Maswali ya Biblia Toka 1 Wathesalonike

 

S: Kwenye 1 The 1, tunajua nini kuhusu mji wa Thesalonika?

J: Thesalonica ulikuwa mji “moto.” Awali uliitwa “Therma” kwa sababu ya chemichemi za moto zilizokuwa karibu na mji huu. Ghuba hii inaitwa “Ghuba ya Thermaiki” (Thermaic Gulf). Mmoja wa majenerali wa Alexander Mkuu, aliyeitwa Cassander, alimuoa dada wa kambo wa Alexander, aliyeitwa Thessalonica. Asimov’s Guide to the Bible uk.1060 inasema kuwa alijenga mji mpya karibu na Therma kwa heshima yake. Mji wa Thesalonike ulikuwa na idadi kubwa ya Wayahudi. Ulikuwa ni mji mkubwa zaidi kwenye jimbo la Makedonia karibu watu 200,000. (Kwa kulinganisha, mji wa Korintho ulikuwa na watu 650,000).

   Mji wa Thesalonike ulikuwa wa kipekee kwa maana ya kuwa ulikuwa mji mkuu wa Kirumi wa jimbo la Makedonia, na mji huru uliotawaliwa na magavana sita waliochaguliwa kwa kura walioitwa “politarchs.” Luka alitumia jina hili kwenye Mdo 17:6, na kuna baadhi ya watu ambao waliotiliashaka usahihi wa Luka kwani msemo huu haufahamiki. Hata hivyo, kuanzia wakati huo wataalamu wa mambo ya kale wamevumbua maandishi kumi na tisa yaliyoandikwa kwenye vitu mbalimbali yanayotumia msemo huu kwenye serikali ya Makedonia.

 

S: Ni kwa jinsi 1 Thesalonike unafanana na nyaraka nyingine za Paulo?

J: Haya ni mambo tuliyoyaona.

 

1 Thesalonike

Nyaraka nyingine

Vitabu vingine

Silwano badala ya Sila. 1 Thess 1:1

Luka mara zote anatumia jina la Sila. Nyaraka za Paulo zinatumia jina la Kigiriki Silwano kwenye 2 Kor 1:9; 2 The 1:1

1 Pet 5:12 (Silwano)

1 The 1:2 kazi ya imani, taabu ya upendo, na saburi ya tumaini; 1 The 5:8

1 Kor 13:13 imani, tumaini, upendo . . ., Gal 5:5, 6; Kol 1:4,5;

Ebr 6:10-12; 22-24; 1 Pet 1:21, 22

Mkazo upo katika furaha. 1 Th 1:6; 2:19; 2:20; 3:9; 5:16

Waraka wa Wafilipi hutumia neno furaha mara 19

 

Neno la Bwana kupitia kwao lilienea kote 1 The 1:8

~Rum 1:8

-

1 The 2:5b Mungu ni shahidi

-

Mwa 21:30; 31:50; Amu 11:10; 1 Sam 12:5; 20:23; 20:42; Mal 2:14

1 The 2:8; 2:17; 3:6 Paulo/Epafrodito watamani kuwaona

Rum 1:9-11; Fil 1:8; 4:1; Fil 2:26; 2 Tim 1:4;

-

Nia ya kutokuwa mzigo, kuuchukua mzigo 1 The 2:6, 9

2 Kor 8:13; 11:9; 12:13, 14, 16; Gal 6:2, 5

Mat 11:30; 20:12; Ufu 2:24

Kujitaabisha au kuomba usiku na mchana 1 The 2:9; 3:10

2 The 3:8; 1 Tim 5:5; 2 Tim 1:3;

Usiku na mchana Ufu 4:8; 7:15; 12:10; 14:11; 20:10; Mdo 26:7 (mchana na usiku, Paulo anasema); Mdo 20:31 (usiku na mchana, Paulo anasema)

1 The 2:18 Paulo aliingiza jina lake hapa

2 The 3:17

2 Pet 3:15-16

1 The 2:19 uwepo wa Bwana wetu Yesu Kristo

2 Tim 4:1

-

Wamekuwa furaha au taji la Paulo. 1 The 2:19

Wamekuwa furaha na taji la Paulo. Fil 4:1

 

Haja yao ya kukutana na Paulo 1 The 3:6

2 Kor 7:7; 1 Tim 3:6

-

1 The 3:8 simama imara katika Bwana

Fil 4:1; Efe 6:10, 16; 2 The 2:15

 

1 The 3:10 kutengeneza mapungufy ya imani yao

Efe 4:12

 

1 The 4:13 msikose kujua

Rum 11:25; 1 Kor 10:1; 1 Kor 12:1

-

1 The 5:5 wana wa nuru

Efe 5:8-11

 

1 The 5:14 onyo dhidi ya uvivu

2 The 3:6, 10

 

1 The 5:21a Jaribuni mambo yote

~Rum 12:2; ~1 Kor 11:28; ~2 Kor 8:8; ~2 Kor 13:5; Gal 6:4

-

1 Thess 5:23 The God of peace

Rom 15:33; Rom 16:20; ~1 Cor 14:33;

Heb 13:20

1 The 5:26 Wasalimuni ndugu wote kwa busu takatifu

Rum 16:16; 1 Kor 16:20; 2 Kor 13:12

~1 Pet 5:14 busu la upendo

 

S: Kwenye 1 The 1, muhtasari wa waraka huu ukoje?

J: Ufuatao ni muhtasari wa waraka huu:

1 Je unamshukuru Mungu kwa ajili ya watu wake? Namna, mazingira na sababu

2-3 Kuitambua huduma ya Paulo

     2:1-16 Maelezo ya kuhubiri kwake: jinsi alivyowasilisha, na jinsi walivyoyapokea

     2:17-3:10 Maelezo kuhusu kutokuwepo kwake: huzuni yake, mipango yake ya sasa, na shukrani

     3:11-13 Sala kwa ajili ya maongozi, upendo na nguvu

4-5 Maelekezo kwa watu wa Mungu

     4:1-12 Maelekezo binafsi: maboresho, usafi wa kingono, na upendo wa kindugu

     4:13-5:11 Tumaini la kurudi kwa Yesu mara ya pili: Wafu katika Kristo na Siku ya Bwana

     5:12-22 Maelezo kwa kanisa: viongozi, watu wote, mtu mmoja mmoja, na kuabudu

 

S: Kwenye 1 The 1:2, Paulo alisema anamshukuru Mungu mara ngapi kwa ajili ya waumini hawa? Kwa nini mara nyingine tunakosa kutoa shukrani kama tunavyotakiwa kwa ajili ya waumini wengine?

J: Paulo alisema alimshukuru Mungu wakati wote kwa ajili yao. Amesema kwenye nyaraka zake zote isipokuwa kwa Wagalatia kuwa anamshukuru Mungu kwa ajili ya watu anaowaandikia. Wakati mwingine hatuwezi kufanya hivyo kama hatutakuwa tunatambua hadhi yao, au hatushukuru njia (hata kama si zenye kufurahisha wakati wote) ambazo Mungu anazitumia kwenye maisha yetu. Lakini licha ya jinsi tunavyohisi, na hata kama mmoja wa waumini hataonekana kama anaweza kutufanyia kitu chochote, tunapaswa kumshukuru Mungu kwa kuwaumba kama kazi nzuri ya mikono yake, wameumbwa kwa mfano wako. Tutakuwa nao tukifurahia urafiki na ushirika nao milele, hivyo ni busara kuanza kuwashukuru sasa.

   Wakati mwingine tunaweza kujawa ubinafsi hata tukamsahau Mungu na watu walio pamoja nasi, na kujifungi kwenye ulimwengu wetu wenyewe ulio mdogo. Kwa busara, tunapaswa kutafuta kuuangalia ulimwengu na maisha yetu kama Mungu anavyoyatazama.

 

S: Kwenye 1 The 1:2 na Fil 1:3, tunawezaje kuwa na shukrani kila wakati tunapoomba?

J: Tunapaswa kuomba bila kukoma, na maombi yetu yanapaswa yajawe shukrani. Shukrani si tu maneno tunayoyasema, bali fikara za namna ya kuisha maisha yetu. Kama wimbo mmoja wa Kikristo unavyosema, “Kabla sijaleta mahitaji yangu, nitaleta moyo wangu.”

 

S: Kwenye 1 The 1:2-8, ni sababu gani hasa ambazo zilimfanya Paulo kushukuru kwa ajili ya Wathesalonike?

J: Zifuatazo ni sababu nane ambazo Paulo alizitoa hapa:

1 The 1:3 Kazi yao iliyotokana na imani

1 The 1:3 taabu yao iliyosukumwa na upendo

1 The 1:3 saburi yao iliyovuviwa na tumaini lao kwa Yesu.

1 The 1:4 Walikuwa wamechaguliwa na Mungu.

1 The 1:6 Walikuwa wafuasi wa Paulo, Sila, na Timotheo na Bwana.

1 The 1:6 Walilipokea neno kwa furaha waliyopewa na Roho Mtakatifu

1 The 1:7 Walikuwa mfano kwa waumini wote walioko Makedonia na Akaya.

1 The 1:8 Kutoka kwao neno la Mungu lilienea kila mahali.

Tunapaswa kuwa na shukrani kwa Mungu kwa ajili ya watu wengine kwa sababu kama hizi.

 

S: Kwenye 1 The 1:6, ni kwa jinsi gani ni sahihi kusema tu wafuasi wa mtu (mbali ya Kristo). Ni kwa jinsi gani si sahihi kusema tu wafuasi wa watu?

J: Paulo anatuambia tumuangalie yeye na viongozi wetu wa kiungu kama ambavyo wao nao wanamfuata Kristo (Fil 3:17; 1 The 1:6; Ebr 13:7). Tunapaswa kuwatii viongozi wetu na kujinyenyekeza kwao katika Bwana (Ebr 13:17). Kwa maneno mengine, tunapaswa kuwatii viongozi wetu, tukitambua kuwa maagizo ya Mungu yanabatilisha vitu vyovyote vilivyo tofauti watakavyovisema. Lakini hatupaswi kumuita mtu yeyote Baba yetu; Mungu tu ndiye Baba yetu kwa mujibu wa Mat 23:9.

 

S: Kwenye 1 The 1:7, je umewahi kufikiria kuwa kielelezo? Ni vitu gani vinanvyo husika na jambo hilo?

J: Kama watu wanajua kuwa u Mkristo, basi wewe tayari ni kielelezo. Swali ni kwamba je u kielelezo kizuri au siyo.

 

S: Kwenye 1 The 1:7-10, ni namna gani tunapaswa kujali jinsi watu wasiokuwa Wakristo wanavyofikiri kuhusu Wakristo? Ni kwa jinsi gani hatupaswi kujali?

J: Tunapaswa kuwa na ushuhuda chanya tunapoishi maisha matakatifu. Tunapaswa kuwapenda watu wengine kwa kweli, na kuonyesha upendo wetu. Hatupaswi kujaribu kuwakwaza watu wengine. Lakini tunatakiwa kukumbuka kuwa injili yenyewe inakwaza. Hatupaswi kujali endapo watu wanakwazika na ujumbe wetu. Tunapaswa kuwapenda watu kuliko tunavyopenda urafiki wetu na wao, hata kuhatarisha kuwashirikisha injili.

 

S: Kwenye 1 The 1:8, ni kwa jinsi gani imani ya Wathesalonike ilivuma kila mahali?

J: Imani yao ilifahamika sana miongoni mwa Wakristo kila mahali. Lakini kama ambavyo pembe husambaza sauti kila mahali bila kubagua, ndivyo neno la Mungu linavyopaswa kuenea kutoka kwetu.

 

S: Kwenye 1 The 1:9, kuna sababu gani tofauti iliyomfanya Paulo kutoa shukrani kwa ajili ya Wathesalonike?

J: Sababu za awali zilikuwa ni jinsi waumini hawa walivyokuwa, na mahali ambako walikuwa wanaenda. Lakini sababu hii ni furaha tu ya kutambua umbali mkubwa ambao wamwkuja kutoka kule walikokuwa.

 

S: Kwenye 1 The 2:1-4, kwa nini Paulo anasistiza kuwa ziara yake haikuwa hasara?

J: Kwa kiasi fulani Paulo alikwamishwa kutimiza malengo yake Makedonia. Mahali pengine, Paulo alikuwa na mafanikio makubwa sana bila upinzani. Sehemu nyingine kama Kipro, kulikuwa na upinzani kutoka kwa mtu mmoja, lakini Mungu alimshughulikia mtu Yule kikamilifu. Lakini baada ya Filipi, walilazimika kuondoka kwenye ukanda wa Makedonia kwa sababu ya upinzani. Huenda Paulo alijiuliza ni mambo kiasi gani zaidi ambayo angeweza kuyafanya endapo upinzani wa shetani usingemzuia kuwepo pale muda mrefu zaidi. Lakini Mung anaweza kuutumia hata upinzani wa shetani kwa utukufu wake. Paulo alikwisha weka alama kubwa sana Filipi na Thesalonike, na upinzani ulimlazimisha kwenda Berea, Athene, na hasa Korintho.

   Kwa mtazamo wa muda mrefu, muda mfupi ambao Paulo alikaa kwenye miji ya Filipi na Thesalonike iliyo Makedonia uliishia kuwa wa manufaa sana. Siku za baadaye, Wamakedonia walikuja kuwa wakarimu sana, hata kujitoa licha ya umaskini wao kwenye 2 Kor 8:1-5. Baadhi ya Wamakedonia wanaweza kuwa walikwenda na Paulo Korintho kwenye 2 Kor 9:2-4, na Paulo alisumbuliwa na mawazo kuwa kanisa la Korintho lingeonekana kuwa choyo mbele ya Wamakedonia. Kwenye historia ya kanisa la awali, Askofu Polycarp aliliandikia barua kanisa la Filipi. Tertullian anayataja makanisa ya kimitume ya Korintho, Filipi, Thesalonike, na Efeso (lakini siyo Athene) kwenye Prescription Against Heretics sura ya 36, uk.260.

 

S: Kwenye 1 The 2:2-4, unawezaje kuielezea huduma ya leo kuwa kimsingi imefanikiwa au imeshindwa?

J: Kwanza kabisa, ni uaminifu kwa kweli ya Mungu na moyo. Ni kwa jinsi gani (kama inawezekana) huduma inajitia matatani? Watu wanabarikiwaje na huduma? Yeremia alikuwa na huduma yenye mafanikio, ingawa katika nyakati zake Baruku alikuwa ni mmoja wa watu pekee tunaowajua waliomfuata. Mafanikio ni kufanya mambo ambayo Mungu anakutaka ufanye, na kuwa jinsi Mungu anavyotaka uwe.

 

S: Kwenye 1 The 2:3, neno la Kigiriki dolo linaweza kumaanisha si kudanganya tu, bali pia kughilibu, kwa ujanja, chambo au mtego. Ni njia gani za “ujanja ambazo hatutakiwi kuzitumia kwenye kazi ya Mungu?

J: Msemo Bait and switch (tega kisha badilisha) unaomaanisha kuahidi kitu komoja lakini kuleta kitu kingine. Tunapaswa kuwasilisha vitu kama vilivyo kweli. Watu wasishangazwe wanapomwamini Yesu, au wanaposikia vitu ambavyo ni tofauti kabisa kuliko walivyosikia kabla hawajamwamini Yesu. Hatunapaswi kushirikisha nusu ya injili, bali injili kamili. Tunapaswa kuwaambia kuhusu jehanamu na mbinguni pia, utiifu na neema, na Yesu kuwa Bwana na Yesu kuwa Mwokozi. Tusitoe au kumaanisha kuwa Mungu anatoa ahadi ambazo hazitaweza kuzitimizwa.

 

S: Kwenye The 2:4, kuna jambo gani lisilokuwa la kawaida kuhusiana na mstari huu?

J: Mstari huu umeundwa na maneno yenye matamshi yanayofanana. Unaweza kutafsiriwa, “Kama Mungu, anayepima mioyo yetu, amethibitisha kwa kupima kufaa kwetu kupewa dhamana ya injili”, kwa mujibu wa The Expositor’s Greek Testament, uk.26-27.

 

S: Kwenye 1 The 2:4, ni kwa namna gani huduma yenye kutaka kuwapendeza wanadamu ingeweza kuonekana tofauti kulinganisha na huduma yenye kutaka kumpendeza Mungu?

J: Huduma ambayo lengo lake la msingi ni kuwapendeza wanadamu, inasistizia mikakati na namba (takwimu). Mengi ya maongezi katika huduma hii ni jinsi ya kupata watu zaidi, jinsi ya kupata fedha zaidi, au jinsi ya kupata fursa mpya za kukua. Huduma ya namna hii inakabiliwa na hatari ya “kubadilika ili kufaa hali au malengo mapya” hata kuweza kuyaacha mambo yake ya msingi.

   Huduma ambayo lengo lake la msingi ni kumpendeza Mungu itasistiza maombi. Mengi ya maongezi yake yatakuwa jinsi ya kuongea na watu wengi zaidi habari za Yesu, jinsi ya kuwajenga washiriki vizuri zaidi, na jinsi ya kuwahudumia watu wengine. Tofauti ya msingi ni kuwa huduma hii inapenda kuwahudumia watu wengine badala ya kuhudumiwa. Jambo hili linaweza kumaanisha kushirikiana na huduma nyingine, au hata kutoa rasilimali zake kwa huduma nyingine, badala ya kutafuta kujenga himaya yake yenyewe.

 

S: Kwenye 1 The 2:5, kuna tofauti gani kati ya kutoa sifa zisizokuwa za kweli, jambo ambalo ni baya, na kutoa sifa za kweli, jambo ambalo linaweza kuwa zuri?

J: Kutoa sifa za uongo hakumwelezi mtu kwa ukweli. Kunaweza kuwa uongo dhahiri, au kunaweza kutoa msistizo kwenye mambo madogo au ya juu juu tu na kuyaacha mambo makubwa na ya msingi. Kuwasifia watu kwa mambo ambayo wameyafanya au mwenendo wao, kukiwa ni kwa kweli, ni njia nzuri ya kuwatia moyo.

 

S: Kwenye 1 The 2:5, ni kwa jinsi gani watu hujifunika kinyago ili kuficha tamaa ya vitu?

J: Huwa wanajaribu kusema, kwa viwango tofauti vya mafanikio, kuwa kuna lengo lingine tofauti, kama vile kuwasaidia watu wengine, kusaidia taasi, n.k. wakati lengo lao la msingi ni  kujipatia vitu. Kuna masomo mengi sana ya uongozi, hakuna upungufu wa watu wanaotaka kuwa viongozi.

   Maana ya moja kwa moja ya neno la Kigiriki, pleonexia, ni hamu ya kupata vitu zaidi.

 

K: Kwenye 2 The 2:8, ni kwa namna gani tunapaswa kuweka mambo yetu wazi, badala ya kuyaficha?

J: Tunapaswa kuweka wazi sehemu kubwa ya maisha yetu, mambo tunayofanya vizuri hata yale tunayoshindwa kufanya vizuri, lakina hatutakiwi kuweka wazi kila kitu. Tusiwaambie watu wengine kitu ambacho Mungu hataki tuseme, hivyo basi muombe Mungu auonyeshe moyo wako wakati wa unaotakiwa kuwa kimya. Ifuatayo ni orodha yenye kufuata alfabeti za Kiingereza za mambo ambayo hatutakiwi kuwaambia watu wengine.

Kukasirisha watu wengine, isipokuwa tu wanapokasirishwa na mambo mengine.

Kujisifia au kuongea kwa kujivuna

Mambo ya siri ambayo watu wengine wamekuambia, bila kujali kama walipaswa kuwaambia watu hao

Mambo ambayo yanaweza kuwavunja moyo au kuwakatisha tamaa watu wengine kudumu katika haki, kama ambavyo mke wa Ayubu alifanya. (Lakini ni jambo jema kuwakatisha tamaa watu kuendelea kufanya dhambi).

Kutukuza dhambi. (Nilipokunywa pombe kwenye baa nilijisikia vizuri sana . . .)

Mambo ya uongo, likiwemo kutoa sifa za uongo

Kutukuza watu wengine, kuwaweka mahali ambapo wanahusudiwa bila kuonywa. (Hata hivyo ni vyema kuheshimu watu wengine).

Maambo yenye kuwadhuru au kuwaumiza watu wengine

Maneno au fikara zisizo na heshima (kuwadharirisha watu wa chini, wasiopendeka, au watenda dhambi wanaoelekea hukumuni)

Kuhukumu watu wengine, ingawa ni sahihi kuyaita “dhambi” matendo ambayo ni dhambi

Kuongea kwa kukusudia kuwa watu wasiamini mamneno yetu

Maneno mengi, yenye kona kona nyingi, na yasiyo na ulazima wa kusemwa, kumwambia mtu maneno mengi kuliko anavyohitaji kusikia

Habari za hila zenye lengo la kuwadhuru watu wengine au kujifurahisha wakati wao wanaumia

Habari binafsi za mtu ambazo hapendi zielezwe kwa watu wengine (bila kujali endapo unafikiri wako sahihi kutokutaka habari hizo zisielezwe kwa watu wengine).

Kutumia maneno ya mtu mwingine kwenye kazi zako bila kusema ulikoyatoa. Usiibe maneno ya watu wengine kwa kuyatumia kama yako bila kusema ulikoyatoa.

Usahihi wenye mashaka (hauna uhakika endapo maneno hayo ni sahihi au la)

Kuongelea tena jambo baya ambalo mtu alilifanya zamani, hata baada ya kuwa uliishaliongelea na kumsamehe. Jambo hilo linapaswa kusahauliwa.

Siri ambazo zinaweza kumfanya mtu asiye na kosa auawe, aumizwe, au afungwe gerezani pasipo kustahili

Mambo ambayo yanawatia watu wengine majaribuni. (Wakati ule nilipokunywa pombe kwenye ile baa, ambapo vinywaji vilikuwa vinauzwa nusu ya bei yake ya kawaida . . .)

Habari zisizofahamika na watu wengine ambazo ulimuahidi mwajiri wako wa sasa au wa zamani, au mteja kuwa hautazitoa kwa watu wengine.

Kutukana watu wengine

Watu waovu wanaweza kutumia kwa manufaa yao

Maneno yasiyo na heshima, yenye kuhusu ngono yasiyopaswa kusemwa mbele ya watoto wadogo

Maneno yanayokufanya usiumheshimu Mungu au wakristo wenzako

Watu wanapaswa kuyaona maisha yako katika vitendo, lakini hupaswi kujiona kuwa unalazimika kusema kitu kila wakati.

 

S: Kwenye 1 The 2:9, kwa nini Paulo alihitaji kufanya kazi ili kujipatia mahitaji yake alipokuwa kwao?

J: Paulo hakuwaomba watu wasiokuwa waumini waumini wachanga aliokuwa anawahubiria wachangie huduma yake. Katika dini ya Kiyahudi, waalimu (marabi) hawakuruhusiwa kuishi kwa kutegemea huduma yao ya kufundisha sheria, kwa mujibu wa New International Bible Commentary, uk.1462. Kwenye baadhi ya nchi za Kiislamu, watumishi wa Kikristo wanadharauriwa kimakosa kama wavivu na watu wasiowajibika wenye kujinufaisha kwa jasho la watu wengine. Lakini mmishenary anayefanya kazi ya pili ili kujipatia mahitaji yake, anayefanya kazi nyingine isiyokuwa ya kidini, hawi na shida hii. Paulo na Petro na wamishenari wa leo wanayo haki ya kuchangiwa kikamilifu na kanisa kwa ajili ya huduma yao. Hata hivyo, kwa ajili ya kufanya kwake kazi miongoni mwa watu aliokuwa anawahubiria, Paulo alichagua kutokuitumia haki yake hiyo.

   Kazi za mikono zilikuwa zinadharauliwa kiasi fulani na Wagiriki na Waroma wa tabaka la juu, lakini hazikudharauliwa na Wayahudi.

 

S: Kwenye 1 The 2:10, kungetokea nini endapo maisha ya mtendakazi wa kikristo, ama mmishenari ama mtumishi mwingine yeyote yule, yangekuwa na lawama?

J: Jambo hilo lingeweza kuathiri ushuhuda wao watu wanapofahamu. Hata waumini wenzao, wanaowaona kama kielelezo, wanaweza kufikiri kuwa kwa kuwa mtumishi huyu ameshindwa kwenye eneo fulani, basi si jambo la ajabu endapo na mimi nitashindwa kwenye eneo hilo. Lakini mtumishi anaweza kutubu na kuendelea kumtumikia Bwana, akiwaambia watu wengine wajiepushe kufanya kosa hilo alilolifanya.

 

S: Kwenye 1 The 2:11-12, ni kwa jinsi gani mstari huu unaweza kuwa muhtasari wa kufanya wafuasi, kutoa ushari nasaha, au hata kushuhudia?

J: Ingawa mstari huu hausemi bayana kitu cha kufanya, una maelezo mengi ya namna ya kufanya huduma hizi. Kutia moyo, kufariji, na kuinua watu wengine. Paulo anasema alifanya hivi kama ambavyo mama mzuri (1 The 2:7) au baba mzuri (1The 2:11) angefanya kuwasaidia watoto wake.

 

S: Kwenye 1 The 2:13, inawezekanaje neno la binadamu mwenye ukomo, asiye mkamilifu , na anayeweza kutenda dhambi, liwe neno la Mungu?

J: Inaweza kuonekana kuwa haiwezekani endapo tutaangalia tu madhaifu ya mwanadamu. Lakini, Mungu Mwenye enzi yote, ambaye hakuna jambo lisilowezekana kwake (Mat 19:26; Marko 10:27; Luka 1:37), aliweza kuwasilisha ujumbe wake kwa Balaamu hata kwa kumtumia punda. Mungu Mwenyezi ana nguvu na ufahamu mkubwa hata anaweza kuwasilisha ujumbe wake kwa wazi kupitia vyombo visivyo vikamilifu. Si tu kwamba Mungu aliongea kwa ufasaha uliotakiwa, lakini pia aliyatunza maneno yake kwa ufasaha na usahihi uliotakiwa kwa hiyo tunaweza kuuelewa ujumba wake.

   Swali zuri zaidi kuuliza ni kuwa, kwa vile tunaweza kuongea kupitia neno la wanadamu, unawezaje kufikiri kuwa Mungu mwenye nguvu zotehana uwezo wa kuongea kupitia neno la wanadamu?

 

S: Je 1 The 2:14-15 kinaweza kuwa kifungu chenye kuwapinga Wayahudi?

J: Hapana. Hakuna mtu anayeweza akasema kwa udhati kuwa kifungu hiki kinawapinga Wayahudi kama kabila au taifa, kwani Paulo alikuwa Myahudi, ambaye kama Rum 3:1-2 inavyoonyesha, aliona faida kubwa sana katika urithi wake. Watu wengine wanaweza kufikiri kuwa kifungu hiki kinaipinga dini ya Kiyahudi.

   Hata hivyo, kifungu hiki hakiipingi dini ya Kiyahudi, kwani kiliandikwa na mtu aliyewapenda Wayahudi na kuwajali sana, ingawa hawakumkubali Kristo, kama Rum 9:1-5 na 10:1 inavyoonyesha.

   Ni muhimu kujua kuwa kuna watu wanaofikiri kuwa vitu kadhaa vinawapinga kwa sababu vinaongelea jambo hasi kuhusu mtu yeyote Yule kwenye kabila au taifa lao. Nahisi kuna mtu atakuja kusema kuwa Biblia inawapinga watu wote, kutokana na ufafanuzi huu wa ajabu, kwani Biblia inasema wote wamefanya dhambi na kuoungukiwa na utukufu wa Mungu, na kuna watu ambao hawapendelei kukosolewa kwa namna yeyote ile au maoni hasi kuhusu kitu chochote kile.

 

S: Kwenye 1 The 2:15, kwa nini Paulo alisema kuwa kuna Wayahudi waliokuwa wanawachukia watu wote, kwani bila shaka Wayahudi hao walikuwa na marafiki na watu wengine waliokuwa wanawajali?

J: Hebu tuchukulie kuwa hivyo, Wayahudi hawa wangewezakuwa wanajifanya kuwa marafiki wa watu wengi. Hata hivyo, kama walikuwa wanawashawishi watu kumkataa Yesu, kwa namna kubwa zaid waliyoweza, walipingana na watu wote.

 

S: Kwenye 1 The 2:16, kwa kuwa Mungu ni mwenye upendo, je watu wanawezaje kufanya dhambi hadi zikafikia kikomo?

J: Rum 11:22 inatuagiza kuzingatia wema na ukali wa Mungu. Mungu ni nafsi yenye upendo zaidiulimwenguni, lakini pia ni mwenye ukali zaidi. Paulo aliwahi kukabiliana na watu waliojaribu kuwazuia watu wengine kusikia neno la Mungu kwenye Mdo 13:8-11 alipomkabile Elima.

 

S: Kwenye 1 The 2:17, maana halisi ya neno la Kigiriki lenye kumaanisha “kumefarakana”, aporthanisthentes, ni kufanywa yatima. Kwa nini Paulo alifanya hima kuona kuwa waumini hawa wachanga “hawawi yatima”?

J: Paulo alifanya hima kuona kuwa yeye na watumishi wenzake hawawi na juhudi ya kuieneza imani. Hata hivyo, wako watu wanaodhani kuwa kulikuwa na jambo lililokuwa la muhimu zaidi. Kwamba wangeweza kupotoshwa au kudanganywa na Wayahudi au watu wenye kufuata mafunzo ya uongo kuiacha imani yao. Vivyo hivyo, tunapomsaidia mtu kuja kw Kristo, tunapaswa kuwalinda dhidi ya waalimu wa uongo.

 

S: Kwenye 1 The 2:18; 2 The 3:17, je kwa kuingiza maneno haya “Mimi, Paulo” hapa kunawezakuonyesha kuwa kitabu hiki kiliandikwa miaka mingi baada ya muda unaoaminiwa kuandikwa lakini si kuwa kiliandikwa na mwandishi mwingine?

J: Hapana. Paulo hakufanya hivi kwenye barua zake, lakini Waraka kwa 1 Wathesalonike uliandikwa na Paulo, Silwano, na Timotheo, na maneno haya hayawi ya kweli kuhusiana na watu wengine, kama vile Timotheo ambaye hakurudi kule walikokuwepo. Maneno haya ni ya kweli kuhusiana Paulo tu, hivyo Paulo aliyasema kuhusiana nay eye mwenyewe tu. Paulo pia amelitaja jina lake kwenye 2 The 3:17.

 

S: Kwenye 1 The 2:19, je tutaweza kuwatambua watu mbinguni?

J: Ndiyo. Kwenye 1 The 2:19 na Fil 4:1, Paulo kuwa waumini hawa ndio waliokuwa furaha na taji yake, na kwa hakika ataweza kuitambua taji yake. Kuna uwezekano kuwa hatutaonekana kama tulivyo sasa wakati tutakapokuwa na miili ya utukufu, lakini tutaweza kutambuana.

 

S: Kwenye 1 The 2:19; 3:13; 4:15; 5:23; 2 The 2:1, 8, 9; 1 Kor 15:23; Yak 5:7, 8; 2 Pet 1:16; 3:4, 12; 1 Yoh 2:28; Mat 24:3, 27, je kuna jambo gani lisilokuwa la kawaida kuhusiana na neno la Kigiriki, parousia, lenye kumaanisha kuja kwa Kristo?

J: Kuna maneno matatu ya Kigiriki yaliyotumika kwenye Biblia yenye kumaanisha kuja kwa Kriso: parousia (kuja na kuwepo kwake baada ya kuja), apokalupsis (kuondolewa utando, kufunuliwa, au apokalipsi), na ephiphaneia (kudhihirishwa au ufunuo ‘epifania’).

Neno hili linamaanisha kuja na kuendelea kuwepo. Kwenye maandiko yasiyokuwa ya Kibiblia, ziara ya mtawala iliitwa parousia.

 

S: Kwenye 1 The 3:1-3 na 6, kwa nini mtu aliyekuwa kwenye nafasi ya Paulo aliweza kufikiri kuwa wao tu ndio ambao wangeweza kuhubiri vizuri zaidi? Kwa nini Paulo hakuwa na fikra kama hizi?

J: Hatujui kuwa Paulo alikuwa na fikra kama hizi, lakini jambo hili lingeweza kufikiriwa na mkristo mwingine aliyekuwa kwenye nafasi kama hii. Tunapaswa kukumbuka kuwa nguvu hazitoki kwetu, bali kwa Mungu. Mungu anaweza na anawatumia watu wengine pia. Mungu hakumhitaji Paulo “zaidi” kuwepo Thesalonike, hasa wakati Paulo angeweza kufanya mambo mazuri mahali pengine. Lakini mkristo wa wastani, kama Timotheo, mungu alipofanya kazi kupitia kwake aliweza kutenda vizuri kabisa.

 

S: Kwenye 1 The 3:1-6, Paulo angeweza kusema “Nimefanya huduma kiasi cha kutosha” na kuacha kuhubiri injili na kufurahia maisha yake. Ni kwa nini unafikiri Paulo aliendelea?

J: Ni dhahiri kuwa Paulo asingeweza kuhubiri injili ya mafanikio, “furahia maisha, kama mimi.” Ingawa Paulo alikuwa mahali ambapo angeweza kufikiri kuwa “Tayari nimefanya huduma kiasi cha kutosha”, hakuna ushahidi wowote ule kuwa aliwahi kufikiri nama hii. Alisukumwa na upendo wake kwa Mungu na upendo wake kwa watu wengine, na hakupenda waende jehanamu. Paulo alikuwa na lengo. Kumbuka, neno “kustaafu” halimo kwenye Biblia.

 

S: Kwenye 1 The 3:3, kwa nini hutupangia kwa makusudi kabisa kupita kwenye majaribu?

J: Mungu hufanya mambo yote kulingana na matakwa yake (Efe 1:11; Mit 16:4; ~Rum 8:28).

   Pia, kila moja ya siku zetu iliandikwa kwenye kitabu cha Mungu kabla ya siku yeyote kati ya hizo hazijatokea kwenye Zab 139:16.

   Wazazi “huchagua kwa majuto” kuwapa wanao viboko vyenye kuumiza na mafunzo yenye maumivu kutokana na makosa ambayo watoto hawa wameyafanya. Wakristo wamekuwa wakijivuna watoto, wake, au waume wao wanapokufa wakati wanajaribu kuokoa maisha ya mtu mwingine au kusimama kwa ajili ya imani yao. Hakuna mzazi anayechagua maumivu ya aina hii bure tu, lakini kwa ajili ya kusudio jema. Vivyo hivyo, Mungu huchagua kuruhusu mambo haya, si kwa kuwa anafurahi kuwaona wanaumia, bali ni kwa ajili ya:

1. Maonyo au mema makubwa zaidi ya muumini (Ebr 12:4-15)

2. Kwa manufaa ya wengine (Fil 1:22-25; Kol 1:24-25)

3. Kwa utukufu wa Mungu (kama vile mfano wa Ayubu)

4. Kwa sababu mwisho wa siku, Mungu atayafanya majaribu yetu kutoonekana kuwa ya maana kulinganisha na utukufu wetu tutakaoupata (Rum 8:18; 1 Pet 4:12-14)

 

S: Kwenye 1 The 3:3, watu waliokuwa wanamtesa Paulo waliweza kuwa na makosa? Walikuwa wanafanya mapenzi ya Mungu, kwani Mungu aliyapanga mateso hayo kwa Paulo tokea awali.

J: Walifanya makosa, na wanawajibika kwa matendo yao maovu. Kuna mambo matatu ya kuzingatia katika jibu la swali hili.

1. Mungu jufanya mambo yote kwa kufuata mapenzi yake (Efe 1:11; Mit 16:4).

2. Mungu hutumia zana mbalimbali kutimiza malengo yake, na Biblia inaonyesha kwa uwazi kabisa kuwa maamuzi maovu ya watu ni baadhi ya zana ambazo Mungu huwa anazitumia (Mwa 50:20).

3. Mungu alipanga tokea awali kutumia makusudio mabaya ya Yuda (Mdo 2:23; Yoh 13:18; Zab 41:9), lakini Yuda anawajibika kikamilifu kwa matendo yake (Marko 14:21; Luka 22:21-22). Vivyo hivyo, kupanga kwa Mungu kutumia maovu ya watu wengine hakupunguzi kuwajibika kwao kwa maauzi maovu.

 

S: Kwenye 1 The 3:8; Fil 4:1 na Efe 6:10-16, kwa kuwa tumeishaokolewa, kwa nini tunaagizwa “kusimama thabiti kwenye imani”?

J: Wakristo wanaweza kupotoshwa au kudanganywa, kama ambavyo Mat 24:24 inaonyesha. Hata wakristo wa kweli wanaweza wakarudi nyuma, au kuficha imani yao kwa sababu ya uoga, na kufanya mambo yasiyompendeza Mungu kwa muda fulani.

 

S: Kwenye 1 The 3:12, 4:9-10, kama wakristo ambao tayari wanampenda Mungu na watu wengine, je tunahitaji upendo wetu kuongezeka? Ni kwa njia gani Mungu anaufanya upendo wetu kwa watu wengine kuongezeka hata kufurika?

J: Tunapaswa kuhitaji kwa uangalifu upendo wetu kwa watu wengine kuongezeka. Upendo huu unaweza kuongezeka kama tutauonyesha kwao na kuwaombea.

 

S: Kwenye 1 The 3:13, je Mungu anaiimarishaje mioyo yetu ili isilaumiwe na kuwa mitakatifu mbele zake?

J: Mungu anaweza kufanya hivyo kupitia kusoma kwetu neno lake, utiifu wetu, kumwabudu kwetu, na kuwapenda kwetu watu wengine. Lakini Mungu anaweza pia kufanya hivyo kwa kupitia njia ambazo hatuwezi kuzitambua. Watu anaowaleta kwenye maisha yetu, (wakiwemo watu wagumu), matukio (yenye kufurahisha na yasiyofurahisha) na kwa kutuwezesha kukumbuka mambo, Mungu anaweza kuiimarisha mioyo yetu katika azma yetu ya kuutafuta utakatifu wake katika maisha yetu. Lakini wakati wote unapaswa kuwa tayari kumruhusu Mungu akubadilishe. Jaribu au mtihani haumuimarishi mtu kila wakati, inategemea na jinsi tunavyoitikia. Mkumbuke mke wa Ayubu aliyesema, “mtukane Mungu na ufe” ukilinganisha na jinsi Ayubu alivyosema.

 

S: Kwenye 1 The 4:1, njia zipi ni nzuri zaidi za kuwatia moyo watu wengine kuisha maisha yanayompendeza Mungu?

J: Watie moyo kuangalia nbali zaidi ya mazingira ya karibu na waelekeze kwa Mungu, mambo ambayo ameyafanya kwao. Waelekeze kwenye namna ambayo Mungu anajishughulisha na maisha yao, na umuhimu wa milele wa mambo wanayoyafanya. Wakumbushe ufupi wa muda wa hapa duniani kulinganisha na ya umilele. Kama inawezakana, kuwa karibu nao, ukiwasaidia, na kuwa nao. Katika mazingira mengine, mtafute mtu ambaye amepitia majaribu kama hayo kwa ajili ya ushauri na kumuegemeza.

 

S: Kwenye 1 The 4:1-7, tunawezaje kuishi maisha matajatifu zaidi?

J: Hebu tujibu swali hili kwa kutumia mfano wa michezo.

Mchezaji anaweza kuboreka kupitia  vitu vya aina tatu: juhudi za msingi, juhudi upili, na vitu vya kuviepuka. Jambo la msingi ni mazoezi sahihi ya mchezo anaoucheza. Wakati mmoja ni mechi, kitu kinachotakiwa ni kucheza mechi. Wakati mwingine ni kufanya mazoezi ya kipengela kimoja bila kuhusisha vingine, kukimbia, au kuinua vyuma vizito. Mwanamichezo hupenda kufanya mazoezi wakati wote kwa ajili ya mchezo wake, lakini kama mwanamichezo atafanya mazoezi wakati ule tu anapojisikia, hatakwenda mbali. Nidhamu inatakiwa, licha ya kuupenda mchezo.

   Jambo la pili ni kula chakula kizuri, kulala muda wa kutosha, na huenda hata kufanya mambo ya ziada, kwa mfano kupiga mpira wa mchezo wa ‘baseball’ husaidia uwezo wa kugonga vizuri mpira wa tenesi.

   Mwisho, ni kuepuka mambo kadhaa. Mambo mengine kama kuvuta sigara, kulewa, nk. Ni mabaya wakati wote. Mambo mengine hayana shida kama yalivyo lakini yanaweza kukuepusha kufikia lengo lako. Kwa mfano, ili uweze kucheza mechi ya ‘baseball’ vizuri hautakiwi kuogelea siku hiyo.

Mwanamichezo wa kiroho hali kadhalika anaweza kuboresha uchezaji wake kwa mambo ya aina tatu: ya msingi, ya upili, na mambo ya kuyaepuka. Jambo la msingi, hakuna jambo mbadala la upendo na utiifu wa kujitoa. Tunapaswa kufurahia kumpenda Mungu na kumtumikia. Lakini hata kama hatujisikii kufanya hivyo wakati fulani, nidhamu inatakiwa ili tuweze kufanya mambo ambayo Mungu anataka tufanye.

   Pili, tunahitaji kula mlo kamili. Mungu anatuagiza tusiwe waroho wenye kujaza midomo na matumbo yetu (Mit 28:7; Fil 3:19a), lakini pia tunatakiwa kuwa waangalifu na “milo” yetu ya vitu vinavyoingia kwenye macho na masikio yetu pia.

   Mwishoni, tunapaswa kuepuka si tu mambo maovu yasiyompendeza Mungu, lakini pia kuepuka mazingira ambayo, kwa upande wetu, yanatutia vishawishi. Pia tunapaswa kuangalia mambo ambayo yanatupotezea muda, ambayo yanaweza yasiwe dhambi, lakini yanatuchukulia muda mwingi na kutuzuia kumtumikia Mungu. Kama undhani Mungu hajakupa muda wa kutosha kufanya jambo ambalo unajua unahitaji kulifanya ili kumtumikia, huenda shida si kuwa Mungu hakukupa zaidi ya masaa 24 kwa siku, bali muda wako hautoshi kwa sababu umeutumia vibaya muda ambao Mungu amekupa.

 

S: Kwenye 1 The 4:9-10, tunapaswa kufanya nini ili kuwapenda waumini wengine zaidi?

J: Unaweza pia ukawatumia vitu mbalimbali mara kwa mara kuonyesha kuwa unawafikiria. Kwa upande mmoja tunaweza kuwaombea kwa mambo wanayoomba tuwaombee, kurafikiana nao. Lakini kwa undani wa mioyo yetu tunaweza kuwajali kwa kweli. Tunaweza kuangalia jinsi wanavyoendelea na maisha, na kuwaulizia na kupendekeza mambo ya kuombea, na kuchukua jukumu la kuwasaidia mahali wanapohitaji msaada. Je ameishawahi kukujia mtu na kukupa kitu ulichokihitaji bila kutarajia? Jambo hili linaweza kukufanya ujisikie vizuri sana, lakini ni vizuri zaidi unapowafanyia watu wengine.

 

S: Kwenye 1 The 4:11-12, kwa nini unadhani “kutulia”, siyo  agizo za ulimwengu “kuishi kwa anasa” au “tumia bila kikomo”?

J: Hatuhitaji kutafuta ummarufu, mamlaka, au ufahari, ama ulimwenguni ama ndani ya kanisa. Kama unafanya kazi yako vema vitu hivi vinaweza kukujia, lakini usivitafute, kwa sababu vinaweza kukuondosha kumtafuta Mungu. Kwenye jamii za magharibi, shida kubwa ya kumjua Mungu si kutokujua, bali vitu vyenye kuondosha mawazo na ari ya kumjua Mungu. Tafuta kutambua na kuviondoa, au angalau kuvipunguza vitu vyenye kukuondosha katika kutembea kwako na Bwana. Lakini kumbuka, matukio yasiyotarajiwa yanapotokea, kama vile kukutana na mtu mhitaji, hayo si mambo yanayokuondosha kumtafuta Mungu, lakini ni kazi kubwa ambayo Mungu anataka uifanye kwa wakati huo.

 

S: Kwenye 1 The 4:12b, kwa nini kuna tunapaswa kukusudia kutokumtegemea mtu yeyote?

J: Ni sahihi kupokea mambo mbalimbali ambayo watu wanafanya kuonyesha upendo wao kwetu, na ni vema kabisa kutegemea watu wengine kukuhudumia wakati unahitaji kweli msaada wa watu wengine kukuhudumia. Lakini unafaa uwe mwenye kutoa kuliko wao, siyo kupokea. Paulo anaagiza kwenye 2 The 3:6 waumini kuishi kwa utaratibu, na kwenye 3:10 “Ikiwa mtu hataki kufanya kazi, basi, asile chakula.” Usiwafanye watu wengine wafanye mambo ambayo unaweza kuyafanya. Kama unaweza kufanya kazi na kuleta hela nyumbani, hupaswi kuwa mvivu na kutegemea watu wengine. Tena, kama huwezi kufanya hivyo, ni sahihi kutegemea watu wengine. Lakini kama unaweza kutafuta hela, hata kama ni kiasi kidogo tu, basi fanya hivyo ili uweze kujitegemeza, angalau kwa kiasi tu.

 

S: Kwenye 1 The 4:13-14, je waumini ambao wamekufa wapo kwenye “usingizi wa nafsi”, au wanao ufahamu huko mbinguni?

J: Waumini waliokufa wana ufahamu huko mbinguni. Mistari mikuu yenye kuonyesha jambo hili ni 2 Kor 5:6, Luka 16:19-31; Fil 1:23; Ufu 6:9-11; Ufu 7:9-11, na mistari mingine yenye kuonyesha waumini wenye ufahamu wakisifu kwenye Kitabu cha Ufunuo. Kwenye 2 Kor 5:8, Biblia inasema, “. . . kutokuwamo katika mwili na kukaa pamoja na Bwana.”

   Concerning the Martyrdom of Polycarp, sura ya 2, uk.39, inasema kuwa kutokuwamo katika mwili ni kuwa na muda wa pamoja na Bwana. Tertullian, akiandika mwaka 198-220 BK, anasema kuwa mke wa kikristo aliyekufa yu katika uwepo wa Bwana kwenye On Exhortation to Chastity, sura ya 11, uk.56.

 

S: Kwenye 1 The 4:13-16, 1 The 5:10, na 1 Kor 15:51, je neno “kulala” linathibitisha kuwa watu waliokufa hawana ufahamu?

J: Kama Yesu alivyowakemea wanafunzi wake kwenye Yoh 11:11-14, aliposema kuwa amelala, alichomaanisha ni kuwa amekufa. Kulala lilikuwa ni neno la kawaida lenye kumaanisha kifo, kama ambavyo mistari hii inaonyesha:

   2 Pet 3:4; Mdo 7:60; 1 Kor 15:6;18, 20;  Mat 27:52; 28:13; Kum 31:16, na vifungu vingine vya Agano la Kale “. . . alilala na baba zake . . .”

   The New Geneva Study Bible, uk.1898, pia inasema kuwa kulala kulikuwa ni sitiari au lugha ya picha ya kifo miongoni mwa watu wasiomwamini Yahwe na kwenye kazi za wakristo. Neno ‘kulala’ lilikuwa ni tafsida ya ‘kifo’ kwenye Homer (Iliad kitabu cha 11 240-241) kwa mujibu wa The Resurrection of Jesus, uk.421.

   Waandishi wa awali wa kikristo pia walielewa kuwa kulala kunamaanisha kufa, kama Athenagoras (mwaka 177 BK) anavyoonyesha kwenye The Resurrection of the Dead, sura ya 16.

   Hivyo mistari hii haithibitishi au kupinga kuwa watu wanakuwa na ufahamu baada ya kufa. Uthibitisho kuwa watu wanakuwa na ufahamu baada ya kufa, soma swali lililotangulia.

 

S: Kwenye 1 The 4:15, kwa kuwa Paulo ameandika, “sisi tulio hai, tuliosalia”, kwa nini Paulo aliuawa kabla ya kurudi kwa Kristo?

J: Mungu hakupenda tujue lini Yesu atarudi. Paulo huenda alitumia pronomino tatu hapa.

“Wao”: Kama Mungu alimwambia Paulo asema, “wao” lingekuwa ni neno ambalo lingemaanisha kuwa kuja kwa Yesu kungetokea baada ya kufa kwa Paulo.

“Mimi”: Kama Paulo angesema “mimi” ingemaanisha kuwa Kristo angerudi kabla ya Paulo kufa.

“Sisi”: “Sisi” ni sawa na kusema wale miongoni mwetu walio hai, na “sisi” ni pronomino pekee ambayo Paulo angeweza  kuitumia ambayo isingefanya kurudi kwa Kristo kuwe tu ama kabla ama baada ya kurudi kwa Kristo.

 

S: Kwenye 1 The 4:15, je Paulo alifikiri kuwa angekuwa hai wakati Yesu anarudi?

J: Angalia swali lililopita linalohusika na matumizi ya pronomino. Paula aliandika jambo hili, bila makosa, kwa kutokubainisha jambo ambalo hakuambiwa. Kuna mambo sita yenye kuonyesha za Paulo kufanya hivi.

1. Paulo hakuwahi kusema kuwa alijua siku ya kurudi kwa Yesu (1 The 5:1-2).

2. Alitegemea kuwa ingekuwa wakati wa uhai wake (1 The 4:15).

3. Paulo alifundisha kuwa amani (1 The5:3) na ukengeufu mkubwa (2 The 2:3-10) vitatokea kabla ya Yesu kurudi.

4. Paulo alikuwa anakutazamia kwa hamu kubwa kurudi kwa Yesu, kama ambavyo tunapaswa tuwe tunafanya, ambako ni tumaini lenye baraka Tito 2:13.

5. Paulo, Kristo, na watu wengine wametuambia tukeshe kwani Yesu yu karibu kurudi (Mat 24:42; Marko 13:35; 1 The 5:4-6; 1 Pet 4:7; Ufu 3:3; 22:20).

6. Kama 1 Tim 3:15 inavyoonyesha, Paulo alifahamu vema dhana ya kuwaagiza watu kuwa na mwenendo mzuri, kwa sababu hasemi ni lini Yesu atarudi. Tazama Mat 24:36-25:13.

Kwa ufupi, Mungu hakumuambia Paulo kila kitu, Paulo ametuambia mambo yale ambayo Mungu amemueleza, lakini Paulo hakutuambia mambo ambayo Mungu hakumuambia. Tazama pia maelezo kuhusu Fil 4:5, 1 Pet 4:7, na Ufu 22:6-20.

 

S: Kwenye 1 The 4:15, kwa nini Mungu hakupenda kutujulisha siku ya kurudi kwa Yesu?

J: Ni kama bwana anayemuambia mtumwa wake kufanya kazi kwa bidii, kwani anaweza kurudi bila wakati wowote ule bila kutarajia kama Luka 12:35-48 inavyoonyesha. Kwenye Biblia, sababu za kuishi “maisha ya kutarajia” yaliyojaa hamu ya kurudi kwake yanaleta nguvu, faraja, raha (1 The 5:18; 2 The 2:15-17) na kuwa makini kuishi bila lawama wakati wowote Kristo atakaporudi (1 The 3:13; 5:23).

 

S: Kwenye 1 The 4:16, je kuja kwa Yesu pamoja na sauti ya malaika mkuu inamaanisha kuwa Yesu ni malaika mkuu kama Mashahidi wa Yehova wanavyofundisha?

J: Hapana. Ingawa kunaweza kukawa na malaika wakuu wengine zaidi ya Mikaeli, hili si jambo la msingi hapa.

   Parapanda ya Mungu wakati wa kuja kwa Yesu haimaanishi kuwa Yesu mwenyewe ataipiga. Vivyo hivyo, inawezekana kuwa sauti ya malaika mkuu ni sauti ya malaika mkuu atakayekuja pamoja na Yesu hapa.

   Hata kama sauti hii hapa ni ya Yesu anayeongea kupitia kwa malaika mkuu, jambo hili halimaanishi kuwa Yesu si Mungu. Haitakuwa na ulazima wowote kabisa, kwa mfano, kwa mtu kusema kuwa Yesu alipokuwa duniani alisema na kutenda kama binadamu, kwa kuwa alikuwa binadamu. Kama maneno haya (1 The 4:16) yanathibitisha kuwa Yesu ni malaika mkuu, basi parapanda ya Mungu inathibitisha kuwa Yesu ni Mungu.

   Watu hawahitaji kutumia mistari isiyokuwa wazi kama huu hapa kupata ufumbuzi wa swali endapo Yesu ni Mungu au la. Tungeweza “kumuuliza Tomaso” kwa kusoma Yoh 20:27-28, “kumuuliza Yohana” kwa kusoma Yoh 1:1, au kumuuliza mwandishi wa Waraka kwa Waebrania kwa kusoma Ebr 1:8-9. Je unamheshima Mwana kama unavyomheshimu Baba kulingana na agizo la Yoh 5:23? Je unamwabudu Yesu, kama malaika wanavyofanya kwenye Ebr 1:6? Je unamdifu Yesu pamoja na Baba, kama wale walioko mbinguni wanavyofanya kwenye Ufu 5:9-13; 11:15.

 

S: Kwenye 1 The 4:16, ni parapanda gani inayoongelewa hapa?

J:Maandiko hayasemi wazi kabisa endapo hii ni moja ya parapanda saba za kwenye Ufunuo 8-11 au ni nyingine.

 

S: Kwenye 1 The 5:1-3, ni kwa kiasi gani watu wanaweza kuujua muda wa siku ya Bwana?

J: Kama Mat 24:36 inavyosema na 1 The 5:1-2 inavyoonyesha, hakuna mtu anayeijua siku wala saa. Lakini kama Mat 24:37-39; Luka 17:26-29, na 1 The 5:3 zinavyosema, utakuwa muda ambao watu wengi hawatakuwa wanafikiria kuja kwa Yesu na siku hiyo haitatarajiwa kabisa na watu wengi.

 

S: Kwenye 1 The 5:4-8 na Efe 4:18; 5:8-11, je inamaanisha nini kuwa wana wa nuru au mchana, kulinganisha na kuwa wana wa giza au usiku?

J: Hatuaibiki endapo watu wataelewa mambo yetu yote. Hatufanyi mambo yeyote maovu kwa siri ambayo hatupendi watu wengine wayajue; badala yake, tunapenda watu wayaone maisha yetu. Hatuusubirii usiku kwa shauku ili tulewe, tufanye sherehe za anasa, au kufanya jambo lingine lisilokuwa sahihi. Badala yake, tunalala salama usiku, kwa sababu tunausubiria mchana kwa shauku, na kuona kuwa tunafanya mambo yanayotakiwa wakati huo.

 

S: Kwenye 1 The 5:9, ni kwa jinsi gani Mungu hakutuchagua sisi kupata ghadhabu, kwani Efe 2:3 inasema kuwa kama watu wengine wote, tulikuwa watu wenye kustahili ghadhabu?

J: Watu wote (isipokuwa Adamu, Hawae, na Yesu) wamezaliwa na asili iliyoanguka ya dhambi, na kwa asili wanastahili ghadhabu. Hata hivyo, Mungu amewapa watoto wake kuzaliwa upya, maisha mapya, na tumaini jipya na lenye uhakika kupitia kwa Yesu aliyechukua adhabu yetu.

 

S: Kwenye 1 The 5:12-13, ni njia zipi tunazoweza kuzitumia kuonyesha heshima kwa watu walio wakubwa kwetu katika Bwana?

J: Kwanza kabisa, waambie wao na watu wengine kuwa unawatambua kuwa ni wakubwa kwako katika Bwana. Waonyeshe kuwa unawajali, na wasaidie katika changamoto zao za maisha endapo unaweza. Heshimu nafasi zao, kama Paulo alivyofanya hata kwa kuhani mkuu kwenye Mdo 23:3-5. Heshimu juhudi zao na kujitoa kwao, kama Paulo alivyofanya kwenye Fil 2:28-30.

 

S: Kwenye 1 The 5:14, kwa kuwa tunapaswa kuvumiliana na watu wote, kwa nini Paulo na Yesu hawaonyeshi kuvumiliana na watu wote?

J: Wawili hawa walikuwa wavumilivu, lakini jambo hili halimanishi hawakuweza pia kuwakaripia watu sana kadri ilivyotakiwa.

   John Chrysostom (karibu mwaka 396 BK) aliandika hivi mwanzoni mwa kazi yake, Commentary on Galatians. “Kwani mtu kuongea na wanafunzi wake kila wakati kwa upole hata wakati wanapohitaji ukali si sehemu ya mwalimu lakini ya mharibifu na adui. Kwa ajili hiyo Bwana wetu naye, ingawa ana kawaida ya kuongea kwa upole kwa wanafunzi wake, mara kadhaa ametumia lugha ya ukali, na wakati mmoja hubariki, na wakati mwingine hukaripia.”

 

S: Kwenye 1 The 5:15, ni mambo gani ambayo watu wanayatumia wakati mwingine wanapojaribu kutoa visingizio vya kuhalalisha kulipa kisasi kwa mambo mabaya ambayo wametendewa?

J: Yafuatayo ni baadhi ya mambo hayo.

Agano la Kale linasema jicho kwa jicho. (Agano la Kale limepitwa na wakati). Sheria ndiyo inayotakiwa kuadhibu watu leo, lakini hatupaswi kujipa mamlaka ya kutekeleza sheria. Katika jamii za magharibi za zamani, sungusungu walikuwa halali kwa kuwa walitambuliwa na sheria, katibu kata, aliwajibika kwa mambo waliyokuwa wanafanya. Watu wenye kuchoma moto watu wengine hayakuwa halali.

Wanastahili (na ninatakiwa kutoa hukumu mambo ambayo watu wote wanastahili).

Wanatakiwa kujifunza (name natakiwa kuwa mwalimu wao).

Watarudia tena kama hawatafundishwa matokeo ya vitendo vyao (na Mungu ameniteua kuwafundisha).

Nahitaji kuwalipa maovu yao (kwani naamini kuwa ni haki yangu).

   Lakini licha ya visingizio wanavyotumia, watu wanaolipiza maovu waliyofanyiwa hawamtii Mungu.

 

S: Kwenye 1 The 5:16-18, ni kwa namna gani kuwa na furaha wakati wote, kuomba bila kukoma, na kushukuru kwa kila jambo kunakwenda pamoja?

J: Tunafurahi, tunaomba, na tunashukuru kwa kuwa tunajua kuwa Mungu anasimamia mambo yote. Mambo yote haya matatu yanatakiwa kufanyika wakati wote. Lakini furaha inatakiwa kutusukuma kuomba. Maombi yetu yanatakiwa yajae shukrani kwa Mungu, na shukrani zetu zinatakiwa zitukumbushe furaha yetu.

 

S: Kwenye 1 The 5:17, je tunapaswa kuomba bila kukoma, au tutumie maneno machache kama Mat 6:7 inavyosema?

J: Vyote. Maisha yetu yote yanatakiwa yawe maisha ya maombi, tukiwa katika ushirika wa karibu na usiokwisha na Mungu. Lakini, hatupaswi kufikiri kuwa Mungu husikia ombi fulani kwa sababu ya kurudia maneno mengi.

 

S: Kwenye 1 The 5:22, je agizo hili “jitengeni na ubaya wa kila namna” linamaanisha nini?

J: Neno la Kigiriki lenye kumaanisha “namna”, eidos, linaweza pia kumaanisha muonekano, mtindo, umbo, picha. Kwa mujibu wa Strong’s Concordance, linatokana na neno lenye kumaanisha “mtazamo.” Tunapaswa kuepuka maovu ya aina yote. Pia, tunapaswa kuepuka kuonekana tunafanya mambo ambayo kweli ni maovu. Isitoshe, 2 Kor 8:22 inaonyesha kuwa Paulo alitaka kufanya mambo sahihi machoni pa watu wote.

   Hata hivyo, 1 The 5:22 haihusishi kuwafanya watu waone tunapofanya mambo mazuri (kama vile kuhubiri injili) kwa sababu wanafikiri kuwa jambo hili ni baya.

 

S: Kwenye 1 The 5:26; Rum 16:16; 1 Kor 16:20; 2 Kor 13:12 na 1 Pet 5:14, je wakristo wanatakiwa kusalimiana kwa busu takatifu?

J: Kwenye utamaduni wa wakati ule, ilikuwa sahihi kusalimia kwa busu takatifu. Kwenye jamii za Kimarekani na Kichina, kitu chenye kufanana na busu ni kukumbatia au kupeana mikono.

 

S: Tunajuaje kuwa Paulo aliandika Waraka wa Kwanza kwa Wathesalonike?

J: Kuna sababu zisizopungua mbili.

1. Waraka huu (1 Thesalonike) unasema hivyo, na kanisa la awali halijawahi kutilia shaka ukweli huu.

2. Tertullian alisema Paulo aliwaandikia Wathesalonike kwenye kazi yake iitwayo Tertullian Against Marcion, kitabu cha 4 sura ya 5, uk.345-350 (mwaka 207 BK). Alisema waraka huu “umetoka kwa mitume, ambao umehifadhiwa kama dhamana takatifu kwenye makanisa ya mitume.”

Bila shaka kuna watu wengine pia walioandika kuhusu waraka huu 1 Wathesalonike) pia.

 

S: JE Waraka wa Kwanza kwa Wathesalonike uliandikwa lini?

J: Tunafahamu kwa ufasaha muda ambao waraka uliandikwa: karibu mwaka 51-52 BK. Kwenye  1 The 3:1-7 waraka huu wenyewe unaonyesha kuwa uliandikwa baada ya Paulo kuondoka Athene na alikuwa Korintho. Mdo 18:12, 17 inasema kuwa Galio alikuwa liwali wa Akaya. Maandhishi yaliyovumbuliwa Delphi yanaonyesha kuwa Galio alikuwa liwali karibu miaka ya 51-52 BK. Wengine wanatafsiri wakati wa kuandikwa waraka huu kuwa mwaka 52-53 BK.

   Kama mtu mwenye kushuku atadai kuwa nyaraka za Paulo ziliandikwa na mtu mwingine miaka mingi baadaye, na maneno ya waraka huu (1 Wathesalonike) kuwa uliandikwa na Paulo ni uongo, mtu huyo ndiye atakayekuwa na wajibu wa kuthibitisha na kutoa ushahidi wowote kuwa maneno haya ni uongo. Kuna taaluma machache sana ambazo mtu anaweza kudai kuwa waraka fulani si wa kweli bila kutoa ushahidi wa aina yeyote ile.

 

S: Kwenye Waraka wa Kwanza kwa Wathesalonike, ni jambo gani lingine tunalolijua kuhusu maandishi ya Galio?

J: Maandishi ambayo wataalamu wa mambo ya kale wanayaita ‘Maandhishi ya Galio’ (Gallio inscription) kwa sasa yapo kwenye jumba la makumbusho la Delphi. Yapo kwenye vipande visivyopungua saba. Mistari ya 5-6 inaongelea agizo la Mfalme Claudius wa Roma, ambaye alitawala miaka ya 41-54 BK, huyu ni Lucius Junius Gallio, liwali wa Akaya. The Dictionary of New Testament Background, uk.53-54, ambako nukuu hii ilichukuliwa, inasema “mpangilio wa matukio unategemea vigezo vingine vya kukokotoa muda. Hata hivyo, wanazuoni wengi zaidi wanaamini kuwa kwa kutegemea maandishi haya, na ukweli kuwa maliwali walifanya kazi kwa mihula ya mwaka mmoja mmoja, inawezekana kuuweka muhula wa Galio alipokuwa liwali wa Korintho [huko Akaya] hadi mwaka 51/52 BK.”

 

S: Kwenye Waraka wa Kwanza wa Wathesalonike, tunawezaje kujua kuwa waraka tulionao sasa umehifadhi kwa uaminifu waraka ulioandikwa mara ya kwanza kabisa?

J: Kuna sababu zisizopungua tatu.

1. Mungu aliahidi kulihifadhi neno lake kwenye Isa 55:10-11; 59:21; 40:6-8; 1 Pet 1:24-25 na Mat 24:35.

2. Ushahidi wa kanisa la awali. Wafuatao ni baadhi ya waandishi wa kikristo walioandika baada ya baraza la kwanza la kanisa la awali lililofanyika Nikea mwaka 325 BK walioongelea mistari ya Waraka wa Kwanza wa Wathesalonike.

Clement wa Roma (mwaka 97/98 BK) anadokezea 1 The 2:12,13 kwenye 1 Clement juzuu ya 1, uk.11

Ignatius (miaka ya 110-117 BK) ananukuu 1 The 5:17 kwenye Ignatius’ Letter to Polycarp sura ya 1, uk.93

Polycarp (karibu mwaka 150 BK) ananukuu mstari wote wa 1 The 5:17 (haya ni maneno mawili kwenye Kigiriki: “ombeni bila kukoma”) kwenye Polycarp’s Letter to the Philippians sura ya 4, uk.34

Melito wa Sardis (miaka ya 170-180 BK) anautaja Waraka wa Kwanza kwa Wathesalonike kama kazi ya Mtume Paulo kwenye Oration on the Lord’s Passion sura ya 9, uk.762

Irenaeus (miaka ya 182-188 BK) ananukuu 1 The 5:23 kama “kwenye Waraka wa Kwanza kwa Wathesalonike” kwenye Irenaeus Against Heresies kitabu cha 5, sura ya 6.1, uk.532

Muratorian Canon (miaka ya 170-210 BK) ANF juzuu ya 5, uk.603 inataja nyaraka mbili za Paulo kwa Wathesalonike, na nyaraka nyingine 11 za Paulo.

Clement wa Alexandria (miaka ya 193-217/220 BK) ananukuu 1 The 2:6-7 kama kazi ya Paulo kwenye The Instructor kitabu cha 1, sura ya 5, uk.214

Clement wa Alexandria (miaka ya 193-205 BK) ananukuu 1 The 2:5, 6, 7 kama kazi ya Paulo Mtume kwenye Stromata kitabu cha 1, sura ya 1, uk.300.

Tertullian alisema Paulo aliwaandikia Waroma, Wagalatia, Wafilipi, Wathesalonike, na Waefeso kwenye Tertullian Against Marcion kitabu cha 4, sura ya 5, uk.350 (mwaka 207 BK). Anasema kuwa Agano Jipya lilikuwa ni kitabu “kilichokuja kutokea kwa mitume, ambacho kimetunzwakama dhamani takatifu kwenye makanisa ya mitume.” Tertullian (miaka ya 198-220 BK) ananukuu 1 The 4:15-17 kwenye Five Books Against Marcion kitabu cha 5, sura ya 15, uk.462.

Hippolytus (miaka ya 225-235/6 BK) ananukuu 1 The 4:12 kama kazi ya Paulo kwenye Treatise on Christ and Antichrist sura ya 66, uk.219

Origen (miaka ya 225-253/254 BK) ananukuu 1 The 2:14,15 kama kazi ya Paulo kwenye Waraka wa Kwanza kwa Wathesalonike kwenye Origen’s Commentary on Matthew kitabu cha 2, sura ya 18, uk.425

Cyprian wa Carthage (karibu miaka ya 246-258 BK) ananukuu kutoka kazi ambayo anasema kuwa ni “Waraka wa Kwanza wa Paulo kwa Wathesalonike” na ananukuu 1 The 4:6. Anasema, “Mtume anasema” na kisha ananukuu 1 The 5:2-3. Haya yamo kwenye Treatise 12 kitabuu cha tatu 88, 89. Pia anasema kuwa 1 The 4:13 iliandikwa na Paulo kwenye The Treatises of Cyprian Somo la 7, sura ya 21, uk.474.

Archelaus (miaka ya 262-278 BK) ananukuu 1 The 5:1, 2 kama maneno ambayo Mtume “Aliwaandikia Wathesalonike” kwenye  Disputation with Manes sura ya 38, uk.212

Adamantius (karibu mwaka 300 BK) ananukuu 1 The 2:14-15 kama kazi ya Mtume Paulo kwenye Dialogue on the True Faith sehemu ya kwanza, sura ya 29a, uk.69. Hataji mstari mwingine wowote wa Waraka wa Kwanza kwa Wathesalonike.

Baada ya Baraza la Nikea

Eusebius’ Ecclesiastical History (miaka ya 323-326 BK)

Athanasius (mwaka 367 BK) anaorodhesha vitabu vya Agano Jipya kwenye Festal Letter 39, uk.552

Hilary wa Poitiers (miaka ya 355-367/368 BK) anataja 1 The 4:17

Synopsis Scripturae Sacrae (miaka ya 350-370 BK au karne ya 5) anazitaja nyaraka mbili za Paulo kwa Wathesalonike kama sehemu ya Agano Jipya. Kazi hii inanukuu waraka wote isipokuwa 1 The 1:1.

Ephraem the Syrian (mwaka 373 BK)

Basil wa Cappadocia (miaka ya 357-378/379 BK) ananukuu 1 The 3:12, 13 kama kazi ya Mtume, “kwa waumini walioko Thesalonike” kwenye On the Spirit sura ya 21.52, uk.33

Ambrosiaster (baada ya mwaka 384 BK)

Cyril wa Yerusalemu (karibu miaka ya 349-386 BK)

John Chrysostom (mwaka 396 BK) aliandika mahubiri 11 ya Waraka wa Kwanza kwa Wathesalonike, ambayo tunayo leo hii. Alisema waraka huu uliandikwa na Paulo, na Timotheo pamoja naye.

Gregory wa Nyssa (karibu miaka ya 356-397 BK) ananukuu 1 The 4:17 kama kazi ya Paulo kwenye On the Making of Man sura ya 22.6, uk.412

Didymus the Blind (mwaka 398 BK)

Epiphanius wa Salamis (miaka ya 360-403 BK)

John Chrysostom (aliyekufa mwaka  407 BK) aliandika maelezo ya Injili ya Yohana, nyaraka za Warumi, 1 Wakorintho, 2 Wakorintho, Wagalatia, Waefeso, Wakolosai, Wafilipi, 1 Wathesalonike, 2 Wathesalonike, 1 Timotheo, 2 Timotheo, Tito, Filemoni na Waebrania.

Rufinus (miaka ya 374-406 BK)

Niceta of Remesianus (miaka ya 366-415 BK) anaongelea 1 The 2:8

Jerome (miaka ya 373-420 BK) anadokezea 1 Thes 4:13. “Na mtume anawazuia Wathesalonike kuhuzunika kwa ajili yao waliokuwa wamelala” kwenye Against Vigilantius sura ya 6, uk.419. Ananukuu 1 Thes 5:17 yote, “Ombeni bila kukoma” kwenye Letter 125 sura ya 11, uk.248

Augustine wa Hippo (miaka ya 388-430 BK) anamtaja mtume kuwa ndiye aliyewaandikia Wathesalonike na ananukuu 1 The 1:13 kwenye On the Predestination of the Saints sura ya 39, uk.517

Augustine anamtaja mtume kuwa ndiye aliyewaandikia Wathesalonike na ananukuu 1 The 4:13-16 kweny The City of God kitabu cha 20, sura ya 20, uk.439

Mfuasi wa mafundisho ya Pelagius John Cassian (miaka ya 419-430 BK) ananukuu 1 The 4:9-10 kama waraka wa Mtume kwa Wathesalonike kwenye Institutes of John Cassian kitabu cha 10.7, uk.268

Socrates’ Ecclesiastical History (miaka ya 400-439 BK) kitabu cha 3, sura ya 16, uk.87 ananukuu sehemu ya 1 The 5:21: “ili kwamba tuweze ‘kujaribu mambo yote, na kulishika lililo jema.’

Speculum (karne ya tano)

Quodvultdeus (karibu mwaka 453 BK) anaongelea 1 The 1:3

Theodoret wa Cyrus, askofu na mwanahistoria (miaka ya 423-458 BK)

Varimadum (miaka ya 445/480 BK)

3. Maandiko ya wapotoshaji na watu wengine

Mpotoshaji Marcion kwa mujibu wa Tertullian

Mpotoshaji Priscillian (mwaka 385 BK) anaongelea 1 The 2:16.

Mpotoshaji Pelagius (miaka ya 416-418 BK)

Mdonasti na mwenye kuligawa kanisa Tyconius (baada ya mwaka 390 BK) anaongelea 1 The 1:3; 2:8

Mpotoshaji mwenye kufuata mafundisho ya Pelagius Theodore wa Mopsuestia (mwaka 428 BK)

4. Hati za kale zenye maandiko tulizonazo za Waraka wa Kwanza kwa Wathesalonike zinaonyesha kuwa kuna tofauti ndogo sana za maandishi, lakini hazina makosa ya kitheolojia yenye mshiko.

p30 1 The 4:12-13,16-17; 5:3,8-10,12-18,25-28; 2 The 1:1-2; 2:1,9-11 (mwanzoni mwa karne ya tatu)

p46 Chester Beatty II (mwaka100-150 BK) ina mistari 17 ya Waraka wa Kwanza kwa Wathesalonike. Kipekee, ina 1 The 1:1; 1:9-2:3; 5:5-9, 23-28 na sehemu nyingine za nyaraka za Paulo na Waebrania. Ubora na alama za stikiometri zinaonyesha kuwa mwandishi mtaalamu aliuandika waraka huu.

Nusu ya kwanza ya karne ya tatu hadi mwaka 1936 - Frederic G. Kenyon kwa mujibu wa The Complete Text of the Earliest New Testament Manuscripts.

Karne ya pili (miaka ya 200 hadi 1935 BK) - Ulrich Wilken kwa mujibu wa The Complete Text of the Earliest New Testament Manuscripts.

Miaka ya 200 - 1968 BK- The Text of the New Testament.

Miaka ya 81-96 - 1988 BK - Young Kyu Kim kwa mujibu wa The Complete Text of the Earliest New Testament Manuscripts.

Karibu mwaka 200 BK - 1975 - Aland na wengine, toleo la tatu.

Karibu mwaka 200 BK - 1998 - Aland na wengine toleo la nne lilifanyiwa marekebisho.

Mwanzoni mwa karne ya pili hadi mwaka 1999 BK - The Complete Text of the Earliest New Testament Manuscripts. Kazi hii imetokana kwa kiasi mwandiko wake kufanana sana na Papyrus Oxyrhynchus 8 (mwishoni mwa karne ya kwanza na mwanzoni mwa karne ya pili) na Papyrus Oxyrhynchus 2337 (mwishoni mwa karne ya kwanza).

p61 Rum 16:23, 25-27; 1 Kor 1:1-2, 2-6; 5:1-3, 5-6, 9-13; Fil 3:5-9, 12-16; Kol 1:3-7, 9-13, 1 The 1:2-3; Tito 3:1-5, 8-11, 14-15; Filemoni 4-7. Karibu mwaka 700 BK

Karibu mwaka 700 - 1968 BK - The Text of the New Testament.

Karibu mwaka 700 - 1975 BK - Aland na wengine toleo la tatu.

Karibu mwaka 700 - 1998 BK - Aland na wengine toleo la nne lililofanyiwa mabadiliko.

p65 1 The 1:3-2:1; 2:6-13 (katikati ya karne ys tatu)

p49 na p65 ziliandikwa na mtu mmoja. Hati hizi ni za aina ya Alexandria.

Karne 3 - 1968 BK - The Text of the New Testament.

Alexandrinus [A] karibu mwaka 450 BK

Vaticanus [B] miaka ya 325-350 BK

Sinaiticus [Si] miaka ya 340-350 BK

Ephraemi Rescriptus [C] karne ya 5

Claromontanus [D] karne ya 5/6

I Washington, D.C. karne ya 5

Bohairic Coptic [Boh] karne ya 3/4

Sahidic Coptic [Sah] karne ya 3/4

Fayyumic Coptic [Fay] karne ya 3/4

Italic [Ital] karne za 4 hadi 13th

Latin Vulgate [Vg] karne za 4 na 5

Gothic [Goth] miaka ya 493-555 BK

Armenian [Arm] kutoka karne ya 5

Georgian [Geo] kutoka karne ya 5

Ethiopic [Eth] kutoka karibu mwaka 500 BK

Peshitta Syriac [Syr P] miaka ya 400-450 BK

Harclean Syriac [Syr H] mwaka 616 BK

Tazama www.BibleQuery.org/1ThessMss.htm kwa maelezo zaidi kuhusu hati za kale za maandiko ya 1 Wathesalonike.