Hadithi za Sahih Muslim



". . . Mkalitangua neno la la Mungu kwa ajili ya mapokea yenu. Enyi wanafiki, ni vema alivyotabiri Isaya kwa habari zenu, akisema, Watu hawa huniheshimu kwa midomo; ila mioyo yao iko mbali nami. Nao waniabudu bure wakifundisha mafundisho yaliyo maagizo ya wanadamu." (Yesu anasema kwenye Mathayo 15:6-8).

Kwa Waislam wa madhehebu ya Suni, maandiko ya kidini yenye umuhimu na mamlaka zaidi baada ya Kurani ni mkusanyo makubwa sita ya Hadithi,zinazodhaniwa kunukuu maneno na matendo ya Muhammad. Maandiko haya ndiyo msingi wa wa Sharia, au Sheria ya Kiislam, ambayo watu wengi wanataka kuianzisha kwenye nchi za Kiislam siku hizi. Sahih Muslim ni seti ya pili kwa mamlaka (baada ya Bukhari). Ni mkusanyiko wa Hadithi 7,190 za Imamu Muslim, aliyekufa mwaka 875 BK. Zifuatazo ni baadhi ya sehemu zake muhimu.

Umuhimu wa Hadithi

"Sehemu hii ya Hadithi inaonyesha kuwa Hadithi ni ufunguo muhimu wa kuielewa Kurani Takatifu, kwa sababu Nabii Mtakatifu, kama mtu aliyekabidhwa Ufunuo, alifaa zaidi na, kwa hiyo, alipewa mamlaka na Mungu ya kutafsiri na kuelezea maana ya Kurani Takatifu."
Sahih Muslim
vol.1 rejeo la 225 chini ya uk. 72.

Sura ya Kurani Iliyopotea

Abu Harb b. Abu al-Aswad aliripoti kwa kutumia mamlaka ya baba yake kuwa Abu Musa al-Ash'ari alisema: "...Tulizoea kukariri Sura inayofanana kwa urefu na uzito na (Sura) Bara'at. Ila nimeisahau isipokuwa sehemu hili ninayoikumbuka: 'Kama kungekuwa na mabonde mawili yaliyojaa utajiri kwa ajili ya mwana wa Adam, mwanadamu angetamani bonde la tatu na hakuna kitu ambacho kingeshibisha tumbo la mwanadamu isipokuwa mavumbi.' Na tulizoea kuikariri hivyo Sura ambayo ilifanana na moja ya sura za Musabbihat, na nimeisahau, lakini nakumbuka (kiasi hiki) kati yake: 'Enyi watu mnaoamini, kwa nini mnasema kitu msicho kitenda' (lxi 2.) na 'kwamba imeandikwa shingoni mwako kama ushahidi (dhidi yako) na utaulizwa kuhusiana na hili kwenye Siku ya Kiyama'" (xvii. 13). Sahih Muslim juzuu ya 2 kitabu cha 5 na. 2286, uk.500, 501.

Tambua kuwa kulikuwa na maneno mengi zaidi ya haya, lakini sehemu ya Sura iliyobaki ilisahauliwa.

Kujitoa kwa Muhammad

Hakuna sehemu kwenye Sahih Muslim inayosema kuwa Muhammad anapaswa kuabudiwa, lakini wanamheshimu sana Muhammad. Moja ya Hadithi ya uongo ilidai kuwa haja kubwa ya Muhammad ilikuwa na harufu nzuri sana, lakini Imamu Muslim na wakusanyaji wengine wa Hadithi waliikataa. Hata hivyo, Hadithi zote zifuatazo zilikubaliwa kwenye Sahih Muslim.

Mwili Maalum wa Muhammad:
Mwili wake ulitoa ubaridi au harufu nzuri kama mfuko wa mtengenezaji/muuzaji manukato, kwa mujibu wa Sahih Muslim juzuu ya 4 kitabu cha 28 na.5758, uk.1247. Pia alikuwa na ngozi ya kupendeza katika al-Tabari juzuu ya 6 uk.80. Muhammad alikuwa ni mtu mwenye sura nzuri zaidi ya watu wote waliowahi kuwaona kwa mujibu wa Sahih Muslim juzuu ya 4 kitabu cha 28 na.5770-5772, 5777, uk.1249.

Kukusanya nywele za Muhammad:
Kila wakati Muhammad alipokuwa ananyoa nywele zake, rafiki zake walipenda kushika kila shungi ili kulihifadhi. Kwa ukarimu Muhammad aliruhusu nywele zake zigawiwe miongoni mwa watu. Sahih Muslim juzuu ya 2 kitabu cha 7 na.2991-2994, uk.656-657.

Kutunza Majasho ya Muhammad:
Anas bin Malik aliripoti kuwa mama yake, Umm Salaim alikuwa akichukua majasho ya Muhammad na kuyaweka kwenye chupa ili yatumike kutengenezea manukato yenye harufu nzuri zaidi. (Sahih Muslim juzuu ya 4 kitabu cha 28 na.5761, uk.1247. Hadithi inayofuatia, 5762 inasema kuwa Muhammad alimuuliza kuwa anafanya nini. Alipoeleza, Muhammad alisema, "Umefanya kitu sahihi." Hadithi inayofatia, 5763 inasema kuwa Umm Salaim alikuwa anatandaza kitambaa ili Muhammad akilalie kusudi aweze kukusanya majasho yake kwenye kitambaa.

Muhammad Alikuwa Anajiamini

"Nitakuwa kiongozi wa wanadamu kwenye Siku ya Kiyama." Watu watamtafuta mtu wa kuwaombea kwa Allah. Adam, Nuhu, Ibrahim, Musa, na Yesu wote watakataa kwa sababu ya makosa yao. Yesu atawaambia waende kwa Muhammad, kisha Muhammad atamwomba Mungu. Sahih Muslim kitabu cha 1 na.378, uk.129-132. Tazama pia juzuu ya 1 kitabu cha 1 na.381, uk.133.

Muhammad alisema kuwa Shetani hakuweza kujifanya kuwa Muhammad, kwa hiyo ndoto zote za Muhammad zilikuwa zinamhusu yeye. Juzuu ya 4 kitabu cha 27 na.5635-5639, uk.1225-1226. Pia Bukhari juzuu ya 8 kitabu cha 73 na.217, uk.139-140.

Lakini Mungu Anaweza Kuja kwa Sura ya Udanganyifu

Sahih Muslim juzuu ya 1 kitabu cha 1 na.349, uk.115 ". . . Kisha Allah alikwa akiwatokea katika umbo tofauti na Umbo lake Mwenyewe, linaloeleweka kwao, na alikuwa akisema: Mimi ni Bwana wako. Nao walisema: Tunakukimbia na kwenda kwa Allah . . ." Tazama pia Bukhari juzuu ya 8 kitabu cha 76 na.577, uk.375; Bukhari juzuu ya 9 kitabu cha 93 na.532, uk.395-396.

Waislam Wanajiamini

"Kwa asili panapokuwepo Uislam, hapawi na nafasi ya Shetani kupenya na kutumia ushawishi wake. Ni lazima apae kutoka sehemu hiyo." Sahih Muslim imetafsiriwa na 'Abdul Hamid Siddiqi juzuu ya 1 kitabu cha 4, uk.210, rejeo la 603 chini ya ukurasa.

Musa na Malaika Wanaopiga Ngumi

"Abu Huraira ameripoti kuwa Malaika wa Kifo alitumwa kwa Musa (amani na iwe kwake) kumwambia wito wa Bwana. Alipokuja (Musa) alimpiga ngumi na jicho lake likang'olewa. Malaika wa Kifo akarudi kwa Bwana na kusema: Umenituma kwa mtumwa wako ambaye hakutaka kufa. Allah alimrudishia jicho lake . . ." Sahih Muslim juzuu ya 4 kitabu cha 29 na.5851, uk.1264. Pia Sahih Muslim juzuu ya 4 kitabu cha 28 na.5852, uk.1265.

Hata hivyo Musa alikuwa na akili zake timamu kwa namna fulani. Watu wengine wanaweza kuona kuwa ilikuwa ni ujinga kuwa Allah alichukua nguo za Musa ili kwamba awafukuze hao malaika. Jambo hili lilikusudiwa kuwaonyesha watu kuwa Musa alikuwa mwanaume wa kawaida, bila ya Musa kukusudia kutokuwa na staha. Sahih Muslim juzuu ya 1 kitabu 3 na.669, uk.193.

Sharia Kama Fadhila kwa Watu Wasio Waislam

Sahih Muslim juzuu ya 3 kitabu cha 24 na.5389, 5390, uk.1185 inasema, "Abu Huraira aliripoti kuwa Mjumbe wa Allah (amani na iwe kwake) alisema: Usiwasalimie Wayahudi na Wakristo kabla hawaja kusalimia wewe na unapokutana na yeyote kati yao barabarani mlazimishe aende kwenye sehemu nyembamba ya barabara."

Jambo hili linaweza kuonekana kuwa ukatili mkubwa, kwa ajili hiyo rejeo la 2559 chini ya ukurasa linaelezea sababu. "Lengo si kuwatesa au kuwatia kwenye shida isiyokuwa ya lazima ila kuwapa njia salama kwenye msongamano wa wasafiri wa Kiislam. Ni muhimu ikumbukwe, hata hivyo, kwamba amri hii haimaanishi kuwa Wakristo na Wayahudi walazimishwe kutoka njiani na barabarani na kutembea pembeni mwa kuta za nyumba au kwenye njia nyembamba na vichochoro. Kitu ambacho maagizo haya yanamaanisha ni kuwa watembee kwenye barabara mbali na umati wa Waislam ili mabaya yoyote yasije yakawafikia."

Aya Zilizobatilishwa kwenye Kurani

"Anas alisema: Allah, Mkuu na Aliyeinuliwa alionyesha (aya) inayohusu watu waliouawa Bi'r Ma'dna, na tuliikariri mpaka wakati ilipobatilishwa baadaye (na aya hiyo ilikuwa kama hivi): 'Wasilisha kwa watu wetu ujumbe kuwa tumekutana na Bwana na alifurahishwa nasi na sisi pia tulifurahishwa naye.'" Sahih Muslim juzuu ya 1 kitabu cha 4 na.1433, uk.329-330. Rejeo chini ya ukurasa wa 330 linasema "jambo hili lilifunuliwa kwenye mandhari maalumu na nafasi yake ilichukuliwa na aya nyingine nyingi zenye maana hiyo hiyo ila inadokeza vitu vingi vingine:" Tazama pia History of al-Tabari juzuu ya 7, uk.156.

Hadithi hii ni ya muhimu kwa sababu badala ya kuonyesha kuwa aya za Kurani bado zipo ila hazitumiki tena kwa sababu zimebatilishwa, kilichotokea ni kwamba aya ilibadilishwa. Kwa hiyo, kama kuna Kurani safi kwenye vibao vya mbinguni (Sura 85:20-22), je ina maneno ya awali au mapya? Kama ina maneno mapya, basi maneno ya awali hayakuwa sehemu ya vibao vya mbinguni. Kwa maana hiyo basi, baadhi ya sehemu za Kurani ya duniani zilidhaniwa kimakosa kuwa sehemu ya vibao vya Kurani ya mbinguni.

Baadhi ya Hadithi zilitanguliwa, kwa mujibu wa vichwa vya sehemu za Sahih Muslim juzuu ya 1 kitabu cha 3 na.682, uk.195-197.

Mitando na Wanawake katka Uislam

Mambo ambayo Sahih Muslim inasema kuhusu wanawake katika Uislam yatajadiliwa kwa kina zaidi kwenye makala ya Uislam Unasema Nini Hasa Kuhusu Wanawake (What Islam Really Says About Women). Ufuatao ni muhtasari wa mawazo yake makuu.

* Ushungi unatakiwa kwa wanawake wote wa Kiislamu Sahih Muslim juzuu ya 2 kitabu cha 7 na.2789, uk.606-607.
* Ushungi hautakiwi kwa vijakazi, yaani watumwa wanawake Sahih Muslim juzuu ya 2 kitabu cha 8 na.3325, 3328 uk.721-722.
* Wakati Muhammad "alipomchukua" Safiyah, Waislam wengine walitaka kuona endapo atamfanya ajitande ushungi ili waone kama atakuwa mke wa kawaida au atakuwa suria au "mateka wa ngono."Alimtaka ajitande ushungi na hivyo kumfanya awe mke wa kawaida. Bukhari juzuu ya 4 kitabu cha 52, sura ya 74 na.143, uk.92.
* Muhammad mwenyewe aliwahi kumgonga Aisha kwa makusudi "kifuani jambo ambalo lilinisababishia maumivu", kwa mujibu wa Sahih Muslim juzuu ya 2 kitabu cha 4 na.2127, uk.462.
* Uzazi wa mpango hauruhusiwi Sahih Muslim juzuu ya 1 rejeo la 208 chini ya uk.66.
* Kufanya tendo la ndoa na mwanamke mateka imeruhusiwa, kwa mjibu wa Sahih Muslim juzuu ya 2 kitabu cha 8 na.3371-3374, uk.732-733.
* Wengi wa watu watakao kuweko Jehanamu ni wanawake. Sahih Muslim juzuu ya1 kitabu cha 1 ao.143, uk.47-48.
* Kuwavua mateka mavazi ni sahihi Sahih Muslim juzuu ya 3 kitabu cha 17 na.4345, uk.953.
* Uzazi wa mpango hauruhusiwi (kwa mujibu wa mwenye kutafsiri) Sahih Muslim juzuu ya 1 rejeo 208 chini ya uk.66.
* Muislam anayemchukua mateka mwanamke asiyekuwa Muislam anaibatilisha ndoa ya awali ya huyo mateka (bila kujali hiari yake) Sahih Muslim juzuu ya 2 kitabu cha 8 na.3432, uk.743.

Waislam na Vita

Mambo ambayo Sahih Muslim inasema kuhusu wanawake katika Uislam yatajadiliwa zaidi kwenye kitabu kiitwacho Is Islam: Peaceful or Warlike? (Je Uislam ni wa: Amani au Vita?)Yafuatayo ni maelezo yake kwa ufupi.

"Imeelezwa kwa mamlaka ya 'Abdullah b. 'Umar kuwa Mjumbe ea Allah alisema nimeamriwa kupigana na watu hadi washuhudie kuwa hakuna mungu isipokuwa Allah, kwamba Muhammad ni mjumbe wa Allah, na kuwa watu wanadumisha maombi, na kutoa zaka" Sahih Muslim juzuu ya 1 kitabu cha 1 na.33, uk.17. Tazama pia juzuu ya 1 kitabu cha 1 na.32, uk.17.

* Asubuhi moja Muhammad alilishambulia kabila ambalo halikuwa linatarajia kuvamiwa Sahih Muslim juzuu ya 1 kitabu cha 4 na.745, uk.209.
* Endapo Muislam atakufa na wengine hawatapigana vita ya njia ya Allah (Jihad), basi watakuwa wamekufa kifo cha unafiki Sahih Muslim juzuu 3 kitabu cha 19 na.4696 uk.1057
* Muhammad alitaka kufanya vitisho vya mashambulizi [ya kijeshi] dhidi ya Wakristo wa Uarabuni huko Syria na Rumi. Sahih Muslim juzuu ya 4 kitabu cha 35 na.6670, uk.1445.
* Ibn Shihab alikataliwa kwa sababu hakuenda vitani Sahih Muslim juzuu ya 4 kitabu cha 35 na.6670, uk.1445-1447.

Nyara za Vita

* Sehemu moja ya tano ya nyara za vita inaenda kwenye hazina na Muhammad anaweza kuichukua Sahih Muslim juzuu ya 2 kitabu cha 5 na.2347, 2348 juzuu ya 2 rejeo la 1463 chini ya uk.519.
* Muhammad alitoa vitu vilivyotekwa nyara kama zawadi kwa watu wenye kuamini miungu mingi ili awashawishi (hongo) kuwa Waislam Sahih Muslim juzuu ya 2 kitabu cha 5 na.2300-2309, uk.504-507; juzuu ya 2 kitabu cha 5 na.2313, uk.510.
* Uso wa Muhammad uligeuka na kuwa mwekundu (kwa hasira) wakati mtu mmoja aliposema kuwa hayakuwa mapenzi ya Allah kuwa zawadi zipelekwe kwa watu wenye kuabudu miungu mingi. Sahih Muslim juzuu ya 2 kitabu cha 5 na.2325, uk.509.

Mazingaombwe ya Uiislam

Husain bin 'Abd al-Rahman was aliumwa na nge na alitumia hirizi kwa kigezo cha Hadithi moja. "Hirizi haisaidii kitu isipokuwa kwenye (ushawishi wa uovu) wa jicho au kuumwa na nge." Sahih Muslim juzuu ya 1 kitabu cha 1 na.625, uk.141.

"...Mvuto wa kijicho/uovu ni kitu halisi." Sahih Muslim juzuu ya 3 kitabu cha 24 na.5426, uk.1192. Tazama pia al-Tabari juzuu ya 39, uk.134.

Muhammad aliwapa watu wa Ansar tabano (dua) ili kuondoa sumu ya kuumwa na nge. Sahih Muslim juzuu ya 3 kitabu cha 24, na.5442-5444, 5448, uk.1192, 1196.

Muhammad alimpa A'isha tabano (dua) ili kuondoa kijicho Sahih Muslim juzuu ya 3 kitabu cha 24 na.5445, 5447-5450, uk.1196.

Ushikiliaji Mno wa Sheria katika Uislam

Unatakiwa kuvua viatu vyako kwa mfuatano maalumu. Sahih Muslim juzuu ya 3 kitabu cha 22 na.5231, uk.1154.

Usinywe maji ukiwa umesimama isipokuwa tu ni maji ya kisima cha Zamzam (kilichoko Makka). Sahih Muslim juzuu ya 3 kitabu cha 21 na.5014-5027, na. uk.1116-1118.

Muhammad alifundisha kuwa ni afya na vema zaidi kupumua mara tatu kamili (au mibwiyo mitatu) wakati wa kunywa. Sahih Muslim juzuu ya 3 kitabu cha 21 na.5029-5031, uk.1118.

Baada ya kula chakula hupaswi kupangusa mikono yako mpaka utakapokuwa umeilamba au umempa mtu mwingine kuilamba. Sahih Muslim juzuu ya 3 kitabu cha 21 na.5037-5042, uk.1119-1120. Tazama pia Abu Dawud juzuu ya 3 kitabu cha 20 na.3838, uk. 1081.

Kuna mabishano makubwa juu ya idadi na urefu wa maombi. Sahih Muslim juzuu ya 1 kitabu cha 4 na.1166-1184, uk.284-286.

Tema mate upande wa kushoto, sio kulia Sahih Muslim juzuu ya 4 kitabu cha 41 na.7149b, uk.1546.

Mianya:
Kwa kijana wa kiume kuwa karibu na mwanamke asiyekuwa mtu wa familia yake, anaweza kunywa maziwa ya mama yake na kuepuka vizuizi. Sahih Muslim juzuu ya 2 kitabu cha 8 na.3424-3427, uk.741.

"Shuraih b. Hani alisema: Nilikuja kwa A'isha kumuuliza kuhusu kupangusa soksi [ili kuziosha]. [A'isha] Alisema: Itakuwa vema zaidi kumuuliza ('Ali) mtoto wa Abu Talib kwani alikuwa anasafiri na Mjumbe wa Allah (amani na iwe kwake). Tulimuuliza na alisema: Mjumbe wa Allah (amani na iwe kwake) aliweka (kiwango cha juu) cha siku tatu mchana na usiku kwa msafiri na siku moja mchana na usiku kwa mkazi." Sahih Muslim juzuu ya 1 kitabu cha 3 na.537, uk.165.

Hata hivyo Sahih Muslim juzuu ya 1 rejeo la 479 chini ya uk.162 linadai kuwa, "Uislam haushurutishi masharti makali kwenye kitu chochote kile. Kwenye Wudu au taratibu za kiibada za kunawa/kutawadha, ruhusa ya kujipangusa kwa soksi imetolewa ili kutoa nafuu kwa watu."

Kwa nini kuna sheria nyingi sana? Sahih Muslim juzuu ya 3 rejeo la 2434 chini ya uk.1115-1116 linatueleza. "Wakati mwingine imehojiwa kuwa kuna faida gani kumfuata Nabii Mtakatifu (amani na iwe kwake) hata kwenye mambo yasiyo ya muhimu kama kula kwa mkono wa kulia au kunywa maji ukiwa umekaa, n.k. Watu hawa walielewa kwa kiasi kidogo kuwa mambo mengi madogo madogo ya maisha ya Nabii Mtakatifu (amani na iwe kwake) yanaunda muundo wa sheria na taratibu za mwenendo unaotawala maisha ya Muislam kuanzia wakati wa kuzaliwa hadi kufa na yanatawala mwenendo wake muda wote wa kuwepo kwake hapa ulimwenguni. Mambo haya madogo madogo yanafundisha fikra za watu juu ya utaratibu wa kuishi wakati wote kwenye hali ya kujitambua, uangalifu na nidhamu."

Mwenye kutafsiri anafahamu jinsi ambavyo jambo hili linafanana na Mafarisayo, lakini anasema baadaye kwenye rejeo hilo hilo chini ya ukurasa, "...Dhumuni halisi la Sunnah si, kama wakosoaji wetu wapinzani wanavyodhani, mzaliwa wa Mafarisayo na washika desturi wasio sisimua, bali ni watu wenye ufahamu, ari na nia ambao wanatekeleza kivitendo mambo wanayoyasema. Waume na wake wa jinsi hii ndio waliokuwa Wandani wa Nabii...."

Elimu ya Hali ya Hewa kwenye Hadithi

"Abu Huraira aliripoti: Mjumbe wa Allah (amani na iwe kwake) alisema: Moto uliwahi kulalamika kwa Bwana ukisema: 'Eh Bwana, baadhi ya sehemu zangu zimezila nyingine.' Kwa hiyo uliruhusiwa kutoa hewa mara mbili, mara moja wakati wa kiangazi na mara nyingine wakati wa kipupwe. Ndio maana utakuta joto kubwa (majira ya kiangazi) na baridi kubwa (majira ya kipupwe). Sahih Muslim juzuu ya 1 kitabu cha 4 na.1290, uk.302.

Matusi na Uongo dhidi ya Wayahudi na Wakristo, na Chuki kwa Wayahudi kwa Ujumla

Wayahudi waliitwa 'Uzair [Ezra], mwana wa Allah. Sura 9:30, Sahih Muslim juzuu ya 1 kitabu cha 1 na.352, uk.117, Bukhari juzuu ya 9 kitabu cha 93 sura ya 24 na.532b, uk.395; juzuu ya 6 kitabu cha 60 sura ya 80 na.105, uk.86. Walimwabudu Ezra kwa mujibu wa Bukhari juzuu ya 1, uk..xvii na juzuu ya 6 kitabu cha 60 sura ya 80 na.105, uk.86.

"Isingekuwa banu Isra'il [Israel], chakula kisingechacha, na milo isingeharibika..." Sahih Muslim juzuu ya 2 kitabu cha 8 na.3472, uk.753.

Abu Huraira aliripoti kuwa panya ni matokeo ya mabadiliko ya umbo ya baadhi ya Wayahudi. Uthibitisho ni kwamba panya hunywa maziwa ya mbuzi lakini hawanywi maziwa ya ngamia. Muhammad alionyesha kuwa alifahamu kuwa Torati ilikataza kula nyama ya ngamia. Sahih Muslim juzuu ya 4 kitabu cha 40 na.7135, uk.1541.

Wayahudi na Wakristo wanakwenda kwenye jehanamu ya moto badala ya Waislam. Sahih Muslim juzuu ya 4 kitabu cha 35 na.6665, uk.1444.

"Wakristo . . . walidai kuwa Roho Mtakatifu alijifanya kuwa mwili katika nafsi ya Yesu Kristo." Sahih Muslim tafsiri juzuu ya 1, uk.127 rejeo la 393 chini ya ukurasa.

"...Wayahudi na Wakristo hawaweki rangi (nywele zao), kwa hiyo wapinge." Sahih Muslim juzuu ya 3 kitabu cha 22 na.5245, uk.1156.

Wayahudi waliharibiwa pale wanawake walipovaa nywele za bandia. Sahih Muslim juzuu ya 3 kitabu cha 22 na.5306-5307, uk.1166-1167.

"Ngozi ya mtu yoyote miongoni mwa Wayahudi ilipochafuliwa na haja ndogo, aliikata sehemu ile na kitu cha kukatia. Hudhaifa alisema: Ningefurahi endapo rafiki yako asingelazimisha ugumu wa kufuata sheria." Sahih Muslim juzuu ya 1 kitabu cha 2 na.523, uk.163.

"Ibn 'Imar aliripoti kuwa Mjumbe wa Allah (amani na iwe kwake) akisema: Utapigana na Wayahudi na utawaua hadi hata jiwe liseme: Njoo hapa Muislam, kuna Myahudi (amejificha nyuma yangu); muue. Sahih Muslim juzuu ya 4 kitabu cha 39 na.6981, pia 6982-6983, uk.1510.

Dajjal [mpinga Kristo] atakuwa na wafuasi 70,000 Wayahudi wa Isfahan watakaokuwa wanavaa mharuma. Sahih Muslim juzuu ya 4 kitabu cha 39 na.7034, uk.1525.

Hitimisho

Wataalamu wa Hadithi hutumia sehemu kubwa ya maisha yao kuamini na kueneza mambo haya. Waislam wengine, walioko Indonesia, Pakistan, na nchi nyingi za Kiafrika, hujitoa kuwashawishi na kuwalazimisha Waislam walegevu kuzifuata. Unaposikia kuwa Waislam wanataka nchi iendeshwe kwa kufuata sheria za Kiislam "Sharia", humaanisha kuwa nchi iendeshwe kwa kufuata Hadithi na Kurani.

Kwa bahati mbaya, wamejitoa sana kwenye tamaduni hizi kwenye Uislam, wamefanya kufuata tamaduni hizi kuchukue nafasi ya kumfuata Mungu. Wakati wa Yesu, Mafarisayo pia walikuwa wameweka tamaduni nyingi sana juu ya Biblia. Yesu alizipitia hizo zote. Ingawa Yesu hakutenda dhambi hakuzingatia sheria za Mafarisayo zilizoundwa na wanadamu zinazohusu Sabato. Mungu anatutaka tuvunje tamaduni ambazo zinapingana naye, lakini pia Mungu anatutaka tufanye kitu kingine zaidi.

Mungu anataka mioyo yetu imtafute. Achana na usalama usio wa kweli wa kuishi kibinafsi huku ukiwa umefungwa na sheria, na mpe Mungu maisha yako, na amri zake zitakupa furaha ukizitii. Yafuatayo ndiyo upasayo kuyafanya.

Tambua kuwa kuna Mungu mmoja tu wa kweli, anayewaita watu waje kwake. Yeye anatupenda na anataka kila mtu asimwamini tu ; bali pia amtii. Tubu dhambi zako za matendo, mambo mabaya ambayo uliyafanya na kuyasema, na mambo mema ambayo ulitakiwa kuyafanya lakini ulishindwa kuyafanya. Tubu dhambi za mawazo. Dhambi zako za kukataa kuamini ukweli ambao uko mbele ya macho yako, za kuamini kitu ambacho ulijua undani mwake kuwa ni uongo. Tubu dhambi za chaguo la kuchagua kuendelea kwenye mtazao wa matendo yako ya kidini unayopendezwa nayo (au matendo nusu-nusu au matendo yasiyokuwepo kabisa), badala ya kumkaribia Mungu ambaye anataka awe Mtawala wa maisha yetu.

Marejeo

Toleo la kwenye mtandao wa kompyuta la Sahih Muslim lililotafsiriwa kwa sehemu lililopo kwenye tovuti hii, http://cwis.usc.edu/dept/MSA/fundamentals/hadithsunnah/muslim/
The Holy Qur-an: English translation of the meanings and Commentary
. Iliyotafsiriwa na 'Abdullah Yusuf 'Ali. Iliyosahihishwa na kuhaririwa na The Presidency of Islamic Researches, IFTA, Call and Guidance. King Fahd Holy Qur-an Printing Complex. (tarehe haijaonyeshwa)
Sahih Muslim
iliyoandikwa naImam Muslim. Kutafsiriwa katika Kiingereza na 'Abdul Hamid Siddiqi. International Islamic Publishing House. (tarehe haijaonyeshwa)
The NIV Study Bible : New International Version
Zondervan Bible Publishers. 1985.

Kwa habari zaidi tembelea www.MuslimHope.com

Hadithi za Sahih Muslim - 2

Palikuwa na kivuli kwenye moyo wa Muhammad. Sahih Muslim juzuu ya 4 kitabu cha 33 na.6522, uk.1418 inasema, "Al-Agharr al-Muzani, ... aliripoti kuwa Mjumbe wa Allah (amani na iwe kwake) alisema: Kunakuwa (nyakati nyingine) na aina fulani hivi ya giza, na ninatafuta msamaha toka kwa Allah mara mia moja kwa siku."

Ni Wakati Gani Inapozuiliwa Kumwomba Mungu?

Taratibu za kidini za maombi katika Uislam ni tofauti na maombi katika Ukristo. Imezuiliwa kusali wakati wa machweo ya jua, na kati ya swala ya asubuhi (kabla ya mawio ya jua) na mawio ya jua, kwa mujibu wa Bukhari juzuu ya 1 kitabu cha 10 sura ya 30 na.558-563, uk.323-325. Waislam hawatakiwi kufanya maombi muda wa mchana wakati ambapo rangi ya njano inakuwepo kwenye jua Sahih Muslim juzuu ya 1 kitabu cha 4 na.1301 juzuu ya 1 rejeo la 841 chini ya uk.304.

Maombi yamezuiliwa baada ya swala ya mchana isipokuwa wakati jua linapokuwa utosini. Abu Dawud juzuu ya 1 kitabu cha 2 sura ya 450 na.1269, uk.335. Nyakati ambazo maombi yamezuiliwa zimeelezwa kwenye Abu Dawud juzuu ya 1 kitabu cha 2 sura ya 450 na.1272-1273, uk.336.

Wanawake wanatakiwa "kuacha kuswali" wakati wa siku zao za mwezi. Sahih Muslim juzuu ya 1 kitabu cha 3 na.652, uk.188-189, juzuu ya 1 kitabu cha 1 na.142, uk.48; Bukhari juzuu ya 1 kitabu cha 6 na.322, uk.194, kitabu cha 6 na.327, uk.196; Sunan Nasa'i juzuu ya 1 na.355-361, uk.281-284; juzuu ya1 na.364-368, uk.285-286.

Omba, la Sivyo Nyumba Yako Itachomwa

Muhammad alisema kiongozi wa swala anatakiwa kuamuru kuchoma moto nyumba za watu waliokosa kuswali [bila sababu]. Sahih Muslim juzuu ya 1 kitabu cha 4 na.1369, uk.315. Toleo la baadaye la Nasa'i juzuu ya 1:851, uk.514 lilisema kuwa Muhammad alifikiria kutoa maagizo kuhusiana na jambo hili.

Hakuna Hakika ya Wokovu

"Alisema ('Ai'isha): Sikuwahi kumwona (Nabii Mtakatifu) baada ya hapo isipokuwa kwenye maombi akiwa anatafuta kuyakimbia maumivu ya kaburi." Sahih Muslim juzuu ya 1 kitabu cha 4 na.1214, uk.290.

Sahih Muslim
juzuu ya 4 kitabu cha 40 na.7079, uk.1534 inasimulia kuhusu malaika wawili waliokuwa wameteuliwa kurekodi matendo ya watu. Waislam wanaamini kuwa malaika mmoja anarekodi matendo mazuri na malaika mwingine anarekodi matendo mabaya.

Sahih Muslim
juzuu ya 2 kitabu cha 5 na.2205, uk.484 inasema, "Hakuna siku ambayo watumishi (wa Mungu) wanaamka na kusikitika bila kutembelewa na malaika wawili. Mmoja wao husema: Oh Allah, mpe vitu zaidi yule ambaye anavitumia (kwa ajili ya Allah), na mwingine husema: Oh Allah, mwangamize yule anayevikatalia."

Hasira za Muhammad

Muhammad aliwalaani watu kwa sababu ya hasira zake za haraka haraka Sahih Muslim juzuu ya 4 kitabu cha 30 na.6297, uk.1373. "Anas b. Malik aliripoti kuwa kulikuwa na binti mjane aliyekuwa na Umm Salaim (aliyekuwa mama wa Anas). Mjumbe wa Allah (amani na iwe kwake) alimwona msichana yatima na kusema: Oh, ni wewe; umekuwa kijana. Na usiendelee tena katika miaka! Yule kijakazi alirudi kwa Umm Sulaim akilia. Umm Sulaim alisema: Oh binti, jambo gani limekusibu? Alisema (yule msichana): Mtume wa Allah (amani na iwe kwake) ameniombea laana kuwa nisiongezeke umri wala (urefu wa) maisha yangu. Umm Sulaim alikwenda kwa haraka akiwa amejifunga kitambaa chake cha kichwani mpaka akamkuta Mjumbe wa Allah (amani na iwe kwake). [Mtume] Alimwambia: Umm Sulaim, ni jambo gani linalokusibu? [Umm] Akasema: Mtume wa Allah, umeomba laana juu ya binti yangu yatima. [Mtume] Alisema: Umm Sulaim, ipi hiyo? [Umm] Alisema: Yeye (binti yatima) anasema umemlaani ukisema kuwa asiongezeke umri au kukua katika maisha yake. Mjumbe wa Allah (amani na iwe kwake) alitabasamu na kisha akasema: Umm Sulaim, hujui kuwa nimefanya jambo hili pamoja na Bwana wangu. Na jambo hili nililolifanya na Bwana wangu ndilo nililolisema kwake: Mimi ni binadamu na ninafurahishwa kama binadamu anavyofurahishwa na ninashikwa na hasira kama binadamu anavyoshikwa na hasira, kwa hiyo kwa mtu yoyote miongoni mwa Umma wangu ambaye nimemlaani lakini hastahili laana hiyo kwa vyovyote vile, na iwe, Oh Bwana, chanzo cha utakaso na kusafishwa na ukaribu na (Allah) kwenye siku ya Kiama.

Muhammad pia alimlaani Mu'awiya, khalifa wa baadaye, kwa sababu hakuwa anaacha kula na kuja Muhammad anapokuwa amemtuma mtu kwake. Sahih Muslim juzuu ya 4 kitabu cha 30 na.6298, uk.1373.

Majina 99 ya Mungu

Majina 99 ambayo Waislam wanamwita Mungu yameelezwa kwenye Sahih Muslim juzuu ya 4 kitabu cha 33 na.6475-6478, uk.1409-1410. Rejeo chini ya ukurasa linayataja haya majina, na mengi yao Wakristo watakubaliana nayo: Muumba, Mwanzo, Mwema, Mpaji, Mkarimu/Mpaji, Mwenye kusamehe, Anaye samehe, Mwenye kusamehe Mkuu, Mwenye upendo, Mwenye kuhifadhi, Mlinzi, Mwenye kutunza, Aliye hai, n.k. Baadhi ya haya majina si ya kawaida, Mlazimishaji, Mwenye kuinua, Mwenye kuheshimu, Mwenye kufurahisha, Mwenye kuzalisha, Mwenye kurudisha nyuma si ya kawaida. Kati ya majina haya yote 99 kuna majina ya Mungu ya kwenye Biblia yanayokosekana: Baba, Bwana Mponyaji wetu, Mwamba wetu, Ngome yetu.

Kinyume (na Biblia), Sahih Muslim juzuu ya 4 kitabu cha 37 na.6731-6732, uk.1468 inasema "inakasirisha zaidi" kwamba mtoto asemwe kuwa katokana na Mungu. Waislam wengi zaidi hawajui kuwa desturi ya maandiko ya Agano la Kale ya kumwita Mungu 'Baba' imeonyeshwa kwenye Hati Toka Bahari ya Chumvi (Dead Sea Scrolls) kabla ya Kristo kuja ulimwenguni. Sura 5:46 inasema Yesu "aliithibitisha" Torati kuwa ilikuja kabla yake.

Yesu ni Neno

"...kwamba Muhammad ni mtumishi wa Allah na Mjumbe wake, kwamba Kristo ni mtumishi [wa Allah] na mtoto wa kijakazi wake na kuwa Yeye (Kristo) ni Neno lake aliloongea na Mariamu na ni roho Yake..."
"Yesu amekuwa akiitwa 'neno' ambalo Allah aliongea kwa Mariamu, ikionyesha kuwa aliumbwa kwa amri ya Allah, bila njia ya kawaida ya baba (Badawi). Kama ulimwengu wote uliweza kuumbwa kwa neno moja la Allah na Adam aliweza kuumbwa bila njia ya baba na mama, inaeleweka kabisa kwamba amri ya Allah inaweza kumuumba mtu bila kutumia njia ya baba."
(Sahih Muslim juzuu ya 1 rejeo la 220 chini ya uk.21-22)

(Sahih Muslim juzuu ya 1 rejeo chini ya uk.127) pia inasema Yesu anaitwa "Neno lake" mbinguni. Rejeo chini ya ukurasa linamaanisha "Amri ya Mungu" (yaani ameumbwa moja kwa noja na Mungu, na si neno au alibadilishwa kuwa mwili.)

Ni Waamini Tu Wanaoingia Paradiso

"...Hakika si wengine bali waamini watakaoingia Paradiso." (Sahih Muslim juzuu ya 1 kitabu cha 1 na.209, uk.65)

Bukhari
juzuu ya 5 kitabu cha 59 na.515, uk.364: "Alisimilia Abu Huraira : ... Nabii alisema, "Oh fulani na fulani! Simama juu na tangaza kuwa hakuna mtu mwingine yoyote isipokuwa muumini ndie atakaye ingia Paradiso..."

Je Muislam Anaweza Kumwamuru Mtu Aende Jehanamu?

Sahih Muslim juzuu ya 1 kitabu cha 1 na.284, uk.91 inasema kuwa Wakristo na Wayahudi wanaomcha Muhammad na hawabadiliki kuwa Waislam watakwenda Jehanamu.

"...Kisha Wayahudi wataitwa, na wataambiwa: mliabudu kitu gani? Watasema: Tulimwabudu 'Uzair [Ezekiel], mwana wa Allah. Wataambiwa: Mnasema uongo; Allah hajawahi kuwa na mke wala mtoto. Mnataka nini sasa? Nao watasema: Tunajisikia kiu, Oh Bwana wetu! Tuliza kiu yetu. Wataongozwa (kuelekea upande fulani) na kuulizwa: Mbona hamuendi kule kunywa maji? Kisha watasukumiwa kuelekea kwenye moto (na watafadhaishwa sana kwamba) ilikuwa ni njozi (na miale ya moto yenye hasira kubwa) itakuwa inajila yenyewe kwa yenyewe, na wataanguka motoni. Kisha Wakristo wataitwa na wataambiwa: Mliabudu kitu gani? Wao watasema: Tulimwabudu Yesu, mwana wa Allah. Wataambiwa: mnasema uongo; Allah hajawahi kujitwalia mke au mtoto. Kisha wataambiwa: Mnataka nini? Watasema: Tuna kiu, Oh Bwana wetu! Tuondelee kiu yetu. Wataelekezwa (kwenye upande fulani) na wataulizwa: Kwa nini msiende kule kupata maji? Lakini watasukumwa na kukusanywa pamoja kuelekea Jehanamu, ambayo ilikuwa kama njozi kwao, na miale ya moto itakuwa inajila yenyewe kwa yenyewe. Wataangukia motoni, hadi watakapomalizika wote isipokuwa yule aliyemwabudu Alah, kama atakuwa ni mcha Mungu au mwenye dhambi ...." (Kisha Allah atatokea kwa Waislam wote waaminifu na wanafiki akiwa na sura ya kudanganya ili awadhihirishe wanafiki. Kisha Allah atatokea kwao katika sura ya kweli [vyovyote ilivyo]. Sahih Muslim juzuu ya 1 kitabu cha 1 na.353, uk.117.

Waislam Wanaojiua Wanaenda Jehanamu

"...Mtu aliyejiua kwa kitu atateswa na kitu kile kile kwenye Siku ya Kiyama ...." Sahih Muslim juzuu ya 1 kitabu cha 1 na.199, 201, 202, uk.62.

Bukhari
juzuu ya 5 kitabu cha 59 na.515, uk.364 na juzuu ya 5 kitabu cha 59 sura ya 37 na.518, uk.367 zinasimulia kuhusu shujaa wa Kiislam aliyejeruhiwa vibaya sana, na alichukua mishale kadhaa toka kwenye podo lake na alijiua na akaenda Jehanamu.

"...Tulipokuwa kwenye mapigano makubwa sana mtu yule alipigana vibaya sana na alijeruhiwa. Ilielezewa: Mjumbe wa Allah, mtu ambaye mara ya kwanza ulimwita kuwa mkazi wa Motoni (Jehanamu) alipigana vibaya sana hata amekufa. Baada ya kusikia hivi Mtume wa Allah (amani na iwe kwake) alisema: Alikuwa amekwisha hukumiwa kwenda Motoni (Jehanamu). Baadhi ya watu walikuwa na mashaka makubwa (kuhusu hatima yake) waliposikia kuwa hakuwa amekufa bali ameumizwa karibu na kufa. Ulipofika usiku hakuweza kuvumilia (maumivu ya) jeraha lake hivyo akajiua." Sahih Muslim juzuu ya 1 kitabu cha 1 na.205, uk.63.

Upande mwingine,
Sahih Muslim juzuu ya 1 kitabu cha 1 na.211, uk.66 inasema kuhusu Muislam mmoja aliyekwenda Maka, akaugua, na kujikata maungio ya vidole vyake. Damu ilimtiririka hadi akafa. Baada ya hapo, Tufail, mtoto wa 'Amr alimwona kwenye ndoto, na alisamehewa na Allah, na mikon yake ilifunikwa.

Muhammad hakujisumbua kumwombea mtu ambaye amejiua mwenyewe. Sahih Muslim juzuu ya 2 kitabu cha 4 na.2133, uk.464.

Je Jehanamu Inafananaje?

"Nu'man b. Bashir alikuwa anahutubu na alisema: Nimemsikia Mjumbe wa Allah (amani na iwe kwake) akisema: Maumivu madogo zaidi kwa wakazi wa Jehanamu kwenye siku ya Kiyama yatakuwa kwa mtu ambaye chini ya nyayo zake kutakuwa na sehemu makaa mawili ya moto na ubongo wake utachemka kwa sababu ya hayo." (Sahih Muslim juzuu ya 1 kitabu cha 1 na.414, uk.139)

Falsafa ya Kiislam ya Majaliwa na Kupangwa kwa Vitu Vyote Toka Awali

"...Mtume wa Allah (amani na iwe kwake) alikuja usiku mmoja kumwona 'Ali na Fatimah (binti wa Nabii Mtakatifu) na alisema: Je huoni (Tahajjud) maombi? Mimi ('Ali) nilisema: Mjumbe wa Allah, hakika nafsi zetu ziko mikononi mwa
Allah na akitaka kutuamsha anatuamsha. Mjumbe wa Allah (amani na iwe kwake) aliondoka niliposema hivi kwake, alikuwa anaupiga mkono wake kwenye paja alipokuwa anaondoka, na nilimsikia akisema: Hakika binadamu hubishia vitu vingi sana." Sahih Muslim juzuu ya 1 kitabu cha 4 na.1701, uk.375. (Muhammad hakuruhusu jambo hili ila hakuwa na kitu kingine tofauti cha kusema.)

Pia, Allah alipanga tokea awali dhambi ya zinaa kwenye Bukhari juzuu ya 8 kitabu cha 77 sura ya 8 na.609, uk.397-398.

Kalamu zimekauka na hatima zimeanza kufanya kazi. Sahih Muslim juzuu ya 4 kitabu cha 31 na.6402 na rejeo la 2892 chini ya uk.1394.

Mambo Mchanganyiko Yahusuyo Uislam

* Unaweza kung'oa jicho la mtu kama anaangalia ndani ya nyumba yako bila ruhusa yako. Sahih Muslim juzuu ya 3 kitabu cha 23 na.5370-5371, uk.1180.
* Utumbo wa mtu mnafiki utamwagika Jehanamu Sahih Muslim juzuu ya 4 kitabu cha 40 na.7122, uk.1539.
* Shetani anaingia kwako unapopiga mwayo. Sahih Muslim juzuu ya 4 kitabu cha 40 na.7130, uk.1540.
* Usiende msikitini baada ya kula kitunguu saumu, kitunguu kibichi, n.k., kwa sababu malaika wanadhurika na vitu hivyo hivyo kama binadamu. Sahih Muslim juzuu ya 1 kitabu cha 4 na.1147, uk.280.
* Miujiza ya siku za mwisho wakati dunia itakapotapika vipande virefu vya fedha Sahih Muslim juzuu ya 2 kitabu cha 5 na.2210, uk.485.
* Kugawanyika kwa mwezi wakati wa uhai wa nabii. Sahih Muslim juzuu ya 4 kitabu cha 37 na.6721, 6724-6730, uk.1467-1468. Habari hii pia ipo kwenye Bukhari juzuu ya 4 sura ya 26 na na.830, uk.533; Bukhari juzuu ya 4 kitabu cha 56 sura ya 26 na.831, uk.533; juzuu ya 4 kitabu cha 56 sura ya 26 na.832, uk.534.
* Watu wote walipigwa na Shetani isipokuwa Yesu Sahih Muslim juzuu ya 4 kitabu cha 31 na.6429, uk.1399.

Kuaminika kwa Hadithi Kulikolindwa

Sahih Muslim inaanza Hadithi zake nyingi kwa kusema "... aliripoti/alisema" au msemo mwingine unaofanana na huo. Mara nyingi misemo inayofanana inarudiwa mmoja baada ya mwingine, huku ukiwa na maneno tofauti kidogo kiasi, watu tofauti wanaoripoti. Kitu cha kufurahisha ni kwamba Sahih Muslim juzuu ya 4 kitabu cha 28 na.5777, uk.1250 inasema kuwa wandani wa Muhammad walikufa mwaka 100 BH (Baada ya Haji). Hii itakuwa karibu mwaka 720 BK. Sasa Imam Muslim, mkusanyaji wa Hadithi alikufa mwaka 875 BK, au miaka 150 baada ya kufa kwa wandani hao. Nyakati nyingine watu ambao walihusika na baadhi ya maelezo walikufa miaka michache tu baada ya Muhammad. Kwa hiyo kwa kiasi kikubwa una maelezo kutoka kwenye vyanzo visivyokuwa na makosa, kama vile mke wa Muhammad, akifuatiwa na miaka 150 hadi 250 isiyokuwa na mtiririko wa uenezaji. Imam Muslim anaweza kuwa anaujua "mnyororo wa uenezaji" wa baadhi ya misemo hii, lakini hakusema ilikuwa ni nini. Kwa hiyo tunaposoma kuwa Abu Hureira au 'Aisha alisema kitu fulani ambacho kilinukuliwa, usidhani kuwa Imam Muslim alisikia maneno hayo moja kwa moja.

Hitimisho:
Kwa kuwa mkusanyaji wa Sahih Muslim, Imam Muslim alikufa mwaka 875 BK (na Bukhari mwaka 870 BK.) Waislam walikuwa na miaka karibu 125 hadi 250 "miaka ya iman" ambayo Hadithi zilikusanywa kwa usahihi.

Jambo hili linatofautiana na kuaminika kwa maandiko ya Agano Jipya. Yesu alikufa mwaka 33 BK, na Agano Jipya liliandikwa mwaka 50 hadi 90 BK, kwa hiyo kuna miaka 17 hadi 40 "miaka ya imani" kwenye kumbukumbu za waandishi wa Injili. Pamoja na hayo, maandiko ya zamani zaidi ya Agano Jipya ambayo yamehifadhiwa yaliandikwa kuanzia mwaka 100 hadi karibu 175 BK, hivyo ni karibu miaka 35 hadi 125 "miaka ya imani" ambamo kile kilichoandikwa kilihifadhiwa kwa njia ya kuaminika.

Hitimisho:
Kutokea kifo cha Yesu hadi kwenye maandiko ya zamani zaidi ya Agano la Jipya yaliyohifadhiwa kuna miaka karibu 77 hadi 142 "miaka ya imani" ambamo ndani yake yanapatikana mafundisho ya kweli ya Yesu. Hivyo, kuna "miaka ya imani" michache zaidi ambamo ndani mwake mnapatikana mafundisho ya Yesu kuliko "miaka ya imani" ambamo ndani mwake mnapatikana Hadithi za Kisuni.

Ujumbe wa Ukweli

Unaweza kuwa huamini kuwa nyingi za nukuu za kwenye andiko hili ni mafundisho ya kweli ya Mungu; mimi pia siamini. Lakini inashangaza sana kuona kuwa zaidi ya watu bilioni moja wametumia Sahih Muslim kama moja ya mamlaka kubwa zaidi za dini na sheria kwa zaidi ya miaka 1,000.

Usivunjike moyo kutafuta mafundusho ya kweli ya Mungu wa kweli; badala yake ongeza wigo wa utafiti wako zaidi ya mambo ambayo watu wamesema kuwa unapaswa kuyaamini. Unajua, nitasema hata hivi, Uislam unasema vitu vichache sana kwa usahihi. Unasema kwa usahihi kuwa Yesu alikuwa nabii wa Mungu. Kama Hadithi na tamaduni za Kiislam zimeshindwa kuwa mwanga wa kiroho, angalia maneno ya Yesu.
Kwa habari zaidi tembelea www.MuslimHope.com

For more info contact www.MuslimHope.com