Chimbuko la Uislam

Ili kuweza kufahamu chimbuko halisi la Uislam inafaa kuyafahamu mazingira ya Uarabuni kabla ya Uislam, mtu aliyeitwa Muhammad na historia ya mwanzo ya Uislam. Elimu kale (akiolojia), Kurani na Hadithi vina mengi ya kusimlia ambayo watu wengi wanaweza kuwa hawajui.

Maka kabla ya Muhammad

Umeishawahi kujiuliza Maka ilikuwaje kabla Muhammad hajazaliwa? Yaelekea ilikuwa sehemu ya kuvutia, kwani ilikuwa ni kituo cha biashara, mahali penye kusanyiko la tamaduni mbalimbali. Palikuwa na wafanya biashara wenye dini mbalimbali. Watu wa kabila la Kureshi wa Maka walimwabudu Hubal, Al-ilah na mabinti watatu wa Al- ilah. Mwamba mweusi kutoka mbinguni uliheshimiwa sana uliwekwa kwenye kona ya kaaba. Kaaba ilikuwa ni kitovu cha kuabudia miungu/sanamu 360 kwa mujibu wa Bukhari juzuu ya 3 kitabu cha 43 sura ya 33 na.658 uk. 396 na juzuu ya 5 kitabu cha 59 sura ya 47 na.583 uk. 406.

Ensaiklopidia ya Uislam (iliyohaririwa na Eliade) uk.303 na kuendelea inasema, watu, kabla ya Uislam, waliomba mara 5 wakielekeza nyuso zao Maka na kufunga nusu siku kwa muda wa mwezi mzima. Wakureshi walifunga siku ya 10 ya Myharram/Muharam. Hii nayo Muhammad aliagiza ifanyike, lakini baadaye ikawa hiari. (Bukhari juzuu ya 5 kitabu cha 58 sura ya 25 na.172 uk.109), pia Bukhari juzuu ya 6 kitabu cha 60 sura ya 24 na.31 uk. 25.

Waarabu kabla ya Uislam walifanya hija (Umrah) Maka. Fiqh us-Sunnah juzuu ya 5 uk.122, na Bukhari juzuu ya 2 kitabu 26 sura ya 33 na.635 uk.371-372 zinasema walidhani kutokufanya 'Umrah ikijuwa ni moja ya dhambi kubwa sana duniani. Walipofika Maka waliifunika kaaba kwa nguo ya Fiqh juzuu ya 5 uk.131, na walikuwa na mwezi mtakatifu uliohitaji kujitenga na vita kabla ya kuja kwa Uislam (Bukhari juzuu ya 2 kitabu cha 23 sura ya 96 na.482 uk.273.

Chimbuko la Neno "Allah"

Kwa ujumla: Neno "Allah" ni kifupi cha neno la kiarabu La-ilah, ambalo maana yake ni "mungu". Wakristo wa kiarabu na wapagani walitumia neno Ilah kwa maana ya Mungu. Hata Biblia za kiarabu na kiindonesia leo hii hutumia neno "Allah" kwa maaana ya Mungu. Wakati wa nyuma neno linalofanana na hilo el lilimaanisha "mungu" wa kweli au uongo katika lugha za mashariki ya kati kama kiugariki, kikaanani na kiebrania. Kabla ya Muhammad, kaaba jengo lililotunza sanamu 360 liliitwa Beit-Allah, au "Nyumba ya Allah". Baba yake Muhammad ambaye alifariki kabla ya Muhammad kuzaliwa, aliitwa Abdullah maana yake, mtumwa wa Mungu. Pia kabila la Wayahudi liliitwa 'Abdullah bin Salam kwenye Bukhari juzuu ya 5 kitabu cha 59 sura ya 13 na. 362 uk.241.

Kwa udhahiri: miongoni mwa sanamu/miungu iliyoabudiwa Maka uliitwa "Allah." Huyu alikuwa mungu maalum wa kabila la Wakureshi naye alikuwa na mabinti watatu maalum. Ukilinganisha na nguzo 4 kati ya 5 za Uislam, watu wa Maka kabla ya Muhammad walifunga kwa pamoja siku moja, walitoa sadaka kwa maskini wao, walisali wakielekeza nyuso zao Maka, na walifanya hija ('Umrah) Maka. Kulikuwa na tofauti nyingi pia, lakini inashangaza kuona muendelezo wa matendo yasiyobadilika yaliyokuwa yakifanyika kwenye ibada za kipagani za kikureshi.

Kama ambavyo kifungu hiki kitaonesha, kama ambavyo mungu maalumu wa kiyunani Zeus alivyotoakana na neno Mungu (theos), jambo kama hilo limetokea miongoni mwa Waarabu kabla ya Uislam.

Wanaomcha Allah

Watu wengi wa kale walimwabudu mungu jua na mungu mke mwezi. Waarabu wa magharibi walikuwa tofauti kwa kumwabudu mungu mwezi na mkewe, mungu mke jua. Kuna sanamu za kabla ya Uislam za alama yake: mwezi mwandamo. Sanamu hii inafanana sana na mwezi mwandamo wa wa Waislam wa Shia, isipokuwa Washia wameongeza nyota ndogo. Wayemen/Sabaeans walikuwa na mungu mwezi kwa mujibu wa Ensaiklopidia ya Uislamu uk.303. Wakureshi wanawezakuwa walimpata mungu huyu kutoka kwao.

Allah alikuwa na mabinti watatu walioitwa Lat, 'Uzza na Manat. Siku moja "Nabii wa Allah" aliafiki na kusema katika Quran (Sura 53:19) kuwa maombezi yao yanapaswa kutumainiwa. Kwa maneno mengine alisema tunapaswa kutumaini msaada wa miungu hawa watatu.

Wafuasi wa Muhammad walishangazwa kuwa amesema hivi. Baadaye, Muhammad alibadilisha mawazo yake na kusema shetani alimdanganya. Kwa vile palikuwa na kosa lililofanyika, aya hizi "zilibatilishwa" au kuondolewa. Aya hizi zinajulikana kama "aya za shetani." Inashangaza kusoma jinsi ambavyo Allah angeweza kuwa na "aya zilizobatiishwa" katika Sura za 13:39, 16:101; juzuu ya 2:106. Sura 41:37 zinataja kwa kutokuafiki watu wanaoabudu jua na mwezi.

Kwa muhtasari, Maka wakati wa Muhammad ulikuwa mji wenye watu toka mataifa mbalimbali. Wasabaiani (Sabaeans), na kabila la Muhammad yaani Wakureshi waliabudu sanamu mwezi iliyoitwa Al-ilah au Allah, pamoja na mabinti zake watatu. Kurani inakataza kuabudu miungu, lakini wanazuoni wa kislam wanakiri kuwa mwanzoni Muhammad aliweka aya zinazosema kuwa maombezi ya mabinti wa Allah yanapaswa kutumainiwa.

Muhammad Kama Mume

Sura 4.3 inasema wanaume wanaweza kuoa wanawake wasiozidi wane, ingawa Sura 33:50 inatoa upekee kwa Muhammad. Kwa mujibu wa mwanazuoni mmoja wa kiislam Ali Dashti, wafuatao hapa chini ni wake na Masuria wa Muhammad.

1. Khadija b. Khuwailid (alikufa kwanza) 13. Asma wa Saba 2. Sawda/Sauda bint Zam'a 14. Zaynab wa Khozayma 3. 'Aisha/'A'isha/Aesha (umri wa miaka 8-9) 15. Habla 4. Omm/Umm Salama/Salaim 16. Asma wa Noman 5. Hafsa ¾ watumwa/masuria ¾ 6. Zaynab/Zainab bint Jahsh 17. Mariam Mkristo 7. Jowayriya/Juwairiya (mateka) 18. Rayhana

8. Omm/Umm Habiba ¾ uhusiano usiokuwa na uhakika 9. Safiya/Saffiya b. Huyai (mateka) 19. Omm Sharik 10. Maymuna/Maimuna wa Hareth 20. Maimuna 11. Fatima/Fatema (kwa muda mfupi) 21. Zaynab/Zainab 3rd 12. Hend/Hind (mjane) 22. Khawla

Muhammad alimuoa Safiya baada ya kumchinja mumewe na watu wa kabila la Banu Quraza (Bukhari juzuu ya 2 kitabu cha 14 sura ya 5 na.68 uk. 35, Bukhari juzuu ya 4 kitabu cha 52 sura ya 168 baada ya na.280 uk.175 - 176.)

Kulikuwa na pigo Saudi Arabia, kwani wanawake wageni walioenda huko kama wafanyakazi wa ndani, walilazimishwa kuwa watumwa wanaotumikishwa kingono (sex slaves). Hata hivyo huwezi kuwashitaki wanaume wa ki-Saudi wanaofanya unafiki wa jinsi hii. Kwa mujibu wa tamaduni za dini yao, inarushusiwa kumlazimisha mtumwa wa kike kulala naye. Tazama Bukhari juzuu ya 3 kitabu cha 34 sura ya 111 na.432 uk.237; juzuu ya 3 kitabu cha 34 sura ya 113 baada ya na.436 uk.239-240; juzuu ya 5 kitabu cha 59 sura ya 31 na.459 uk.317; juzuu ya 8 kitabu cha 76 sura ya 3 na.600 uk.391; Sahih Muslim juzuu ya 2 kitabu cha 8 sura ya 560 na.3571 uk.732-733.

Gazeti la London Economist (6 Jan.1990) liliripoti kuwa Waislam wa Sudan wanawatumikisha wanawake na watoto wa kabila la Wadinka. Tarehe 4 Mei 1992, toleo maalum la Newsweek linalohusu utumwa pia liiripoti kuwa Waislam bado wanawatumikisha Waafrika sawa na gazeti la Austin American Statesman la tarehe 2/2/96. Jarida la Reader's Digest la 3/1996 uk.77-81 liliripoti kuwa "Kurudi kwa aibu kwa utumwa Afrika" ni jambo la ukandamizaji wenye kuvunja moyo.

Muhammad Mwenye Mafanikio

Muhammad pamoja na watu wake waliteka nyara misafara ya wafanya biashara na wasafiri mbalimbali. Bukhari juzuu ya 3 kitabu cha 37 sura ya 8 na.495 uk.280 inasema "wakati Allah alipomfanya mtume kuwa tajiri kutokanana na ushindi" 1/5 ya mateka ya vita iliwekwa katika hazina na Sahih Muslim juzuu ya 2 kitabu cha 5 sura ya 401 na.2348 uk.519 inasema familia ya Muhammad ilikuwa na hisa ndani yake. Utekaji nyara wa mali za watu wa kwanza kufanywa na Waislam ulijulikana kama Nakha la Raid. Wakati wa mwezi wa kusimamisha vita kwa muda, wafuasi wake waliushambulia msafara kwa kuuvamia na kuua mtu mmoja, na kuwafanya watu waliosalia kuwa watumwa, na kuchukua nyara. Muhammad mwenyewe aliongoza uvamizi wa pili pale Badr. Muhammad aliongeza utajiri wake kwa kuyashambulia makazi ya Wayahudi ya Khaibr. Yeye na wafuasi waliokuwa waaminifu kwake walijitwalia nyara na wake (Je Muhammad alihitaji mke mwingine?) wa Wayahudi wanaume 700-1000 wa kabila la Banu Quraiza waliowakata vichwa baada ya kujisalimisha.

Muhammad Mtenda Dhambi

Wakati Biblia inasema Yesu alikuwa hana dhambi, hivi ndivyo Kuran na Bukhari Hadith zinavyosema kuhusu Muhammad. Katika sura 40:55 na 48:1-2, Allah anamwambia Muhammad kuomba msamaha kwa ajili ya dhambi zake (au udhaifu wake). Sasa, watu hawahitaji msamaha kwa ajili ya madhaifu ya miili bali maadili. Sahih Muslim juzuu ya 1 kitabu cha 4 sura ya 268 na.1695 uk.373 inasema Muhammad aliomba, "Nilijikosea mwenyewe na kufanya toba ya dhambi zangu. Nisamehe dhambi zangu . . ." Bukhari juzuu ya 1 kitabu cha 2 sura ya 13 na.19 uk.23; juzuu ya 1.12.57 na.781 uk.434; juzuu ya 6.60.3 na.3 uk.4; juzuu ya 8.75.3 na.319 uk.213; na juzuu ya 8.75.62 kabla ya na.407 uk.271 kabla ya kueleza dhambi za Muhammad. Mambo bayana yaliyoelezwa kwenye Bukhari juzuu ya 1.4.70 na.234 uk.148; Bukhari juzuu ya 8.82.1 na.794-795 uk.520 ni kukata watu mikono na miguu, kuchoma macho yao, na kuwanyima maji hadi kufa baada ya kukatwa miguu na mikono. Angalia Bukhari juzuu ya 8.82.3 na.796 sura ya 4 uk.797; Bukhari juzuu ya 6 sura ya 150 kabla ya na.198 uk.158-159 pia Fiqh us-Sunnah juzuu ya 1 uk.133.

Bila shaka utakubali kwamba hizi ni dhambi nzito sana. Kwa vile Muhammad alifanya hivi, alihitaji sana msamaha. Swali la kidadisi ni hili: "Ni nani hasa anayelipa gharama ya dhambi zako?" Yesu alisema alilipa fidia ya dhambi zetu. Uislam haufundishi kuwa kuna mtu yeyote aliyelipa gharama. Je, dhambi zako zinalipwaje, au Allah anazifumbia macho baadhi ya dhambi na kuadhibu nyingine??

Watu wengine wanaweza kufikiri kuwa uovu hauna madhara yoyote ili mradi mtu anajiita Muislam. Katika karne hii Waislam wanawaua wakiristo na kufanya mauaji ya kinyama kwenye vijiji vyao katika nchi za Sudan, Nigeria na Indonesia. Wakati watu walioitwa wakristo waliwaua Waislam, watu walisema kuwa wanafanya kinyume cha tabia ya Kristo. Wakati Waislam wanawaua Wakristo, wanaomwabudu Mungu wa kweli, sijawahi kusikia mtu yeyote akisema wanafanya kinyume cha tabia ya Muhammad.

Nisamehe kwa kusema bila kuficha kiasi hiki, lakini mauaji ya watu wanaomwabudu Mungu yanayofanywa na Waislam lazima yaachwe. Waislam wanapohalalisha mauaji haya kwa sababu hata nabii wao alifanya hivyo, watu hushangazwa na nabii wao, na Allah wao ambaye anatengua neno lake, na chimbuko la Uislam.

Mfikirie Nabii Asiyekuwa na Dhambi

Tofauti na Muhammad, kuna mmoja ambaye
alisema kuwa ni nabii wa Mungu
alitimiza mamia ya unabii na maana zake
hakuwahi kusamehewa, kwa sababu hakuwa na dhambi inayohitaji kusamehewa
Hakuwahi kuua, wala kutishia maisha ya msafiri yeyote yule
Alikuwa na kiwango cha juu sana cha uadilifu (hakuruhusu ufanyaji tendo la ndoa kwa kutumia nguvu)
aliahidi kulipa adhabu ya dhambi zetu
aliteseka na kufa kwa ajili yako, na
hana kaburi, kwani alifufuka kutoka katika wafu.

Mtu huyu ni Yesu Kristo. Wakristo hawasemi kuhusu Yesu kuwa: "amani ya Mungu na iwe juu yake", Yesu ndiye mfalme wa amani; amani ya Mungu ipo juu yake. Lakini, tumaini langu ni kuwa utaweza kujua namna ya kuona kuwa amani na upendo vya Yesu vinaishi moyoni mwako.



For more info contact www.MuslimHope.com