na jambo hili, lakini maoni yote mawili ni sahihi. Mwenye dhambi ni mtu aliyetengwa na Mungu. Kutenda dhambi kutufanya kuwa wenye dhambi, lakini hata kwa kuzaliwa tulizaliwa katika hali ya kutengwa na Mungu mara ya kwanza. HIvyo tunazaliwa tukiwa wenye dhambi kwa asili, na baada ya kufanya dhambi tunakuwa wenye dhambo kwa matendo.

S: Kwenye Rum 5:20, ni kwa namna gani sheria inaongeza dhambi?

J: Rum 4:15 na 5:12 zinajibu swali hili, zikionyesha kuwa Mungu hahesabi dhambi kuwa uovu mahali ambapo hakuna sheria. Kwa maneno mengine, Mungu hahesabu dhambo za bila kukusudia hadi wakati mtu anapojua kuwa ni dhambi. Rum 7:7-13 inatoa maelezo zaidi, na kuhitimisha kwa kusema kuwa sheria ilitolewa ili dhambi iweze kutambuliwa kuwa dhambi.
Bible Knowledge Commentary: New Testament uk.460 inasema kuwa neno ambalo tafsiri nyingine zinasema "ilipoongezwa" inafaa liwe "ilipokuja." Hiki ni neno kilekile kilichotumika kwenye Gal 2:4 kuelezea ndugu wa uongo walioingizwa kwa siri ndani mwa ndugu wa kweli.

S: Kwenye Rum 6:1, 15, kwa nini hatutakiwi kufanya dhambi ili neema izidi?

J: Swali hili ni kama kuuliza hivi. Kwa kuwa tunamshukuru daktari kufanya upasuaji ili kuokoa maisha baada ya ajali la gari, tunapaswa kujiingiza kwenye ajali, tunaweza kusema hivyo?
Njia pekee inayoweza kulifanya swali hili liwe na maana ni kama tutashindwa kushukuru Mponyaji ambaye tunamfahamu sana, kutokuyapa uzito unaostahili madhala ya dhambi, na kutokujali kuwa and do not mind being spiritual road kill.
Kama John MacArthur, Jr. anavyosema, "Kwa nini tunadahani kuwa watu wanaoishi kwenye mazoea yasiyobadilika ya uzinifu, uasherati, uhusiano wa kimwili na watu wa jinsi moja, uongo, na aina zote za uovu ulikithiri wamezaliwa mara ya pili kweli?"

S: Kwenye Rum 6:5; 8; na 1 Kor 15, tunafahamishwa kuwa waumini walikufa na Kristo lakini bado hawajafufuliwa pamoja naye, au waliishafufuliwa pamoja na Kristo kwenye Kol 2:13 na Efe 2:5-6?

J: Mahali tulipo kwa sasa ni kuwa tumekwishafufuliwa katika roho zetu kupitia Kristo, na miili yetu itafufuliwa pamoja na Kristo siku atakapokuja. Licha ya mistari inayoongelea jambo hili kwenye swali hili, mistari hii ya nyongeza inayoonyesha kuwa Paulo alifundisha mambo yote haya mawili.
Rum 6:11
unasema, "Vivyo hivyo ninyi nanyi jihesabuni kuwa wafu kwa dhambi na walio hai kwa Mungu katika Kristo Yesu."
Rum 8:10-11
inaonyesha pande zote hizi mbili kwa wazi kabisa: "Na kama Kristo akiwa ndani yenu, mwili wenu umekufa kwa sababu ya dhambi; bali roho yenu i hai [wakati uliopo], kwa sababu ya haki. Laini, ikiwa Roho yake yeye aliyemfufua Yesu katika wafu anakaa ndani yenu, yeye aliyemfufua Kristo Yesu katika wafu ataihuisha [wakati ujao] na miili yenu iliyo katika hali ya kufa, kwa Roho wake anayekaa ndani yenu."
Vivyo hivyo, Kol 3:1-4 pia inaonyesha pande zote hizi mbili. "Basi mkiwa mmefufuliwa pamoa na Kristo [wakati uliopita], yatafuteni yaliyo juu Kristo aliko, ameketi mkono wa kuume wa Mungu. Yafikirini yaliyo juu, siyo yaliyo katika nchi. Kwa maana mlikufa, na uhai wenu umefichwa [wakati uliopo] pamoja na Kristo katika Mungu. Kristo atakapofunuliwa, aliye uhai wetu, ndipo nanyi mtafunuliwa [wakati ujao] pamoja naye katika utukufu."
Rum 6:5; 8, na 1 Korinto hazikanushi kuwa tumekwishafufuliwa pamoja na Kristo katika roho zetu na kwa nafasi tuliyo nayo. Badala yake zinathibitisha kuwa ni ufufuo wa kiroho tu, bali pia ufufuo ujao wa miili yetu. Vivyo hivyo, Kol 2:13 na Efe 2:5-6 hazikanushi ufufuo ujao wa miili; badala yake zinathibitisha kuwa siyo tukio la wakati ujao tu, bali pia maisha ya wakati huu ya kiroho.

S: Kwenye Rum 6:7, kwa kuwa Wakristo wamekufa katika Kristo, na wamewekwa huru na dhambi, ni kwa nini Wakristo bado wanafanya dhambi?

J: Ingawa Wakristo wataishi bila dhambi yoyote ile mbinguni, hili siyo jambo ambalo mstari huu unaongelea. Rum 6:7 haisemi kuwa Wakristo hawafanyi dhambi, ila tu kuwa wamewekwa huru na utumwa wa dhambi.
Hata hivyo, kama ambavyo watumwa wanaweza wasiwe wamesikia au wameamini ujumbe kuwa wamewekwa huru, wakati mwingine Wakristo wanafanya mambo kana kwamba bado ni watumwa wa dhambi. Kama Mkristo atasema, "Ni lazima nifanye dhambi, sina jinsi nyingine," Mkristo huyo atakuwa anasema uongo.
Neno "kuwekwa huru" linamaanisha "kuondolewa mashtaka yaliyothibitishwa kuwa si ya kweli tena." Kitenzi kipo kwenye wakati mkamilifu uliopita, wenye kunyesha kuwa kitendo kilifanyika wakati uliopita ila matokeo yake yanaendelea hata wakati uliopo.

S: Kwenye Rum 6:19, wakati Paulo anaongea "kwa jinsi ya kibinadamu," je anarahisisha hapa?

J: Ndiyo. Paulo anatoa ufananisho rahisi wa kibinadamu kwa namna ambayo wasomaji wake wanaweza kuelewa. Mtu yoyote yule ni mtumwa ama wa mtawala aitwaye "dhambi", au mtawala aitwaye "Utiifu."
Maoni yaliyorahisishwa ya ukweli bado ni ya kweli, ilimradi yametambuliwa kuwa ni urahisisho na si taswira geu ya ukweli.

S: Kwenye Rum 7:6b, tunatumikaje katika hali mpya ya Roho, si hali ya zamani, ya andiko, kwa kuwa Yesu alisema kwenye Luk 16:16-17 kwamba hakuna nukta [maelezo] yoyote yatakayoondoka kwenye torati?

J: Torati haijabadilishwa, ama na Yesu ama na mtu mwingine yoyote yule. Hata hivyo, Yesu aliitimiza torati kikamilifu kwa ajili yetu, na sasa tunatumika katika hali mpya ya Roho, si katika hali ya zamani ya andiko. Yesu alisema kwenye Luk 16:16 kuwa torati na manabii vilikuwapo mpaka wakati wa Yohana Mbatizaji. Agano la Kale limechakaa kwa mujibu wa Ebr 8:13.
Jambo hili linatofautiana na dhana ya Kiislamu ya kutenguliwa. Maneno yaliyotolewa kupitia Mtume Muhammad yanaweza "kufuta" maneno ya awali ya Muhammad, Yesu, au nabii mwingine yoyote, wakati wowote na wakati wowote utakaompendeza. Yesu hakuifuta torati/sheria bali aliitimiza kwa ajili yetu, na sasa tunatumika kwa njia tofauti.
Kwa mfano, Agano la Kale lilizuia kula nyama ya ngamia, kamba wadogo, na nguruwe. Yesu, aliposema kuwa chakula chote ni safi (Mat 7:19), hakubadilisha sheria ya Agano la Kale, bali alitutaka tutumike kwa namna mpya.
Kama wazo la nyongeza, Waislamu mara kwa mara husema kuwa Wakristo hawatimizi sheria zinazohusu vyakula za Agano la Kale. Ukweli ni kwamba hata Waislamu nao hawazitimizi sheria hizi, kwa sababu wanachukulia kitendo cha Muhammad kula nyama ya ngamia kilikuwa sawa. Vivyo hivyo Wakristo nao hawawakosoi Waislamu (au mtu mwingine yoyote) anayekula nyama ya ngamia. Jambo la msingi ni kuwa kama Waislamu wangekuwa wanamkosoa Yesu au Wakristo kuwa wanafundisha mambo ambayo yanachukua nafasi ya sheria, sababu yoyote ambayo wangetoa ingeweza kumkosoa Muhammad pia kwa kula nyama ya ngamia na kudai kuwa anatangua baadhi ya mambo.

S: Kwenye Rum 7:14-24, je Paulo anaongelea jambo lililotokea kabla au baada ya kumkubali Yesu?

J: Kwa mtazamo wa matukio halisi, Wakristo wamepitia mapambano haya kwenye Rum 7:14-24 kabla na baada ya kumkubali Yesu.
Kabla ya kumkubali Kristo:
Baadhi ya watu walio bado kumkubali Kristo wanafanya bidii kupambana na asili yao ya dhambi; wengine wameacha kabisa kupambana na wamesalimu amri. Ni kweli kuwa baadhi ya madhehebu yenye mafundisho ambayo yanachukuliwa na Wakristo wengi kuwa si ya kweli, na baadhi ya wanasaikolojia wanaohusika na mienendo wamewafanya watu waacha mazoea maovu, kama kutumia madawa ya kulevya, lakini huu ni ushindi mdogo wa mbinu ukilinganisha na vita inayoendelea dhidi ya asili ya dhambi.
Baada ya kumkubali Kristo:
Baada ya kumkubali Yesu, bado tuna asili yetu ya kale ya mwili. Hata hivyo, sasa tunaye Kristo ambaye anatupa motisha na matumaini, na Roho Mtakatifu ndani mwetu, anayetusaidia kushinda. Tatizo si matendo ya nje ya dhambi tu ambayo tunayafanya. Tatizo ni kubwa zaidi. Mioyo na mawazo yetu imeharibikiwa ndani mwetu, na Mungu anatupa si tu msamaha lakini pia utakaso na mchakato wa kubadilishwa ili tuzidi kufanana na Kristo.

S: Kwenye Rum 8:7, je tunapaswa kutafuta maana ya kiroho kwenye Biblia badala ya maana iliyo wazi?

J: Tunapaswa kuwa waangalifu kuhusu kudhania kuwa kuna ukinzani wowote kati ya maana iliyo wazi na "maana ya kiroho." Kuna viwango tofauti vya kuelewa, na kuna kweli nyingi zenye kina kwenye Biblia, lakini kweli zinakamilishana, vinginevyo si kweli zote.
Tunaweza kudhani kuwa Mungu alikusudia neno lake lieleweke na watoto wake. Mtu anaposema kuwa anataka ufahamu wa siri au maalumu ili aweze kuyafahamu mambo ambayo Mungu hakuwaruhusu Wakristo wengine wote kuyaelewa, basi "ufahamu maalumu" wao unashukiwa kuwa wa kubuniwa na wao wenyewe.
Wakati mzazi, waziri mkuu, au jenerali anatoa amri, wanataka itekelezwe kama walivyokusudia, siyo kupewa tafsiri mpya na kufanya iwe tofauti na vile walivyosema. Badala ya kuuliza endapo tunapaswa kuitafsiri Biblia "kwa maneno yenyewe" dhidi ya "kiroho" dhidi ya "maana iliyo wazi" dhidi ya "kiistiari," tunapaswa kukusudia kuitafsiri Biblia kwa namna ambayo Mungu na waandishi wake wanadamu walikusudia.

S: Kwenye Rum 8:9-11, 14-15, je mtu anaweza kuwa Mkristo wa kweli lakini asiwe na Roho Mtakatifu akaaye ndani mwao?

J: Mistari hii inasema hapana. Kuna wakati mfuasi wa Mashahidi wa Yehova aliniambia kuwa hakuwa na Roho Mtakatifu anayeishi ndani mwake, kama ambavyo Mashahidi hufundisha kwa kawaida kuwa ni watu 144,000 tu walio na Roho Mtakatifu anayeishi ndani yao. Nilimwonyesha Rum 8:9-11, na alikaribia kutoa machozi. Ingawa nilipenda kumwambia kuwa kwa ajili hiyo anatakiwa kumkubali Yesu na kumpata Roho Mtakatifu ndani mwake, hivyo sivyo ilivyotokea. Juma lililofuata, alikuja tena ofisini kwangu na kuniambia, kuwa anadhani Roho Mtakatifu yupo ndani mwake.

S: Kwenye Rum 8:9-11, 14-15, kama ni lazima Roho Mtakatifu aishi ndani ya mtu ili awe mwana wa Mungu, na kunena kwa lugha ni uthibitisho wa Roho Mtakatifu, je waumini wasionena kwa lugha hawajaokolewa, kama ambavyo makanisa ya Upentekosti wa mwili mmoja yanavyosema?

J: Hapana. Kunena kwa lugha si uthibitisho pekee wa Roho Mtakatifu, na wala si uthibitisho wa msingi, kama Gal 5:22-24, na 1 Kor 13:1 zinavyoonyesha. Gal 5:22-24 inaorodhesha tunda (siyo matunda) la Roho. Kwenye 1 Kor 12:29-31 inaonyeshwa kuwa si waumini wote wanaonena kwa lugha, kama wote wasivyotenda miujiza na wote wasivyokuwa waalimu. Kwenye 1 Kor 12:31-14:1 inaonyeshwa kuwa sehemu muhimu zaidi ni upendo, na Yoh 14:15, 21 inaonyesha kuwa tunda muhimu la maisha ya kikristo ni kutii maneno ya Yesu.

S: Kwenye Rum 8:9-11, 15, kama ni lazima Roho Mtakatifu awe ndani ya mtu au vinginevyo mtu huyo hawi wa Kristo, inamaanisha kuwa a) watoto wadogo wote wanaokufa wanakwenda jehanamu kwa kuwa Roho Mtakatifu hayumo ndani mwao, au b) je Roho Mtakatifu yumo ndani ya watoto wadogo, au c) maoni mengineyo?

J: Jibu ni maoni mengineyo, kwa kuwa Maandiko hayafundishi maoni a) au b). Kuna mambo matatu ya kuzingatia katika kujibu swali hili.
1.
Isipokuwa Yesu, na Yohana Mbatizaji (Luk 1:40-44), watoto hawana Roho Mtakatifu. Tumezaliwa tukiwa tumetengwa na Mungu (Efe 2:3).
2.
Mungu ameonyesha kwenye neno lake kuwa watu wote wanaookolewa wataokolewa kupitia kwa Kristo (Yoh 14:6; Ebr 9:15; 10:10, 14, 19).
3.
Hata hivyo, kama ambavyo Mungu alikuwa huru kuwaokoa watu wakati wa Agano la Kale kabla ya injili na hata kabla ya sheria, Mungu anaweza kuokoa kama apendavyo kupitia kwa Kristo.
Muhtasari:
Hebu tuwe waangalifu tunapojaribu kuweka mipaka ya jinsi Mungu anavyopaswa kutenda. Ni kweli kuwa Mungu hatendi kinyume na mambo aliyoyafunua kwenye Maandiko, lakini tunapaswa kuwa waangalifu kutokwenda zaidi yay ale yaliyoandikwa, kama 1 Kor 4:6 na Mit 30:5-6 zinavyotukumbusha.

S: Kwenye Rum 8:9, kwa nini Roho Mtakatifu anaitwa Roho wa Kristo?

J: Ni Roho wa Kristo kwa sababu zisizopungua tatu:
1.
Miongoni mwa washiriki wa Utatu Mtakatifu, Roho Mtakatifu alitumwa na Baba na Yesu.
2.
Miongoni mwa washiriki wa Utatu Mtakatifu, Roho Mtakatifu ndani ya maisha yetu anamwakilisha Yesu.
3.
Mafundisho ya kina ya Utatu Mtakatifu yanaonyesha kuwa washiriki wa Utatu Mtakatifu wanaishi kila mmoja ndani ya mwingine, inaweza kuwa kwa njia hiyo hiyo Roho anaishi ndai yetu.

S: Kwenye Rum 8:15 na Efe 3:14-15, ni kwa namna gani Mungu ni Baba yetu?

J: Kitabu kiitwacho Now That's a Good Question, uk.13-14 kinasema kwamba mwanazuoni wa Kijerumani aligundua kuwa katika vitabu vyote Kiyahudi visivyokuwa vya Biblia vilivyokuwa Italia hadi karne ya 10 BK, hakuna hata Myahudi mmoja (mbali ya kwenye Biblia) aliyesema kuwa Mungu ni Baba yake . . . Eh Mungu, wewe ni Baba yetu. Yesu alifanya hivyo, na Paulo anatuhimiza kufanya hivyo pia.
Kwenye Agano la Kale, watu walimwita Mungu Baba yao kwenye Isa 63:16 (mara mbili), na Isa 64:8. Mungu anawakumbusha watu wake kuwa walimwita "Baba yangu" kwenye Yer 3:4. Kwenye sehemi nyingi nyingine (Zab 68:5; Isa 9:6; Yer 3:19; 31:9; Mal 1:6; 2:10, n.k.). Mungu anaitwa Baba, lakini siyo ‘Baba yangu/yetu.'

S: Kwenye Rum 8:16, 17, je watu wote ni watoto wa Mungu kwenye kifungu hiki?

J: Hapana. Ingawa kanisa la Mormoni Church linafundisha kuwa watu wote ni watoto wa kiroho wa Mungu (na miungu wote wanawake wake zake), Rum 8:15 inasema bayana kuwa tu watoto wa Mungu kwa kuasili. Ingawa ni kweli kuwa kila mtu, mnayama, mmea, na pepo ni sehemu ya uumbaji wa Mungu, Warumi 8 inaongelea watu tu waliozaliwa upya.

S: Kwenye Rum 8:17, je tunaweza kuinuliwa na kuwa miungu kama, ambavyo dhehebu lenye mafundisho yanayochukuliwa na Wakristo wengine kuwa ya uongo la Mormoni linavyosema?

J: Hapana. Kosa hili ni la zamani sana, muda mrefu kabla ya Umormoni. Adamu na Hawa walijaribiwa na mafundisho ya makosa ya kwenye Mwa 3:4. Shetani mwenyewe alipenda kuwa kama Mungu kwenye Isa 14:12-15.
Kama Daudi alivyosema kwenye Zab 23:6, ". . . Nami nitakaa nyumbani mwa Bwana milele." Hivyo, wanaume wa Kimormoni hawatakuwa na sayari zao wenyewe, au harimu ya miungu wanawake wake zao. Mmormoni mmoja aliniambia, "Nafikiri Mungu alifanya makosa mengi sana, na niltakapofanyika mungu, nitakuwa bora zaidi." Hivyo, lengo la Mkristo, kumtumikia Mungu milele mbinguni, na lengo la Wamormoni wengi ni tofauti sana.

S: Kwenye Rum 8:19-22 na 5:12-14, je kulikuwa na vifo vya wanyama kabla ya wanadamu kuanguka dhambini?

J: Wakristo wana maoni mawili kuhusiana na jambo hili.
Ndiyo.
Mistari hii kwenye Warumi inaongelea kifo cha wanadamu tu, hivyo Biblia haisemi. Ushahidi wa kisukuku unaonyesha kuwa wanyama wadogo na wakubwa waliliwa kabla ya wanadamu kunguka dhambini.
Hapana.
Mistari hii inaongelea vifo vya wanyama wote wenye kujifahamu. Ingawa mimea, vijidudu vidogo, na wanyama wa daraja la chini wasiokuwa na "nafsi-maisha" (yaani kujitambua) walikufa kabla ya kuanguka kwa wanadamu, wanyama wa daraja la juu hawakufa kwabla ya kuanguka kwa wanadamu dhambini.

S: Kwenye Rum 8:19-22, kwa nini Mungu aliruhusu uovu kwenye ulimwengu ulioanguka?

J: Magazeti na Biblia vinaunyesha kuwa ulimwengu una mabo maovu na mazuri. Kwa mujibu wa Yoh 9:1-3, mtu aliyekuwa kipofu hakuzaliwa na hali hiyo kwa sababu ya dhambi zake au za wazazi wake. Kwenye Luk 13:1-5, Wagalilaya waliouawa, na wale ambao mnara wa Siloamu uliwaangukia, wangeweza kustahili vitu hivi, lakini wastahili kama ambavyo mtu mwingine yoyote alistahili.
Rum 8:19-22 inaonyesha kuwa baada ya anguko la wanadamu, Mungu aliviweka viumbe vyote kwenye uharibifu. Binadamu mwenye uharibifu hakuruhusiwa kuishi kwenye sehemu ya uumbaji isiyo na uharibifu. Tunayo majanga ya asili, dhukuma za kipindi kifupi, na binadamu kukosa ubinadamu kwa watu wengine. Kuanzia wakati wa anguko la mwanadamu, 1 Yoh 5:19 inasema dunia nzima ipo kwenye ushawishi wa mwovu. Mungu wa dunia hii shetani kwenye 2 Kor 4:4. Shetani ni mkuu wa dunia hii kwenye Yoh 12:31; 14:30, 16:11; Efe 6:12; na Kol 1:13. Tazama ufafanuzi wa Efe 2:2 kwa maelezo zaidi.

S: Kwenye Rum 8:21, je uhuru wa Mkristo unahusisha uhuru wa kufanya kitu chochote tunachotaka?

J: Dhehebu lenye mafundhisho ambayo Wakristo walio wengi wanayochukulia kuwa ya uongo liitwalo Familia ya Upendo (Family of Love), lilifundisha kuwa wanatakiwa kuwa na uhuru wa kufanya ngono nje ya ndoa zao.
Yaelekea kuwa jambo hili lilitokea wakati wa Agano Jipya pia, kwa sababu Paulo aliongelea jambo hili kwenye 1 Kor 5:9-11 na Rum 6:1.
1 Kor 5:9-11
inasema kuwa hatupaswi hata kula pamoja na watu wanaojiita Wakristo lakini wanafanya mambo haya.
Rum 6:1
inaonyesha kuwa haiwezekani kuwa na fikra hizi na kuishi ndani ya Kristo.
Jambo moja la kushangaza nililowahi kulisikia ni hili: "Ni kiasi kidogo zaidi ambacho ninaweza kufanya na bado niwe ndani ya Yesu?" Jibu ni kwamba: "Kama bado unafikiri namna hii, bado hujawa ndani yake."

S: Kwenye Rum 8:26, je Roho Mtakatifu ni Mpatanishi, au Kristo ni Mpatanishi wetu kama 1 Tim 2:5 inavyosema?

J: Roho Mtakatifu anaongea kwa niaba yetu kwenye maombi. Hakutupatanisha/hakutulipia dhambi zetu msalabani, au kutupatanisha kama Kuhani Mkuu, kama ambavyo Yesu pekee alivyofanya.

S: Kwenye Rum 8:28, ni kwa jinsi gani Mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendao wale walioitwa kwa jina lake katika kuwapatia mema katika mambo yote ?

J: Mamilioni ya miaka kuanzia sasa, au kwa muda wowote unaohesabiwa kutoka mbinguni, tunaweza kuangalia jinsi Mungu alivyotumia mambo yote katika maishani yetu, hata maovu, kutufundisha, kutusaidia kukua, na kutufanya tuwe bora.

S: Kwenye Rum 8:28-39, rafiki yangu alikuwa ananisomea kitabu cha Charles Stanley kuhusu Kutopoteza Wokovu na alipofika kwenye sehemu inayoongelea upendo wa Mungu usiokuwa na masharti, alilipinga jambo hilo kwa kuuliza ni mahali gani kwenye Biblia panaposema kuwa upendo wa Mungu hauna masharti?  Yeye ni mshiriki wa dhehebu la ‘Kanisa la Kristo' na maoni yake ni kuwa moja ya masharti la kuokolewa ni kubatizwa kwa maji—hivyo upendo wa Mungu na wokovu wake kwetu vinategemea sharti la kubatizwa. Je ingefaa nimjibu vipi?

J: Charles Stanley ana maandiko mazuri sana kuhusu Biblia na wokovu, na yuko sahihi.
Zab 145:17 inasema kuwa Mungu anawapenda watu wote aliowaumba, jambo hili linahusisha rehema zake alizionyesha hata kwa watu waliooptea milele.
Hata hivyo, Biblia haisemi kuwa Mungu ni "mwenye upendo wote," kwa sababu ni haki na ghadhabu, siyo upendo kwa shetani na mapepo vilivyomfanya awatupe kwenye ziwa la moto. Si watu wote watakaoenda mbinguni, bali ni wateule tu ambao Mungu aliwajua na kuwachagua tangu asili.
Lakini Mungu ana upendo maalumu kwa baadhi ya watu wanaoitwa wateule (wanaokwenda mbinguni). Ingawa Rum 8:28-39 inasema kuwa hakuna kitu kinachoweza kututenganisha (sisi tulioitwa) na upendo wa Mungu. Kwa wateule, upendo unawezaje kuwa bila masharti?
Je upendo wetu "ulianzisha" upendo wa Mungu kwetu, au upendo wa Mungu ulianzisha upendo wetu kwa Mungu? Kwenye 1 Yoh 4:10, 19 tunaona kuwa Mungu alitupenda kwanza. Kwenye Yoh 6:65 Yesu alisema, "Kwa sababu hiyo nimewaambia ya kwamba hakuna mtu awezaye kuja kwangu isipokuwa amejaliwa na Baba yangu." Walkalvinisti na watu wasiokuwa Wakalvinisti hawakubaliani endapo jambo hili ni kwa watu wote au baadhi:
Wakalvini wa kiwango cha juu (Five-point Calvinists):
Baba amewawezesha baadhi ya watu tu. Hivyo, Yesu hakufa kwa ajili ya baadhi ya watu, na hawakuukataa wokovu ambao Yesu aliutoa kwao, kwa sababu Mungu hakukusudia kuwapa fursa yoyote ya kuupokea wokovu. Mungu hafanyi mambo yasiyokuwa na faida.
Mtu mwingine yoyote:
Baba amewawezesha watu wote kwa kutenda mambo mbalimbali kabla ya itikio lao la wito wa Mungu, lakini baadhi yao wamechagua kutupilia mbali kile walichopewa. Mungu Mwana alihuzunika sana kwa ajili ya jambo ambalo halikufanikiwa kwa watu wa Yerusalemu (Mat 23:37-39).
Hata hivyo, washiriki wengi wa dhehebu la ‘Kanisa la Kristo' hawaitambui Efe 2:4, 8-10. Matendo yetu ni hayahusiki kabisa kutufanya tupate wokovu. KWA NJIA YA IMANI . . . SI KWA MATENDO. Imani imeelezwa bayana kabisa hapa, na ubatizo wa maji ni kazi ambayo inaashiria imani yetu, lakini tunaokolewa kwa neema ya Mungu, siyo maji. Unapotakiwa kuchagua kati ya maneno ambayo mshiriki wa dhehebu la ‘Kanisa la Kristo' na maneno ya Mtume Paulo, fuata maneno ya Mtume Paulo.

S: kwenye Rum 8:29, je inawezekana mtu ambaye Mungu alimjua tangu asili kwenda jehanamu?

J: Hapana. Kitenzi "kujua tangu asili" hapa kinamaanisha kuwa Mungu alijua kabla hata ya ulimwengu kuumbwa asili kuwa watakwenda mbinguni. Swali hili lina mantiki isiyokuwa ya kweli. Kwa kuwa Mungu yu juu ya muda, swali hili ni kama kuuliza, "Je inawezekana mtu ambaye ameishakwenda Toledo awe hajawahi kufika Toledo?"

S: Kwenye Rum 8:29 na Efe 1:4, je maoni kuwa Mungu aliwachagua watu tangu asili ni mafundisho ya Kikalvinisti tu?

J: Hapana. Mistari hii inaonyesha kuwa maoni haya ni mafundisho ya Biblia kwa Wakristo wote, Wakalvinisti na wasio Wakalvinisti pia. Wakalvinisti wanaweza kuwa wanakosea vitu kadhaa kuhusiana na dhana ya Mungu kuwachagua wateule tangu asili, lakini baadhi ya Wakalvinisti wana mawazo mazuri pia.
Mungu anafahamu kwa uhakika vitu vyote
kuhusiana na hali ya baadaye, lakini ufahamu wake hauondoi uhuru wetu au kupunguza wajibu wetu. Hatuwezi kusema "Mungu alijua kuwa nitafanya jambo hili, kwa hiyo sikuwa na jinsi nyingine, nililazimika kufanya hivyo." Kwenye Mdo 2:23, Yesu Kristo alitolewa kwa Wayahudi kwa shauri la Mungu lililokusudiwa na kwa kujua kwake tangu zamani, lakini watu waliomsulubisha walikuwa na hatia ya dhambi (Yoh 19:11). Ufuatao ni mfano. Tunaweza kusoma kitabu kuhusu George Washington kuvuka Mto Delaware zaidi ya miaka 200 iliyopita. Ufahamu wetu unaokaribia uhakika kutoka kwenye kitabu hiki haukumlazimisha George Washington kuvuka mto huu. Fikiri kama tungeweza kurudi miaka 400 iliyopita nyuma kwenye mashine ya muda, tukiwa na hiki kitabu. Hatutakuwa tumefanya jambo lolote litakalo mlazimisha George Washington kufanya kitu chochote kile.
Mungu yuko juu ya muda (Tit 1:2), pia yuko ndani yake, na ufahamu wake uliokuwepo tangu asili haukutulazimisha kufanya kitu chochote.
Kiendo cha Mungu kutujua sisi tangu asili kilitangulia kitendo chake cha kutuchagua tangu asili kwenye mistari miwili inayoongelea mambo haya kwa pamoja (Rum 8:29; 1 Pet 1:2). Wakalvinisti wana desturi ya kubadilisha mfuatano wa vitendo hivyo. Mungu humchagua mtu yoyote anayemchagua, kisha anamfahamu tangu asili. Waarminia (siyo Waarmenia) wana desturi ya kusema kuwa Mungu alichagua kabla ya mwanzo wa muda kwa kutumia ufahamu wake wa tangu asili. Hata hivyo, kama ni kweli kuwa Mungu yuko juu ya muda, basi mambo yote haya mawili yanaweza kuwa yalifanyika kwa wakati mmoja.
Enzi kuu ya Mungu haipingani na utashi wetu
, ingawa Wakalvinisti wana kawaida ya kusema kinyume ya hivyo. Kuna mambo yaliyotokea ambayo "hayakuingia kwenye mawazo ya Mungu" kama kutoa kafara ya watoto wadogo kwenye Yer 32:35, na kufa kwa watu ambao haikuwa wafe kwenye Eze 13:19. Kuna mambo yanayotokea yenye kumhuzunisha Mungu. Lakini kwa upande mwingine, mambo yote yanafanyika kwa mujibu wa mpango wa Mungu (Efe 1:11). Je inawezekanaje mambo haya mawili kwenda pamoja? - kwa dhana ya "kutoa mamlaka/enzi kwa mtu au asasi nyingine." Mungu angeweza kusimamia vitu vyote, kiasi kwamba kusingekuwa na kitu ambacho kisingemfurahisha na sisi sote tungekuwa kama maroboti. Hata hivyo, Mungu ambaye ana uwezo wa kufanya mambo yote, alichagua kutoa enzi/mamlaka yake kwa muda na kwa mipaka, kiasi kwamba tumepewa uwezo wa kuchagua kumtii au kutomtii yeye. Mungu anamthamini sana mwanadamu, aliyeumbwa kwa mfano wake, kiasi kwamba watu walikuwa na uhuru wa kuchagua kumpenda Bwana. Mungu anathamini sana jambo hili, hata anawaruhusu watu wamkatae na kupata matokeo ya uchaguzi wao.
Utashi ni nini?
Martin Luther aliandika kitabu kizima Bondage of the Will ambapo alisema utashi ulikuwa ni mafundisho ya uongo. Luther hakuwa sahihi hapa, kwa sababu alipitiliza ukomo wa Kibiblia. Tunazaliwa na uwezo wa kuchagua ambao unatumikishwa na dhambi (kama ambavyo Luther angekubali), lakini tunao uhuru kutenda unaotuwezesha kuomba msaada. Tunao utashi, na mtu anayetawaliwa na madawa ya kulewa anayo hiari pia. Mtu anayetawaliwa na madawa anaweza asiwe na nguvu ya kuyaondoa mazoea yake haya, lakini anaweza kujivuta hata kufika kwenye kituo cha tiba ya madawa ya kulevya, ama kuanguka chini na kusema "Nisaidie." Kuna watu wanaotofautisha kati ya utashi ulio huru na usioelemea upande wowote wa maadili (ambao hauelezwi kwenye Biblia), na kitu tulicho nacho, wananchokiita uhuru wa kutenda. Watu wengine, hasa Wakristo kwenye kanisa la awali, walitumia msemo hiari walipoongelea dhana ya Kibiblia.
Kwa ufupi
, Mungu alituchagua tangu asili, na pia tunao utashi, kama tukiuelewa kwa usahihi. Kabla ya muda kuanza, uchaguzi wa Mungu wa watu watakaoenda mbinguni haukuwa wa kigeugeu au bila ufahamu, bali kila siku ya maisha yetu iliandikwa kwenye kitabu cha Mungu (Zab 139:16) kama alivyotuchagua.

S: Je Rum 8:29-30 inafundisha maoni ya kizushi ya uyuniveso, kuwa hatimaye watu wote wataokolewa?

J: Hapana. Rum 8:29-30 inasema kuwa watu wote waliojulikana na kuchagulia tangu asili watatukuzwa. Kitu ambacho mstari huu haujakiongelea ni kuwa watu wote walijulikana na kuchaguliwa tangu asili kupata wokovu.
Hivi ndivyo dhehebu la uongo la Mch. Moon liitwalo ‘Unification Church' linavyofundisha kwenye kitabu chao cha Divine Principle (toleo la tano la mwaka 1977), na baada ya hapo tutaangalia jinsi Biblia inavyofundisha.
Divine Principle
, uk.190, "Lengo kuu la Mungu la kuwarejesha watu ni kuwaokoa wote. Kwa hiyo, lengo la Mungu ni kuiondosha kabisa jehanamu, baada ya kwisha kipindi kinachotakiwa kukamilisha malipo ya fidia bima yote."
Divine Principle
, uk.191, "Siku za mwisho zitakapokuja, hata roho chafu zitawashukia watu waishio duniani wenye kiwango kinachofanana, na kwa kushirikiana nao zitashiriki katika kuyatimiza mapenzi ya Mungu. Mwishoni, baada ya muda utakiwao kupita, lengo la pamoja la viumbe litafikiwa."
Divine Principle
, uk.200, "Ingawa muda wa wokovu wao unaweza kutofautiana, watu wote walioanguka dhambini wamepangiwa kuokolewa."
Biblia:
Adhabu ya watu wasioamini haina mwisho na ni ya milele (Mat 18:8; 25:41, 46; Yuda 7). Ni moto usiozimika (Isa 66:24; Mat 3:12; Luk 3:17).
Ufu 14:11 inasema, "Na moshi wa maumivu yao hupanda juu hata milele na milele, wala hawana raha mchana wala usiku, hao wamsujudio huyo mnyama na sanamu yake, na kila apkeaye chapa ya jina lake."

S: Kwenye Rum 8:32, je neno "mengine" limo kwenye toleo la Kigiriki kama lilivyo kwenye toleo la Mashahidi wa Yehova lijulikanalo kama ‘New World Translation' (lililorekebishwa mwaka 1970 BC, uk.1227)?

J: Hapana, halipo. Toleo la Mashahidi wa Yehova linaongezea neno "mengine" kwenye maandishi ya mlazo sehemu mbalimbali kama vile mara nne kwenye Kol 1:16-20. Maandishi ya mlazo yanaonyesha kuwa neno hili halimo kwenye toleo la Kigiriki. Hata hivyo, neno "mengine" halipo kwenye Rum 8:32 au Fil 2:9 kwenye toleo la Kigiriki, na wahariri wa ‘New World Translation' walipuuzia kuliweka kwenye maandishi ya mlazo. Pia waliongeza neno hili "wengine" kwenye Mdo 10:36, na kuliweka kwenye mabano mraba.

S: Kwenye Rum 8:39, je inawezekana kupoteza wokovu?

J: Wakristo wa kweli hawakubaliani kuhusu jambo hili. Tazama ufafanuzi wa Ebr 6:4-12 na Efe 1:14 kwa maelezo zaidi.

S: Je Rum 9:5 inaonyesha kuwa Kristo ni Mungu?

J: Ndiyo. Aland na wengine hawataji tofauti za maandishi kwenye hati za kale zenye aya hii, hivyo jambo hili linahusika na tafsiri za Kiingereza tu. Kwanza, kuna tafsiri tofauti za Kiingereza, kisha maelezo kutoka kwenye vitabu mbalimbali vyenye kufafanua Maandiko.
Bible Knowledge Commentary: New Testament
, uk.476 inasema, "Huu ni uthibitisho dhahiri wa uungu wa Kristo. Kuna watu wanaoyachukua maneno haya kuwa sentensi tofauti (tazama ukingoni mwa tafsiri ya Kiingereza iitwayo NIV), lakini maandishi ya NIV yanaonekana kufaa zaidi." Expositor's Bible Commentary juzuu ya 10, uk.103 na Expositor's Greek Testament juzuu ya 2, uk.658-659 zinasema kuwa maandishi yaliyozoeleka, yanayomwelezea Kristo kuwa "Mungu" yanafaa zaidi kwa sababu:
a)
Kwenye Kigiriki, kiwakilishi rejeshi "ndiye" kinaweza tu kuwa kinaonge kiima kilichotangulia cha sentensi, Kristo.
b)
Uhusiano wa kibinadamu wa Kristo na Israeli umeelezwa kama wito wa maelezo yenye kufanana na haya ya upande wa uungu wake.
c)
Huu hauwezi kuwa wimbo wa kumsifu Mungu Baba, kwa kuwa msemo "mwenye kuhimidiwa" umewekwa kabla ya yule anayesifiwa.
d)
Kwenye Kigiriki kibainishi kinatumika pamoja na maneno yaliyotangulia, "aliye juu ya mambo yote."
e)
Ingawa baadhi ya tafsiri zimerekebisha maandishi kuwa "wv o, hon ho" badala ya "o wv, ho on" "ambaye Mungu wake yu juu ya wote, ahimidiwe milele," hakuna mamlaka ya hati yenye maandishi yanayounga mkono marekebisho haya.
Hitimisho:
Ndiyo, mstati huu unathibitisha uungu wa Kristo.

S: Kwenye Rum 9:8-9, 27 na 11:13-17, 26, je Wayahudi wote watakwenda mbinguni au la?

J: Hapana. Kuna watu wachache ambao watumia vifungu hivi viwili vya Warumi kufikiri hivi. Hata hivyo, Warumi 8-9 inafundisha kuwa ni watoto wa ahadi, si wa kimwili, watakaokwenda mbinguni. Rum 9:27 inasistiza kuwa ni wana wa Israeli wa kimwili tu watakaokuwa wamebaki ndio watakaokolewa. Rum 11:13-17, 26 inaongelea "mwaliko ulio wazi" wa Mungu kwa Wayahudi leo, na kukubali kwao mwaliko kwa idadi kubwa siku zijazo.
Kwa nyongeza, Yesu aliwaambia viongozi wa kidini wa Kiyahudi kwenye Yoh 8:24, kuwa kama hawamwamini yeye ni Kristo, hakika watakufa katika dhambi zao. Kwenye Mat 23:33, aliwauliza waalimu wa sheria na Mafarisayo jinsi gani wataepuka hukumu ya jehanamu. Gal 5:2 pia inaonyesha kuwa Kristo hana maana kwa watu wanaotumaini tohara.
Tazama ufafanuzi wa Yer 31:37 kwa maelezo zaidi.

S: Kwenye Rum 9:13 na Mal 1:2-3, kwa nini Mungu alimchukia Esau? Je jambo hilo lilikuwa haki?

J: Kwa mujibu wa R.C. Sproul kwenye Now That's a Good Question, uk.570, "Kwanza kabisa, hii ni nahau ya Kiebrania. Ni aina ya usemi wa Kiebrania tunayoiita usambamba kinzani, ambapo Maandiko huongea kwa kutumia mambo yanayokuwa kinyume. Ili kuweza kuielewa nahau hii, tunapaswa kuona kuwa maana yoyote aliyokuwa nayo Mungu kuwa anamchukia Esau, inamaanisha kinyume cha kumpenda Yakobo . . . kwenye mandhari [ya Agano la Kale] ambamo maandishi ya aina hii yanapatikana, Biblia inaposema kuwa Mungu anampenda Yakobo, inamaanisha kuwa anamfanya Yakobo kuwa mpkeaji wa neema na rehema zake. Anampa Yakobo zawadi ambayo hampi Esau. Anampa Yakobo rehema. Anazuia rehema hizo hizo zisiende kwa Esau kwa sababu hadaiwi rehema na Esau na anabaki kuwa na haki [ya kuzuia rehema] . . . Myahudi anaelezea tofauti hii kwa kutumia misemo kinzani."

S: Kwenye Rum 9:18, kwa nini hatuwezi kumlaumu Mungu kwa kuufanya moyo wa Farao uwe mgumu?

J: Mara sana Mungu alisema kuwa ameufanya moyo wa Farao kuwa mgumu. Lakini mara saba Mungu alisema kuwa Farao aliufanya moyo wake kuwa mgumu. Natuanze kwa kujifahamisha dhana ya kuufanya moyo kuwa mgumu kabla ya kuangalia ni kwa jinsi gani Mungu aliufanya moyo wa Farao kuwa mgumu.
Kuufanya kuwa mgumu moyo
wa mtu asiyemcha Mungu kunawafanya wazidi sana kuwa waovu. Kwa upande mwingine, Mungu alisema aliwafanya manabii Ezekieli na Yeremia kuwa wagumu, na walifanywa kuwa namna nzuri. Eze 3:8-9 inasema, "Tazama, nimeufanya uso wako kuwa mgumu juu ya nyuso zao, na kipaji cha nyuso zao, na kipaji cha uso chako kuwa kigumu juu ya vipaji vya nyuso vyao. Kama almasi ilivyo ngumu kuliko gumegume, ndivyo nilivyokifanya kipaji chako."
Kwenye Yer 1:18 na 15:20, Mungu alimfanya Yeremia kuwa kama ukuta ambao ungewazuia watu wote.
Hivyo "kufanya mgumu" hakumaanishi kuwa ni kitu kiovu wakati wote, lakini kufanya mgumu kunamaanisha kuwa mtu aliyefanywa hivyo atazidi sana katika namna hiyo, kama ambavyo udongo wa mfinyanzi unavyokuwa mgumu.
Kwa kutuma mapigo, Mungu
anaweza kuwa aliilainisha mioyo ya watu, lakini jambo hilo liliufanya moyo wa Farao kuwa mgumu. Ni kwa kiasi gani Mungu aliufanya moyo wa Farao kuwa mgumu bila kutumia vitu toka nje kama vile mapigo? Maandiko hayasemi kitu kuhusiana na jambo hili. Hata hivyo, kazi ya Mungu iliufanya moyo wa Farao uende kwenye uelekeo ambao Farao alikuwa ameishapenda uende.
Yafuatayo ni mambo ambayo baadhi ya waandishi toka kwenye kanisa la awali walisema kuhusiana na jambo hili.
Tertullian
(mwaka 198-220 BK) "Mungu anaufanya moyo wa Farao kuwa mgumu. Hata hivyo, alikuwa anastahili kushawishiwa kuelekea kwenye uharibifu wake, alikuwa tayari ameishamkana Mungu, tayari amewakataa wawakilishi wa Mungu tokana na kiburi chake, aliwatwisha watu wake mizigo mingi sana, na (kujumulisha yote) kama Mmisri" (Five Books Against Marcion kitabu cha 2 sura ya 14, uk.308.
Origen
(mwaka 225-254 BK) alikuwa na wazo hilohilo aliposema kuwa kama ambavyo joto hilihilo kutoka kwenye jua hilohilo linaufanya udongo kuwa mgumu na kuiyeyusha nta, ndivyo ulivyo utendaji wa Roho wa Mungu anayefanya mioyo ya watu wakaidi na kuilainisha mioyo ya watu wenye kutubu (Origen's de Principiis kitabu cha 3 sura ya 1.11, uk.311. Pia ufafanuzi uliopo uk. 384).
Tazama pia swali linalofuata kwa maelezo zaidi.

S: Kwenye Rum 9:18, ni nani aliyekuwa na wajibu upi katika kuufanya moyo wa Farao na ile ya watu wengine kuwa migumu?

J: Kuna mambo manne ya kuzingatia katika kujibu swali hili.
A. Mungu anawajibika:
A1.
Vitu vyote vinavyotokea vinaruhusiwa na Mungu. Kwa maneno mengine, hakuna jambo linalotokea isipokuwa lile ambalo Mungu ameliruhusu (Yak 4:15; Ayu 1:12; 2:6; Zab 103:19).
A2.
Jambo lolote ambalo Mungu ameliamuru lazima litokee (Isa 43:13; 55:10-11; Rum 11:29). Mungu aliahidi (yaani aliamuru) kuwa Waisraeli wataodoka Misri baada ya kuwa watumwa kwa miaka 400 (Mwa 15:13-14).
A3.
Mungu alimuumba Farao na alimruhusu kuishi.
A4.
Mungu alitenda kupitia historia na alimfanya Farao kuwa mfalme wa Misri wa wakati ule.
A5.
Mungu alituma mapigo Misri.
A6.
Hatima ya mambo yote, hata yale ambayo hayakuingia moyoni mwake (Yer 19:5; 32:35), yalifungamanishwa, yanafungamanishwa, na yatafunganishwa pamoja kwenye mpango wa Mungu (Efe 1:11; Rum 8:28; Mit 16:4).
B. Mungu hawajibiki
kwa mambo ambayo aliamuru lakini hakuyasababisha moja kwa moja, kama vile uovu.
B1.
Mambo mengine yanamfanya Mungu apate ghadhabu kubwa (Yer 5:29; 8:19; 12:8; Eze 8:6).
B2.
Kuna mambo yanayomhuzunisha Mungu (Yer 4:19-22; 9:1; Luk 19:41-44; Mat 23:37-39).
C. Wajibu wa Farao:

C1.
Farao hakulazimishwa. Ukweli ni kwamba, kwa watu wengi mapigo yangekuwa "kivutio" cha kuchagua jambo sahihi.
C2.
Farao alifanya maamuzi yake mwenyewe.
D. Mungu na Farao waliwajibika kwa pamoja:
D1.
Farao pia aliufanya moyo wake kuwa mgumu, na kitendo cha Farao kuufanya moyo wake kuwa mgumu kilitajwa kabla Mungu hajaufanya moyo wa Farao kuwa mgumu.
Tazama ufafanuzi wa Kut 7:22 kwa maelezo zaidi.

S: Kwenye Rum 9:19-22 na 11:8, 10, Mungu anawezaje kutufanya tuwajibike kwa jambo ambalo anatufanye tuwe?

J: Mfano unaweza kusaida. Fikiria binadamu wote tungezaliwa na kuishi maisha yetu kwenye meli. Fikiria kuwa meli hii ina karibia kuzama, na mitumbwi wa uokoaji ulikuwepo kwenye meli. Kama tungebaki kwenye meli na kuzama, tuna wajibika kwa kifo chetu wenyewe. Hatukuwajibika kwa kuzaliwa kwenye meli, lakini tunawajibika kwa kutokuchagua kwetu kutoka kwenye meli. Kufanya hivi hakutakuwa si makosa tu bali pia hatari na haitakuwa na maana kwa mtu yoyote yule kulaumu mazingira ya kuzaliwa kwake kuchagua kwake kukataa kutumia mtumbwi wa uokoaji uliokuwepo.
Hivyo, hatukuwa na jinsi ya kusababisha au wajibu wa namna tutakavyozaliwa, na ukweli kwamba tulikuwa na asili ya dhambi. Hata hivyo, watu wanawajibika kwa kutokuchagua kuja kwa Mungu kwa ajili ya utakaso wa asili yao ya dhambi na msamaha wa dhambi zao.

S: Kwenye Rum 9:19, kwa nini neno la Mungu linasema kuwa maswali haya hayafai?

J: Sababu mbili tofauti zimetolewa hapa.
Fikra:
Swali lolote si zuri, kama fikra ni ile ya kumjibu Mungu vibaya (mstari wa 20). Badala ya kujaribu kujifunza njia za Mungu, maswali yanalenga kumfanya Mungu ajihalalishe mwenyewe.
Maneno yaliyosemwa:
Hata wakati yanapoulizwa kwa fikra yenye heshima, maswali bado si mazuri kwa sababu yanatokana na mawazo yasiyokuwa sahihi. Tunapaswa kufahamu mambo mawili ya kweli:
1.
Mungu anayo haki ya kutufanya tuwe vyovyote vile apendavyo (msatari wa 21).
2.
Pia, kama mistari ya 21-23 inavyoonyesha, Mungu hakuwafanya wateule tofauti na wapotovu, sote tunazaliwa tukiwa tumeumbwa kutoka kwenye ‘mfinyanzi' uleule. Tofauti si asili yetu, lakini hatima yetu. Kwa watu wengi, neno halitachanganyika na imani (Ebr 4:2), na Mungu atamwaga ghadhabu yake ya haki kwao.

S: Kwenye Rum 9:19, je watu wanao utashi?

J: Ndiyo, kwa kufuata tafsiri sahihi ya utashi.
Hapana, hakuna kitu nje ya mapenzi ya Mungu aliyoyakusudia na aliyoyasema
. Ikiwa utashi unamaanisha uwezo wa kufanya jambo lililo nje ya mipaka, ufahamu, au uwezo wa kudhibiti wa Mungu, basi hakuna mtu, hata Adamu au shetani, aliye na utashi. Hata hivyo, hivi sivyo inavyomaanisha watu wanaposema kuhusu utashi mara nyingi.
Ndiyo, tunafanya mambo ambayo yako nje ya mapenzi yaliyokusudiwa ya Mungu.

Utashi mara nyingi humaanisha kuwa Mungu amechagua kutupa uwezo wa kweli wa kuchagua, na kufanya mambo zaidi ya yale ambayo Mungu anataka. Mungu anajua maamuzi yetu yote, lakini ni sisi tunayoyafanya. Nia zetu ni "huru" kwa maana ya kuwa hazilaimishwi na Mungu. Sisi si vibaraka au maroboti. Hata hivyo, utashi wetu hauko "huru" kabisa kwa sababu umefungwa na dhambi. Mlevi wa madawa ya kulevya ambaye anayetamani sana madawa ana uhuru wa kuacha kabisa mara moja, lakini nia yake ipo kifungoni.
Watu wasiokuwa Wakristo wanasema kuwa wana utashi, ukiwa ni pamoja na kuwa kila mmoja ana wajibu wakiasi fulani na uwezo wa kumuitikia Mungu. Wakristo Wakalvinisti wanasema kuwa waumini wana uhuru wa kuchagua, lakini watu wasiokuwa waumini hawana. Mhubiri mkubwa wa karne ya kumi na tisa (na Mkalvinisti) Charles Spurgeon alisema tuna "utashi", lakini ni mtumwa wa asili yetu ya dhambi, maneno ambayo yanafanana na jinsi Wakristo wasiokuwa Wakalvinisti wanavyosema.
Hata hivyo, Wakalvinisti wengine wanasema kuwa ingawa watu wana "nafasi ya kuchagua", hawana uhuru wa kuchagua, siyo tu kwa sababu Mungu hajachagua kutupa, bali pia Mungu anadhaniwa kuwa angeweza kutotupa uhuru huu na kubaki kuwa mwenye enzi.
Mkalvinisti Loraine Boettner (uk.222) anasema, "Zaidi ya hayo, kama tunakubali kuwa tuna uhuru wa kuchagua kwa maana ya kuwa uwezo mkamilifu wa kufanya mambo yatokee uko mikononi mwa mwanadamu, tunaweza pia kuandika ‘uhuru wa kuchagua' kwa herufi U na K; kwani katika wakati huo mwanadamu amekuwa kama Mungu, - sababu ya kwanza, chimbuko la asili la matendo -- na tuna nusu mungu wengi sana kama tulivyo na uhuru wa kuchagua. Isipokuwa enzi ya Mungu imeondoshwa, hatuwezi kuuruhusu uhuru huu wa mwanadamu."
Boettner anachanganya mambo hapo. Kama Boettner angesema kuwa ‘hatuwezi kukubaliana na dhana ya uhuru wa kuchagua yenye kumaanisha kuwa mwanadamu anaweza kufanya mambo zaidi ya yale ambayo Mungu ameyaruhusu,' kisha Wakristo wote wangeafikiana na Boettner. Hata hivyo, kama Mungu amechagua ‘kutoa mamlaka' kwa watu kwa muda, ambapo Mungu ameamuru mambo fulani, kama hatima ya watu ya milele itakuwa namna moja au nyingine kutegemea na itikio lao la utendaji kazi wa Mungu ndani ya maisha yao, na Mungu hajalazimisha itikio hilo, basi Boettner amekosea, isipokuwa tu mtu anaweka maana yake mwenyewe kwenye neno ‘kamili' la Boettner kuwa maelezo haya ni marudio yasiyokuwa ya lazima kimantiki ambayo mtu yoyote angeweza kuafikiana nayo.
Maelezo kuhusu uhuru wa mwanadamu ambayo yametolewa zaidi kwenye Biblia, na ambayo Wakristo wasiokuwa Wakalvinisti na wengi wa Wakalvinisti wanaweza kukubaliana, yalikuwa sehemu ya hotuba ya R.C. Sproul aliyoitoa Austin, Texas (Marekani) mwezi Machi 9, 1991. Maelezo yafuatayo yametokana na hotuba ya R.C. Sproul aliyoitoa Austin Machi 9, 1991.
"Siamini kuwa Wakristo tumeikana dhana ya muhimu sana ya uhuru na wajibu wa binadamu - japo kwa sekunde moja. Na litakuwa jambo lenye kuumiza sana kwangu kama nitaikana dhana ya uhuru wa mwanadamu. Lakini wapendwa, ningeweza kuvumiliana na jambo hilo. Kama ningetakiwa kuikana dhana ya kuwa Mungu ni mwenye enzi, ningekuwa nimeukana ukristo. Ningekuwa nimeliacha tumaini, kwa sababu ningetambua kuwa sasa ninaishi kwenye ulimwengu ambao hauko chini ya mamlaka ya ulinzi na usimamizi wa Mungu." Hivyo R.C. Sproul anasema kuwa enzi ya Mungu ni muhimu kwake kuliko uhuru wa mwanadamu, lakini anaamini kuwa mambo yote haya mawili ni ya kweli. Hapa pia, Sproul haongelei uhuru kamili, lakini anaongelea uhuru wa kweli.
Kwa muhtasari:
Wote wanakubali kuwa kila mtu ana wajibu wa kumtii Mungu, lakini ndani mwao hakuna mtu aliye na nguvu ya kutii kwa sababu ya asili yetu ya dhambi. Wengi wa Wakristo wa madehehbu ya ‘Reformed' wanasema kuwa Mungu hajawahi kuwapa watu wasiokuwa wateule fursa, uchaguzi, au uwezo wa kuitikia wito wa Mungu kwa namna yoyote ile. Kama Mkristo mmoja wa dhehebu la ‘Reformed' alivyosema, mwanadama anaweza kuwa ama roboti wa Mungu au roboti wa shetani.
Kama maelezo ya nyongeza, baadhi ya wanatheolojia wenye mlengo wa ‘Reformed' wa wastani (Spurgeon, Packer, Bunyon, n.k.) wanavyosema, Mungu huwapa watu wote nafasi ya kweli ya kuitikia injili. Wengine (Pink, Gill, Hoeksma) wanasema Mungu hatoi nafasi ya kuitikia injili kwa watu wote. Wengine wanasema kuwa tunaweza kutoa nafasi ya kweli kuitikia injili kwa watu wote kwa kuwa hatuwajui wateule, lakini Mungu asingeweza kutoa nafasi ya kweli ya kuitikia.
Tafadhali angalia swali linalofuata kwa uthibitisho wa Maandiko wa "utashi/uhuru wa kuchagua" kwa maana ya kwamba ingawa nia zetu zimefungwa na dhambi, vyote vina uwezo wa kufanya uchaguzi wa kweli kuitikia wito wa Mungu.

S: Kwenye Rum 9:19, je watu wako kama maroboti au vikaragosi, au Mungu aliamua kumpa kila mtu uwezo wa kufanya uchaguzi wa kweli na kuitikia wito wa Mungu?

J: Yos 24:22-23 inaonyesha kuwa ama watu wanaweza kufanya uchaguzi, au kuwa Mungu ametosheka kuwa watu wake wapotoshwe katika kufikiri kuwa wanachagua kufanya agano naye.
Mungu amewapa watu uwezo wa kuuhuzunisha moyo wake (Yer 9:1; Mat 23:37-39, n.k.). Ingawa baadhi ya Wakalvinisti wanasema kuwa maneno haya yamemweleza Mung kwa kutumia umbo la binadamu, na Mungu haelekei kuhisi hivi, jambo hili linazua matatizo mengi na magumu kuyatatua. Kwa nadharia tete, kama mistari yote ya kwenye Biblia inayoongelea kuhuzunishwa na kukatishwa tamaa kwa Mungu haichukuliwi kama ilivyo, basi huenda mistari yote inayoongelea hasira na ghadhabu vya Mungu nayo pia haihukuliwi kama ilivyo. Huenda mistari yote inayoongelea upendo wa Mungu itakuwa itakuwa inamwelezea Mungu kwa kutumia umbo la binadamu na Mungu na Mungu hawajali au kujihusisha na sisi pia. Hivyo, ama mistari inayoelezea hisia za Mungu ina maana, au Mungu ametumia wino kwenye Biblia bila ulazima wakati angeweza kusema matokeo uchaguzi wa wanadamu, na kusema kwamba alikuwa aina fulani ya kompyuta tu.
Tazama ufafanuzi wa Mwa 50:19-20; Kum 1:39, na Yos 24:21-24 kwa habari kamili kuhusu uwezo wa watu wa kuchagua.
Tazama swali linatofuata kwa maelezo ya kina ya uwezo wa binadamu wa kuchagua.

S: Kwenye Rum 9:19, kama watu hawako sawa na maroboti au vikaragosi, Biblia inasemaje kuhusu uwezo wa binadamu wa kuchagua?

J: Niwie radhi kwa kutoa maelezo marefu sana kuhusu jambo hili, lakini Wakalvinisti wengi wanashindwa kuona kuwa Mungu anawapa watu uchaguzi halisi na wa kweli kuhusu kumtafuta yeye. Nitaeleza mambo mawili kuhusu Mungu, kisha mambo kadhaa kuhusu binadamu.
MUNGU BABA NA YESU:
Mungu Baba alimchagua, na kumwita, na kumtuma Yesu kuwa Mwokozi wetu (Mat 12:18; 1 Pet 2:6; Ebr 5:4; 3:2; Luk 23:35; na Isa 48:15; 49:1, 6).
Hata hivhyo,
uchaguzi, ufahamu, na mpango wa Mungu Baba haukukanusha ukweli kwamba Kristo mwenyewe bado alichagua kwa hiari yake kuja na kutii (Yoh 10:18; Luk 22:42; na Ebr 10:9).
BINADAMU:
Watu wote ni wenye dhambi na wamepotoka. Bila ya msaada wa Mungu, hakuna mtu atakayemtafuta Mungu, kwa mujibu wa Rum 3:11, ambayo inafafanua Zab 14:2 na 53:2.
Hata hivyo, Daudi
mwenyewe alisema kuwa alimtafutu Mungu kwenye Zab 63:1 na 27:4, 8.
Isitoshe, watu wengine wengi
kwa msaada wa Mungu, wamechagua kumtumikia Bwana.
Yos 24: 22, ". . . Ninyi mmekuwa mashahidi juu ya nafsi zenu, ya kuwa mmemchagua Bwana, ili kumtumikia yeye," alisema Yoshua kuhusu Waisraeli.
Mat 6:33, "Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa."
Watu wengi wanamtafuta Mungu (1 Nya 16:10, 11; 2 Nya 15:12; 30:19; Ezr 6:21; Zab 34:10; 69:32; 70:4; Mit 28:5; Zek 8:21, 22; Mal 3:1
Elekeza moyo wako kumtafuta Mungu (2 Nya 11:16; 19:3; 20:3, 4; 34:3; 1 Nya 22:19; na Hos 3:5).
1 Nya 28:8, 9; 2 Nya 7:14; 15:2, 13; 31:21; Zab 9:10; na Isa 45:9 ni ahadi za kutokuachwa kwa watu wanaomtafuta Mungu.
Zab 22:26, ". . . Wamtafutao Bwana watamsifu."
Zab 24:6, "Hiki ndicho kizazi cha wamtafutao, wakutafutao uso wako, Ee Mungu wa Yakobo."
Zab 40:16; 105:3, 4; 119:2, 45 wote wakutafutao washangilie na kukufurahia.
Zab 119:94, ". . . Nimejifunza mausia yako."
Mit 1:28-29, ". . . Watanitafuta kwa bidii, wasinione. Kwa kuwa walichukia maarifa."
Mit 8:17, ". . . Wale wanitafutao kwa bidii wataniona."
Isa 51:1, ". . Ninyi mnaomtafuta Bwana."
Isa 55:6, "Mtafuteni Bwna, maadamu anapatikana, mwiteni maadamu yu karibu."
Yer 29:13, "Nanyi mtanitafuta na kuniona, mtakaponitafuta kwa moyo wenu wote."
Yer 50:4, " . . . Wana wa Israel . . . na wana wa Yuda . . . watamtafuta Bwana, Mungu wao."
Hos 10:12, ". . . Kwa maana wakati umewadia wa kumtafuta Bwana."
Amo 5:4, 6, 14; 5:14 mtafute Bwana nanyi mtaishi.
Pia,
kwa msaada wa Mungu, watu wanaweza kuchagua kufanya mapenzi ya Mungu.
Yoh 7:17, "Mtu akipenda kuyatenda mapenzi yake, atajua habari ya yale mafunzo, kwamba yanatoka kwa Mungu, au kwamba mimi nanena kwa nafsi yangu tu."
Yon 2:8, "Watu waangaliao mambo ya ubatili na uongo hujitenga na rehema zao wenyewe."
Zab 83:16, Mungu hafanya mambo mbalimbali ili watu wamtafute.
Zab 119:30, "Nimeichagua njia ya uaminifu . . ."
Zab 119:173, ". . . Nimeyachagua mausia yako."
Isa 7:15, 16, "Siagi na asali atakula, wakati atakula wakati ajuapo kuyakataa mabaya na kuyachagua mema."
Isa 56:4, "Kwa maana Bwana awaambia hivi matowashi, wanaozishika sabato zangu, na kuyachagua mambo yanipendezayo . . ."
Mit 8:10, 16:16, tumeamriwa kuchagua hekima badala ya fedha.
Yoh 5:35, "Yeye [Yohana] alikuwa taa iwakayo na kung'aa, nanyi mlipenda kuishangilia nuru yake kwa muda.
Yoh 7:17, "Mtu akipenda kuyatenda mapenzi yake, atajua habari yale mafunzo, kwamba yanatoka kwa Mungu."
Mdo 20:21 "Nikiwashuhudia Wayahudi na Wayunani wamtubie Mungu, na kumwamini Bwana wetu Yesu Kristo."
Efe 1:13, "Nanyi pia katika huyo mmekwisha kulisikia neno la kweli."
Kum 30:19, ". . . Chagua uzima, ili uwe hai."
Rum 11:32, ". . . Maana Mungu amewafunga wote pamoja katika kuasi ili awarehemu wote. (Neno ‘wote', pantas ni hilohilo lililotumika mar azote hizi mbili).
2 The 2:10, ". . . Hao wanaopotea; kwa sababu hawakukubali kuipenda ile kweli."
Tit 2:11, "Maana neema ya Mungu iwaokoayo wanadamu wote imefunuliwa."
1 Pet 1:22, "Mkiisha kujitakasa roho zenu kwa kuitii kweli."
2 Pet 1:10, ". . . Jitahidini zaidi kufanya imara kuitwa kwenu na uteule wenu."
Kinyume chake,
watu wanawajibika kwa kutokumtafuta Mungu wao.
Isa 9:12-13; Hos 7:10 Mungu amekasirika kwa sababu watu hawajamrudia au kumtafuta. Je Mungu amekasirika kwa ajili ya jambo ambalo aliamuru kuwa wasilitende, na amekasirishwa na jambo ambalo hakuchagua kuwawezesha kufanya?
Yer 30:15, ". . . Kwa sababu ya ukubwa wa uovu wako, kwa sababu dhambi zako zmeongezeka, nimekutenda haya."
Mit 1:29, "Kwa kuwa walichukia maarifa, wala hawakuchagua kumcha Bwana."
HITIMISHO:
Kwa kuwa wito wa Mungu haukuondoa uchaguzi wa Yesu, na Biblia inasema kuwa kwa msaada wa Mungu tunaweza kumchagua yeye (Mungu), hivyo, kuitwa kwetu na Mungu hakutuondolei uhuru wetu wa kuchagua.

S: Kwenye Rum 9:19, je inawezekana kuwa watu wasiokuwa Wakristo hawana uhuru wa kuchagua, Wakristo wana uhuru wa kuchagua?

J: Hapana, lakini hili ni wazo lenye kufurahisha ambalo rafiki yangu Mkalvinisti aliwahi kuniambia. Hata hivyo, sijawahi kusikia Mkalvinisti mwingine yoyote akisema hivi. Kuna mambo manne ya kuzingatia wakati wa kuangalia sababu za wazo hili kutokuwa sahihi.
Mungu ni mwenye enzi kuu
, kwa maana ya kwamba anafahamu vitu vyote vinavyokwenda kutokea, ikiwemo kila jambo tunalokwenda kulichagua. Pia anadhibiti undani wa kila kitu anachotaka kukidhibiti, na hakuna atomu moja inayotembea bila ya kuruhusiwa na Mungu. Hata hivyo, Mungu anaweza kujizuia. Anaweza kuchagua kwa muda na kwa kikomo alichoweka "kumpa mtu au asasi nyingine enzi au mamlaka yake" kama kuturuhusu tuchague kwa namna ambayo sisi, na siyo Mungu, tuwajibuke na matokeo ya uchaguzi wetu.
Uhuru wa kuchagua ni nini?
Kama uhuru wa kuchagua utafafanuliwa kuwa ni uhuru mkamilifu, kiasi cha kuwa hata hana uwezo wa kuudhibiti, uhuru wa kuchagua wa aina hii haupo. Hata hivyo, waandishi Wakristo wa awali waliandika kuwa uhuru wa kuchagua ni uwezo wetu wa kuchagua mambo yanayomoendeza Mungu, na una matokeo yake makubwa. Hata hivyo, uhuru wetu wa kuchagua umefungwa na dhambo, sawa na jinsi uhuru wa kuchagua wa mlevi wa pombe au madawa ya kulevya ulivyofungwa na dhambi zao. Wanaweza wasiwe na nguvu zao wenyewe zitakazowawezesha kujiondoa kwenye utumwa wa ulevi husika, lakini wanaweza wakajikwaa na kufika kanisani au kitui cha kurekebisha mwenendo, na kulia wakiomba msaada.
Wakalvinisti wengi
hawakubaliani na dhana kuwa watu wana uhuru wa kuchagua kwa maana halisi ya maneno haya; hawakubali kuwa watu wanaweza kufanya uchaguzi. Wanachosema kinakaribia kumaanisha kuwa binadamu tu maroboti. Baadhi ya Wakalvinisti hawakubali kuwa tuna uhuru wa kuchagua kwa sababu Mungu ni mwenye enzi kuu. Wakalvinisti wengine, pia Martin Luther, hawakubali kuwa tuna uhuru wa kuchagua kwa sababu tumeanguka na kufungwa na dhambi. Swali hili linamaanisha kuwa Wakalvinisti hawakubaliani na uhuru wa kuchagua kwa sababu ya pili.
Watu wasiokuwa Wakalvinisti
wanakubali kuwa Mungu ni mwenye enzi kuu, na kuwa utashi wa mwanadamu umefungwa na dhambi. Hata hivyo, sababu zote hizo mbili hazifanyi uchaguzi wetu kuwa mzaha, au wajibu wa binadamu kwa mambo asiyoweza hata kuitikia ni fumbo lisilokuwa na ulinganifu.

S: Kwenye Rum 9:33, kuna kitu gani kisichokuwa cha kawaida kuhusiana na neno hili "uangushayo"?

J: Neno hili halimaanishi kutega. Badala yake, maana yake inakaaribiana sana na kuanguka toka kwenye mteremko wa ghafla.

S: Kwenye Rum 10:3, je Mungu aliwezaje kuwaadhibu Waisraeli kwa haki kwa ajili ya kutokujua kwao?

J: Hakuna mfano kwenye Maandiko wa Mungu kumwadhibu mtu kwa ajili ya kutokujua kusikokuwa na hatia. Hata hivyo, kuna kutokujua kwengine kuliko na hatia. Kwa mfano, wazazi wazuri hawamwadhibu mtoto mchanga kwa kutokujua, lakini mwalimu mzuri anamwadhibu mwanafunzi kwa kutokujua wakati anapoacha kusoma kazi yake ya nyumbani. Wayahudi, pamoja na sisi leo, tuna "kazi ya nyumbani" ya kulijua neno la Mungu.

S: Kwenye Rum 10:4, ni kwa namna gani Kristo ni mwisho wa sheria?

J: Kristo ni mwisho wa sheria kwa namna mbalimbali.
1.
Yesu mwenyewe alitimiza sheria kikamilifu.
2.
Kama kuhani mkuu, Kristo alitimiza sheria kwa ajili yetu. Alitoa kafara kwa ajili yetu mara moja tu (Ebr 9:13-14).
3.
Lengo la sheria ni kutuongoza kwenda kwa Yesu. Ebr 10:1 inasema kuwa sheria ni kivuli cha mema yatakayokuja.
4.
Kristo ni mwisho, au hatima ya sheria. Kafara za Agano la Kale "zilifunika" dhambi (Ebr 9:9-10; 10:2-4) kabla ya Kristo kuziondoa kabisa dhambi.
Neno "mwisho" au "hitimisho" limetiliwa mkazo kwenye maandishi ya Kigiriki kwa kuwa ni la kwanza kwenye sentensi.

S: Kwenye Rum 10:5, je tunaishi kwa kutimiza sheria, au sheria huleta mauti kama Rum 8:2 inavyosema?

J: Kielelezo kinaweza kusaidia hapa. Kwamba sheria ya kibinadamu inaleta uzima au mauti inategemeana na mtizamo wako. Mtu anayeweza kuwa mtuhumiwa wa kosa la jinai na mwuaji aliyehukumiwa kifo wana mitizamo tofauti.
Kama utaitimiza sheria kikamilifu, jambo hilo litakuletea uzima. Hata hivyo kuvunja sheria ambayo unaweza kuijua kunaleta hukumu na mauti.

S: Kwenye Rum 10:9-10, je kusema tu "Yesu ni Bwana" ndilo jambo pekee la kufanya ili kwenda mbinguni?

J: Hapana, hivi sivyo mstari huu unavyofundisha. Kwenye Mdo 8:13, Simoni yule mchawi "aliamini," ingawa Petro alisema kuwa anakwenda kuangamia kwenye Mdo 8:18-20. Neno la Kigiriki la "kuamini" kwenye Mdo 8:13, ni episteuse, na si neno lililotumika mara nyingi kwenye Biblia kwa "kuamini." Neno linalotumika mara nyingi ni pestuvo, lenye kumaanisha kutumaini na kuwa na imani iokoayo. Neno lililotumika kwenye Mdo 8:13 linamaanisha kukubali kiakili.


S: Kwenye Rum 10:11, kwa nini mstari huu unasema "hatatahayarika," wakati unapoongelea Isa 28:16 ambao kwenye toleo la Kimasoretiki (Agano la Kale la Kiebrania) unasema, "hatafanya haraka"?

J: Rum 10:11 inafanana na matini ya Kigiriki ya Agano la Kale [Septuajinti] "hataaibika kamwe," si kama matini ya Kimasoretiki. Kwenye sehemu nyingine nyingi pia, nukuu za Agano Jipya zinakaribiana na matini ya toleo la Kigiriki [Septuajinti] kuliko ya Kiebrania [Kimasoretiki].
Neno "hatafanya haraka" kwenye Isa 28:16 kwenye matini ya Kimasoretiki ni chuwah (Strong's 2363), ambalo maana yake halisi ni "fanya haraka." Maana hii inaeleweka vizuri kama unafahamu "atafanya fanya haraka" kuwa haraka kutoka vitani baada ya kushindwa. Hata hivyo, neno hili linamaanisha pia hisia, kama "kufadhaika sana" kwenye Ayu 20:2. Hivyo matini ya Kimasoretiki nay a Kigiriki (Septuajinti) zina maana zinazofanana hapa, lakini Septuajinti ni fasaha na rahisi zaidi kwa watu wasioongea Kiebrania kuelewa.

S: Kwenye Rum 10:11, nini ni msingi wa kusema kuwa jiwe lisilohai linamwakilisha mtu?

J: Kwa ufananisho, Mungu ni jiwe lenye kukwaza kwenye Isa 8:14. "Naye atakuwa . . . ni jiwe la kujikwaza na mwamba wa kujikwaa." Zab 118:22 inasema, "Jiwe walilolikataa waashi limekuwa jiwe kuu la pembeni." Mwandishi wa zaburi haongelei majengo; huu ni ufananisho unaoendana vizuri kabisa na Masiha.

S: Kwenye Rum 10:12, je, ni kweli kwamba "‘Bwana' anayeongelewa hapa hawezi kutambuliwa kwa uhakika kutoka kwenye muktadha huu" kama Mashahidi wa Yehova walivyofundisha (Wachtower 2/1/1977 uk.95)?

J: Hapana 1 Kor 12:4-6, na mistari mingine mingi inaonesha kuwa Yesu Kristo ndiye anayeongelewa.

S: Kwenye Rum 10:13, je ni kweli kuwa tunatakiwa kuita jina "Yehova" ili tuweze kuokolewa kama Mashahidi wa Yehova wanavyofundisha?

J: Hapana. Badala yake yatupasa kumwita Mungu wa kweli na aliye hai. Waisraeli wa kale hawakuwa na neno "Yehova," kama ambavyo hawakuwa na herufi yenye kutamkwa "J." Je kutokuwa na herufi yenye kutamkwa "J" kunamaanisha kuwa watakatifu wote wa kwenye Agano la Kale hawakumwabudu Mungu wa kweli? Na bila shaka wazo hilo ni la kijinga. Mungu anataka zaidi mioyo yetu, na maneno na matendo yanayobubujika kutoka mioyoni mwetu, kuliko jinsi tunavyotamka.

S: Kwenye Rum 10:13, je mtu anaweza kumpokea Yesu kuwa Mwokozi lakini si Bwana?

J: Hapana. Kwa bahati mbaya watu wengine wanadai tunapaswa kumpokea Yesu kuwa Mwokozi tu, na kumpokea kuwa Bwana ni sehemu ya pili. Upande mmoja wa hoja hii unasema kuwa ubwana wa Yesu ni jambo la hiari. Upande wa pili unaofuatwa na Complete Book of Bible Answers, uk.190, hausemi kuwa ubwana wa Yesu ni jambo ambalo mtu ana hiari ya kulichagua bali unasema kuwa kujitoa kwa Yesu si uamuzi ambao watu wasioamini wanatakiwa kuelezwa kuufanya kabla ya kuupokea wokovu, kama kulivyo kumpokea Yesu kuwa Mwokozi [kunavyoelekea]. Kumkubali Yesu kuwa Bwana kunakuja polepole kadri muumini anavyoenenda naye.
Kwenye Now That's a Good Question, uk.122-123, R.C. Sproul anaeleza kuwa kuokolewa bila kumpokea Yesu kuwa Bwana ni kupotosha injili ya kweli kunakoitwa antinomia (mafundisho kuwa watu waliookolewa na Yesu wameondolewa wajibu kutimiza sheria ya maadili). Wakalvinisti wanadai kuwa Zane Hodges na Charles Ryrie wanafuata mafundisho haya.
Hata hivyo Yesu alikanusha mafundisho haya ya antinomia kwenye Mat 7:21-28 na Yoh 14:21-24. Kwa kifupi, watu wanaompenda Yesu watayatii mafundisho yake, na watu wasiompenda Yesu hawatayatii mafundisho yake. Pia kwenye Kol 2:6, Biblia inasema, "Basi kama mlivyompokea Kristo Yesu, Bwana." Kwenye kifungu hiki, Biblia haiongelei watu wanaojaribu kumpokea Yesu kuwa Mwokozi na si kuwa Bwana.

S: Kwenye Rum 10:13, ikiwa kila mtu anayemwita Bwana ataokoka, je unawezaje kujua kuwa ulipomwita Mungu akuokoe ulifanya hivyo kwa moyo wote?

J: Hebu tujiulize swali rahisi zaidi kama mfano. Je unajuaje kuwa ulikusudia kula chakula cha mchana jana?
1. Je ulikula chakula hicho kwa bahati mbaya au kwa kukusudia?
2. Je hukujua kuwa ulitaka kula chakula cha mchana kabla ya kukila?
3. Je kuna mtu yoyote aliyekuwa anakuslazimisha kula chakula, badala ya kufanya ambacho ulitaka ukifanye kwa hiari yako mwenyewe?
Kama ulikula chakula cha mchana jana, na majibu kwa maswali matatu yaliyotangulia yalikuwa "hapana," basi ulikusudia kula chakula cha mchana.
Kwa namna hiyo hiyo, kumwitia Bwana si jambo gumu, kama kufaulu mtihani. Ikiwa umemwitia Yesu kwa kukusudia, unajua kitu ulichokuwa unafanya, haukulazimishwa, na ulipenda kufanya hivyo kwa hiari, hivyo kama ulimwitia Yesu akuokoe, kwa hakika ulimwitia Yesu akuokoe.

S: Kwenye Rum 10:14-15, je mtu yeyote anaweza kwenda mbinguni hata kama hawakuwahi kuisikia Injili?

J: Kuna watu waliokwisha kwenda kabla ya kuisikia injili. Kama uthibitisho, Henoko, Ibrahimu, Ayubu, na waumini wengine kwenye Agano la Kale waliyafuata mambo ambayo Mungu aliwafunulia, lakini hawakusikia mambo ambayo kwao yalikuwa ni siri ya Agano Jipya.
Kumbuka, hatima ya yote, Mungu ndiye aokoaye, si injili, na si itikio letu la injili. Tazama pia swali lifuatalo kwa maelezo zaidi.

S: Kwenye Rum 10:14-15, je kuna mtu yoyote anayeweza kwenda mbinguni ikiwa hajawahi kuisikia injili, baada ya Yesu kufufuka kutoka kwa wafu?
Wengine hawakubali.
Lakini hii haimaanishi kuwa hawakuwa na fursa. Ikiwa mtu ambaye hakuwahi kusikia injili ataifuata kweli anayoijua na kumwitikia Roho Mtakatifu ambaye anafanya kazi maishani mwake, Mungu anaweza kuhamisha mbingu na dunia ili kumletea kweli. Mungu kwa neema yake anaweza kumfanya Mkristo aje na kuwaeleza habari njema ya Kristo. Mfano mmojawapo kwa jinsi hii ni kwenye Mdo 10:2, 22, 31 ni Mrumi aliyemcha Mungu aliyeitwa Kornelio, aliyekuwa mwenye haki, mwombaji, na mwenye kuwasaidia wahitaji. Mungu alimtuma malaika kumwambia Kornelio atume watu wamwite Petro.

Wengine hawakubaliani kabisa.
Ingawa 2 The 1:8 inasema kuwa watu ambao hawaitii injili ya Yesu wataadhibiwa kwa maangamizi ya milele, Rum 4:15 na 5:12 zinasema kuwa dhambi haihesabiwi mahali pasipokuwa na sheria. Ingawa Maandiko hayasemi kuwa watu wana nafasi ya kutubu baada ya kifo, au wakati wa Milenia (miaka elfu moja ya utawala wa Yesu hapa duniani). Angalia ufafanuzi wa 1 Pet 3:19 (maswali mawili) na 1 Pet 4:6 kuhusu Yesu kuhubiri injili kwa wafu. Angalia ufafanuzi wa Ufunuo 20 kuhusu fursa za kutubu zinazoweza kuwepo wakati wa milenia. Mwishoni, kwa Mungu ndiye mwenye kuokoa watu, anaweza kuwafanya watoto wadogo au mtu yoyote mwingine kwenda mbinguni bila kuisikia injili, ikiwa anapenda kufanya hivyo.
Jambo la muhimu zaidi
kuhusiana na ujumbe wa Rum 10:14, inayosema watu hawawezi kumwita Mungu bila kumwamini, hawawezi kuamini bial kusikia, na hawawezi kusikia, na hawawezi kusikia bila ya muhubiri. Kama jambo hili lingekuwa sanjari na Rum 10:13, aya hii ingesema kuwa hakuna mtu ambaye angeokolewa bila kumwita Mungu; hata hivyo, Rum 10:13 haiko sanjari. Badala yake, inasema tu, "Kila atakayeliita jina ka Bwana ataokoka."
Rum 10:13-14 haitoi sababu yoyote ile ya nguvu kusema kuwa mtu yoyote mzima ambaye hakujua kumwita Bwana atakwenda jehanamu.

S: Kwenye Rum 11:17-24, je tunajua kitu gani kuhusu ukuzaji wa mzeituni?

J: Mizeituni ilikuwa miti ya thamani sana, lakini ilihitaji kazi kubwa. Wakati wa vita, Waisraeli hawakuruhusiwa kukata mizeituni kwenye Kum 20:19-20, na hivyo kupunguza uwingi wa chakula nchini angalau kwa miaka 20. Jambo hili pia linaweka wazi ni kwa nini kukata mizeituni kulikuwa janga kwenye Hab 3:17 na Kum 28:40.
Wycliffe Bible Dictionary,
uk.1366-1367, ina sehemu inayoelezea kwa undani ukuzaji wa mizeituni. Kwenye hitimisho inasema, "Mizeituni ilikuzwa kutokana na vipande vilivyopandikizwa kwenye tawi la mti pori uliozeeka wakati machipukizi yakiwa na urefu wa karibu mita moja (futi tatu). Pia machipukizi mapya yanaweza kuchipua kutoka kwenye mizizi au kisiki cha mti mama uliozeeka (Zab 128:3; Isa 11:1). Hapawi na matunda kwa miaka mitatu hadi minne, na hakuwi na mavuno mengi kwa miaka 17 hadi 18. Muda wote huu mzeituni unahitaji uangalizi wa makini, udongo unatakiwa kutifuliwa na kuwekwa mbolea wakati wa majira ya kuchipua na kumwagiliwa kwa uaminifu . . . na kuangaliwa ipasavyo, mzeituni wenye ukubwa kamili utatoa nusu tani ya mafuta kwa mwaka na kuendelea hadi utakapofikia umri wa kushangaza" (New International Bible Dictionary, uk.802 na Encyclopedia Britannica 1972 juzuu ya 16, uk.936 zina picha za miti za mizeituni zenye umri wa miaka 1,000. Kama ningekuwa mti ningependa kuwa mzeituni, wenye nguvu, unaojikinga dhidi ya wadudu, na kuishi miaka elfu moja!

S: Kwenye Rum 11:17-24, ni kwa nini mtu apandikize matawi ya mzeituni mwitu kwenye mzeituni wa kupandwa?

J: Kwa kawaida watu wanapenda kufanya kinyume chake. Watu wanapenda kuwa na mti pori wa matunda, wenye kuweza kustahimili baridi kali, ukipandikizwa na matawi ya miti ya kupandwa itoayo matunda yapendezayo. Kuna mambo matano ya kuzingatia katika kujibu swali hili.
1.
Paulo alikuwa anatoa mfano. Hakuwa anawaelekeza watu jinsi ya kulima mizeituni, bali alitoa mfano wa jinsi ambavyo watu wa mataifa walivyopandikizwa. Kama Wycliffe Bible Dictionary, uk.726 inavyosema, "Kugeuzwa huku kwa mpangilio wa maneno kunaongeza msisimko wa lugha ya picha inayowasilisha kweli ya milele ya kukataa kwa taifa la Israeli, na muundo wa Israeli ya kweli -waumini wote."
2.
Mimea mingi haijapandikizwa kabisa. Mara nyingi watu hupandikiza tawi la mti wa kupandwa ikiwa litakuwa dhaifu, limeshambuliwa na wadudu, au ugonjwa. Paulo anasema bayana kuwa matawi haya yalikatwa kwa sababu ya kutoamini kwenye Rum 11:20.
3.
Kulinganishwa kwa Waisraeli na mzeituni kulikuwa tayari kunafahamika kwao, kwenye Yer 11:16 na Hos 14:6. Hivyo, ulinganisho huu kwa kutumia muda, mizizi ikiwa wahenga wa mti wa vizazi vya kwenye mti wa familia, wtu wa mataifa ndio waliopandikizwa, na si kinyume chake.
4.
Kama Paulo angesema kuwa Wayahudi walikuwa mzizi wa mzeituni pori, na watu wa mataifa matawi ya mti wa kupandwa, basi watu wa mataifa wangeweza kufikiri kuwa Mungu aliwapandikiza kwa sababu Mungu alihitaji sifa zenye kutamanika ndani yao, kilinganisha na kuwa jambo hili lote lilikuwa neema. Zaidi ya hayo, si watu wa mataifa waliokuwa wamepandwa bali Wayahudi.
5.
Kama ulinganishi uliotumika ungekuwa watu wa mataifa kuwa mzizi pori na Waisraeli matawi ya mti uliopandwa, jambo hili lingekuwa kinyume kwa kiasi kikubwa sana. Watu wa mataifa walipandikizwa kwa wateule wa Mungu, na si kinyume chake.
Kuna watu wanaosema kuwa matawi ya miti ya porini wakati mwingine hupandikizwa kwenye miti ya kupandwa ili kuipa nguvu. Inavyoonekana, ikiwa matawi yote yangekuwa ya miti ya kupandwa, mizeituni isingekuwa inakua kiasi kikubwa. Hata hivyo, wengine wanasema kuwa jambo hili huwahalifanyiki. Pamoja na haya yote, Paulo alitumia mpangilio huu ili kufundisha kuhusu kukatwa kwa Israeli na kupandikizwa kwa watu wa mataifa, na si kilimo cha miti. Paulo anaweza kuwa alimaanisha jambo hili pia kwenye Rum 11:24 aliposema kuwa kupandikizwa kwa tawi la porini kwenye shina la mti wa kupandwa kulikuwa "kiyume cha asili."
Hitimisho:
Paulo anatuambia bayana ni kwa nini Waisraeli ndio waliokuwa shina kwenye ulinganishi huu. Kwenye Rum 11:18, Paulo anawaagiza kukumbuka kuwa si wao (watu wa mataifa) wenye kuutegemeza mzizi bali mzizi unawategemeza wao.

S: Kwenye Rum 11:20, vitu gani ni miongoni mwa vizuizi vya Wayahudi kumzalia Mungu matunda?

J: Walikuwa hawana imani. Na kwa kuongezea walisumbuliwa na kutokuamini. Pamoja na hilo, walipungukiwa upendo kwa watu waliopotea (kama Yona).
Kuabudu sanamu na dhambi nyingine hadi wakati wa kupelekwa uhamishoni (Hos 9:10).
Kutolifurahia neno la Mungu (Yer 6:10).
Kuzongwa na mahangaiko ya ya ulimwengu huu, kama kwenye aina ya tatu ya udongo (Mat 13:23).
Kulifanya neno la Mungu kuwa kama mpangilio tu wa sheria za jinsi ya kuishi.
Kusahau haja ya kuishi kwa saburi (Ebr 10:23, 32-35).
Kusahau maagizo ya kuwafundisha watoto wo (Kum 6:4).

S: Kwenye Rum 11:22, inawezekanaje Mungu awe mkali na mpole, bila kujipinga mwenyewe?

J: Hapa duniani, askari polisi anaweza kuwa mpole kwa kumsaidia mgeni anayehitaji msaada. Askari huyo huyo anaweza kuwa mkali kwa kumpiga risasi mwuaji anayejaribu kumwua mtu mwingine. Ikiwa mwanadamu anaweza kuwa mpole na mkali, hupaswi kupata shida kuelewa kuwa Mungu anaweza kuwa hivyo hivyo. Kama ambavyo Hank Hanegraaff wa Christian Research Institute anavyosema, "Utakatifu wake hauwezi kufifishwa, lakini rehema zake hazizuiliwi." Tazama ufafanuzi wa Rum 13:10 kwa maelezo zaidi kuhusu ni jinsi gani Mkristo anaweza kuwa askari polisi.

S: Kwenye Rum 11:25, "utimilifu wa mataifa" unamaanisha nini?

J: Maneno haya yanamaanisha kuwa Israeli iliondolewa sifa ya kuwa watu wa Mungu mpaka wakati ambapo watu wa mataifa watakaoamini watakapoingia kwenye ufalme wa Mungu.

S: Kwenye Rum 11:26, je Waisraeli wote watakwenda mbinguni?

J: Hapana kulingana na Yoh 8:24 na Mat 23:33. Tazama ufafanuzi wa Rum 9:8-9, 27 kupata jibu la swali hili.

S: Kwenye Rum 11:26-27, je Mungu bado atatimiza baadhi ya ahadi kwa wana wa Waisraeli kwa jinsi ya kimwili siku zijazo?

J: Hii ni moja ya tofauti za msingi kati ya Wakristo wanaofuata theolojia ya agano (inayoitafsiri Biblia kupitia maagano ambayo Mungu amefanya na wanadamu), na Wakristo wanaofuata theolojia ya dispensheni (inayoamini kuwa Mungu hutumia njia maalumu katika kushughulika na watu kwenye kipindi husika cha historia ya wokovu).
Wanatheolojia wa mlengo wa agano wanakataa.
Ahadi zote za wakati ujao zitatimizwa si kwa Israeli ya kimwili lakini kwa Israeli ya kiroho, yaani kanisa, linalojumuisha waumini wote wa kweli kutoka kwenye mataifa yote.
Wanatheolojia wa Kidispensheni wanakubali.
Ahadi nyingi zitatimizwa kwa Israeli ya kiroho, lakini Israeli ya kimwili bado itairithi nchi ya Palestina milele. Watu 144,000 kwenye Ufunuo 7 na 14 wanatoka katika kabila za Israeli.

S: Kwenye Rum 11:32, ni kwa namna gani Mungu amewafunga watu wote kwenye uasi?

J: Mungu hakutupilia mbali viwango vyake vya haki au kushusha viwango vya ukamilifu ili kuingia mbinguni. Badala yake, Mungu ameurehemu uasi wao kupitia kwa Yesu, damu yake msalabani.
Jambo hili linaweza kufanana na ukweli kuwa Mungu aliumba viumbe wa aina zisizopungua tano:
Wasiojua mema na mabaya: wanyama
Wasio na kubaki hivyo: malaika wa madaraja mbalimbali
Wasio na dhambi kuwa wameanguka: mapepo
Walioanguka kuwa wasio na dhambi: wateule
Walioanguka na kubaki hivyo: wapotofu Rum 11:32 inaonyesha kuwa watu wote, isipokuwa Adamu, Hawa, na Yesu, wamo kwenye makundi mawili ya mwisho.

S: Kwenye Rum 12:1, tunajitoaje kafara kwa ajili ya Mungu?

J: Rum 12:1 haisemi kuwa tunapaswa kuwa kafara iliyouawa au kuchomwa, bali dhabihu iliyo hai. Ni kweli, dhabihu iliyo hai inaweza kutaka kutambaa na kutoka madhabahuni, na hatupaswi kufanya hivyo.

S: Kwenye Rum 12:6-8, kwa nini orodha ya karama ni tofauti na ile ya kwenye 1 Kor 12:7-11; 13:8 na Efe 4:7-13?

J: Ni jambo jema kuwa karama zilizoorodheshwa ni tofauti. Kama zingefanana, watu wangeweza kudhani kuwa hii orodha kamilifu ya karama, na kwamba hakuna karama zozote ambazo hazimo kwenye orodha hiyo. Orodha hizi zimetolewa kama mifano ya aina za karama. Mungu ana uhuru wa kutoa karama zaidi, na hata aina zaidi za karama kama apendavyo na kama kanisa linavyohitaji.

S: Kwenye Rum 12:13; 1 Tim 5:10 na Mat 25:35-45, Biblia inasema nini kuhusu kukarimu watu wengine?

J: Kwanza tuangalie amri za Biblia kwa ujumla kisha ufafanuzi wa amri hiyo.
Amri Chanya:
Rum 12:13 na 1 Tim 5:10 zinatuambia tuwe wakarimu; hili ni jambo la kufanya kwa Wakristo na wasio Wakristo pia. Kwenye Mat 25:35-45, Yesu alisema ukimpa mtu chakula, maji ya kunywa, nguo, au ukiwasaidia maskini, wageni, wagonjwa, au wafungwa, utakuwa umemfanyia yeye. Ebr 13:2 pia inasema kuna watu waliowakaribisha malaika pasipo kujua.
Mifano Hasi:
Ayu 31:32 inasema kuwa kutokumkarimia mgeni ni dhambi. Miongoni mwa dhambi nyingine, watu wa Sodoma na Gomora hawakukarimia wengine kwenye Eze 16:49.
Ufafanuzi:
Kwenye 2 Yohana 9-11, Biblia inasema kuwa watu wanaoeneza mafundisho potofu hawapaswi kukarimiwa. Pia 1 Kor 4:11-13 inasema hatupaswi kushirikiana na mtu yoyote anayejiita ndugu (muumini) lakini anaishi maisha ya uovu.
Mwandishi toka kanisa la Awali
Clement wa Rumi (mwaka 96/98 BK) atakuwa alifikiri kuwa ukarimu ni wa muhimu kwa sababu alitoa mifano minne.

S: Kwenye Rum 12:20 na Zab 25:21-22, kumpalia makaa mtu kichwani pake kunamaanisha nini?

J: Wakristo kuanzia kwa Chrysostom hadi nyakati za leo wametafsiri maneno haya bila kupingana wakisema Wakristo hawatakiwi kulipa kisasi. Hata hivyo, kuna maoni manne kuhusu maana ya kupalia makaa ya moto kichwani.
Kuonyesha kukosa mantiki kwa adui:
John Chrysostom kwenye Epistle to the Romans mahubiri ya 22 juzuu ya 11, uk.509 anasema kuwa kicheko cha fadhili na upole cha Mkristo anapokuwa ametukanwa kinaonyesha kutokuwepo kwa uadui na ujinga na kutohitajika kwa mashitaka ya adui.
Kusaidia Kujutia Maovu:
Ukiwa mwema kwa adui zako kutawafanya wajihisi aibu na kuwathibitishia hatia wanapotambua kuwa watenda maovu dhidi yako nawe unawatendea upendo. Kamusi iitwayo New Bible Dictionary (Eerdmans' 1962, uk.242) na tafsiri ya Biblia iitwayo Geneva Study Bible zinasema kuwa makaa ya moto kwenye Rum 12:20 yanawakilisha aibu. Tafsiri ya Biblia iitwayo NIV Study Bible, uk.1726 inasema kuwa jambo hili linaweza kusaidia kumleta mtu kwenye toba.
Adhabu:
Zab 140:10 inasema kuwa makaa ya moto kumwangukia mtu kichwani ilikuwa ni adhabu ya watenda maovu. Kuwa mwema kwao kungewafanya wajisikie aibu na kumwachia Mungu kisasi. Tafsiri ya Biblia iitwayo NIV Study Bible, uk.981-982 na Bible Knowledge Commentary: Old Testament, uk.961 zinaongelea maoni haya.
Kusaidia Kujitakasa:
Kupalia makaa ya moto kunafanana na Mungu alivyoweka kaa la moto katika kinywa cha Isaya kwenye Isa 6:5-7. Kulikuwa na desturi ya zamani ya Kimisri ambapo mtu aliyefanya kosa au uovu alionyesha kujuta kwake kwa kubeba karai la makaa ya moto kichani pake. Hata hivyo, jambo hili lilionyesha aibu, si kwamba wema wetu unatakasa dhambi ya mtu kwa namna fulani.
Msaada wa Jumla:
Maoni ya nne ambayo watu wengine wanayashikilia ni kuwa nyakati za kale wakati moto wa mtu umezimika, alizunguka kijijini akiwa na kikapu kichani, na majirani waliweka kila mmoja kaa moja la moto hata pangekuwa na makaa ya kutosha kuwasha moto. Hata hivyo, sijaona kazi yoyote inayosema kuwa zamani za kale watu walibeba masufuria vichwani mwao kwa kusudi hili. Inaonekana kuwa kaa moja la moto lingezimika kabla ya kuongeza makaa mengine.

S: Kwenye Rum 13:1-6 na 1 Pet 2:13-14, ni kwa jinsi gani tunapaswa kuzitii mamlaka?

J: Tunapaswa kutii na kuheshimu makusudio na maagizo halisi ya sheria. Tunapaswa kuepuka kutenda maovu, na kutokuwa na muonekano wa uovu (2 Kor 8:20-21; 1 The 5:22). Hata hivyo, sheria za kitaifa ziko juu ya sheria za kijimbo, sheria za Mungu ziko juu ya sheria za mataifa. Tunapaswa kutokuzitii sheria zozote za nchi zinazopingana na sheria ya Mungu.

S: Kwenye Rum 13:1-2, Mungu anatuambia, "Kila mtu na aitii mamlaka iliyo kuu; kwa maana hakuna mamlaka isiyotoka kwa Mungu; na ile iliyopo umeamriwa na Mungu. Hivyo amwasiye mwenye mamlaka hushindana na agizo la Mungu; nao washindanao watajipatia hukumu." Je agizo hili linamaanisha kuwa serikali kama zilizoongozwa na Hitler, Stalin, Pol Pot n.k. zilitoka kwa Mungu na watu hawakutakiwa kuzipinga? Napata shida kuliamini jambo hili. Nitafurahi kupata maelezo kuhusu jambo hili.

J: Hebu nitoe jibu fupi kwanza, kisha jibu refu. Kwa kifupi, Hapana, hatupaswi kutii amri zilizo kinyume na amri za Mungu (kama vile usiue, n.k.). Stalin, Pol Pot, Hitler, n.k. walikuwa watu waovu, ambao Mungu aliwaruhusu kutawala. Lakini kumbuka Biblia inamtaja "mfalme" wa ulimwengu huu, ndiye Shetani. Ingawa watu hao ni waovu, tunapaswa kuheshimu mamlaka ya serikali, kwa kiwango ambacho haipingani na mamlaka ya Mungu.
Wakristo wa kwanza walipambana na jambo hili, kwa sababu serikali ya Kirumi iliwaamuru, kwa kuwatishia mateso na kifo, kumtolea sadaka mfalme na kumwabudu au kuiabudu miungu ya Kirumi. Walifahamu kuwa wanapaswa kutii sheria zote za Kirumi isipokuwa pale zilipopingana na sheria ya juu zaidi, sheria ya Mungu mwenyewe. Namna walivyoliweka jambo hili ni kuwa kulikuwa na sheria "halali," na "zisizo halali," kitu ambacho kwenye Kigiriki ni kama kuleta utani mbele ya kifo kwa kuchezea maneno. Kwa hiyo, ingawa walitakiwa kutokutii sheria zilizowataka kutoa sadaka kwa miungu mingine, walijua kuwa walipaswa kutii sheria nyingine ambazo zilikuwa zinaendana, au angalau hazikupingana na sheria ya Mungu. 
Hebu tufanye kama tunaishi miaka ya 1940 wakati wa utawala wa Nazi wa Ujerumani. Hapana shaka kuwa Hitler alikuwa mwovu, na amri za kuwapeleka Wayahudi kwa serikali yake hatukupaswi kuitii. Lakini bado tungetakiwa kuzitii sheria za usalama barabarani, na (kwa bahati mbaya) kulipa kodi za mapato.
Jambo hili lingekuwa tata zaidi ikiwa tungeitwa kutumika jeshini. Nilisoma sehemu nyingine kuwa ilikuwa dhahiri kwa Mjerumani wa kawaida kuwa Wayahudi wengi walikuwa wanakwenda kwenye kambi (za mateso), lakini hakuna aliyekuwa anarudi, na hewa kwenye makambi hayo ilikuwa ina harufu ya nyama ya watu. Kama tungejiunga na jeshi tungejiona kuwa tumo kwenye jeshi ovu, na ama tujisalimishe kwenye majeshi ya muungano mara nafasi inapotokea, au, vema zaidi, tuwe walinzi wa wafungwa, na kuwaacha Wayahudi watoroke. Kulikuwa na afisa wa jeshi la Nazi aliyeitwa Oskar Schindler, ambaye ni askari pekee wa Nazi anayeheshimiwa Israeli. Alijionea mwenyewe mambo yaliyokuwa yanatokea kwenye kambi za mateso, na alijitahidi kuwaokoa Wayahudi wengi zaidi kadri alivyoweza. Kuna filamu maarufu sana kuhusu yeye inayoitwa Schindler's List. Jambo lisililojulikana sana ni kuwa kulikuwa mwanachama wa pili wa chama cha Nazi aliyefanya kazi nchini China aliyeitwa John Rabe, ambaye pia alifanya kila aliloweza kuokoa maisha ya Wachina huko Nanjing na sehemu zingine.

S: Kwenye Rum 13:1-2, 4, mwandishi mwenye kushuku Bart Ehrman anauliza ikiwa Wakristo walitakiwa kutii mamlaka (ya Kirumi) iliyokuwa inatawala, au mamlaka ya Kirumi ilijawa maovu na ufisadi kwenye Ufu 17:18 (Jesus, Interrupted, uk.97-98).

J: Nilimwuuliza binti yangu mwenye umri wa miaka 14 swali hili, na aliweza kuliona jibu wazi kabisa: mambo haya yote mawili ni kweli. Paulo aliishi wakati wa mmoja wa wafalme waovu na wenye kuchukiza zaidi wa Kirumi: Nero. Paulo angeweza kujua katika muda alioishi jinsi ambavyo mfalme wa Kirumi alivyokuwa mwovu; hakuwa na haja ya kungoja hadi kitabu cha Ufunuo wa Yohana kiandikwe (karibu miaka 50 baada ya kuuawa kwake kama shahidi wa imani) kujua kuwa mamlaka zilizokuwa zinatawala zilijawa na maovu mengi sana. Hata hivyo, Paulo anatufundisha kutii mamlaka zinazotawala. Wakristo wa awali walitii mamlaka zilizokuwa zinatawala, isipokuwa wakati amri zao zilikwenda kinyume na amri za juu zaidi za Mungu.

S: Kwenye Rum 13:7, ni kwa jinsi gani maafisa wa serikali Kirumi waliokuwa wapagani na mafisadi walikuwa watumishi wa Mungu?

J: Serikali ya Kirumi wakati wa Paulo ilikuwa fisadi kupita kiasi. Watu walijilimbizia mali kwa kuwa magavana wa majimbo kama vile Sicily. Watu hawa hawakuwa watumishi wa Mungu ama kwa kuchagua kutokana na dhamira zao ama kwa uadilifu wa mienendo yao. Badala yake, walikuwa watumishi wa Mungu kwa namna moja (na hiyo tu) kwamba kwa kuwa walikuwa serikali halisi, na Wakristo walitakiwa kuwatii ili mradi hawapingami na sheria za Mungu. Kwa jumla, Wakristo wa awali walikuwa wanatii sheria sana, isipokuwa walikataa kumwabudu Mfalme wa Kirumi pamoja na kumwabudu Kristo. Kwa sababu hii, makumi ya maelfu yao waliuawa kwa ajili ya imani yao.
S: Kwenye Rum 13:8, kwa nini Wakristo huwa na deni?

J: Rum 13:8 haisemi kutokuwa na deni kabisa, bali kutokuacha deni liendelee kuwepo, isipokuwa kupendana ndugu na ndugu. Kwa maneno mengine, sehemu ya kwanza ya mstari huu inasema tunaweza kuwa na deni, lakini tunapaswa kulipa madeni yetu. Wakati mwingine sheria za ajabu na zisizo za kawaida zinaweza kumweka huru mtu kutokana na masharti ya kisheria ya kulipa deni halali. Hata hivyo, bila kujali sheria za ajabu ajabu za kibinadamu, bado tunapaswa kumtii Mungu.

S: Kwenye Rum 13:9-10, je kumpenda jirani yako kama nafsi yako kunajulisha sheria yote? Vipi kuhusu kumpenda Mungu pia, kama Mak 12:29-30 inavyosema?

J: Hapa Paulo almezitaja amri kuu nne kati ya kumi. Ni kweli kuwa amri tano na nusu za mwisho zinaweza kuelezwa kuwa ujumla kama "mpende jirani yako kama nafsi yako." Amri nne na nusu za kwanza zinaweza kuelezwa kwa ujumla kama "mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa nguvu zako zote." Hivyo tunaweza kusema kuwa "mpende jirani yako kama nafsi yako" inaelezea kwa ujumla sheria zote zinazohusu mahusiano ya waumini na watu wengine.
Jambo la pili ni kuwa ni vigumu kuwa na nguvu za kumpenda kwa kweli jirani yako kiroho, kihisia, kifedha, na kwa namna nyingine zote, kama humpendi Mungu kwanza.

S: Kwenye Rum 13:10, kwa kuwa hatupaswi kuwa na nia mbaya dhidi ya majirani zetu, je muumini anaweza kuwa askari polisi na kuwatia watu nguvuni?

J: Ndiyo. Kwa sababu ya upendo kwa watu wengine, kwa ajili ya jamii, na kwa ajili ya kutekeleza sheria dhidi ya watenda mabaya, askari polisi aliye muumini anaweza kuwatia watu nguvuni watu, na kutumia nguvi kama itakuwa muhimu kufanya hivyo. Hata hivyo, wanapaswa kufanya hivyo bila chuki, kijicho, hasira, au nia mbaya wivu dhidi ya mkosaji. Polisi mzuri hapaswi kuwa na fikra ya kuwa yuko juu ya sheria, au kwamba aangaliwe kwa namna maalumu na watu wengine.


S: Kwenye Rum 13:11-14, kifungu hiki kina umuhimu gani?

J: Watu wanaweza kuchagua kuishi jinsi yoyote wanayopenda. Hata hivyo, Rum 14:12 inasema kuwa watatoa hesabu ya jinsi walivyoishi. Kwa kuwa hatujui mwisho wa maisha yetu hapa duniani utakuja lini, Rum 13:11-12 inatueleza umuhimu wa kuamka na kuitambua hali halisi ya mambo yaliyopo.
Kama maelezo ya ziada, Augustine wa Hippo (mwaka 388-430 BK) alisema kuwa Rum 13:14 ilisaida kumfanya amgeukie Mungu. Kabla ya kumwamii Kristo, Augustine alikuwa anaikishi na hawala yake aliyekuwa amezaa naye mtoto wa kiume.

S: Kwenye Rum 14:2, 14, 17, 20-21, ikiwa Wakristo wa madehebu ya Katoliki na Orthodox watajiepusha kula nyama zisizokuwa za samali kwenye kipindi cha Kwaresima, je Wakristo wengine wote wanapaswa kufanya hivi hivi ili kuepuka kuwakwaza ndugu waliodhaifu? Vile vile kama Wakristo wengine wanaokataza kutumia pombe, je Wakristo wote wanapaswa kujiepusha nayo?

J: Ufuatao ni muhtasari wa mambo unayotakiwa kufanya.
1.
Fanya jambo unaloamini kuwa ni sahihi, lakini usiwadharau waumini wengine wanaofanya tofauti na wewe.
2.
Usiache kitu unachoamini kisemwe vibaya na watu wengine, kama hakijakatazwa na Biblia. (Angalia Kol 2:16-20).
3.
Ikiwa muumini mwingine atakukumbusha swala hili, mweleze kuwa ni sawa kulifanya, ila mwambie kuwa kama hivi ndivyo anavyoamini, hautalifanya mbele yake.
Ni muhimu kufanya jambo la 2 na 3 kwa pamoja. Kama hautalifanya wakati huo, watu wanaweza kudhani kuwa umekubali kutokufanya hivyo tena. Watapokuja kufahamu kuwa umefanya tena wakati hawapo, litatoa sura ya unafiki. Hivyo jiepushe kulifanya mbele zao, lakini wafahamishe kuwa bado unaamini kuwa ni sahihi na haumaanishi kuwa utaacha kabisa kulitenda.

S: Kwenye Rum 14:5, je inaruhusiwa kufanya kazi Jumamosi au Jumapili, au hairuhusiwi?

J: Wakristo wa kweli, wakati ule wa zamani na wakati wa sasa, hawaafikiani. Tazama ufafanuzi wa Kut 20:8 ili kupata jibu. Paulo aliagiza kufanya changizo kwa ajili ya Wakristo wa Yerusalemu waliokuwa na shida siku ya kwanza ya juma kwenye 1 Kor 16:2. Wakristo wa awali waliabudu siku ya Jumapili, kwa mujibu wa kumbukumbu zifuatazo:
Letter of Ignatius to the Magnesians
sura ya 9, uk.62 (mwaka 106-117 BK) "Tukiacha kuendelea kushika Sabato, bali kuishi katika kuishika Siku ya Bwana, ambayo ndani mwake maisha yetu pia yaliletwa naye kupitia kifo chake."
Letter of Ignatius to the Ephesians
sura ya 5, uk.51 (mwaka -107/116 BK) "Kwa hiyo, mtu asiyekusanyika pamoja na kanisa, amedhihirisha kiburi chake kwa kufanya hivi, na kujihukumu mwenyewe."
Didache
(Teaching of the Twelve Apostles) [karibu mwaka 125 BK) sura ya 14, uk.381 (Inaonyesha bila kutaja) "Lakini kila siku ya Bwana, kusanyikeni pamoja, na kuumega mkate, na kushukuru baada ya kuwa mmeungama makosa yenu, ili sadaka yenu iwe safi."
Letter of Barnabas
sura ya 10, uk.143 (mwaka 100-150 BK) [kwa kudokeza] inasema kuwa Wakristo wanaadhimisha "siku ya nane" [yaani Jumapili] kwa sababu hiyo ndiyo siku ambayo Yesu alifufuka kutoka kwa wafu. Kisha alipaa mbinguni.
Justin Martyr
(karibu mwaka 150 BK) "Lakini jumapili ni siku ambapo sisi sote hukusanyika kwa pamoja, kwa sababu ni siku ya kwanza ambapo Mungu, baada ya kubadilisha giza na mada, aliuumba ulimwengu; na Yesu Kristo Mwokozi wetu siku iyo hiyo alifufuka kutoka kwa wafu. Kwa kuwa alisulibiwa siku moja kabla ya Saturn (jumamosi); na siku moja baada ya Saturn, ambayo ndiyo siku ya jua, alitokea kwa mitume na wanafunzi wake, na kuwafundisha mambo haya, ambayo tumeyawasilisha kwako [Mfalme Adrian] pia il uyafikirie" (First Apology of Justin Martyr sura ya 67, uk.188).
Dionysius wa Korintho (mwaka 170 BK) [sehemu tu] "Tumepita siku hii takatifu ya Bwana, ambapo tulisoma barua yako, kutokana na kuisoma mara kwa mara tutaweza kupata maonyo, kama ilivyokuwa katika kuisoma ile ya kwanza uliyotutumia iliyoandikwa na Clement" (Kipande cha 2 juzuu ya 8, uk.765).
Irenaeus (mwaka 180-188 BK) [kwa mujibu wa taarifa toka kwa mtu mwingine) ametajwa kwenye kazi iliyopewa jina lake iitwayo Questions and Responses to Orthodoxy "Hii [desturi], ya kutopiga goti jumapili, ni ishara ya kufufuka, ambako kutokana nako tumewekwa huru, kwa neema ya Kristo, kutoka dhambini, na kutoka mautini, ambavyo vimefishwa chini yake. Sasa desturi hii ilianza tangia nyakati za mitume, kama mbarikiwa Irenaeus, mfia imani na askofu wa Lyons, anavyotangaza kwenye makala yake iitwayo On Easter, ambamo anaitaja pia Pentekoste; kwenye (sikukuu) hiyo hatupigi goti, kwani ina umuhimu sawa na siku ya Bwana, kwa sababu zilizokwisha elezwa kuhusiana nayo." (Maelezo chini ya ukurasa yanasema kuwa jumapili inayoongelewa hapa inaweza kuwa ni jumapili ya Pasaka (ANF juzuu ya 1 Fragments of Irenaeus kipande cha 7, uk.569-570).
Clement wa Alexandria (mwaka 193-202 BK) (kwa sehemu tu, siku ya Bwana ni siku ya nane) "Na siku ya Bwana Plato anaoingea kinabii kwenye kitabu cha kumi cha Republic, kwa maneno haya: ‘Na siku saba m kila mmoja wao kwenye uwanda, siku ya nane walipaswa kuanza safari na kuwasili baada ya siku nne'" (Stromata kitabu cha 5 sura ya 14, uk. 466).
Tertullian
(mwaka 200-220/240 BK) anasema kuwa wakati sikukuu za Kiyahudi zilikuwa Sabato na utakaso, Wakristo waliifanya jumapili kuwa siku yao ya kupumzika/sikukuu (Ad Nationes kitabu cha 2 sura ya 13, uk.123).
Origen
(mwaka 225-254 BK) "Lakini kama ingekuwa wazi kwenye Maandiko Matakatifu kuwa Mungu alishusha mana kutoka mbinguni kwenye siku ya Bwana, na hakushusha yoyote siku ya sabato, Wayahudi na waelewe kuwa tangu wakati huo siku ya Bwana wetu iliwekwa juu ya sabato ya kweli." (Homilies on Exodus, iliyotafsiriwa na Rufinus, aliyetafsiri kwa uhuru sana, hotuba 7 sura ya 5, uk. 308).
Cyprian wa Carthage (karibu mwaka 253-258 BK) [sehemu] "Kuhusiana na kuiadhimisha siku ya nane kwenye tohara ya mwili ya Kiyahudi, sakramenti hiyo ilikwishatolewa kwenye kivuli na matumizi yake; lakini Yesu alipokuja, ilitimizwa katika kweli. Kwa kuwa siku ya nane, yaani siku ya kwanza baada ya sabato, inapaswa kuwa siku ile Bwana atafufuka tena na inapaswa kutuhuisha, na kutupa tohara ya roho, siku ya nane, yaani siku ya kwanza baada ya Sabato, na siku ya Bwana, ilitimizwa kwa njia ya mfano; mfano ambao ulikoma wakati na kwa njia ya kuja kwa kweli, na tohara ya kiroho ilifanywa kwetu" (Letters of Cyprian barua ya 58 sura ya 4, uk.354).
Archelaus (mwaka 262-278 BK) [sehemu] aanaeleza jinsi Kristo anavyoizidi sabato kama Bwana wa sabato [The Disputation with Manes sura ya 42, uk.216).
Anatolius wa Alexandria (mwaka 270-280 BK) (sehemu) "Kufufuka kwa Bwana, kuliotokea kwenye siku ya Bwana, kutatuongoza kukusherehekea kwa kanuni hiyo hiyo; jambo hili linafaa lifanyike mwanzoni mwa Pasaka . . ." (Paschal Canon sura ya 16 juzuu ya 6, uk.151).
Victorinus wa Petau
(aliyeuawa kwa ajili ya imani yake mwaka 304 BK) "Katika siku hii pia, kwa sababu ya mateso ya Bwana Yesu Kristo, ama tunafanya kituo cha safari ya msalaba kwa ajili ya Mungu, au tunafunga. Siku ya saba Mungu alipumzika kutoka kwenye kazi zake zote, na akaibariki, na kuitakasa. Kwenye siku inayotangulia tumezoea kufunga kwa umakini wote, ili kwamba kwenye siku ya Bwana tuweze kuchukua mkate wetu huku tukitoa shukrani. Na jioni kabla ya sabato uwe mfungo mkali, ili tusije kuonekana kuwa tunaiadhimisha sabato yoyote pamoja na Wayahudi, ambayo Kristo mwenyewe, Bwana wa sabato, anasema kupitia manabii wake kuwa "Roho yake yachukia;" sabato ambayo aliitangua kwa mwili wake, japokuwa alikuwa amemwamuru Musa kuwa kutahiri kusivuke siku ya nane, siku ambayo mara kwa mara hutokea siku ya sabato, kama tunavyosoma jinsi ilivyoandikwa kwenye injili" (On the Creation of the World, uk.341-342).
Baraza la Elvira
(mwaka 306-307 BK) [kanuni 21 za maandiko zisizopingwa] "Mtu yoyote anayeishi kwenye mji hahudhurii ibada za kikanisani jumapili tatu mfululizo, na afukuzwe kwa muda mfupi ili kuifanya fedheha ifahamike" (Kanuni ya 21).
Petro wa Alexandria
(mwaka 306, 285-311 BK) anaongelea siku ya nne na kuwa Yesu aliteseka siku ya sita [ijumaa] kwa ajili yetu. Kisha anasema, "Lakini siku ya Bwana tunaisherehekea kama siku ya furaha, kwa sababu katika hiyo alifufuka, katika siku ambayo tumeipokea desturi kuwa hatutakiwi kupiga goti (The Canonical Epistle Kanuni ya 15, uk. 278).
Methodius (karibu mwaka 260-312 BK) [ameiongelea kwa sehemu siku ya nane] "Mwanawe mwenyewe kudhihirisha kwa manabii kuja kwake tena ulimwenguni katika mwili, ambapo furaha na ufahamu wa siku ya nane ya kiroho itahubiriwa . . . kabla ya kanisa kuposwa kwa Neno kutolewa kwa ahadi kwa Neno, kupokea uzao wa kimungu, na kutabiri tohara ya siku ya nane."
Miongoni mwa waasi na vitabu vya uongo

Muasi Bardaisan/Bardesan (mwaka 154-224-232 BK) anasema kuwa sisi [Wakristo] hukutana siku ya kwanza ya juma (Book of the Laws of Diverse Countries, uk.733).
Constitutions of the Holy Apostles
(karibu mwaka 375/390 BK) "Lakini ishikeni sabato na karamu ya siku ya Bwana; kwa sababu sabato ni kumbukumbu ya uumbaji, na siku ys Bwana inahusu kufufuka kwa Yesu" (Kitabu cha 7 sehemu ya 2.23, uk. 469).
Constitutions of the Holy Apostles
(karibu mwaka 375/390 BK) "Lakini kusanyikeni ninyi wenyewe kila siku, asubuhi na jioni, mkiimba zaburi na mkiiomba katika nyumba ya Bwana: asubuhi mkisema zaburi ya sitini na mbili, na jioni ya mia moja na arobaini, lakini hasa siku ya sabato. Na kwenye siku ya kufufuka kwa Bwana wetu, ambayo ndiyo siku ya Bwana[jumapili], kutaneni kwa bidii zaidi, pelekeni sifa kwa Mungu aliyeuumba ulimwengu kupitia kwa Yesu . . ." (Kitabu cha 2 sura ya 8.59, uk.423).
Mambo yaliyotofautiana na hili yalitajwa na Justin Martyr (aliyeandika karibu mwaka 138-165 BK) [Dialogue with Trypho ch.47], anawaita wanaotunza sabato "dhaifu wa imani," na Eusebius wa Kaisaria (mwaka 324 BK) anawaelezea waasi wa Ebioni kuwa watunza sabato.

S: Kwenye Rum 14:5, je Paulo alikuwa anaongelea sabato hapa?

J: Swali hili linahusisha vyote, sabato na siku takatifu za Kiyahudi. Wakristo wana maoni mawili. Paulo hakubainisha wazi sikukuu za Agano la Kale wala sabato. Paulo alitumia msemo wa jumla "siku maalum" alipoziongelea siku hizi mbili..
Kinyume cha maoni haya, wenye kutafsiri ya Biblia yenye mlengo wa Kikalvinisti, New Geneva Study Bible, uk.1791, wanafikiri kuwa Paulo alikuwa akiongelea siku takatifu za Kiyahudi. Inasema, "Kama angekuwa anaongelea sabato jambo la kawaida zaidi lingekuwa kusema, ‘Mtu mmoja anaichukulia sabato kuwa juu ya siku zingine."
Ni hoja inayohitaji kujadiliwa
kuongeza vizuizi kwenye maneno ya Rum 14:5, kwa sababu mahali pengine (Kol 2:16) Paulo anasema bayana kuwa hatupaswi kuwahukumu watu wengine "kwa sababu ya sikukuu au mwandamo wa mwezi, au sabato." Hivyo, Paulo aliowaongelea waumini wenye maoni tofauti na kutowahukumu watu wengine kwa sababu ya sikukuu na sabato.

S: Kwenye Rum 14:5, wakati Paulo alipopata fursa nzuri kabisa ya kuyapatia ufumbuzi malumbano kuhusu sabato, kwa nini alikataa kufanya hivyo?

J: Kwa sababu jambo ambalo Paulo alikuwa analiongelea lilikuwa muhimu kuliko maoni yetu kuhusu sabato. Ingawa Paulo alijibu kwa njia isiyokuwa ya moja kwa moja swali kuhusu chakula (Rum 14:14, 17, 20), wazo kuu la kifungu hiki si chakula wala sabato, bali mambo yafuatayo:
1.
Wakristo watiifu wanaweza kutofautiana kwenye mambo yasiyo na umuhimu, na jambo hili LINAKUBALIKA tu. Hatupaswi kuwadharau waumini wenye maoni tofauti na ya kwetu (Rum 14:1-4, 10-13).
2.
Usiache jambo ulifikiriyo kuwa jema kusemwa vibaya (Rum 14:16-17).
3.
Usiwe kikwazo kwa wengine. Kama unajua jambo fulani LINAKUBALIKA, linaweza kuwa dhambi kwa ndugu walio dhaifu, ambao hawalifanya kwa imani (Rum 14:13-15, 20-21, 23).
Tazama pia ufafanuzi wa 1 Kor 8:9-13 kwa maelezo zaidi.
S: Kwenye Rum 14:15, ni kwa jinsi gani "kula" tu kunaweza kumharibu Mkristo mwenzako?

J: Chakula hakimdhuru kimwili muumini mwenzako, lakini Paulo anaongelea jinsi ambavyo kula kwako kunaweza kuiharibu imani ya Mkristo mwenzako. Ikiwa Mkristo mmoja anafikiri si sahihi kula kitu fulani, na Mkristo mwingine anamjaribu Mkristo wa kwanza ili aende kinyume na dhamira yake, jambo hili linaweza kuumiza imani ya Mkristo wa kwanza.

S: Kwenye Rum 15:24, 28, je Paulo aliweza kwenda Hispania?

J: Paulo aliwaandikia Warumi akiwa safarini kwenda Yerusalemu (Rum 15:25), kwa hiyo kama alisafiri, basi atakuwa alienda Hispania baada ya Warumi kuandikwa. Ufuatao ni uthibitisho kuwa alifanya hivyo.
a)
Paulo alikuwa amekusudia kwenda Hispania (Rum 15:24, 28).
b)
Eusebius alitoa maoni kuwa alikwenda (History 2:22:2-3).
c)
Paulo alikwenda kulingana na 1 Clement sura ya 2 mistari 34-39, uk. 603, na kitabu cha uongo cha Acts of Peter (karne ya 4?) sura ya 1-3.

S: Kwenye Rum 15:33, inakuwaje Bwana ni Mungu wa amani, kwani Kut 13:3 inasema Mungu ni shujaa wa vita?

J: Biblia hasemi kuwa Mungu ni mpatanishi tu, au kuwa Mungu ni wa amani tu. Badala yake, Biblia inasema kuwa Mungu ni mwenye ghadhabu na ni Mungu wa amani pia. Na kwa jinsi hiyo hiyo, kama shujaa wa vita anaweza kuamuru na kulinda amani ya watu wengine, Mungu anaweza kuamuru amani.

S: Kwenye Warumi 16, je orodha hii ndefu ya watu katika mji ambao Paulo alikuwa bado hajautembelea inaonyesha kuwa waraka huu haukuandikwa kwa Warumi (Asimov's Guide to the Bible, uk. 1097) au kwamba Warumi 16 haikuwa sehemu ya Waraka kwa Warumi (Asimov's Guide to the Bible, uk. 1093)?

J: Hapana. Miongoni mwa watu zaidi ya 28 ambao Paulo amewataja, mmoja wao alitoka Asia, watatu walikuwa ndugu za Paulo, na wengine walikuwa watenda kazi wenza ambao Paulo aliwajua kutoka Korintho na sehemu nyingine. Kwa kuongezea, hakuna panaposema kuwa Paulo alikutana na kila mmoja wa watu hawa; wengine wanaweza kuwa watenda kazi ambao Paulo alisikia habari zao kupitia kwa watu wengine na alitaka kueleza kufurahishwa nao.

S: Kwenye Rum 16:7, je Androniko na Yunia walikuwa mitume, kwa kuwa walitambulika kati ya mitume?

J: Hapana. Hii ina maana kuwa Androniko na Yunia walijulikana sana na mitume. Kama wazo la ziada, hawakutajwa kabisa na waandishi Wakristo wa awali hadi mwaka wa 325 BK.

S: Kwenye Rum 16:13, je Rufo aliyetajwa hapa ni Rufo yule yule wa kwenye Mak 15:21, aliyekuwa mwana wa Simon Mkirene?

J: Inawezekana, lakini si lazima iwe hivyo. Kulikuwa na watu wengi sana walioitwa Rufo wakati ule.

S: Kwenye Rum 16:15, ni kwa jinsi gani Yesu Kristo alifichwa hadi alipokuja, kwani nabii nyingi sana za Agano la Kale zinamwongelea Masiha?

J: Kama ambavyo mtu anaweza kueleza siri kwa njia ya fumbo bila kuifafanua, Agano la Kale mara kwa mara linataja fumbo la kuja kwa Masiha, bila kuelezea kufanyika mwili kwa Yesu.

S: In Rom 16:23, what archaeological evidence is there for Erastus?
S: Kwenye Rum 16:23, ni uthibitisho gani wa kiakiolojia uliopo kuhusu Erasto?

J: Kwenye Rum 16:23, Paulo anamsalimia Erasto, mtunza hazina wa mji (Korintho) aliokuweemo Paulo wakati anaandika waraka huu. Huyu aweza kuwa Erasto yule yule wa kwenye e Tim 4:20 na Mdo 19:22.
Mwaka 1929, wakati wa Korintho ilipochimbwa, maandishi yafuatayo yalipatikana: "Erasto, afisa mwangalizi wa majengo ya umma, alitengeneza njia ya wenda kwa miguu kwa gharama zake mwenyewe."

S: Kwenye Warumi, ni lini waraka huu uliandikwa?

J: Huenda ilikuwa msimu wa baridi sana wa 56/57 BK.

S: Tunajuaje kuwa Waraka wa Warumi uliandiwa na Paulo kweli?

J: Kuna njia nyingi zinazoonyesha hivyo:
Kitabu cha Warumi chenyewe kinasema hivyo, na kanisa la awali halikuwahi kutilia shaka jambo hili.
Orodha ya Vitabu Vitakatify ya Muratoria
(mwaka 170-210 BK) sura ya 3 (ANF vjuzuu ya 5), uk. 603 inasema kuwa Mtume Paulo aliyaandikia makanisa saba kwenye nyaraka zake: Wakorintho (nyaraka 2), Waefeso, Wafilipi, Wakolosai, Wagalatia, Wathesolanike (nyaraka 2), Warumi. Paulo aliwaandikia Filemoni, Tito, na nyaraka mbili za Timotheo.
Irenaeus
(mwaka 182-188 BK) alinukuu Rum 1:1-4 kama barua ambayo Paulo amewaandikia Warumi (Irenaeus Against Heresies kitabu cha 3 sura ya 16.3, uk. 441). Pia Rum 8:36 maagizo ya Paulo kupitia barua yake kwa Warumi kwenye Irenaeus Against Heresies kitabu cha 2 sura ya 22.2, uk. 390).
Irenaeus (mwaka 182-188 BK) "Kwa hiyo, Paulo anapoelezea udahifu wa kibinadamu, anasema: ‘Kwa maana najua ya kuwa ndani yangu, yaani, ndani ya mwili wangu, halikai neno jema,' akionyesha kuwa ‘jambo jema' kwa wokovu wetu halitoki kwentu, bali kwa Mungu. Na tena: ‘Ole wangu, maskini mimi! Ni nani atakayeniokoa na mwili huu wa mauti?' Kisha analeta mada ya Mkombozi, [akisema], ‘Neema ya Yesu Kristo Bwana wetu'" [Gal 6:18; 1 The 5:28; 2 The 3:18] (Irenaeus Against Heresies kitabu cha 3 sura ya 20.3, uk. 450).
Tertullian
(mwaka 207/208 BK) anasema kuwa Paulo ndiye aliyeandika nyaraka za Wagalatia, Wakorintho, Wafilipi, Wathesalonike, Waefeso na Warumi kwenye Five Books Against Marcion kitabu cha 4 sura ya 5, uk. 350).
Tertullian (mwaka 198-220 BK) "Lakini ni kwa vipi Paulo . . . kama pia kwenye Waraka kwa Warumi: ‘Wala si hivyo tu, ila na mfurahi na katika dhiki, pia; mkijua ya kuwa dhiki worketh patience, and patience experience, and experienkazi yake ni kuleta saburi; na saburi ni uthabiti wa moyo; na kazi ya uthabiti wa moyo ni tumaini; na tumaini halitahayarishi' [Rum 5:3-5a]. Na tena: ‘Na kama tu watoto, basi tu warithi; warithi wa Mungu, warithio pamoja na Kristo; naam, tukiteswa pamoja ili tupate na kutukuzwa pamoja naye. Kwa maana nayahesabu mateso ya wakati huu wa sasa kuwa si kitu kama utukufu utakaofunuliwa kwetu.' Na kwa hiyo, anasema baada ya hapo: ‘Ni nani atakayetutenga na upendo wa Kristo? Je ni dhiki au shida, au adha, au njaa, au uchi, au hatari, au upanga? (Kama ilivyoandikwa, ya kwamba: Kwa ajili yako tunauawa mchana kutwa, tumehesabiwa kuwa kama kondoo wa kuchinjwa.) Lakini katika mambo hayo yote tunashinda, na zaidi ya kushinda, kwa yeye aliyetupenda. Kwa maana nimekwisha kujua hakika ya kwamba, wala mauti, wala uzima, wala malaika, wala wenye mamlaka, wala yaliyopo, wala yatakayokuwapo, wala wenye uwezo, wala yaliyo juu, wala yaliyo chini, wala kiumbe kinginecho chote hakitaweza kututenga na upendo wa Mungu ulio katika Kristo Yesu Bwana wetu'" [Romans 8:17-39] (Scorpiace sura ya 13, uk. 646).
Hippolytus
(mwaka 222-235/6 BK) alinukuu Rum 1:17 kama kazi ya Paulo (Treatise on Christ and Antichrist ch.64 p.218. See also Against the Heresy of One Noetus sura ya 4, uk. 225).
Origen
(mwaka 225-254 BK) "Lakini Paulo, kama mtu anayependa ukweli, anaongea kuhusu watu fulani wenye busara miongoni mwa Wagiriki, wakati maneno yao ni ya kweli, kuwa ‘Walipomjua Mungu hawakumtukuza kama ndiye Mungu wala kumshukuru.' Na anashuhudia kuwa walimjua Mungu, na anasema, jambo hili pia halikutokea bila ya kibali cha Mungu, kwenye maneno haya: ‘Kwa sababu Mungu aliwaonyesha' nadhani alikuwa anadokeza kwa mbali watu waliootoka kwenye vitu vyenye akili kuwa watu wenye ufahamu, anapoongeza, ‘Kwa sababu mambo yake yasiyoonekana tangu kuumbwa ulimwengu yanaonekana, kufahamika kwa kazi zake; yaani, uweza wake wa milele na Uungu wake; hata wasiwe na udhuru; kwa sababu, walipomjua Mungu hawakumtukuza kama ndiye Mungu wala kumshukuru'" [Rum 1:19-21a] (Origen Against Celsus kitabu cha 3 sura ya 47, uk. 483).
Novatian
(mwaka 250-257 BK) anasema Rum 1:20 iliandikwa na Mtume Paulo (Treatise Concerning the Trinity sura ya 3, uk. 614).
Cyprian wa Carthage
(karibu mwaka 246-258 BK) alisema "Waraka wa Paulo kwa Warumi" kwenye Treatises of Cyprian - Testimonies sura ya 45, uk. 546.
Kwenye Baraza la Saba la Carthage (mwaka 258 BK) [sehemu] Paulus wa Obba alinukuu nusu ya mistari miwili, Rum 3:3b-4a, kama kazi ya Mtume Paulo kwenye uk. 570.
Adamantius
(karibu mwaka 300 BK) Adamantius ananukuu Rum 7:12 kama kazi ya Paulo (Dialogue on the True Faith sehemu ya pili sura ya 20, uk. 105). Tazama pia kazi hiyo hiyo sehemu ya kwanza sura ya 21, uk. 64.
Victorinus wa Petau
(aliyeuawa kwa ajili ya imani 304 BK) anaongelea Agano la Kale na Agano Jipya kwenye kazi yake iitwayo Commentary on the Apocalypse of the Blessed John, uk. 345. Ameziorodhesha nyaraka za Paulo kuwa ni Warumi, Wakorintho, Wagalatia, Waefeso, Wathesalonike, Wafilipi, Wakolosai, Timotheo, na ananukuu 1 Tim 3:15 kwenye sura ya 16, uk. 345. Anaendelea kunukuu 1 Kor 15:53 kwenye uk. 346).
Methodius
(karibu mwaka 260-312 BK) ananukuu Rum 8:19-21 kama "Paulo anavyoshuhudia kwa wazi kabisa." (Discourse on the Resurrection sehemu ya 1 sura ya 8, uk. 365).

S: Kwenye Warumi, tunajuaje kuwa Maandiko tuliyonayo leo yanawakilisha maandishi halisi yaliyoandikwa awali?

J: Kuna sababu zisizopungua tatu.
1.
Mungu aliahidi kulihifadhi neno lake kwenye Isa 55:10-11; 59:21; 40:6-8; 1 Pet 1:24-25 na Mat 24:35.
2. Ushahidi wa kanisa la awali.
Wafuatao ni watu walioandika kabla ya baraza la kanisa la Nika walioongelea mistari mbalimbali ya Waraka wa Warumi.
Clement wa Rumi
(mwaka 96-98 BK) alinukuu Rum 1:32b (1 Clement sura ya 34 juzuu 1, uk. 14; juzuu ya 9, uk. 239).
Polycarp
(karibu mwaka 150 BK) Rum 14:10b, 12 nukuu 1 ˝ ya Polycarp's Letter to the Philippians sura ya 6, uk. 34.
Orodha ya vitabu vitatatifu ya Muratorian
(mwaka 170-210 BK) ANF juzuu ya 5, uk. 603 inasema kuwa Paulo aliyaandikia makanisa saba kwenye nyaraka zake, Wakorintho (nyaraka 2), Waefeso, Wafilipi, Wakolosai, Wagalatia, Wathesalonike (nyaraka 2), Warumi. Paulo aliandika Filemoni, Tito, nyaraka mbili kwa Timotheo.
Theophilus wa Antiokia
(aliandika mwaka 168-181/188 BK) alinukuu Rum 2:7 na 2:8, 9 kwenye Theophilus to Autolycus kitabu cha 1 sura ya 14, uk. 93. Alinukuu sehemu ya Rum 13:7, 8 kwenye Theophilus to Autolycus kitabu cha 3 sura ya 14, uk. 115. Hizi ni sehemu pekee ambazo anaongelea Waraka wa Warumi.
Christians wa Vienna na Lugdunum
(mwaka 177 BK), uk. 778, ananukuu 3/4 ya Rum 8:18.
Irenaeus
(mwaka 182-188 BK) ananukuu Rum 1:1-4 kama waraka wa Paulo kwa Warumi (Irenaeus Against Heresies kitabu cha 3 sura ya 16.3, uk. 441). Pia anaongelea Rum 8:36 kama kazi ya Paulo kwenye barua yake kwa Warumi (Irenaeus Against Heresies kitabu cha 2 sura ya 22.2, uk. 390).
Passion of the Scillitan Martyrs
(mwaka 180-202 BK), uk. 285 (sehemu, Paulo) "Ni vitu gani vilivyomo kwenye kifua chako? Speratus alisema, vitabu na nyaraka za Paulo, mtu mwenye haki."
Clement wa Alexandria
(mwaka 193-217/220 BK) alinukuu Rum 16:19 iliyoandikwa na mtume kwenye Waraka kwa Warumi (The Instructor kitabu cha 1 sura ya 5, uk. 214).
Tertullian
(mwaka 198-220 BK) alisema, "tMtume anawaonya Warumi" na ananukuu Rum 13:1 kwenye Scorpiace sura ya 14, uk. 647).
Hippolytus
(mwaka 225-235/6 BK) alinukuu Rum 1:17 kama kazi ya Paulo kwenye Treatise on Christ and Antichrist sura ya 64, uk. 218).
Commodianus (karibu mwaka 240 BK) [sehemu] anaongea kuhusu Sulemani na Mtume Paulo (Instructions of Commodianus sura ya 31, uk. 209).
Theodotus ambaye huenda alikuwa Mmontanisti (karibu mwaka 240 BK) andokeza Rum 8:15; Gal 4:6 kwenye barua yake sura ya 19, uk. 45).
Origen
(mwaka 225-254 BK) ananukuu Rum 9:16 kama "kwenye Paulo" [kwenye matoleo ya Kilatini na Kigiriki] (Origen Against Celsus kitabu cha 3 sura ya 1, uk. 307).
Novatian
(mwaka 257 BK) anaongelea Rum 1:20 kama kazi ya Mtume Paulo (Treatise on the Trinity sura ya 3, uk. 614).
Treatise Against Novatian
(mwaka 254-256 BK) sura ya 12, uk. 661 inanukuu Rum 14:4 kama kazi ya mtume. Inanukuu sehemu za Rum 2:11 kwenye sura ya 16, uk. 662).
Cyprian
(karibu mwaka 246-258 BK) ananukuu kutoko "Waraka wa Mtume Paulo kwa Warumi" kwenye Treatise 12 kitabu cha tatu 17 miongoni mwa sehemu nyingine.
Moyses na wengineo kwa Cyprian
(mwaka 250-251 BK) ananukuu Rum 8:35 kama kazi ya mtume (Letters of Cyprian Barua ya 25 sura ya 4, uk. 303).
Kwenye Baraza la Saba la Carthage (mwaka 258 BK) kwenye uk. 570, Paulus wa Obba ananukuu nusu ya mistari, Rum 3:3b-4a, kama kazi ya mtume.
Dionysius wa Alexandria
(karibu mwaka 246-265 BK) anaongelea 1/3 ya Rum 14:23 kama kazi ya mtume (Epistle to the Bishop Basilides kanuni ya 4, uk. 96).
Archelaus
(mwaka 262-278 BK) alinukuu Rum 5:14 kama Maandiko alipokuwa akilumbana na Manes (Disputation with Manes sura ya 29, uk. 202).
Adamantius
(karibu mwaka 300 BK) aliongelea Rum 2:16. Pia ananukuu Rum 6:13 kama kazi ya mtume, na ananukuu Rum 7:12 kama kazi ya Paulo.
Victorinus askofu wa Petau
huko Austria (aliyeuawa kwa ajili ya imani yake 304 BK) Analitaja Agano la Kale na Jipya kwenye kazi yake iitwayo Commentary on the Apocalypse of the Blessed John, uk. 345. Aliorodhesha nyaraka za Paulo kuwa ni Warumi, Wakorintho, Wagalatia, Waefeso, Wathesalonike, Wafilipi, Wakolosai, Timotheo, na ananukuu 1 Tim 3:15 kwenye sura ya 16, uk. 345. Pia alinukuu 1 Kor 15:53 kwenye uk. 346.
Peter wa Alexandria
(mwaka 306, 285-311 BK) Rum 10:8-10 (The Canonical Epistle kanuni ya 5, uk. 271). Alinukuu nusu ya Rum 2:11 kwenye Canonical Epistle kanuni ya 7, uk. 272).
Methodius
(karibu mwaka 260-312 BK) alinukuu Rum 8:19-21 kama "Paulo anavyoshuhudia wazi" (Discourse on the Resurrection sehemu ya 1 sura ya 8, uk. 365).
Athanasius
(karibu mwaka 318 BK) alinukuu Rum 1:26 "Kama Paulo alivyosema, mtumishi mtakatifu wa Kristo" (Against the Heathen sura ya 26, uk. 17).
Lactantius (karibu mwaka 303 hadi karibu mwaka 325 BK) anadokeza Rum 1:22 kwenye Divine Institutes kitabu cha 2 sura ya 3, uk. 44. Anadokeza Rum 1:21-23 kwenye Divine Institutes kitabu cha 4 sura 1, uk. 101.
Alexander wa Alexandria
(mwaka 313-326 BK) alinukuu Rum 8:32 kama kazi ya Mt. Paulo (Epistles on the Arian Heresy Waraka wa 1 sura ya 8, uk. 294).
Kutoka Nikewa hadi Efeso (mwaka 325-431 BK)

Eusebius wa Kaisaria
(mwaka 318-339/340)
Aphrahat/Aphraates (mwaka 337-345 BK) anautaja Waraka wa Warumi kama Maandiko (Select Demonstrations).
Philo wa Carpasia
(karne ya 4) aliongelea Rum 10:15.
Serapion
(baada ya mwaka 362 BK).
Itikio la Marius kwa Muariani Candidus (mwaka 359-362 BK)
Victorinus wa Rumi
(baada ya 363 BK)
Athanasius
(mwaka 367 BK) aliorodhesha vitabu vya Agano Jipya kwenye Festal Letter 39 uk. 552).
Hilary wa Poitiers
(mwaka 355-367/368 BK) alinukuu Rum 1:2-4 kama kazi ya Paulo (On the Trinity kitabu cha 7 sura 25, uk. 129).
Hilary wa Poitiers (mwaka 355-367/368 BK) alinukuu Rum 6:10-11 "Tena kwa Warumi [mtume mbarikiwa] aliandika" (On the Trinity kitabu cha 9 sura 13, uk. 159).
Synopsis Scripturae Sacrae
(mwaka 350-370 BK au karne ya 5) iliutaja Waraka wa Paulo kwa Warumi kama sehemu ya Agano Jipya. Ilinukuu Rum 1:1.
Orodha ya Vitabu Vitakatifu ya Cheltenham
(Katalogi ya Mommsen) [karibu mwaka 360-370 BK]
Tito wa Bostra
(kabla ya mwaka 378 BK)
Ephraim Mshamu
(mwaka 350-378 BK)
Basil wa Cappadocia
(mwaka 357-378/379 BK) alinukuu Rum 11:36 kama kazi ya Paulo (Spirit sura ya 5, uk. 5).
Sinodi ya Laodikia
huko Frigia (mwaka 343-381, 363 BK)
Ambrosiaster
(baada ya mwaka 384 BK)
Cyril wa Yerusalemu
(karibu mwaka 349-386 BK) aliitaja Rum 8:14 kama waraka wa Paulo aliowaandikia Warumi (Mhadhara wa 14.29, uk. 102).
Apollinaris wa Laodikia
(karibu mwaka 390 BK)
Ambrose wa Milani
(mwaka 370-390 BK) alinukuu Rum 1:24-25 kama kazi ya "Paulo, aliyejazwa Roho wa Mungu" (On the Christian Faith kitabu cha 1 sura ya 16.101, uk. 218).
Ambrose wa Milani (mwaka 370-390 BK) alinukuu rum 8:32 kama Maandiko (On the Christian Faith kitabu cha 1 sura ya 17.109, uk. 219).
Gregory wa Nazianzus
(mwaka 330-391 BK)
Pacian wa Barcelona
(mwaka 342-379/392 BK) alinukuu Rum 2:4-5 kama kazi ya Mtume Paulo (On Penitents sura ya 11.2, uk. 84).
Gregory waElvira
(baada ya mwaka 392 BK) aliongelea Rum 7:22 na vifungu vingine
Amphilochius
(hadi mwaka 394/397 BK) kwenye Iambi ad Seleucum
Gregory wa Nyssa
(karibu mwaka 356-397 BK) anasema Rum 1:1 ni kazi ya Paaulo kwenye Against Eunomius kitabu cha 2 sura ya 4, uk. 105 na Waraka kwa Warumi kwenye Against Eunomius kitabu cha 2 sura ya 9, uk. 117.
Didymus Kipofu
(mwaka 398 BK)
Diodore
(mwaka 398 BK)
Mtu wa ufarakano Lucifer wa Cagliari, Sardinia (mwaka 361 hadi karibu mwaka 399 BK)
Kazi ya Kishamu iitwayo Book of Steps (Liber Graduum)
[mwaka 350-400 BK]
Syrian Catalogue of St. Catherine's
(karibu mwaka 400 BK)
Macarius/Symeon
(karne ya 4/5)
Asterius wa Emesa
(karibu mwaka 400 BK)
Macarius/Symeon
(karne ya 4/5)
Maximinus of Turin
(karne ya 4/5)
Epiphanius wa Salamis
(mwaka 360-403 BK)
Papa Innocent I wa Rumi (karibu mwaka 405 BK)
Rufinus
(mwaka 374-406 BK)
Gaudentius
(baada ya mwaka 406 BK) aliongelea Rum 8:35 na mistari mingine
Chromatius
(aliyekufa mwaka 407 BK)
John Chrysostom
(mwaka 392-407 BK) aliandika mahubiri 32 ya Waraka wa Warumi.
Severian
(baada ya mwaka 408 BK)
Niceta wa Remesianus
(mwaka 361 hadi karibu mwaka 415 BK)
Rufinus
(mwaka 374-406 BK) akitafsiri kazi ya Origen (mwaka 225-254 BK) alinukuu Rum 1:1-4 kwenye Waraka wa Paulo kwa Warumi (de Principiis kitabu cha 2 sura ya 4.2, uk. 276).
Orosius/Hosius wa Braga
(mwaka 414-418 BK)
Baraza la Kanisa la Carthage
(mwaka 393-419 BK)
Jerome
(mwaka 317-420 BK) alinukuu Rum 7:6 kama "anavyosema mtume" (Letters of Jerome barua ya 69 sura ya 7, uk. 146).
Augustine wa Hippo
(mwaka 388-430 BK) alisema kuwa mtume aliandika Waraka wa Warumi kwenye City of God kitabu cha 20 sura ya 1, uk. 421).
Mpelagini nusu John Cassian (mwaka 419-430 BK) alinukuu Rum 14:10, 11 kama "Mtume . . . akiandika kwa Warumi" kwenye Seven Books of John Cassian kitabu cha 3 sura ya 7, uk. 566).
Nilus
(karibu mwaka 430 BK) aliongelea Rum 7:12.
Marcus wa Eremita
(baada ya mwaka 430 BK)
Baraza la Kanisa la Efeso (Juni-Sept 431 BK) lilidokeza Waraka wa Warumi.
Baada ya Efeso (mwaka 431 BK)

Vincent wa Lerins
(karibu mwaka 434 BK)
Socrates
(karibu mwaka 400-439 BK) [Socrates' Ecclesiastical History]
Cyril wa Alexandria
(mwaka 444 BK)
Hesychius wa Jerusalem
(hadi mwaka 450 BK) (jina linatamkwa HESS-us)
Speculum
(karne ya tano)
Baraza la Kanisa la Chalcedon
(mwaka 451 BK)
Quodvultdeus
(karibu mwaka 453 BK)
Eucharius
(karibu mwaka 424-455 BK) Instructiones
Theodoret wa Cyrus
(askofu na mwanahistoria) [mwaka 423-458 BK]
Patrick wa Ireland
(mwaka 420-461 BK) aliutaja Waraka wa Warumi kuwa Maandiko
Papa Leo I wa Roma (mwaka 440-461 BK)
Prosper wa Aquitaine (mwaka 426-465 BK) alidokezea Waraka wa Warumi
Varimadum
(mwaka 445/480 BK)
Ushahidi wa waasi na vitabu vya uongo

Marcion
(karibu mwaka 160 BK) aliutaja Waraka wa Paulo kama wa Paulp, kwa mujibu wa Adamantius na Tertullian.
Tatian (aliyekufa mwaka 170 BK) alidokezea Rum 1:20 kwenye Address of Tatian to the Greeks sura ya 4, uk. 66.
Mwasi Manes (mwaka 262-278 BK) aliuchukulia kuwa Maandiko alipokuwa ananukuu Rum 5:14 (Disputation with Manes sura ya 29, uk. 202).
Mmanekazimu (dini yenye kushikilia dhana mbili zinazopingana inayohusisha mambo kadhaa ya kikristo, kinostia, na kipagani) mwasi Faustinus wa Milevis/Milevum (baada ya 383 BK)
Mwasi Priscillian (karibu mwaka 385 BK) anaongelea Rum 8:11
Mdonati (dhehebu lililodai kuwa ni watu tu walioishi maisha yasiyokuwa na lawama ndio waliokuwa sehemu ya kanisa) mwasi Tyconius (baada ya mwaka 390 BK)
Muariani (uasi maarufu ulioukana uungu wa Kristo ukidai kuwa Mwana wa Mungu aliumbwa na Baba na hivyo hakuwa pamoja na Baba milele, wala hakuwa na asili moja na Baba) aliyevuka mpaka Eunomius wa Cyzicus (karibu mwaka 360-383/394 BK)
Mwasi Pelagius (mwaka 416-418 BK)
Mpelagia (kundi la Wakristo wanaokana dhana ya dhambi ya asili na kupangwa kwa vitu vyote toka awali (predestination), akitetea uzuri wa asili wa wanadamu na uhuru walionao wa kuchagua) mwasi Theodore wa Mopsuestia (mwaka 392-423/429 BK)
Mpelagia mwasi Julian wa Eclanum (karibu mwaka 454 BK)
Mambo yote haya yangali yapo leo.
3.
Hati za kale zenye Maandiko tulizonazo za Waraka wa Warumi zinaonyesha tofauti kidogo za maandishi, lakini hakuna makosa makubwa ya kitheolojia.
p10
(=Papyrus Oxyrhynchus 209) Rum 1:1-7 (karne ya 4). Maandishi ya Kialexandria
Karne ya 4-1968 (Text of the New Testament).
p26
Rum 1:1-16 karibu mwaka 600 BK. Inafanana na Sinaiticus na Alexandrinus.
Karibu mwaka 600 BK-1968 (Text of the New Testament).
p27
Rum 8:12-22, 24-27; 8:33-9:3; 9:5-9 (karne ya 3).
Karne ya 3-1968 (Text of the New Testament).
p31
Rum12:3-8 karne ya 7. Inafanana na Sinaiticus
Karne ya 7-1968 (Text of the New Testament).
p40
Rum 1:24-17; 1:31-2:3; 3:21-4:8; (herufi 2 kati ya 19 za 6:2), herufi 7 kati ya 62 za 6:3) 6:4-5; (herufi 7 kati ya 56 za 6:15); 6:16; 9:17, 27 (karne ya 3) Maandishi ya Kialexandria.
Karne ya 3 -1968 (Text of the New Testament haiongelei 6:2-3, 15).
p46
Chester Beatty II mwaka 100-150 BK, Rum 5:17-6:3; 6:5-14; 8:15-25,27-35; 8:37-9:32; 10:1-11:22; 11:24-33; 11:35-15:9; 15:11-16:27, na sehemu nyingine za nyaraka za Paulo na Waebrania. (Mistari 233 ya Warumi) [Complete Text of the Earliest New Testament Manuscripts] inasema kwenye uk. 197-198 kwamba ubora na alama za stichiometri (stichiometric marks) zinaonyesha kuwa iliandikwa na mwandishi mtaalamu.
Nusu ya kwanza ya karne ya 3-1936, Frederic G. Kenyon kwa mujibu wa Complete Text of the Earliest New Testament Manuscripts.
Karne ya 2, mwaka 200 BK-1935, Ulrich Wilken kwa mujibu wa Complete Text of the Earliest New Testament Manuscripts.
Mwaka 200 BK-1968 (Text of the New Testament).
Mwaka 81-96 BK-1988, Young Kyu Kim kwa mujibu wa Complete Text of the Earliest New Testament Manuscripts.
Karibu nwaka 200 BK-1975, Aland na wengineo, toleo la tatu.
Karibu mwaka 200 BK-1998, Aland na wengineo toleo la nne.
Mwanzo mwa karne ya pili hadi mwaka 1999 (Complete Text of the Earliest New Testament Manuscripts). Wazo hili linatokana kwa sehemu na maandishi ya mkono yanayofanana sana na Papyrus Oxyrhynchus 8 (mwisho wa karne ya kwanza au mwanzo wa karne ya pili) na Papyrus Oxyrhynchus 2337 (mwisho wa karne ya kwanza).
p61
Rum 16:23, 25-27; 1 Kor 1:1-2, 2-6; 5:1-3, 5-6, 9-13; Fil 3:5-9, 12-16, Kol 1:3-7, 9-13, 1 The 1:2-3; Tit 3:1-5, 8-11, 14-15; Flm 4-7 (karibu mwaka 700 BK).
Karibu mwaka 700 BK-1968 (Text of the New Testament).
Karibu mwaka 700 BK-1975, Aland na wengineo, toleo la tatu na mwaka 1998, Aland na wengineo, toleo la nne lililorekebishwa.
p94
Rum 6:10-13, 19-22 (karne ya 5/6).
p113
(Papyrus Oxyrhynchus 4498) Rum 2:12-13, 20 (karne ya 3).
Uncial 0220
(karibu mwaka 300 BK) Rum 4:23-5:3; 5:8-13 (karibu mwaka 300 BK). Hati hii inafana na Vaticanus kila sehemu isipokuwa Rum 5:1. Ingawa Rum 5:8-13 ipo pia, imeharibika mno kiasi kwamba haiwezi kutengenezwa upya.
Vaticanus
[B] (mwaka 325-350 BK).
Sinaiticus
[Si] (mwaka 340-350 BK).
Old Syriac
(karibu mwaka 400 BK).
Syriac Peshita
(mwaka 443-).
Ephraemi Rescriptus
(mwaka 444 BK).
Bohairic Coptic
[Boh] (karne ya 3/4).
Fayyumic Coptic
[Fay] (karne ya 3/4).
Sahidic Coptic
[Sah] 3(karne ya 3/4).
Alexandrinus
[A] (karibu mwaka 450 BK).
Gothic
[Goth] (mwaka 493-555 BK).
Ephraemi Rescriptus
[C] (karne ya 5).
Armenian
[Arm] (kuanzia karne ya 5).
Claromontanus
[D] (karne ya 5/6).
Ethiopic
[Eth] (kuanzia karibu mwaka 500 BK).

Tazama www.BibleQuery.org/romMss.html for kwa maelezo zaidi kuhusu hati za awali za Waraka wa Warumi.