Maswali ya Biblia Injili ya Marko

 

Maswali yanayohusu Injili zaidi ya moja yamejadiliwa kwenye Injili ya Kwanza yalikotokea au vinginevyo kwenye sehemu ya Injili.

 

S: Kwenye Marko, je kuna mambo gani ambayo ni pekee kwa Injili hii?

J: Marko ni Injili ya vitendo. Mara nyingi Marko inatumia msemo "mara mjoa." Inamsistiza Kristo mtumishi. Aliponya, alilisha, alitoa pepo, na alitoa maisha yake kuwa fidia/malipo ya ukombozi wa watu wengi. Kristo ni tumaini la watu wa kawaida. Aya kuu ni Marko 10:45.

Kwa upande wa lugha, wako watu wanaoona kufanana kwa maneno kwenye Waraka wa Petro na Injili ya Marko. Marko alikuwa mkalimali wa Petro. Marko ina misamiati myepesi kuliko Injili zote.

Kuhusu kufanana, karibu 90% ya mistari ya Marko inalingana na mistari iliyo kwenye Injili ya Mathayo.

Kuhusu dini za uongo, Marko 1:9-11, na Mathayo 3:16-17 ni vifungu vizuri vyenye kuonyesha Upentekste wa Mungu Mmoja kuwa Mungu Baba, Mwana na Roho Mtakatifu si nafsi moja wala "namna" tatu za nafsi moja.

 

S: Kwenye Mak, kwanini hakuna orodha ya uzao wa Yesu kama ilivyo kwenye Mathayo na Luka?

J: Yaelekea malengo ya Marko ya kuandika yalikuwa tofauti kwa kiasi fulani na malengo ya Mathayo na Luka.

Mathayo iliandikwa kwa Wayahudi, ambao walisistiza orodha ya uzao, na Injili ya Mathayo inasistiza kuwa Kristo ni Mfalme, na orodha ya uzao ni muhimu kwa wafalme.

Marko inasistiza kuwa Kristo ni mtumwa, na kuongelea zaidi kuhusu matendo na huduma vyake.

Luka inasistiza ubinadamu wa Yesu, na hakuna shaka kuwa iliandikwa kwa wasomaji ambao wengi wao walikuwa Wayunani (Wagiriki). Injili ya Luka ina mafundisho mengi ya Yesu aliyoyatoa kwa njia ya mifano.

Yohana inasistiza kuwa Yesu ni Mungu, na inakazia ishara saba alizozifanya Yesu.

 

S: Kwa kutumia kwake msemo wa "mara moja", Marko anatoa picha ya kuwa huduma ya Yesu ilichukua miezi michache tu, kuanzia kuvunja masuke wakati wa mavuno kwenye Marko 2 hadi Pasaka kwenye sura ya 11. Jesus, Interrupted, uk.42.

J: Nimesoma maandiko ya kikristo yaliyoandikwa waliandika kabla ya baraza la kwanza la kanisa la awali lililofanyika Nikea mwaka 325 BK isipokuwa vitabu viwili tu, na mengi ya maandiko ya Wanostisia (Gnostic) na Waebioni (Ebionite), na sijamwona mwandishi yeyote wa miaka iliyoltangulia baraza la Nikea Mkristo au Mnostisia aliyedhani kuwa Marko alionyesha kuwa huduma ya Yesu ilichukua miezi michache tu. Wanazuoni wanapaswa kuwa waangalifu kutokusoma kanuni zao wenyewe za kubuni kwenye maandiko ya zamani. Nina uhakika kuwa watu tofauti wanaweza kupata mawazo ya kila namna kwenye Biblia kama watafanya bidii ya kutosha.

 

S: Kwenye Mak 1:2, je Marko anaongeza maneno ya Mal 3:1 hapa?

J: Marko anafafanua Malaki kabla ya kunukuu Isaya.

Kwenye matini ya Kimasoretiki (Kiebrania) ya Agano la Kale, Malaki 3:1 inasema: "Angalieni namtuma mjumbe wangu, naye ataitengeneza njia mbele yangu . . ."

Kwenye Septujinti (Agano la Kale kwa Kigiriki, LXX), Malaki 3:1 inasema: "Angalieni namtuma mjumbe wangu, naye ataikagua njia kabla yangu . . ."

Marko 1:2 inasema, "Tazama, namtuma mjumbe wangu mbele ya uso wako, atakayeitengeneza njia yako." Angalia nyongeza hii "mbele ya uso wako" na "yako" badala ya "yangu."

Mambo mawili ya kuzingatia katika kujibu swali hili.

1. Marko alibadilisha pronomino, ambazo hazibadilishi maana hapa.

2. Kwa kuwa "mbele yangu" ni msemo wa mwisho, kuongeza msemo "mbele ya uso wako" kwa lengo la kusistiza kwa njia ya kurudia hakubadilishi maana pia.

S: Kwenye Mak 1:2, je Isaya alisema maneno haya yote?

J: Hapana, hii ni orodha ya nabii tatu (Kutoka 23:20 (LXX), Malaki 3:1 (Kimasoretiki), na Isaya 40:3 (LXX)). Orodha hii inaonyesha desturi iliyokuwa inatumika sana ya kunakiri vifungu mbalimbali vyenye somo moja. Kila unabii unahusisha matarajio ya matumaini ya mtangulizi wa Masihi na onya endapo hakusikilizwa. Msemo unaotumika kuielezea desturi hii ni "testimonia chain."

 

S: Kwenye Mak 1:2, je kuna tofauti gani kati ya mistari hii ya Agano la Kale kwenye tafsiri za Kimasoretiki na Septujinti (LXX)?

J: Marko 1:2 ni ‘testimonia chain', (ambayo pia inaitwa kuunganishwa) kwa mistari mitatu.

Kutoka 23:20 kwenye matini ya Kimasoretiki inasema, "Tazama, mimi ninamtuma malaika aende mbele yako, ili akulinde njiani na kukupeleka mpaka mahali pale nilipopatengenezea." Tafsiri ya Septujinti (LXX) inasema, "Na, tazama, ninamtuma malaika wangu mbele ya uso wako, ili kwamba akupeleke kwenye niliyokutengenezea.

Malaki 3:1 kwenye matini ya Kimasoteriki inasema, "ataisafisha njia", wakati ambapo tafsiri ya Septujinti (LXX), "ataikagua njia."

Isaya 40:3 kwenye tafsiri ya Kimasoretiki inasema, "yeye aliaye . . . inyoosheni njia kuu nyikani." Tafsiri ya Septujinti (LXX) inasema, "aliaye nyikani . . . yanyoosheni mapito."

 

S: Kwenye Mak 1:4, ondoleo la dhambi ni kitu gani hasa?

J: Ondoleo la dhambi ni sawa na msamaha wa dhambi. Kabla ya kuja kwa Yesu, Waisraeli walikuwa wakijitakasa mara kwa mara kwa kuosha miili yao. Yerusalemu ilikuwa na "mikvahs" nyingi ambavyo vilikuwa ni visima vya kufanyia ibada ya kujitakasa kwa kujiosha. Wayahudi pia walianzisha "ubatizo" wa mara moja wa watu wa mataifa waliokuwa wanabadilika na kushika dini ya Kiyaahudi ili kuwaondoa unajisi wao wa kipagani. Ubatizo wa maji ni kitu tunachokifanya kama ishara ya wokovu wetu. Pia ni ishara ya dhamira nzuri kwa Mungu (1 Petro 3:21).

 

S: Kwenye Mak 1:4, 9 na Luk 3:3, kwa kuwa ubatizo ulikuwa kwa msamaha/ondoleo la dhambi, kwa nini Yesu alibatizwa, kwa sababu yeye hakuwahi kutenda dhambi kwa mujibu wa Waebrania 4:15; 2 Korintho; 2:5:21, Yohana 8:46, na 1 Peter 1:19?

J: Yohana Mbatizaji yaelekea alikuwa na swali hilohilo kichwani mwake alipomuuliza Yesu kwa nini anataka abatizwe kwenye Mathayo 3:14. Yesu aligusia jibu la swali hilo kwenye Mathayo 3:15-16. Yesu hakusema kuwa alikuwa anabatizwa kwa ajili ya msamaha wa dhambi, bali alisema ilikuwa ni kwa lengo la "kutimiza haki yote." Tunapaswa kufuata mfano wa Yesu, na Yesu alibatizwa.

 

S: Kwenye Mak 1:5, kwa kuwa nchi yote ya Uyahudi walikwenda kumwona Yohana, je msemo huu unamaaanisha kuwa kila mtu alikwenda?

J: Hapana. Aya hii haisemi kuwa kila mtu, bali inamaanisha kuwa watu wengi kutoka sehemu zote za Uyahudi walikwenda kumwona Yohana.

 

S: Kwenye Mak 1:8, Yesu anabatizaje kwa Roho Mtakatifu?

J: Mambo manne ya kuyazingatia katika kujibu swali hili.

1. Mtu anapotubu na kumwamini Kristo, anazaliwa upya ndani ya Yesu na anabatizwa na Roho Mtakatifu.

2. Kisha Roho Mtakatifu huishi ndani mwake.

3. Wakristo wote wana Roho Mtakatifu (Warumi 8:10, 11, 15).

4. Kuwa na Roho Mtaka tifu kunatokea kabla ya ubatizo wa maji, kama Matendo 10:44-48 inavyoonyesha.

 

S: Kwenye Mak 1:10, kwa kuwa Roho Mtakatifu alishuka kutoka mbinguni kama hua, je jambo hili linaonyesha kuwa Roho Mtakatifu si nafsi, kawa Mashahidi wa Yehova wanavyofikiri?

J: NHapana. Kuwa na uwezo wa kuonekana kama hua hakuzuii akili, hisia, au tabia nyingine za Roho Mtakatifu. Vivyo hivyo kwenye Agano la Kale, kuonekana kwa Mungu kama kichaka kilchokuwa kinaungua hakukumpunguzia kwa namna yeyote ile uungu wake.

 

S: Kwenye Mak 1:12, kwa nini Roho Mtakatifu alimwongoza Yesu kwenda nyikani kujaribiwa?

J: Maandiko hayatoi sababu ya kufanya hivyo. Huenda jambo hili lilitakiwa kushughulikiwa kabla ya Yesu kuanza huduma yake. Kama wewe ni Mkristo, je kuna majaribu ambayo unatakiwa kuyashinda kwa uthabiti kabla ya Mungu kukutumia kwa njia kubwa?

 

S: Kwenye Mak 1:14, je "injili ya ufalme wa Mungu" ni sawa na "injili ya Kristo"?

J: Ndiyo, isipokuwa wakati huu Yesu hakuhubiri kuhusu kufa, kufufuka na kurudi kwake mara ya pili.

 

S: Kwenye Mak 1:15, je ufalme wa Mungu ulikuwa umekaribia kwa namna gani?

J: Ufalme wa Mungu ulikuwa umekaribia, upo pamoja nasi hapa, na utakuja.

Ulikuwa umekaribia: Yesu ni mfalme wa wafalme, na mahali alipo ufalme wa Mungu unaweza kusemwa kuwa umekaribia.
Upo pamoja nasi hapa: Ufalme wa Mungu upo pamoja na waumini leo. Hata hivyo, haujatokea duniani kwa kwa namna yeyote inayoonekana. Mtu anayemwamini Yesu anafanyika raia wa ufalme wa Mungu.

Utakuja: Ufalme wa Mungu hautaonekana kwa macho mpaka hapo Msihi atakapokuja tena kuanzisha utawala wake hapa duniani.

 

S: Kwenye Mak 1:24, kwa nini mapepo yalimkiri Yesu hadharani?

J: Maandiko hayasemi sababu ya kufanya hivyo. Huenda yalitaka kuifanya siri ya Yesu kuwa Masihi ifahamike mapema zaidi, lakini hii haielekei kuwa ndiyo sababu. Kuna uwezekano zaidi kuwa yalitegemea kuwa kama yangemkiri Yesu, angeweza kuyaacha ili yaendelee kukaa ndani ya watu. Huenda hii ndiyo ilikuwa sababu yao ya msingi, au badala yake, mapepo si lazima yafanye mambo yao kimatiki.

 

S: Kwenye Mak 1:24-26, je palikuwa na pepo moja au mapepo mengi ndani ya huyo mtu?

J: Inaweza kuwa vyovyote kati ya mambo hayo mawili. Mambo manne ya kuyazingatia katika kujibu swali hili.

1. Wakati Marko 1:24 inatumia "tuna", inaweza kuwa inaongelea mapepo mengi, pepo moja na mtu aliyepagawa, au nafsi nyingi (multiple personalities) kwenye mtu aliyepagawa au pepo moja.

2. Kwenye Mak 1:25-26, Yesu alimwongelesha pepo mmoja tu.

3. Inawezekana pepo lilikuwa moja lakini lilijieleza kama mapepo mengi.

4. Hakuna kitu kinachosema kuwa pepo linatakiwa kuwa moja kama mnyama. Hakuna sehemu ya Maandiko inayozuia mapepo kuwa kama mimea, au chembechembe zinazoweza kujigawa, ingawa Maandiko hayasemi kitu kuhusu kukisia huku.

 

S: Kwenye Mak 1:34, 3:11-12, Luk 4:34-35, na Luk 4:41, kwa nini Yesu hakuyaruhusu mapepo kuongea?

J: Nyakati hizi zote zilikuwa mwanzoni mwa huduma ya Yesu. Marko 1:34 inasema ilikuwa ni kwa sababu mapepo yalijua Yesu alikuwa ni nani. Mtu aliyeponywa mwanzoni mwa huduma ya Yesu aliamriwa kutokumwambia mtu yeyote Yule (Marko 1:44-45). Wakati Petro alimkiri Yesu kuwa Kristo, Yesu aliwaamuru wanafunzi kutokumwambia mtu yeyote wakati ule (Mathayo 16:20; Marko 8:30). Hivyo, sababu yenye uwezekano mkubwa ni kuwa Yesu hakupenda kuwa itangazwe wakati ule kuwa alikuwa Masihi. Alitaka watu wayaone maisha, mafundisho, na miujiza vyake na wapate fursa ya kuamua wao wenyewe.

 

S: Kwenye Mak 1:37, kwa kuwa watu "wote" walimtafuta Yesu, je ilikuwa ni kila mtu aliyekuwa anamtafuta?

J: Karibu kila mtu kwenye mkoa wa karibu alikwa anamtafuta Yesu kwa sababu moja au nyingine. Kwa bahati mbaya, jambo hili halimaanishi kuwa kila mtu alikuwa anatafuta wokovu toka kwa Yesu. Watu wengi walimtafuta kwa furaha tu ya kuona miujiza.

 

S: Kwenye Mak 1:38, kwa nini Yesu hakukaa mahali pamoja kwa muda mrefu?

J: Ni dhahiri kuwa Yesu hakuthamini kurudia rudia mafundisho na miujiza alivyofanya ili kuwavuta watu waje kwake. Mara watu walipopata ufahamu wa kutosha kufanya uamuzi kuhusu yeye, Yesu alikwenda sehemu kwa watu wengine waliokuwa bado kumuona.

 

S: Kwenye Mak 1:44-45, kwa nini mtu yule aliyeponywa ukoma hakumtii Yesu na alimwambia kila mtu kuhusu kuponywa kwake?

J: Maandiko hayasemi sababu ya kufanya hivyo, lakini leo hii tunaweza kuona watu wanaopenda Baraka na vitu vizuri vya ukristo, lakini hawana fikra ya utiifu au wajibu. Jambo hili linaweza kuwa kubwa zaidi kwenye dini nyingine mbali ya ukristo. Kuna watu wanaoliona jambo hili kuwa ndio msistizo wa New Age na harakati nyingine za kiroho kama ahadi ya kiroho bila wajibu.

 

S: Kwenye Mak 2:4, watu waliomleta mtu aliyekuwa amepooza waliwezaje kufumua paa na kumteremsha mgonjwa?

J: Nyumba za kawaida za wakati ule zilijengwa kwa kutumia makuti/nyasi, udongo na miti. Kitu pekee walichotakiwa kufanya ni kuondoa makuti/nyasi na kuchimba udongo.

Jambo hili huenda lilimuaibisha mgonjwa na marafiki wake, lakini huenda hawakuwa wanalifikiria, bali walichokitaka wao kilikuwa ni rafiki wao kuponywa. Je uko tayari kupita kwenye dari kwa ajili ya rafki yako?

 

S: Kwenye Mak 2:7, kwa nini waandishi waliona kuwa Yesu amekufuru kwa kumwambia mtu aliyekuwa amepooza kuwa dhambi zake zimesamehewa?

J: Wayahudi wakifahamu kuwa ili mtu aweze kusamehewa na kurejeshewa mahusiano na aliyekosewa ni lazima mkosaji aombe msamaha na mtu aliyekosewa atoe msamaha. Wakati Yesu alipokuwa anatoa msamaha alisimama kwenye nafasi ya Mungu. "Kufanya dhambi" tu kusingekuwa kumkosea Yesu - bila Yesu kuwa Mungu.

 

S: Kwenye Mak 2:10, je ingeweza kuwa kufuru kwa Yesu kusema dhambi za mtu aliyekuwa amepooza zimesamehewa kama Yesu asingekuwa Mungu?

J: Kwenye muktadha huu, ndiyo. Hata hivyo, Yesu baadaye alitangaza msamaha Mungu kwa watu wote waliotubu na kumgeukia yeye , na tunaweza kutangaza kwa jina la Mungu jambo ambalo Yesu alilitangaza. HIvyo, inakubalika kwa Waprotestanti au mapadri kutangaza kuwa dhambi za mtu zimesamehewa, kwani hawasemi kuwa wao wenyewe wanayo mamlaka ya kusamehe bali wanatangaza kitu ambacho Mungu amesema. Ni dhahiri kuwa usemi huu ulikuwa mgumu kueleweka na baadhi ya watu waliokuwa wanamsikiliza Yesu. Lakini wakati mwingine Mungu hutuambia maneno ambayo yanakuwa magumu kuyanyambua na kmuelewa yeye kwa upya na kina.

 

S: Kwenye Mak 2:15, je Yesu alikuwa na nyumba yake mwenyewe?

J: Kuna mambo matatu ya kuzingatia katika kujibu swali hili.

1. Mama wa Yesu aliishi mahali fulani na "nyumbani" kwa Yesu kulikuwa Kapernaumu, hivyo huenda Yesu alikuwa na nyumba huko.

2. Katika aya hii, neno "yake" linauwezekano mkubwa zaidi wa kumuongelea Mathayo kuliko Yesu, hivyo maneno haya yasema kuhusu nyumba ya Mathayo, si ya Yesu.

3. Kwa hakika, kwa mtazamo mwingine, Yesu, kama Mungu, anamiliki nyumba zote duniani. Hata hivyo, hii siyo maana ya neno "yake" hapa.

 

S: Kwenye Mak 2:17, ni kwa nini Yesu alisema kuwa hakuja kuwaita wenye haki?

J: Yesu hakumwacha mtu yeyote Yule, kama Rum 3:3-10, 23-24 inavyoonyesha, kwani hakuna mtu aliyekuwa na haki. Kitu ambacho Yesu alikimaanisha hapa ni kuwa hakuwa anawaokoa watu waliokuwa wanafikiri kuwa walikuwa wenye haki sana hata hawakumhitaji mwokozi.

 

S: Kwenye Mak 2:18-20, kwa nini wanafunzi wa Yesu hawakuwa wanafunga?

J: Wayahudi wengi walikuwa wanafunga kwa sababu ya desturi na mapokeo, si kwa ajili ya kujitoa kwao kwa Mungu, na wanafunzi hawakupaswa kufunga kwa sababu hii. Wakristo bado wanafunga leo, ili waweze kupata muda zaidi wa kusali, na kama nyingine ya kuonyesha masikitiko au udhabiti wa maombi yao kwa Mungu.

Kwa utani kiasi, unaweza kumtazama mkristo yeyote anayetakiwa kupunguza paundi/kilo kadhaa za a mwili wake, utamwona mtu aliye na uwezo mkubwa sana wa kuelezea maombi yake kwa njia ya kufunga.

Kwa ukweli, Wakristo pia hufunga ili kujisogeza karibu na Mungu. Yesu hakupinga kufunga, ila kwa kuwa wanafunzi wake walikuwa pamoja naye hawakuwa na sababu ya kufunga kwa ajili ya jambo hilo wakati ule.

 

S: Kwenye Mak 2:21-22 na Mat 9:16-17, je mifano miwili ya mavazi na wineskins inamaanisha nini?

J: Mafarisayo walikuwa wanasema kuwa walipaswa kufuata mapokeo ya kufunga wakati ambapo Yesu ambapo Yesu alikuwa anahubiri injili alikuwa anasema kitu kipya.

Kwa nje, baadhi ya vitu vipya haviwezi kupachikwa kwenye vitu vya zamani, kwa sababu vitu vya zamani haviwezi kuvistahimili.

Kwa ndani, wakati mwingine vitu vyenye kuwekwa ndani ya vingine haviwezi kuwekwa kwenye vitu vyenye namna zilizochakaa, bila kuziharibu namna hizo za zamani.

Kibayana kuhusu injili, huwezi kuipachika kwenye kitu ulichokuwa unakifahamu kuhusu Agano la Kale; si jambo la kubadilisha misemo iliyomo kwenye Agano la Kale, lakini ni "fumbo" ambalo halikuelezewa mpaka wakati Kristo alipokuja.

Isitoshe, hakuna uhakika endapo neno "kuu kuu" kwenye mifano hii miwili linamaanisha Agano la Kale, au Agano la Kale pamoja na desturi za Mafarisayo zilizoongezwa. Bila kujali aina ya mapokeo ya kidini Kiyahudi au dini yeyote ile ambayo mtu anaweza kuwa nayo, habari njema (Injili) si kitu unachoweza kukiongezea tu kwenye mapokeo yaliyokuwepo awali.

 

S: Kwenye Mak 2:23-24, ni kitu gani kilichochukuliwa kuwa makosa kuchuma masuke ya nafaka?

J: Agano la Kale halisemi makosa yeyote yaliyokuwepo katika kufanya hivi. Hata hivyo, Mafarisayo walichukuliwa kuchuma kokote kwa nafaka, hata kama ni kiasi kidogo tu, kuwa ni kitendo cha kuvuna. Kwa kuwa kuvuna nafaka kulikuwa ni kazi, kitendo hiki kilizuiliwa kwenye siku ya sabato.

 

S: Kwenye Mak 2:26, je ilikuwa ni katika siku za Abiathari, au baba yake Ahimeleki?

J: Abiathari na Ahimeleki waliishi wakati huo, ingawa Ahimeleki, baba wa Abiathari, aliuawa muda mfupi baadaye. Neno la kigiriki, epi Abiathar archiereos, linamaanisha "wakatii wa Abiathari kuhani mkuu." Si tu kwamba Abiathari alikuwa hai wakati huo bali pia alikuwepo jambo hili lilipotokea. Msemo huu unafanana na kusema "wakati wa Daudi, mtawala wa Israeli, ingawa Daudi alikuja kuwa mtawala wa Israeli baadaye.

Kwa ufupi, ulikuwa ni wakati wa Abiathari, ambaye alikuja kuwa kuhani mkuu baadaye. Tunapaswa kuwatii wazazi wetu katika Bwana, lakini kuna nyakati ambazo tunatakiwa kutokutii maagizo ya wazazi wetu ya moja kwa moja au kupingana na matakwa yao yasiyoelezwa moja kwa moja, endapo mambo wanayoyataka si mapenzi ya Mungu.

 

S: Kwenye Mak 3:31-35, je Yesu alitenda dhambi kwa kutokumheshimu mama yake hapa?

J: Hapana, kwa sababu hawakuwa wanamwomba Yesu akatishe mahubiri yake ili awaone wakati ule, na Yesu alijua kuwa Mungu Baba alipenda yeye ahubiri sasa. Familia ya Yesu ilifikiri kuwa Yesu alikuwa amerukwa na akili kwenye Mak 3:20-21. Mfano, ikiwa mama yake alimtaka asihubiri tena, Yesu angepaswa kutokuitii amri hii (ya mfano) ili aitii amri ya Mungu.

 

S: Kwenye Mak 3:31-35, kwa nini Yusufu hakuwepo hapa?

J: Maandiko hayasemi kitu chochote. Hata hivyo, mapokeo ya kanisa yanasema kuwa Yusufu alikuwa na umri mkubwa sana kuliko Mariamu na huenda alikuwa ameishakufa wakati huo.

 

S: Kwenye Mak 4:10-20, kwa nini Yesu alieelezea maana ya mifano hii kwa wanafunzi wake kumi na mbili tu?

J: Maandiko hayasemi kwa nini makutano hawakusikia maelezo yote, lakini Yesu alipenda sana wanafunzi wake wasielewe vibaya. Kwa hakika, mtu yeyote mingoni mwa makutano angependa awe mwanafunzi wa Yesu na afundishwe na Yesu na wanafunzi kumi na mbili pia.

Hii ni namna mambo yalivyo leo hii. Kila mtu anaweza kusikia kitu kuhusu Injili, lakini akitaka kujifunza kwa ukamilifu, atahitaji kusoma neno la Mungu na kujifunza pamoja na wakristo wengine.

 

S: Kwenye Mak 4:11-12, kwa nini Yesu hakuielezea injili kiufasaha badala yake azungumza kwa mifano ili watu wasimwelewe, wasitubu, na kusamehewa? Je hakuwa amekuja kuokoa watu wote? (Ahmad Deedat alileta wazo hili.)

J: Yesu alikuwa anaongelea Isa 6:9, 10. Yesu aliongea kwa mifano ili awarehemu watu! Yafuatayo ni mambo manne ya kuzingatia wakati wa kujibu swali hili.

1) Mungu anapenda watu wote waokolewe (2 Pet 3:9; Eze 17:23).

2) Lakini kuna baadhi ya watu ambao wamechagua kulikataa neno la Mungu na kuna matokeo ya jambo hilo katika maisha haya. Watu wa aina hii hufanywa kuwa wagumu kwenye kusikia kwao na kwenye mioyo yao (Kut 8:15, 32; 9:17, 34;Pr28:14; Rum 1:18-20; Ebr 3:12-15; Zek 7:12).

3) Kwa watu wanaomkataa Mungu, ni vema kwao kutokujua kweli kuliko kuijua na kuikataa kwa mujibu wa 2 Pet 2:20-22.

4) Mfano hoo unafaa sana kwa sababu watu wanaotaka kumfuata Mungu wanaweza kusaidiwa kufahamu maana yake, na mfano hauwezi kueleweka na watu ambao hawapendi kumfuata Mungu.

Kama mtu ameishaikataa kweli anayoifahamu ya Mungu, Mungu halazimiki kumpa kweli zaidi.

 

S: Kwenye Mak 4:14-20 na Luk 8:5-15, kwenye mfano wa mpanzi, watu wanafananaje na aina nne za udongo?

J: Ifuatayo ni mifano michache.

1. Kuna watu ambao hawaijali kabisa injili. Shetani amekuwa akifanya kazi ndani mwao kiasi kwamba Injili haiwezi kuzama kwenye udongo mgumu. Wako watu wanaoupinga sana ukristo. Wengine hawaupingi, lakini kama nilivyosikia, "nitakuja kwenye kipindi cha kujifunza Biblia kama sitakuwa na kitu kingine chochote cha kufanya."

2. Wengine wanapenda kuipokea injili mara wanapoisikia, lakini wanakumbwa na matatizo au mateso.

3. Wako wanaokuwa kwenye injili, lakini wanasongwa na mahangaiko ya maisha haya, au majaribu ya jamii yao. Tamaa ya vitu, kuangalia picha chafu na/au za kikatili, na ulevi ni baadhi ya "miiba" ya kujiangalia nayo sana kwenye nchi za magharibi.

4. Watu wengine huitikia na hudumu katika imani. Miongoni mwao, watu tofauti huzaa matunda ya kiasi tofauti.

 

S: Kwenye Mak 4:14-20, kwenye mfano, je mpanzi hakukosa kuwa mwangalifu na mbegu?

J: Kutokuwa mwangalifu na mbegu, hapana; mwenye kupanda mbegu kwa ukarimu, ndiyo. Hakuna "aina ya tano" ya udongo ambayo ingeweza kuzaa matunda isipokuwa tu mpanzi alisahau kupanda mbegu ndani yake. Ukweli ni kwamba, udongo huo ungeweza kutoa kisingizio kuwa "Ningeweza kuwa udongo wenye kuzaa sana, lakini namlaumu mpanzi kwa kutokupanda mbegu juu yangu." Mtu mwingine anaweza kumlaumu mpanzi kwa "kupanda mbegu zake kwa ukarimu sana", kuupa nafasi kila aina ya udongo ingawa hata kama nafasi hiyo ingepotea. Hata hivyo, hakuna mtu atakayeweza kumlaumu mpanzi kwa haki kwa kuwa mchoyo na mbegu.

 

S: Kwenye Mak 4:22, ni aina gani za vitu vitakavyodhihirishwa baadaye?

J: Kila tendo, zuri na baya, litadhihirishwa kwenye siku ya hukumu. Kwa sababu kila neno lisilo maana ambalo tunalisema tutapaswa kulitolea hesabu kwa mujibu wa Mat 12:36-37. Mungu huhukumu mwenendo, na kuna mtu aliwahi kusema kuwa mwenendo ni jinsi unavyokuwa wakati unapofikiri kuwa hakuna mtu anayekuona.

 

S: Kwenye Mak 4:24, Luk 6:38, na aya nyignine, je inamaanisha nini kusema kuwa kipimo utumiacho/utoacho ndich utakachopkea?

J: Ay azote hizi zinasema jambo moja la msingi kuwa "tumia au poteza", lakini kuna vitu vitatu vya kuvifanya tokana na aya hizi.

Mak 4:24 inasistiza kuwa kwa kadri unavyotumia karama na hekima vya Mungu ndivyo utkavyopewa zaidi. Kama hutumii kidogo ulichopewa, hat hicho kitachukuliwa toka kwako.

Luk 6:38 inafanana na aya iliyotangulia, lakini inasistiza vitu tunavyowapa watu wengine, ikiwa ni vitu vizuri, au msamaha na rehema, kama Luk 6:37 inavyosema.

Mat 18:35; 6:12 inasema kuwa Mungu atatusamehe kwa jinsi tunavyosamehe watu wengine. Kipimo cha rehema na msamaha tunatoa kwa watu wengine kinaonyesha kiasi tutakachopokea.

Kwa ufupi: baadhi ya vipengele vya hukumu ya Mungu kwenye siku ya mwisho, na baraka zake katika maisha haya, ni thabiti na zinafanana kwa watu wote. Vipengele vingine vinategemea na ufahamu alionao mtu (Rum 4:15; 5:13; 2 Pet 2:21-22, n.k.). Baadhi ya vitu ambavyo mtu anapokea vinategemea na kitu/vitu alivyotoa kwa watu wengine.

 

S: Kwenye Mak 4:31, kwa nini aya hii inasema kuwa chembe ya haradali ni ndogo kuliko chembe nyingine zote, kwani kuna chembe ndogo zaidi?

J: Chembe ya haradali ilikuwa ni ndogo kuliko chamber zote, lakini ikilinganishwa na nini? Ingawa Maandiko hayasemi, watu wote wanakubaliana kuwa chembe ya haradali ilikuwa ni ndogo zaidi ya chembe walizozifahamu. Haikuwa ni chembe ndogo kuliko zote zilizokuwa zinapandwa kwenye mashamba.

 

S: Kwenye Mak 4:32, kwa nini mharadali unasemwa kuwa ni mmea mkubwa kuliko yote wakati, kwa kuwa kuna mimea mikubwa kuliko huu?

J: Yesu hakuwa anafundisha somo la elimu ya mimea hapa. Yesu alikuwa anaongea kwa manufaa ya watu waliokuwa wanamsikiliza, na aliongea kwa kutumia maneno ambayo wamgeweza kuyaelewa. Mharadali ulikuwa ni mmea uliokuwa mkubwa zaidi katika mimea iliyotambuliwa kuwa ni ya msimu.

 

S: Kwenye Mak 4:34, kwa nini Yesu alifundisha kila kitu kwa mifano?

J: Kwa kutumia njia hii maalumu ya kufundishia, Yesu aliweza watu wote walipenda kujifunza, na kuwaficha watu ambao hawakutaka kunfuata.

 

S: Kwenye Mak 4:38, je Yesu angewezaje kulala wakati wa dhoruba?

J: Yesu anaweza kuwa alichoka baada ya kuhubiri kwa muda mrefu sana. Pia, huenda Mungu Baba alipenda Yesu awe kwenye usingizi mzito wakati huu ili kuwaonyesha wajibu wao wa kuomba.

 

S: Kwenye Mak 4:39, je upepo ungewezaje kutulia haraka namna hii?

J: Upepo ni matokeo ya tofauti ya shinikizo wa sehemu mbili. Ingawa upepo unaweza kutulia mara moja kwa kawaida, kifungu hiki cha Maandiko kinaonyesha kuwa kutulia kwa upepo kulikuwa ni muujiza.

 

S: Kwenye Mak 5:1, je nchi ya Wagerasi ilikuwa wapi?

J: Hili ni eneo lilikuwa karibu na mji wa Gerasa, ulikuwa karibu kilometa 56 (maili 35) kusini mashariki mwa Bahari ya Galilaya kwenye nchi ya sasa ya Yordani. Kilometa moja na nusu hivi (maili moja) kusini mwa kijiji cha sasa cha Khersa kuna kilima chenye mwinuko mkali wa meta 36 (yadi 40) toka ufukoni. Kilometa tatu (maili mbili) kuna makaburi mawili yaliyochongwa ambayo yalikuwa yanatumika kama kama nyumba pia.

 

S: Kwenye Mak 5:3-4, je mtu huyu aliyepagawa mapepo angewezaje kuwa na nguvu nyingi kiasi cha kukata minyororo na kuvunja pingu?

J: Hata watu ambao hawakuwa wamepagawa mapepo wanafahamika kufanya matendo makubwa ya ujasiri wanaapokuwa kwenye mazingira ya shinikizo la kufa au kupona. Nimewahi kusikia king'ora cha mlipuko wa kiwanda cha kemikali (ambao kwa bahati nzuri haukutokea), na mwendesha mashine ya kemikali aliuruka uzio wa mnyororo wenye urefu wa meta mbili na nusu (futi nane). Aliporudi kweny kiwanda, aligeuka na kuuangalia tena uzio akishangaa, kwani ni kama hakuamini kitu alichokuwa amefanya.

Pia nimewahi kusikia kuhusu mwanamke ambaye gari lililokuwa limeegeshwa lilipokuwa karibu kumgonga mtoto wake aliyekuwa ameshikilia pembe moja ya hilo gari.

 

S: Kwenye Mak 5:6, kwa nini mtu aliyepagawa mapepo alikuwa akimkimbilia Yesu ili kumwabudu?

J: Ingawa Maandiko hayasemi, tunaweza kukisia kwa njia moja hapa. Kama pepo lilifikiri kuwa Yesu alikuwa anamjia na kwamba hangeweza kutoroka, basi huenda lilikuwa linataka kumshambulia Yesu kabla ya kumwomba Yesu amwache.

 

S: Kwenye Mak 5:9 na Luk 8:30, ni kwa sababu gani pepo liliitwa "Jeshi?"

J: Kikosi cha askari wa Kirumi cha wakati ule kilikuwa na wanajeshi karibu 5,000 hadi 6,000. Kwa maneno mengine, huyu mtu hakuwa anasumbuliwa na pepo mmoja bali mapepo 5,000 au 6,000. Mungu hatatizwi na idadi ya matatizo tunayokuwa nayo, Yeye anaweza kuyatatua matatizo yote.

Jambo lisiloeleweka vizuri ni endapo kila pepo lililopo leo limekuwa likiishi hivyo peke yake tokea kwenye bustani ya Edeni au la. Kuna uwezekano kuwa mapepo yanajizalisha (kama vijidudu) ama ndani ama nje ya udongo wenye rutuba wa binadamu. Hata hivyo, wazo hili ni la kukisia tu.

 

S: Kwenye Mak 5:10-14 na Luk 8:32, kwa nini Yesu anaonekana kufanya makubaliano na mapepo?

J: Ingawa Yesu alikuwa na uhuru wa kufanya hivyo, Maandiko hayasemi kuwa alifanya kitu chochote kile zaidi ya kuwapa ruhusa. Yesu hakuyapa mapepo msaada wowote ule; nguruwe walizama kwenye maji.

 

S: Kwenye Mak 5:10-14, je Wakristo wanapaswa kufanya makubaliano na mapepo nyakati za leo?

J: Hakuna ushahidi kuwa tunapaswa kufanya hivyo. Hatuna ufahamu kama aliokuwa nao Yesu. Kwa vile mapepo yanaweza kuona kwa kutumia namna nyingine mbali na zetu, yanaweza kuwa na ufahamu mkubwa zaidi kuliko sisi. Hata hivyo, kwa kuwa hakuna uhakika kuwa yanaaminika, hakuna haja yeyote ya kutufanya tulazimike kuongea nayo, isipokuwa kuyaamuru kufungwa au kuondoka.

 

S: Kwenye Mak 5:12 na Luk 8:30-33, je ni kwa nini mapepo yalitaka kwenda kwenye nguruwe?

J: Maandiko yanatupa fursa kidogo na ya muda mfupi tu ya kuona mawazo yaliyokuwemo kwenye mawazo ya mapepo. Inaelekea kuwa mapepo yalikuwa yanawaza kuwa kuingia kwenye nguruwe lilikuwa jambo zuri kuliko kwenda shimoni kwa wakati ule.

Maandiko hayasemi endapo mapepo yalisababisha nguruwe wazame kwenye maji kwa makusudi, au yaliwafanya wazame kwa bahati mbaya, au hata kama walijua kuwa nguruwe wangezama. Mwisho, Maandiko hayasemi endapo mapepo na shetani yana akili timamu au huwa na wazimu wakati mwingine.

 

S: Kwenye Mak 5:13, kwa nini alidaiwa kuangamiza nguruwe 2000 ili kumponya mtu mmoja? (Ahmad Deedat alileta wazo hili)

J: Mambo mawili ya kuzingatia katika kujibu swali hili.

a) Natumaini kuwa Deedat atakubali kuwa sisi binadamu tuna thamani kuliko nguruwe. Binadamu, iwe ni Saudi Arabia, India, au nchi za magharibi wanaua wanyama wakati wote kwa ajili ya chakula. Nguruwe hawa, waliofugwa na watu wasiokuwa Wayahudi walioishi upande wa mashariki wa Bahari ya Galilaya, walifugwa kwa ajili ya kitoweo, si kama kondoo au ng'ombe wa maziwa, hakuna lengo linguine la kufuga nguruwe.

b) Yesu hakuwaua nguruwe. Wakati jeshi la mapepo limemtoka mtu aliyekuwa amepagawa, lilikwenda kwa nguruwe, na jambo hilo lilisababisha nguruwe kuzama majini.

c) Ninashangaa kuona anajifanya kuwahurumia nguruwe, wakati Kurani inasema kuwa Nabii wa Allah, aliyekuwa na busara kuliko Musa, alimwendea mvulana mdogo na kumvunja shingo lake na kumuua. (Hapana, mvulana huyu hakufufuliwa au kufanyiwa kitu chochote baada ya hapo; alibaki mfu tu.) Habari hii imo kwenye Sura 18:63-82. Kwenye hadithi za Bukhari juzuu ya 1 kitabu cha 3 na.124, uk.92 kinafafanua habari hii kwenye kisa cha al-Khidr. Abu Dawud juzuu ya 3 na.4688-4690, uk.1319 inahalalisha jambo hili kwa kusema kuwa mvulana huyu aliyeuawa na al-Khidr alizaliwa kafiri. Sasa je kuwa mvulana mdogo asiyemwamini Mungu ndilo jambo la kumfanya mtu akatwe shingo lake machoni pa Waislamu?

 

S: Kwenye Mak 5:17 na Luk 8:37, kwa nini makutano walimwambia Yesu aondoke?

J: Watu hawa waliona vizuri kabisa wema na nguvu vya Yesu, lakini bado walimwambia aondoke. Walikuwa wanafuga nguruwe, ambao wangekosa soko miongoni mwa watu wa Mungu waliokuwa wanaifuata sheria ya Mungu. Leo hii, itikio la kawaida la kuuona wema na pendo la kweli la Mungu ni kujaribu kuuondoa. Siku hizi jambo hili ni kweli hasa kwa watu "wanaouza nguruwe" za kiroho.

 

S: Kwenye Mak 5:18-20, kwa nini Yesu hakumruhusu mtu aliyetolewa mapepo kumfuata?

J: Hapana shaka Yesu aliona kuwa kitendo cha mtu aliyeponywa mapepo kuishi na watu walikuwa wanamfahamu kingekuwa huduma kubwa zaidi miongoni mwao kuliko mtu wa kawaida wa mataifa kwenda kuishi na Wayahudi ambao hawakuwa wanamjua na walikuwa wameishaona miujiza ya Yesu.

Leo hii tunaweza kuwa na desturi ya kupenda kufanya huduma za "maonyesho" zaidi, lakini Mungu anaweza kuwa na makusudi makubwa zaidi kwa kututuma sehemu nyingine au kutuacha mahali tulipo. Badala ya kuuliza kuwa kwa nini Mungu hakuweki kwenye huduma mahali pengine, unapaswa kuuliza ni jinsi gani unaweza kutumika vizuri zaidi mahali ulipo.

 

S: Kwenye Mak 5:27-34, wakati mwanamke aliyekuwa anatokwa damu alipogusa vazi la Yesu, kwa nini Yesu aliuliza kwa sauti kuwa ni nani aliyemgusa?

J: Kuna majibu mawili yanayoweza kutolewa.

1. Kwa kuwa Yesu alichukua baadhi ya tabia za kibinadamu ambazo zina mipaka, kama kutokujua kila kitu, alipokuja hapa duniani, ni kweli kwamba Yesu hakumjua mtu aliyekuwa ameponywa kimiujiza kwa kuguza vazi lake.

2. Bila kujali kama alimjua mtu huyo, Yesu alimtaka aje mbele. Kulikuwa na kazi ambayo ilikuwa bado kukamilika, ambayo ni Yesu kuongea naye na kutangaza kuwa imani yake imemponya, na kwenda kwa amani na kuwekwa mbali na mateso aliyokuwa nayo.

 

S: Kwenye Mak 5:30-33, kwa kuwa Yesu aliweza kujua kitu kilichokuwa ndani ya mtu huyo, kwa nini alimuuliza?

J: Yesu aliuliza kwa faida ya huyo mwanamke si yeye mwenyewe. Alitaka kumsaidia, lakini alimpenda mwanamke mwenyewe aombe kwanza.

 

S: Kwenye Mak 5:35 na Luk 8:49, kwa nini wajumbe wa Yairo hawakutaka kumsumbua Yesu mara baada ya binti Yairo kufa?

J: Ingawa Yesu aliweza kuponya magonjwa, wajumbe hawa wanaelekea kudhani kuwa angeweza kumfufua mtu aliyekwisha kufa.

 

S: Kwenye Mak 5:39 na Luk 8:52-53, kwa nini Yesu alisema kuwa binti Yairo hakuwa amekufa bali alikuwa amelala?

J: Kuna majibu mawili yanayoweza kutolewa.

Kuzimia: Huenda binti hakuwa amekufa kabisa bali alikuwa amezimia karibu ya kufa. Maandiko hayasemi kuwa alikuwa amekufa. Badala yake Luk 8:49 inasema watu wengine walisema kuwa alikuwa amekufa, Luk 8:53 inasea "walijua" kuwa amekwisha kufa, na Luk 8:55 inasema kuwa roho yake "ikamrejea." Hata hivyo, jibu lifuatalo lina uwezekano mkubwa zaidi wa kuwa sahihi.

Kifo: Binti alikuwa amekufa kabisa. Hata hivyo, kifo kinachukuliwa kuwa ni hatua ya mwisho ya kimwili, na Yesu alitumia sitiari ya kuwa alikuwa amelala tu, kwa sababu alijua kuwa kuwa anakwenda kumfufua.

 

S: Kwenye Mak 5:41 na Luk 8:54, kwa nini Yesu alisema "Msichana, nakuambia, inuka?"

J: Kama Yesu angesema tu "inuka", huenda wafu wote wangeinuka. Isingesaidia kwa Yesu kusema "inuka", na kufanya wafu wote wainuke, na kisha kusema tena, "nina wazo tofauti . . ."

 

S: Kwenye Mak 5:42 na Luk 8:56, kwa nini Yesu aliwaambia wazazi wa binti wasimwambie mtu yeyote kuhusu muujiza huu?

J: Jambo linaloweza kuwa linahusika hapa ni muda; huenda Yesu hakutaka muujiza huo uelezwe wakati bado yupo kwenye mji ule. Watu wangeishia kuufahamu kwa hakika, lakini Yesu hakutaka watu zaidi wamfuate "kwa ajili ya kuonekana na watu wengine tu."

 

S: Kwenye Mak 5:41; 7:34, kwa nini Marko anafafanua msemo wa Kiaramu kwa wasomaji wake?

J: Injili ya Marko iliandikwa kwa Kigiriki (Kiyunani), na ingawa watu wengi Palestina walikuwa wanaongea lugha zote mbili (Kigiriki na Kiaramu), Marko alitarajia kuwa wengi wa wasomaji wake Wagiriki wasingeyafahamu baadhi ya maneno ya Kiaramu. Tofauti na wazo hili, Papias anasema kuwa Injili ya Mathayo iliandikwa kwanza kwa Kiebrania.

Mtindo wa Marko wa uandishi unaonekana kufanana sana na Kiaramu kuliko hata Mathayo. "Kwa kweli, moja ya dosari ya Kigiriki cha Injili hii inaonekana kuwa ni uwingi wa misemo yenye mfumo wa Kiaramu, iliyotafsiriwa neno kwa neno, kana kwamba Marko alikuwa anaandika kwa Kigiriki lakini anafikiri kwa Kiaramu."

 

S: Kwenye Mak 5:41, je Yesu alisema Kiaramu au Kigiriki?

J: Hapana shaka kuwa Yesu aliongea Kiaramu, kama inavyodhihirishwa na misemo yake ya Kiaramu. Hata hivyo, watu wengi Galilaya na Dekapoli waliongea lugha zote mbili lakini walipendelea zaidi kuongea Kigiriki. Kwa kuwa Yesu alitokea sehemu hiyo, kuna uwezekano kuwa aliongea na watu kwa kutumia lugha zote mbili.

Ifuatayo ni baadhi ya misemo maalumu ya Kiaramu iliyorekodiwa

A1. "Wana wa ngurumo" (Mak 3:17)

A2. "Msichana, nakuambia, inuka!" (Mak 5:41)

A3. "Funguka" (Mak 7:34)

A4. "akimwapiza" (Mat 5:22)

A5. "Abba, Baba" (Mak 14:36)

A6. "Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha" (Mat 27:46; Mak 15:34)

A7. "Kwamba ataponya siku ya sabato; kusudi wapate neno la kumshitakia" (Luk 6:7) ni msemo wa Kigiriki wenye sarufi ya ajabu (kitenzijina kikamilisho chenye kujitegemea) chenye kuinyesha tofauti ndogo ya maana ya maneno ya Kiaramu, kwa mujibu wa A Wandering Aramean, uk.12-13.

Yesu aliongea Kiebrania kwenye maono ya Paulo kwenye Mdo 26:13-15.

Ifuatayo ni misemo yenye kuonyesha kuwa Yesu aliongea Kigiriki pia.

G1. Petros, Petra (Mat 16:15-18)

G2. Majina kama Filipo na Andrea yalikuwa kwa Kigiriki. Jina Bartimayo ni mchanganyiko wa Kiaramu na Kigiriki.

G3. Mwisho, ni vigumu kuamini kuwa kuwepo kwa Injili zisizopungua tatu zilizoandikwa kwa mara ya kwanza katika Kigiriki, na Paulo na waandishi wengine wa nyaraka waliandika kwa Kigiriki, kwamba Yesu asiijue lugha ambayo hata wavuvi wa Galilaya waliijua.

 

S: Kwenye Mak 6:1, je nchi ya kwake Yesu ilikuwa ni ipi?

J: Hii itakuwa ni eneo la Nazareti lililo Galilaya.

 

S: Kwenye Mak 6:1-6, kwa nini watu wengi kwenye mji wa Yesu hawakuamwamini?

J: Kuna watu walioamini. Hata hivyo, watu wengi walikuwa na shida ya kufikiri kuwa mtu aliyewahi kuwa mtoto, akakua mahali hapohapo ambapo nao wamekua, akawa mtu mkubwa, hata awe Masihi (Kristo).

 

S: Kwenye Mak 6:5, je kushindwa kwa Yesu kufanya muujiza wowote hakuthibitishi kuwa yeye si Mungu, kama Mashahidi wa Yehova wanavyodai kwenye Reasoning from the Scriptures, uk.150 (1989)?

J: Hapana. Kuna mambo mawili ya kuyazingatia katika kujibu swali hili.

Hapa duniani, Yesu, kwa hiari yake, alijifanya kuwa hana utukufu na kutwaa namna ya mtumwa, kama Fil 2:6-7 inavyosema. Yesu alitii, aliteswa, na kupata maumivu ya mwili alipokuwepo hapa duniani.

Kuamua kutokufanya muujiza ni tofauti na kutokuwa na uwezo wa kufanya muujiza. Bila kujali kujifanya hana utukufu kwa Yesu, Mungu Baba angeweza kuamua kuufanya muujiza ufanyike, lakini kwa sababu ya uhaba wa imani yao alichagua kutokufanya hivyo.

 

S: Kwenye Mak 6:5, kwa nini Yesu hakuweza kufanya muujiza wowote ile mkubwa kwenye mji wa nyumbani kwake?

J: Kwa kuwa watu, kwa ujumla wao, walikataa kumwamini mvulana wa mji wao, kufanya muujiza kusingeongeza imani yao. Jambo hili lingeweza pia kuwa ni kitendo cha huruma cha Yesu. Kwenye 2 Pet 2:21-22 Maandiko yanasema ni vema ni bora kwa mtu kutoijua njia ya haki kuliko kuijua kisha kuiacha.

 

S: Kwenye Mak 6:8-9, kwa nini wanafunzi hawakuweza kuchukua mkoba, mkate, wala pesa za kibindoni?

J: Sababu ni kwamba Bwana aliwakataza kufanya hivyo. Tunaweza kukisia kuwa alitaka wamegemee Mungu na watu wengine, badala ya fedha zao wenyewe.

 

S: Kwenye Mak 6:10 na Luk 9:4-5, kwa nini wanafunzi hawakuruhusiwa kwenda kwenye nyumba zaidi ya moja kwenye mji mmoja?

J: Yesu hakusema, lakini tunaweza kuona sababu kadhaa za kiutendaji za kutokwenda kwenye nyumba zaidi ya moja.

1. Kulikuwa na uwezekano mkubwa wa watu kukwazika, au mafarakano miongoni mwa watu yatokanayo na mgawanyo wa kazi ya kuwatunza wageni.

2. Jambo hili pia lingeweza kuwachanganya watu, bila kutaja wanafunzi, kwa kujisumbua na mahali pa kuishi.

 

S: Kwenye Mak 6:11, kama uliishi wakati ule, na ulipata unabii wa kitu ambacho Yuda Iskarioti angefanya, je ungeweza kumkaribisha nyumbani kwako?

J: Ndiyo, kama ungejua kuwa hivyo ndivyo Yesu anavyotaka ufanye. Jambo la muhimu zaidi kujiuliza wakati wa kufanya uamuzi wowote ule ni, "je Yesu angependa ufanye nini?"

 

S: Kwenye Mak 6:17-18, ni kwa nini haikuwa halali kwa Herode Antipas kumuoa mke wa kaka/mdogo yake?

J: Yohana Mbatizaji alilifahamu Agano la Kale vizuri sana. Kitendo cha Herode kumuoa mke wa kaka/ndugu yake wakati kaka/ndugu yake akiwa bado anaishi kilikuwa kinyume na Law 18:16; 20:21.

 

S: Kwenye Mak 6:20, ni kwa jinsi gani Herode Antipas alimwogopa na kumheshimu Yohana Mbatizaji, kwani baadaye alimuua Yohana?

J: Kwa kuzingatia kujitoa kwa Yohana kuyaacha maisha rahisi ili kuishi nyikani, na ujasiri wa Yohana kuhubiri ukweli bila kujali gharama yake, Herode alimheshimu Yohana kwa dhati. Licha ya ukubwa wa heshima ya Herode, kiapo chake cha haraka haraka kwa binti wake wa kufikia na hofu yake ya kufahamika kuwa mtu aliyevunja kiapo chake, vilikuwa na nguvu kuliko heshima na haja yake ya kufanya jambo lililokuwa sahihi, kama Mak 6:22-28 inavyoonyesha.

Ingawa jambo hili linaweza kuonekana la ajabu, haja ya baadhi ya watu ya kutokuvunja ahadi zao, na haja yao ya kuonekana wenye haki ni kubwa kuliko haja yao ya kuwa wenye haki kikweli.

 

S: Kwenye Mat 14:6-10, Mak 6:21, na Mwa 40:20-22, kwa kuwa Herode alimuua Yohana Mbatizaji kwenye siku yake (Herode) ya kuzaliwa, na Farao alimuua mkuu wa waokaji wake siku yake (Farao) ya kuzaliwa, je aya hizi zinamaanisha kuwa tusisherehekee siku za kuzaliwa, kama Mashahidi wa Yehova wanavyosema kwenye Reasoning from Scriptures, uk.68-69 (1989)?

J: Hapana. Herode na Farao ndio waliokuwa waovu, sio siku ya kuzaliwa. Tukio lenyewe halikuwa zuri wala baya. Vilevile kwa kuwa mambo haya yalitokea ndani ya nyumba haimaanishi kuwa hatupaswi kuingia ndani ya nyumba yeyote.

 

S: Kwenye Mak 6:38 na Mak 8:5, ni kwa nini kuwa kila mara kabla ya kuwalisha makutani Yesu aliwauliza wanafunzi wake kiasi cha chakula kilichopo?

J: Kwa kuangalia baada ya tukio, ni kiasi gani cha chakula alichoanza nacho Yesu ambacho hakikuonekana kuwa cha maana. Yesu angeweza kuwalisha watu wote hao kwa kutumia chembe moja ya mkate, kama angependa kufanya hivyo. Badala yake, Yesu alitaka wanafunzi wake waone kuwa chakula kilichopo hakikutosha kuwalisha watu wote, palikuwa na chakula kingi zaidi mwishoni kuliko mwanzoni, na matumizi ya namba muhimu 12 na 7 yanaonyesha kuwa kiasi kinashohusika hakikuwa cha bahati tu.

 

S: Kwenye Mak 7:2-5, kulikuwa na kosa gani kula bila kuosha mikono?

J: Mafarisayo waliipanua dhana ya Agano la Kale ya vitu visafi na najisi hata kugusa maeneo mengi sana. Jambo hilo halikuwa na shida, lakini walipofanya maoni yao kuwa sawa na neno la Mungu ndipo mgongano ulipotokea kati yao na Yesu. Kwenye 1 Kor 4:6 na Mit 30:5-6 Maandiko yanaonyesha kuwa si sahihi kwenda zaidi ya neno la Mungu.

 

S: Kwenye Mak 7:7-8, je unawezaje kujua endapo amri imetoka kwa Mungu au watu?

J: Kama husomi Maandiko wewe mwenyewe inaweza kuwa vigumu kujua.

Mkatoliki mmoja aliyeitwa Paulo, aliyekuwa Mkristo wa kweli, alikuwa kwenye kikundi cha kusoma Biblia nilichokuwa nakiongoza mwaka mmoja. Ilikuwa inashangaza kuona kuwa mara nyingi alielezea vitu ambavyo ni vya msingi sana na kuniuliza kama vimo kwenye Biblia. (Mara vitu hivyo vilikuwa vimo kwenye Biblia). Baadaye, aliniambia sababu ya kuuliza maswalli yote hayo. Alisema kuwa alijifunza mambo hayo alipokuwa mdogo akiwa kwenye shule ya kikatoliki, na hawakutofautisha kati ya mambo ambayo kanisa la Katoliki lilikuwa linafundisha, na mambo ambayo Biblia inafundisha.

Mwalimu Mkristo, toka kwenye kundi lolote, anaposhindwa kutofautisha kati ya neno la Mung na mafundisho yao wao wenyewe yaliyo zaidi ya maneno ya Mungu, wanaongeza umuhimu wa mafundisho yao kwa kuwaletea wanafunzi wao shida ya kuelewa mambo ambayo Mungu amefundisha hasa. Aya za 1 Kor 4:6 na Mit 30:5-6 zinawatahadharisha Wakristo wote kutongeza neno la Mungu. Huenda hii ni moja ya sababu za hukumu ya waalimu kuwa kubwa zaidi, kwa mujibu wa Yak 3:1-2.

 

S: Kwenye Mak 7:7-8, je hatutakiwi kufuata amri zozote za watu?

J:Sivyo hivyo kabisa, kama Rum 13:1 na 1 Pet 2:13-18 zinavyoonyesha, tunatakiwa kutii mamlaka za kibinadamu. Lakini Mak Mark 7:10-14 inaonyesha kuwa Yesu alipinga kabisa kutokutii amri za Mungu kwa lengo la kutii amri za wanadamu.

 

S: Kwenye Mak 7:15, wakati Yesu aliposema kuwa hakuna kitu chenye kumwingia mtu kinachoweza kumfanya najisi, je alikuwa anaongelea mambo yaliyohusu nyakati za Agano la Kale au mafundisho ya Agano Jipya?

J: Tazama maelezo ya Mat 5:10-21 kupata jibu la swali hili.

 

S: Kwenye Mak 7:18, kwa nini Yesu alishangazwa na kutokufahamu kwao?

J: Hawa hawakuwa makutano lakini wanafunzi wenyewe wa Yesu ambao hawakufahamu. Yesu alifikiri kuwa wangeweza kuelewa kwa sasa kuwa kwenye ufalme wa mpya si chakula kilicho nje chenye umuhimu, bali mambo yaliyo ndani ya mtu.

 

S: Kwenye Mat 7:18, kwa kuwa wanafunzi hawakuwa na Roho Mtakatifu hadi siku ya Pentekosti, je walitegemewa kufahamu kitu chochote alichowaambia Yesu?

J: Wakati mwingine watu wanaelewa vibaya mambo ambayo Roho Mtakatifu anayafanya na yale ambayo hatafanyi. Roho Mtakatifu huushuhudia ulimwengu kwa habari ya dhambi, na hutufahamisha kweli, lakini bado watu wanaweza kufahamu sehemu ya kweli bila ya kuwezeshwa na Roho Mtakatifu.

 

S: Kwenye Mak 7:26, kwa nini mwanamke aliitea Msirofoinike?

J: Kiutawala, Foinike ilikuwa sehemu ya jimbo la Rumi la Syria. Marko anaweza kuwa alitumia neno hili kutofautisha na Walibifoinike waliotoka kaskazini mwa Afrika.

 

S: Kwenye Mak 8:10, je Dalmanutha iko wapi?

J: Iko kusini mashariki mwa Bahari ya Galilaya. Kuna pango lililopatikana kusini mwa uwanda wa Genezareti lililoitwa "Talmanutha."

 

S: Kwenye Mak Mk 8:11-12, kwa nini Yesu hakuwatii Mafarisayo au angalau kuwaridhisha kwa kuwapa ishara itokayo mbinguni kama walivyohitaji?

J: Jambo hili lilikuwa mara baada ya Yesu kuwalisha wati 4,000. Je muujiza mwingine ungethibitisha nini kwa Mafarisayo? Hawakutaka kwenda kumuona Yesu, lakini wangeweza kusikia kuhusu muujiza huu. Zingatia kuwa ombi lao halikutokana na imani, bali lililetwa na kutokuamini.

 

S: Kwenye Mak 8:23-25, kwa nini Yesu anaonekana kuhitaji kujaribu mara tatu ili kumponya mtu aliyekuwa kipofu?

J: Maandiko hayasemi kitu chochote kuhusu jambo hili. Huenda mtu huyu alikuwa na shida zaidi ya moja. Bila kujali kitu kilichokuwepo, Mungu hung'ang'ania kadri inavyohitajika katika kutuponya. Angalia pia swali lifuatalo kwa maelezo zaidi.

 

S: Kwenye Mak 8:24, kwa nini mtu aliyeponywa upofu alianza kuwaona watu kama miti?

J: Huenda mishipa ya fahamu inayowezesha kuona haikuwa inapokea mwanga vizuri. Inawezekana kuwa palikuwa na sababu nyingi za upofu wake, kati ya mboni, konea, na mishipa ya fahamu inayowezesha kuona.

Vinginevyo, mtu anaweza kuwa alikuwa anaona vizuri kabisa mwanzoni, lakini ubongo wake haukuwa umezoezwa kutengeneza sampuli. Ubongo wa watu hupokea taswira ya iliyogeuka chini-juu ya vitu wanavyovionaUbongo wetu hugeuza taswira. Kwenye filamu ya Moody Science, kuna mtu aliyepewa jozi maalumu ya miwani iliyokuwa inageuza taswira chini-juu. Baada ya kuivaa kwa muda wa kutosha, ubongo wa mtu huyu ulijirekebisha kikamilifu na hakuwa na shida tena ya kutembea au kuchukuliana – angalau mpaka miwani inapokuwa imeondolewa, wakati ambapo ubongo wa mtu huyu ulipotakiwa kujifunza upya.

Tazama http://www.answersingenesis.org/docs/4146.asp uone mifano ya kisasa inayosisimua ya watu wanaoweza kuona kwa macho lakini bado hawawezi kutambua vitu mwanzoni.

 

S: Kwenye Mak 8:38, kwa nini Yesu hajiiti kwa wazi kabisa kuwa ni Mwana wa Adamu?

J: Yesu hakulazimika kufanya hivi hapa. Alijiita kuwa Mwana wa Adamu kwenye Mak 2:5-12. Yesu alisema kwenye Mak 2:8a-12, "Mbona mnafikiri hivi mioyoni mwenu? Vyepesi ni vipi, kumwambia mwenye kupooza, Umesamehewa dhambi zako, au kusema, Ondoka, ujitwike godoro lako, uende? Lakini mpate kujua kwamba Mwana wa Adamu anayo amri duniani ya kusamehe dhambi, (hapo amwambia Yule mwenye kupooza), Nakuambia, Ondoka, ujitwike godoro lako uende nyumbani kwako. Mara akaondoka, akajitwika godoro lake, akatoka mbele yao wote; hata wakastaajabu wote, wakamtukuza Mungu, wakisema, Namna hii hatujapata kuiona kamwe!"

 

S: Kwenye Mak 8:38, inamaanisha nini kuwa Yesu atawaonea haya watu wanaomwonea haya kwenye ulimwengu huu?

J: Wafafanuzi wa maandiko wana maoni ya aina mbili hapa.

1. Waamini walioteuliwa watakaomuonea haya Yesu wataaibika watakapoenda mbinguni. Kuna Wakristo ambao wameamini kweli, lakini wamechukua vitu vingi sana vya ulimwengu hata wanashindwa kusimama kwa ajili ya Yesu, au kuwashirikisha watu wengine injili.

2. Watu wanaoitwa Wakristo ambao wanamwonea haya Yesu watajikuta kuwa hawaendi mbinguni kabisa. Kwenye 2 Tim 2:12 Maandiko yanasema pia kuwa kama tukimkana Yesu, naye atatukana. Kuna watu wanaokataa kumpkea Yesu kwa sababu mbalimbali za kihisia. Yuda alitokea kuvunjika moyo alipotambua kuwa Yesu hachukui hatua yeyote ya kijeshi kwa wakati ule. Kuna watu wanaodai kuwa binadamu ni wazuri sana hata hawahitaji kuokolewa, au kwamba tunahitaji kafara ni "jambo la kizamani sana." Wengine hawataki mtu yeyote awaangalie toka mbinguni na kuwahukumu kwa mambo wanayowafanya.

Kwa hakika wote hawa wanaweza kuwa sahihi, kwa sababu Yesu hakubainisha "kiwango hicho cha aibu/haya" kwenye aya hii. Ni jambo muhimu kumwamini Yesu, kumkana, na kutubu (kama Petro aivyofanya), lakini jambo lililo muhimu zaidi ni kutokuwa umetoa maisha yako kwake.

 

S: Kwenye Mak 9:24, kwa nini baba alitumia lugha ya picha inayotumia maelezo au picha vyenye kupingana kuelezea kitu fulani?

J: Baba alikuwa na hisia zinazopingana ndani mwake. Alisema, "Naamini" kwa sababu aliamini kweli, lakini pia alisema "Nisaidie kutokuamin kwangu" kwa sababu alijua kuwa alikuwa na mashaka ya kweli pia.

Sisi pia tunapaswa kuwa wakweli kuhusu hisia zetu mbele za Mungu. Mungu ana nguvu nyingi sana kiasi cha kuweza kushugulikia mashaka yetu, na tunapo weka wazi hisia zetu kwa kuzikiri kwake, Mungu hushughulikia mara moja mambo tunayoyakiri kwake.

 

S: Kwenye Mak 9:25, mara nyingi zaidi Yesu amekuwa akiyaambia mapepo kutoka tu, lakini wakati huu kwa nini Yesu anayaambia kutoka na kutokuingia tena?

J: Kwenye Luk 11:24-26, Yesu alisema kuwa pepo chafu linapomtoka mtu huwa linajaribu kumrudia tena likiwa na mapepo mengine saba. Kwa hiyo, ni muhimu kuwa wakati mtu aliyekuwa amepagawa mapepo anawekwa huru, amgeukie Yesu ili kwamba mapepo yasiweze kumrudia kwa nguvu kubwa zaidi.

 

S: Kwenye Mak 9:34, je wanafunzi walitakiwa kumwambia Yesu kwa nini walikuwa wanabishana, au walipaswa kukaa kimya kama walivyofanya?

J: Huenda walikaa kimya kwa sababu ya kutahayarika au aibu. Mungu anajua mambo tunayowaza na kusema, iwe tunayakiri au la, lakini ni vema kumwambia kitu kilichomo moyoni mwetu, hata kama ni upuuzi na majivuno. Kwa njia hiyo Mungu atatutakasa na vitu vyote hivyo mara moja kama utakuwaradhi kukiri.

 

S: Kwenye Mak 9:38-40, kwa nini Yohana na wanafunzi wengine walimzia mtu aliyekuwa anatoa mapepo?

J: Kwa kuwa mtu huyu hakuwa pamoja nao, wanafunzi wa Yesu walidhani kuwa Mungu hawezo kumtumia. Leo hi waamini hufanya kosa hili hili, wakifikiri kuwa waamini wengine wa kweli ambao hawashiriki kwenye kanisa lao, hawawezi kutumiwa na Mungu au wanatumiwa kwa njia ndogo tu.

 

S: Kwenye Mak 9:38-40 na vifungu vingine vya Maandiko, je shetani na athari zake vina "uhalisi wa kiasi?" Je huwa anaweka mawazo yake kwenye vichwa vyetu?

J: Shetani na mapepo yake ni viumbe halisi vyenye akili na hisia. Hawa wanaweza kutoa wazo, lakini hawawezi "kuwapagaa" waamini. Ingawa wanaweza kutoa mawazo, tunazo nguvu za kuyakataa na kuendelea mbele. Ingawa wana nguvu, na nguvu zao hazitakiwi kupuuziwa, ulinzi wetu chini ya damu ya Kristo bado una nguvu zaid. Kwa mfano, nimewahi kusikia kuhusu mganga wa kienyeji (mchawi) aliyemlaani Mkristo, na laana ilimrudia mganga huyo. Katika mfano mwingine ambao hauhusiani na huu, nimewahi kusikia kuhusu mganga mwingine wa kienyeji (mchawi) aliyesema kuwa mmishenari wa kikristo atakufa baada ya siku 30. Kwenye siku ya 30, mganga huyo alikufa.
Kama watoto wa Kristo, hatuna sababu yeyote ya kujadiliana na shetani, kumdhihaki shetani, au hata kujaribu kuwasiliana naye au mapepo yake kwa namna yeyote ile.

 

S: Kwenye Mak 9:48, ni kwa nini funza hawatakufa jehanamu?

J: Sitiari ya Yesu haiongelei wanyama wadogo, lakini kuoza na kuharibika bali kuoza na kuharibika jehanamu. Mtazamo mwingine ni kwamba kwa kuwa aya inasema "funza wao" na sio "funza", ni sitiari ya mwili wa mtu anayekwenda jehanamu.

 

S: Kwenye Mak 9:49, je maneno "atatiwa chumvi kwa moto" yanamaanisha nini?

J: Kuna taafsiri kuu tatu za kitu ambacho ayah ii inakongelea:

Waamini, ambao wanapitia mateso na utakaso

Wapotevu, wanaoenda jehanamu

Kila mtu anayejaribiwa na kuhukumiwa. Tafsiri hii inaweza kuunganisha tafsiri nyingine mbili.

Kwa kuhitimisha, mistari ya 43-48 inaongea kuhusu jehanamu, na wa 50 unaongea kuhusu waamini. Mstari wa 49 ni wa mpito, na maneno "kila mtu" yanaongelea wapotevu walioelezwa kabla ya maneno haya, na waamini walioelezwa baada ya hapo.

 

S: Kwenye Mak 9:49-50, maneno "atatiwa chumvi kwa moto" yanahisiana vipi na "chumvi ikiwa si chumvi tena?"

J: Wakati ule Mafarisayo walifundisha kuwa Israeli ilikuwa ni chumvi miongoni mwa mataifa ili iyasafishe. Chumvi ilikuwa ni kiungo muhimu cha kuhifadhia vitu visioze au kuharibika. Msemo "atatiwa chumvi kwa moto" unamaanisha kuhifadhi chakula kwa moto, kama vile kukausha matunda. Ikiwa hata moto unaweza kuhifadhi, chumvi inaweza kupoteza nguvu yake ya kuhifadhi kama itachujwa kwa maji, endapo chumvi itafifilishwa na vitu vingine.

 

S: Kwenye Mak 10:13, kwa nini wanafunzi walikuwa wanawazuia watu kuleta watoto wao kwa Yesu?

J: Wanafunzi walikosea kwa kufanya hivyo. Huenda walikuwa wanafikiri kwa makosa kuwa kwa kwa watoto hawawezi kuyaelewa mafundisho ya Yesu kwa akili zao kama watu wazima, wasipoteze muda wa Yesu.

 

S: Kwenye Mak 10:13-15, kwa nini Yesu alitaka watoto wadogo waje kwake?

J: Sababu pekee ambayo Yesu aliitoa ni kuwa "Ufalme wa Mungu ni wao." Yesu alikuwa anawatumia watoto kama zana ya kufundishia, kuwa sote tunatakiwa kuwa na unyenyekevu na utayari wa kufundishwa walivyonao watoto ili tuweze kufika kwa Mungu. Hatuwezi kufika kwa Mungu na kiburi, bali tunatakiwa kukiri kuwa hatujitishelezi sisi wenyewe. Tunatakiwa kuwa tayari kukiri kuwa Mungu ana ufahamu mkubwa zaidi kuliko wetu, na kwamba tunamhitaji na tukotayari kukua.

Pamoja na hayo, Yesu aliwapenda watoto bila shaka, na aliona kuwa thamani ya nafsi ya mtoto ni sawa na ya mtu mzima.

 

S: Kwenye Mak 10:18 na Luk 18:19, je Yesu hakuwa "mwema" kwani alimtilia shaka mtu aliyemwita mwema?

J: Yesu ni mwema kwa maana zote za neno ‘mwema.' Yesu anamtilia shaka mtu anayemwita mwema wakati hajakubali kuwa Yeye (Yesu) ni Masishi/Kristo, na anaonekana kutumia neno "mwema" kirahisi rahisi tu.

Sawa na Yoh 8:7, wakati Yesu alipowaambia watu waliokuwa wanamshitaki mwanamke aliyekutwa akizini "Yeye asiye na dhambi miongoni mwenu na awe wa kwanza kumtupia jiwe", Yesu mwenyewe hakutupa jiwe lakini jambo hili halithibitishi kuwa Yesu alikuwa na shambi. Yesu hakuwa na dhambi kwa mujibu wa Ebr 4:15.

 

S: Kwenye Mak 10:18 na Luk 18:19, Yesu aliuliza "Kwa nini kuniita mwema? Hakuna aliye mwema ila mmoja, ndiye Mungu." Kwa kuwa Yesu hakuukana uzuri au uungu wake, alikuwa anasema nini?

J: Yesu anauliza swali fupi ambalo, kwa nje, linaonekana kuwa jepesi sana: kwa nini unamwita mwema? Hebu tuangalie mambo matatu mepesi kisha maelezo zaidi.

a) Yesu hakuthibitisha au kukana kuwa alikuwa mwema hapa. (Ingawa sehemu nyingine za Maandiko zinasema kuwa alikuwa mwema.)

b) Yesu aliuliza swali tu. Hakuthibitisha au kukana kuwa ni Mungu hapa. (Ingawa sehemu nyingine za Maandiko Yeye ni Mungu.)

c) Yesu anaonekana kupendezwa sana na kitu ambacho mtu huyu alikubaliana nacho na kitu alichoamini.

Kwa maelezo haya, ndipo tutaona kitu gani unakubaliana nacho na uko tayari kuamini.

Hakuna mtu mwingine yeyote kwenye Injili, iwe mtu aliyeamini au asiyeamini, anayelezewa akimwita Yesu "Mwalimu mwema." Je mtu huyu aliyekuwa anauliza swali alikuwa na hisani na mwenye kusifia mno, au Yesu aliuliza, je alikuwa anathibitisha jambo linguine zaidi ya hilo?

Je "mtu mwema" ni nani, machoni pa Mungu mtakatifu? Je ni mtoza ushuru mwenye dhambi, aliyekuwa amewadanganya watu wengi sana maisha yake yote, lakini anamlilia Mungu amrehemu? Hapana, yeye anatubu dhambi zake, lakini bado alikuwa ni mwovu. Kwa upande mwingine, je sisi tu wema kwa namna yeyote ile kuliko mtoza ushuru yule? Hapana. Kwa viwango vya Mungu, kumwita mtu yeyote hapa duniani "mwema" ni kujidanganya.

Kwa ajili hiyo basi, je wema ni nini? Je ni kitu chema watu wanapochagua kitu kwa kupiga kura, wakati jamii inakukubali, au wakati mtu anafikiri mawazini mwake mwenyewe kuwa kitu fulani ni kizuri, hata kama watu wengine wana mawazo tofauti kuhusu kitu hicho hicho? Hapana, hatuna viwango vya Mungu, isipokuwa Mungu na kitu ambacho amesema kuwa ni chema. Hakuna mtu aliye mwema kabisa, isipokuwa Mungu.

Kwa kuzingatia mambo yote haya, je unakubali kuwa Yesu alikuwa mwema?

 

S: Kwenye Mak 10:18 na Luk 18:19, je Yesu alikuwa Mungu, kwani hakuna mtu aliye mwema isipokuwa Mungu?

J: Yesu hakumwambia mtu Yule kuwa endapo alikuwa Mungu au hakuwa Mungu. Badala yake, alisema kuwa mtu huyu alikuwa anatumia neno "mwema" kirahisi rahisi. Mungu ndiye chanzo cha wema, na vitu vingine vyote vilivyo vidog kwake tunavyoviita vyema ni kivuli tu cha wema wa Mungu.

Unajua Wakristo, Wayahudi, Waislamu, na hata waabudu sanamu wa Kirumi waliokuwa wanawaua Wakristo walikuwa wema wote, angalau kwa jinsi walivyouelewa wema. Linaweza kuwa jambo la kushtusha kwenye masikio ya watu watu wengi wa magharibi, lakini dini zote hazina mawazo yanayofanana kuhusu jambo hili, kuwa unatakiwa kufanya jitihada kufanya mema. Kwa Wahindu, watu wengi hujaribu kutafuta kutalamika, ufahamu wa kweli, kwa kupata uzoefu katika mambo yote mema na mabaya. Hii ndio sababu mshika dini wa Kihindu akifanya ubadhirifu au kuiba, watu wanaweza kushtushwa na unafiki anaoshutumiwa nao, lakini unaweza usiwe unafiki kabisa. Kwake yeye, inaweza kuwa kwamba hakuna mgongano katika kujaribu kkufikia kutalamika, utambuzi wa ulimwengu unaotuzunguka, au kitu chochote kingine, na kwa kutaka kupata uzoefu wa uovu. Hata hivyo, siyo Wahindu wote watakao kubali; kuna watakao sistizia "karma" (hali ya uwepo wa mtu katika siku zijazo inayotokana na matendo ya mtu katika maisha yake ya sasa na yaliyopita) zaidi.

 

S: Kwenye Mak 10:18 na Luk 18:19, je watu wa zamani walizitumiaje aya hizi?

J: Hizi ni aya ambazo zina jozi zenye vitu vingi vinavyoweza kutumiwa kwa namna nyingi nzuri.

Mfano kwetu

Clement wa Alexandria (mwaka 193-217/220 BK) kwenye Who is the Rich Man That Shall Be Saved? sura ya 4, uk.592 anatumia kifungu hiki kunyesha kuwa tunapaswa kuwa wema na kuwasaidia maskini kuliko kutegemea mali.

Tertullian (mwaka 198-220 BK) alisema kuwa Mungu ni mwema, na ana huruma, na inafaa kwetu kuwa wema kwa watu wengine, na kuwa wapatanishi (On Modesty sura ya 2, uk.75).

Dhidi ya Unostisia

Irenaeus (mwaka 182-188 BK) anasema kwa kuwa Yesu alimwita Mungu Baba "mwema", basi atakuwa ni mwema kwelikweli. (Irenaeus Against Heresies kitabu cha 1 sura ya 20, uk.345).

Hippolytus, mwanafunzi wa Irenaeus (225-235/6 BK) pia kwenye Refutation of All Heresies kitabu cha 5 sura ya 2, uk.50 na kitabu cha 7 sura ya 20, uk.113 inatumia aya hii kuthibitisha kuwa Marcion na Unostisia si sahihi. Kama Mungu Baba aliyeumba vitu ni mwema, basi mafundisho ya kizushi ya Marcion na Unostisia vinaanguka.

Waebioni wanakubali kuwa Yesu Mwana wa Baba, lakini wanasema kuwa Yesu alikuwa Mungu kwa maneno tu. Kwa sababu wao pia wanasistiza kuyafuata mambo yaliyoagizwa kwenye Agano la Kale, unaweza kuona kuwa walipingana vikali sana na Wanostitia waliodai kuwa Agano la Kale ni ovu na limepotoshwa. Kwenye Clementine Homily 3 (tarehe ambayo haina uhakika) sura ya 57, uk.248-249 nao pia walitumia aya hii dhidi ya watu waliosema kuwa Mungu wa Agano la Kale ni mwovu. Badala yake, kwenye maandiko ya Kiklementina na maandiko yote ya Kiebioni tuliyonayo hayajawahi kutumia ayah ii kukanusha kuwa alikwa Mungu.

Dhidi ya waabudu sanamu

Origen (mwaka 225-254 BK) anasema kuwa kama Yesu alimridhia Mungu Baba, ni kwa kiasi gani jua litashindwa kumfanya ntu yeyote anyenyekee na kuliabudu. Kisha Origen anaogeza kuwa tunapaswa kumwomba Neno la Mungu, na zaidi sana kwa Baba yake (Against Celsus kitabu cha 5 sura ya 15, uk.548).

Uungu wa Kristo

Novatian (mwaka 250/254-256/7 BK) "Zaidi ya hayo, Bwana mwenyewe: ‘Kwa nini unaniuliza kuhusu kitu kilicho chema? Mungu pekee ni mwema.' ... "lakini kwenye Maandiko hayohayo Kristo pia ametajwa kuwa mwema. Kwa hiyo basi hakuna, endapo wanasema kwa usahihi, kuwa kuna mmoja aliye mwema, hata wema wawili. Ni kwa namna gani basi, kwa mujbu wa imani itokanayo na Maandiko, inasemekana kuwa kuna mmoja tu aliye mwema? Lakini kama hawadhani kuwa fikra hizi zinaweza kuingiliana kwa namna yeyote ile na ukweli kuwa kuna Bwana mmoja, kwamba Yesu Kristo ni Bwana, wala na ukweli kuwa Bwana wetu ni mmoja. Kwamba Paulo pia ni bwana wetu, au kuingiliana na ukweli kuwa kuna mmoja aliye mwema, kwamba Kristo pia huitwa mwema; kwa mantiki hiyohiyo, hebu na tufahamu kuwa tokana na ukweli kuwa Mungu ni mmoja, hakuna kikwazo kinachojitokeza kwenye ukweli kuwa Kristo pia amenenwa kwa uthabiti kuwa ni Mungu" (Concerning the Trinity sura ya 30, uk.642-643).

Dhidi ya Uariani

Hilary wa Poitiers (mwaka 367 BK) aliandika kuwa wakati Waariani walionyesha Isa 65:16; Mak 10:18; 1 Tim 6:15, jambo hilo lingemnyima Mwana ukweli, wema au nguvu.

Gregory wa Nyssa (mwaka 382-383 BK) aliandika, "Hata hivyo, ni rahisi kuonyesha kuwa hata neno ‘mmoja'haliwatenganishi Baba na Mwana . . . Kwani anasema, ‘Mimi na Baba tu umoja' (Yoh 10:30). Hivyo basi, kama wema ni mmoja, na aina maalumu ya umoja imeazimiwa kwa Baba na Mwana, inamaanisha kuwa Neno, anapoelezea uzuri wa ‘mmoja', amesema kwenye mtajo ‘mmoja' cheo cha ‘wema' pia kwake Yeye mwenyewe, aliye mmoja na Baba, na hajatengwa na umoja wa asili" (Against Eunomius kitabu cha 11 sura ya 2, uk.232-233 kwenye Nicene and Post-Nicene Fathers Second Series juzuu ya 5.

 

S: Kwenye Mak 10:19, kwa Yesu anataja amri sita tu kati ya kumi?

J: Yesu hakuwa na lengo la kutaja amri zote hapa, bali kutoa mifano. Kutokuwepo kwa maelezo marefu hapa si kisingizio cha kukana mambo ambayo Yesu na wamafunzi wake wameyafundisha kwenye sehemu nyingine.

 

S: Kwenye Mak 10:21-22 na Luk 18:20-23, kwa nini Yesu alimwagiza mtu aliyekuwa tajiri kuuza mali zake zote?

J: Inaonekana kuwa mtu huyu alizipenda mali zake sawa na jinsi alivyompenda Mungu, na Yesu alimwambia kuwa anahitaji kabadilika.

 

S: Je Mak 10:21-22, inawafundisha watu kuuza vitu vyote walivyo navyo pia?

J: Hapana, kwa sababu Yesu hakumwambia mtu mwingine yeyote tunayemjua kuuza mali zake. Hata Paulo alikuwa na mali, kama joho kwenye 2 Tim 4:13. Kwenye Mdo 5:4, wakati Anania alipoadhibiwa, Maandiko yanasema bayana kuwa hakuadhibiwa kwa sababu ya kuchukua sehemu ya fedha zake mwenyewe, bali kwa kumdanganya Mungu na kudai kuwa hakuchukua sehemu yeyote ya fedha.

Hata hivyo, aya hii bado ni changamoto kwetu leo hii. Uchaguzi unapkuja kati ya Yesu na mali, mtu huyu ambaye alionekana kuwa mwema hakuwa tayari kumchagua Yesu badala ya mali. Kama na endapo mtu anafanya hivyo leo hii basi mtu huyo anakuwa amelaaniwa na mali zake nyingi sana alizonazo. Soma Mit 30:7-9 kwa maelezo zaidi.

Wakati unachagua kiasi gani utoe kwa ajili ya kazi ya Mungu, ifuatayo ni orodha ya vitu unavyoweza kuvifikiria.

1. Maelfu ya watu wanakufa kila siku kwa njaa

2. Watu wengi sana hawajawahi kusikia habari njema

3. Hela zetu zinaweza kutumika kuwasaidia kutimiza mahitaji haya

4. Kristo anatufundisha kuwa tuwe maskini ili watu wengine waweze kuwa matajiri (2 Kor 8:9)

5. Kwa kuwa maisha yetu hapa duniani ni mafupi sana, wakati Yesu atakapokuja muda utakuwa umekwisha

 

S: Kwenye Mak 10:21, je aya hii inapaswa kuwa na maneno "jitishwe msalaba" au la?

J: Maneno "Jitwishe msalaba" yapo kwenye The Greek New Testament According to the Majority Text, lakini kuondolewa kwake kumeelezwa kuwa ni tofauti ya maandishi. Wataalamu wengi wa Biblia hawayakubali maneno haya, na Aland na wenzake (toleo la 3) haliyaonyeshi kuwa ni tofauti ya maandishi.

Kwa vyovyote itakavyokuwa, hakuna shaka kuwa maneno haya yatakuwemo kwenye Mathayo.

Tertullian (mwaka 197-217 BK) "Kama unataka kuwa mwanafunzi wa Bwana, ni vema ‘uchukue msalaba wako, na kumfuata Bwana." Msalaba wako, yaani, matatizo na mateso yako mwenyewe, au mwili wako tu, ambao unafanana na msalaba" (Tertullian On Idolatry sura ya 12, uk.68).

Tertullian (mwaka 197-217 BK) "Unapaswa kuuchukua msalaba wako na kuubeba ukimfuata Bwana wako, kama Yeye mwenyewe alivyokuagiza" (A Treatise on the Soul sura ya 55, uk.231).

S: Kwenye Mak 10:23-24, je haiwezekani kwa watu wenye mafanikio kumfuata Yesu?

J: Kuna jibu moja tu, lakini lina sehemu mbili.

Hapana: Watu walio na mali wanaweza kuja kwa Mungu. Ibrahimu alikuwa tajiri sana, kwa vigezo vyote vya nyakati zile za zamani na za siku hizi. Hata hivyo, watu wenye mali wanapaswa kuwa tayari kwa ajili ya Mungu kitu chochote kilicho cha thamani zaidi kwao – kama Ibrahimu alivyofanya kwa mtoto wake Isaka.

Ndiyo: Kama mali zako zinakumilki wewe, na unapenda mali kuliko unavyompenda Mungu, unapaswa kuchagua kitu kimoja au kingine, na mahali pako pa kuishi milele panategemea uamuzi wako.

 

S: Kwenye Mak 10:29, je kila mtu aliyeacha vitu vyote na kumfuata Yesu amehakikishiwa baraka hizi, au hawatakuwa na manufaa yeyote ikiwa wakifanya mambo haya lakini wakawa hawan upendo, kama 1 Kor 13:2 inavyosema?

J: Yesu anatupa ahadi apa, lakini kuna masharti yaliyodokezwa. Unapaswa kumfuata, na kuendelea kumfuata Yesu. Unapaswa kumpenda Mungu na watu wengine ili uweze kumfuata Yesu, na huwezi kumpenda Mungu endapo hutakuwa unawapenda watu wengine.

 

S: Je Mak 10:29-30 na Luk 18:29-31 zinaweza kuchukuliwa kuwa ahadi ya mafanikio ya kifedha kwenye maisha haya ya sasa?

J: Hapana. Ahadi hii ilitolewa kwa Wakristo wa awali kwa jinsi ileile ilivyo kwetu sisi. Hatuwezi kupata uhakika zaidi wa mafanikio ya kifedha kuliko Paulo, mitume wengine, na Wakristo wa kale, ambao kimsingi walikuwa watumwa na watu maskini. Aya hii haiongei kuhusu utajiri, lakini kuhusu familia na nyumba.

 

S: Kwenye Mak 10:30, je tunavipataje vitu hivi vyote kwenye maisha haya?

J: Kila mmoja wetu hana nyumba 100 na mashamba 100 kama mali zake. Pia hatuna kaka na dada 100 wa kuzaliwa nao na mama wazazi na ndugu 100. Badala yake, kama kaka na dada katika mwili mmoja - kanisa – tuna vitu vyote hivi kwa pamoja ili tuweze kushirikishana mmoja na mwingine, kama Mak 3:33-35 inavyoonyesha.

 

S: Kwenye Mak 10:34, je Yesu alikuwa afufuke siku ya tatu au baada ya siku tatu?

J: Hati za kale zenye maandiko ya Marko zinatofautina.

Baada ya siku tatu: Sinaiticus, Vaticanus, Ephraemi Rescriptus, Bezae Cantabrigiensis, Sahidic Coptic, Bohairic Coptic.

Siku ya tatu: Alexandrinus, Byzantine Lectionary, Gothic, Armenian, Ethiopic, Georgian, Origen.

 

S: Kwenye Mak 10:35-37, je Yakobo na Yohana walikwenda kwa Yesu kumuomba kuketi upande wake wa kulia na kushoto, au mama yao ndie aliyefanya hivyo kwenye Mat Mt 20:20?

J: Jibu lipo kwenye Mat 20:20 yenyewe, ambapo Maandiko yanasema mama yao alikwenda "pamoja na wanawe." Walikuwa pamoja Yesu alipokuwa anaulizwa.

 

S: Kwenye Mak 10:38, je Yesu alikuwa anaongelea kikapu na ubatizo gani?

J: Kikapu na ubatizo havikuwa meza ya Bwana na ubatizo wa maji (Yesu alikuwa amekwishabatizwa na Yohana). Badala yake, Yesu alikuwa anaongelea vitu ambavyo viliwakilishwa navyo. Damu ya Yesu, iliyowakilishwa na kikombe, ilikuwa inakaribia kumwagwa msalabani, na Yesu alikuwa anakaribia kuzikwa na kufufuka, mambo ambayo yliwakilishwa na ubatizo.

 

S: Kwenye Mak 10:38-40, kwa kuwa Yesu alikuwa amewaambia kwanza gharama ya kupata jibu la ombi lao, na kisha [inadaiwa] aliwakatalia ombi lao, kwa nini basi bado walitakiwa kulioa gharama?

J: Yesu hakuwakatalia ombi lao, lakini alisema kuwa kutoa au kukatalia hitaji lao hakukuwa ndani ya mamlaka yake. Kisha Yesu aliwaambia kitu cha kufanya, lakini aliacha kazi ya kutoa ombi hili kwa Baba.

Aya hii ni nzuri sana kwa kuthibitishia Utatu Mtakatifu. Wakati Baba na Mwana ni umoja, aya hii inathibitisha kuwa kuna tofauti kati yao, tofauti na umodali (mani kuwa nafsi tatu za Utatu Mtakatifu zinawakilisha namna tatu za ufunuo wa Mungu, na si nafsi tatu tofauti tatu zinazoishi pamoja kwenye asili ya Mungu). Siku za leo madhehebu ya Upentekosti wa nafsi moja (imani kuwa kuna nafsi moja ya Mungu ambayo imejidhirisha kwa njia mbalimbali ikiwa pamoja na Mungu Baba, Mwana na Roho Mtakatifu) na kanisa linguine linalojiita "local church" yanafundisha umodali.

 

S: Kwenye Mak 10:45, je kifo cha Yesu msalabani kilikuwa fidia ya ukombozi wa kila mtu, au baadhi ya watu si wengine?

J: Yafuatayo ni maelezo ambayo Biblia inayatoa kuhusu ujumla na ukomo wa ukombozi.

Ujumla wa ukombozi:

Watu wote wameagizwa kuitii injili (Mdo 17:30; 2 Thess 1:8)

Kila mtu amwaminiye (Yoh 3:16)

Imefunuliwa kwa wote (Tito 2:11)

Mungu anataka watu wote waokolewe (1 Tim 2:4)

Fidia ya ukombozi kwa watu wote (1 Tim 2:6)

Umetolewa [kwa ukweli kabisa] kwa wote (Mdo 2:38-40; Ebr 4:2)

Kipatanisho kwa dhambi za ulimwengu wote (1 Yoh 2:2)

Yesu atawavuta wote kwake (Yoh 12:32)

Ukomo wa ukombozi:

Hakuna mtu awezaye kuja kwa Yesu isipokuwa amejaliwa na Mungu Baba (Yoh 6:65)

Mungu anaweza kutoa rehema kwa baadhi ya watu, kama vile Yakobo, ambayo haitoi kwa wengine, kama vile Esau, ingawa bado ni mwenye haki kwa watu wote (Rum 9:14-18)

Injili haina maana kwa watu wasioipokea kwa imani (Ebr 4:2)

Mafarisayo waliyakataa makusudi ya Mungu kwao (Luk 7:30)

Wako waliomkataa Bwana aliyewanunua (2 Pet 2:1). Neno la Bwana ni mamlaka na ni hilohilo kwenye Yuda 4, ambapo linamwongelea Yesu.

Mungu aliwafahamu kabla sio tu watu watakaomkubali, lakini pia alimjua kabla kila mtu atakaye mkubali. Mungu aliwachagua (aliamua) kabla watu watakaomkubali.

Kama unafikiria jambo hili, Wakristo wote, wanaofuata mafundisho ya Calvin na wale wasioyafuata, wanakubaliana kuwa kuna ujumla na ukomo wa ukombozi ¾ lakin jambo hili halifuti tofauti za msingi baina ya Wakalvinisti, Arminianist na watu wengine wasiokuwa Wakalvinsti.

Tofauti ya msingi kati ya mafundisho ya Calvin na yale yasiyo ya Calvin (ikiwa ni pamoja na Wesleyan Arminianism, nay ale yajulikanayo kama ‘4-point Calvinism', na mengine yote yaliyo kati ya hayo) ni kwamba je Mungu Mwenye enzi yote, mwenye upendo, na wa haki, aliwachagua watu watakaokwenda jehanamu kuwa watakuwa ama:

Wasio Wakalvinisti: Malengo yaliyoshindwa, ambapo Mngu alimpa kila mtu kitu kinachotakiwa ili kwenda mbinguni, lakini wokovu aliouleta Yesu ulishindwa kuwaokoa baadhi ya watu. Walipotea kwa sababu makosa yao ya hiari ya mioyo yao.

Wakalvinisti: Hukumu iliyokusudiwa ya moto wa milele jehanamu, kwa sababu wokovu wa Yesu ulileta matokeo yaliyokusudiwa kwa 100% kwa watu waliokusudiwa, na Mungu alichagua kwa hiari kutokutoa njia yeyote ya wokovu kwa watu wengine. Hapakuwahi kuwa na kitu chochote wapotofu wanachoweza kufanya, au watapenda kufanya kubadilisha nia ya Mungu ya kutowapa nafasi ya kuepuka mapenzi ya siri ya Mungu.

Wasio Wakalvinisti: Kama wokovu unawezekana kwa watu wote na unaleta matokeo yaliyokusudiwa kwa baadhi yao, basi hautaleta matokeo yaliyokusudiwa kwa sababu baadhi ya watu wangeweza kuukataa au vinginevyo ulitakiwa pia uende pamoja na imani. Watu wasiofuata mafundisho ya Calvin wanasema kuwa hivi ndivyo Luk 7:30 na Ebr 4:2 zinzvyosema. Wakalvinisti wanaweza kuitikia kuwa jambo hili lingeufanya wokovu utegemee binadamu kwa sehemu, kuifanya imani iwe aina ya matendo yanayotakiwa kuleta wokovu. Watu wasiofuata mafunzo ya Calvin wanaweza kuitikia kuwa Ukalvisti unachanganya zawadi ya wokovu inayotolewa na Mungu, na kupokea zawadi ya wokovu kitu ambacho ni wajibu wa mwanadamu. Imani si kazi, kama Efe 2:8-9 inavyoonyesha, na baadhi ya Wakalvinisti hawapaswi kuwaiga Wakatoliki katika kufananisha matendo ambayo yanastahili malipo ya namna fulani na "sifa isiyotegemea matendo" ya imani na kutambua kutokuweza kwetu.

Wakalvinisti: Kama wokovu ni kitu chenye kuwezekana baadhi ya watu, ni kitu kinacholeta matokeo yaliyokusudiwa kwa watu wote ambao kinawezekana, basi hapukuwahi kuwepo nafasi yeyote kwa baadhi ya watu. Mtazamo usiofurahisha wa "malengo yaliyoshindwa" unashughulikiwa, lakini kwa hasara ya upendo uliopotea na haki isiyoweza kuelezewa. Kwenye 2 Thess 1:8, Mungu angewafanya watu wawajibike kwa kutokuitii injili ambayo Mungu hakuwapu kuitii. Mtu aliye jehanamu anaweza kusema, "Nimekuja hapa kwa sababu niliamini kuwa Mungu hakunipenda kiasi cha kutosha, Yesu hakufa kwa ajili ya dhambi zangu, Mungu alikusudia kuwa niendelee kuwa mwenye dhambi, na nipo hapa kwa sababu nimeamini kweli. Mtu aliyepotea anaweza pia kutafuta wokovu kupitia madhehebu ya kisasa zaidi yenye imani au matendo yanayochukuliwa na waamini wengine kuwa mageni au potofu, kwa sababu nafasi ya kuupata wokovu na upendo wa Mungu kupitia kwenye madhehebu ya jinsi hiyo ni kubwa kwao kuliko kuupata kupitia ukristo.

 

S: Kwenye Mak 10:51, kwa nini Yesu alimuuliza mtu aliyekuwa kipofu kuwa litaka amfanyie kitu gani?

J: Yesu anataka kumuuliza, hata kama anajua kitu anachokitaka. Wakati mwingine kitu ambacho tunakitaka na kitu ambacho ni bora zaidi huwa havifanani. Mtu aliyekuwa kipofu alitakiwa kuomba apate kuona, na Yesu alimpa hitaji lake hilo baada ya kuomba. Wakati mwingine, Mungu anangojea kutupa mahitaji yetu leo hadi tunapomwomba bayana.

 

S: Kwenye Mak 10:52, inakuwaje kuwa ni imani ya mtu aliyekuwa kipofu, wala si ya Yesu, iliyomfanya apone?

J: Inafurahisha kuona kuwa Yesu alisema bayana kabisa kuwa ni imani ya mtu huyu aliyekuwa kipofu ndiyo iliyomponya. Ingawa Mungu hajafungwa kufanya kazi kupitia imani yetu, Mungu huchagua kufanya kazi kupitia imani yetu, kama Efe 2:8 na Rum 4:3, 16 zinavyoonyesha.

 

S: Kwenye 10:52, kwa nini Yesu alisema mtu aliyekuwa kipofu "imani yako imekuponya" badala ya kusema tu kuwa unaweza kuona?

J: Si tu kwamba macho yake na sehemu nyingine za mwili wake zilikuwa zinafanya kazi kama kawaida, lakini pia mtu huyu aliyekuwa kipofu aliponywa kiroho ndani ya Yesu.

 

S: Kwenye Mak 11:8-10, kwa nini watu walitandaza nguo zao na matawi ya mtende mbele ya punda?

J: Desturi hii ilikuwa ni ishara ya heshima na mshangao mkubwa. Jambo hili linaweza kuwa sawa na mfumo wa maaskari wa Ulaya ya Zamani za Kati uliohisisha mtu kuweka koti juu ya tope lilichanganyika na mchanga ili kwamba mwanamke wa familia ya kifalme aweze kukanyaga koti na kujiepusha na tope.

 

S: Kwenye Mak 11:13, kwa kuwa hukuwa muda wa mitini, je Yesu kwenye Injili hakufahamu msimu kama Ahmad Deedat anavyodai?

J: Hapana, Deedat hayuko sahihi kabisa hapa. Mtini uliiwakilisha Israeli, na huu ulikuwa ni unabii kuwa taifa ambalo limewakilishwa na mtini halitazaa matunda na litanyauka kiroho.

 

S: Kwenye Mak 11:13, 23, 30 kwa kuwa mtu aliye na imani anaweza kuihamisha milima, kwa nini Yesu hakuufanya mtini utoe matunda?

J: Yesu angeweza kufanya hivyo, lakini alichagua kutokufanya hivyo. Yesu hakuwa na haja na mitini na miti yake; Yesu alikuwa anawafundisha wanafunzi hapa. Mti mtini uliliwakilisha taifa la Israeli, na Yesu aliulaani mti mtini ili kuonyesha mambo yatakayotokea kwao ikiwa, kama mti mtini, hawatazaa matunda ya imani wakati Yesu atakapokuja kwao.

 

S: Kwenye Mak 11:15-18 na Luk 19:45-46, kwa nini viongozi wa Kiyahudi hawakumkamata Yesu, mgeni aliyekuwa na mjeledi, mara moja?

J: Mambo manne ya kuzingatia katika kujibu swali hili.

1. Makutano walikuwa wamemsifu Yesu muda si mrefu sana kuwa ni Masihi wakati akiingia Yerusalemu kwa shangwe kwenye Mat 21:1-11, 15-16; Mak 11:1-10 na Luk 12:12-15.

2. Yesu alikuwa akiwaponya watu kimiujiza, na ni vigumu kumkamata kwenye umati wa watu waliokkuwa wamepnywa naye.

3. Kabla ya hapo, makutano walikuwa wamesikia kuwa Yesu amemfufua Lazaro kwa mujibu wa Yoh 12:9-11, 17-19.

4. Jambo la muhimu zaidi ni kuwa, tokana na sababu zilizotangulia, Mak 11:18 inasema kuwa ingawa makuhani na waalimu walikuwa wakitafuta njia ya kumuua Yesu, walimwogopa kwa sababu umati wote ulikuwa umestajabishwa naye. Makuhani hawakupinda maasi, na malipizo ya Warumi ambayo yangesababishwa nao. Luk 19:47-48 inasema jinsi hiihii, na kwenye Lk 12:19, Mafarisayo walilalamika kuwa waliona kama ulimwengu wote ulikuwa unamfuata Yesu.

 

S: Kwenye Mak 11:16, kwa nini hakumruhusu mtu yeyote achukue chombo kati ya hekalu?

J: Yesu hakuwa anapinga utoaji kafara unaofaa, lakini alikuwa anawapinga watu waliokuwa wamebeba vyombo vilivyojaa hela.

 

S: Kwenye Mak 11:17, ni kwa jinsi gani watu walifanya mambo kama wezi hekaluni?

J: Ni kwa njia zisizopungua tatu:

Kutozo bei kubwa: Kuuza vitu hekaluni kwa bei kubwa sana.

Kurasimisha: Makuhani hawakukubali mnyama aliyekuwa na dosari, kama kidonda kilichosababishwa na kusafiri umbali mrefu, hovyo watu walilazimika kununua wanyama waliouzwa hekaluni kwa bei ya juu.

Kumwibia Mungu katika matoleo: Wauzaji na watu waliokuwa wanakuja kuabudu walifikiria zaidi biashara badala ya kumwabudu Mungu.

 

S: Kwenye Mak 11:23, kwa nini Yesu aliitaja imani inayong'oa milima?

J: Yesu alikuwa akifundisha kuwa kitu killichotakiwa ni imani ndogo tu ya kweli, iliyotumika kwenye maombi kuweza kung'oa milima. Imani ni kama mbegu; inaweza kukua. Pia, Yesu alisema maneno haya akiwa karibu na Yerusalemu, na siku za mwisho Mlima wa Mizeituni, ulio karibu kilimeta 4 (nusu maili) mashariki mwa Yerusalem, t can grow. Also, Jesus said this near Jerusalem, utagawanyika sehemu mbili, kwa mujibu wa Zak 14:4.

 

S: Kwenye Mak 11:23, je Yesu aliahidi kutupa vitu vyote kabisa tutakavyomwomba kwa imani?

J: Mungu anatupa kitu chochote tumwombacho, kinachokuwa na sifa zifuatazo:

Kitu: Mungu hawezi kutoa "kitu" ambacho siyo kitu, kama jambo linalopingana kimantiki, kama vile maji yasiyolowa, kitu chenye kinachoondokesha ambacho hakiwezi kuondoshwa, n.k.

Kwa imani: Mungu hawezi kutupa kitu ambacho tunakiomba kwa mashaka kama Yak 1:6-7, au kitu ambacho hakijaombwa kwa imani, bali kwa lengo la kukitumia kwa tama zetu kwa mujibu wa Yak 4:3. Tunapaswa kuomba kwa kufuata mapenzi ya Mungu kwenye 1 Yoh 5:14. Kuomba kwa imani kunamaanisha kuwa ndani ya Mungu na Mungu kuwa ndani yetu kama kwenye Yoh 15:7.

Kama tutasamehe: Mak 11:25 inaongeza sifa ya Zawadi nzuri: Kabla ya Mak 11:23, Yesu alifundisha kuwa Mungu ni Baba mwema, anayetupa vitu vizuri, siyo vibaya, kwa mujibu wa Mat 7:9-11 na Luk 11:11-13. Kwa hiyo, wakati mwingine muumini mtiifu anapoomba kwa imani na Mungu akasema "Hapana" au "Ngojea", kama kwenye Ayu 1:1; Fil 2:25; 2 Tim 4:20; na 2 Kor 12:8-9.

 

S: Kwenye Mak 11:25-26, je kama Mkristo wa kweli hasamehi atakwenda jehanamu?

J: Kwa namna fulani swali hili ni la kinadharia tu kwani Mkristo wa kweli husamehe. Hakuna Mkristo wa kweli atakayekataa kumsamehe mtu mwingine, kwa sababu jambo hilo litaonyesha kuwa hajawahi kukubali kupokea msamaha wa Mungu, na kwa sababu hiyo si Mkristo wa kweli. Ni wazi kwamba, ni muhimu sana kumsamehe mtu yeyote.

 

S: Kwenye Mak 11:29-33, kwa nini Yesu hakujibu kiwazi swali aliloulizwa kuhusu mamlaka aliyokuwa nayo?

J: Yesu hakulazimika kujibu swali lolote lile. Ingawa Yesu alijibu maswali mengi ya watu kwa ujumla, hakuwa anajibu kiwazi maswali ya watu waliokuwa wanatafuta majibu yake kwa lengo la kumtega. Yesu angeweza kusema tu, "Sihitaji mamlaka yako kwa sababu ninayo mamlaka ya Baba kama yalivyothibitishwa na uponyaji wa watu wengi ninaoufanya." Hata hivyo, watu hawa wangeweza kuwa tayari waliishalitambua jambo hilo.

 

S: Kwenye Mak 12:1-9, je mfano huu unamaanisha nini?

J: Mungu aliitoa nchi, nchi ya ahadi, kwa Wayahudi. Hata hvyo, Wayahudi hawa hawakumpa Mungu utiifu, ibada isiyogawanyika, zaka, na kafara alivyoviamuru. Aliwatumia manabii, ambao waliwatukana na kuwaua. Mwishoni, Mungu alimtuma Mwana wake, Yesu, ambaye walimuua.

 

S: Kwenye Mak 12:6, ni kwa jinsi gani wakulima hawa walitegemewa kumheshimu mtoto wa mwenye shamba?

J: Wangemheshimu mtoto huyo endapo:

1. Wangekuwa wana heshima kwa mamlaka yeyote ile halali, au

2. Utiifu kwa sheria, au

3. Akili za kutambua kuwa kumuumiza mwana kutawaletea kulipizwa kisasi kwa uhakika, au

4. Hofu inayofaa kwa askari wa bwana wao.

Wangemuua mtoto wa mwenye shamba endapo tu tamaa yao ya shamba imewatia upofu kabisa hata hawawezi kufikiri. Inashangaza lakini ni kweli kuwa watu wanaweza kuwa na tama kubwa sana hata maamuzi yao yanafanya waonekane kuwa wanataka hela za haraka haraka na anasa zaidi kuliko kuwa hai siku inayofuata.

Leo hii inastaajabisha kuona jinsi watu ambao wangeweza kufanya maamuzi mazuri zaidi wakifanya maamuzi mabaya kwa sababu ya tamaa ya mali. Mara nyingi zaidi watu hawa hata hawafahamu jinsi ambvyo tama ya mali imeathiri uwezo wao wa kufanya maamuzi – mpaka siku za baadaye sana.

 

S: Kwenye Mak 12:10 na Luk 20:17, je jiwe kuu la pembeni ni nini?

J: Ni jiwe la kwanza ambalo juu yake msingi wa jengo unajengwa.

 

S: Kwenye Mak 12:10-11 na Luk 20:17-18, kwa nini watu/wajenzi walilikataa jiwe kuu la pembeni?

J: Mwisho wa mambo yote, mtu atataka kuwa ama sehemu ya jengo lile lile ambalo Yesu analijenga, au kutokuwa. Hakuna kuwa kati kwa kati; huwezi kuwa sehemu ya jengo kwa nusu.

 

S: Kwenye Mak 12:13, je Maherodi walikuwa ni watu gani?

J: Neno hili linafanana na Masadukayo. Watu hawa waliitwa "Maherodi" kwa sababu waliunga mkono ukoo wa kitawala wa Herode kama wafalme wa Uyahudi.

 

S: Kwenye Mak 12:13-17 na Luk 20:21-25, je Yesu hakujibu kiwazi swali kuhusu kulipa kodi?

J: Alilijbu kiwazi. Walijaribu kumtega kwa kumuuliza endapo wanapaswa kulipa kodi kwa Kaisari au la. Kama Yesu angesema "Hapana" angeweza kukamatwa na Warumi kwa kushawishi watu kutokulipa kodi. Kama Yesu angesema "Ndiyo" makutano ambao waliuchukiwa utawala wa Warumi wangeweza kuacha kuwa marafiki zake.

Yesu alijibu swali hili kwa kusema kuwa tunapaswa kumpa Kaisari vitu vilivyo vya Kaisari, na Mungu vitu vilivyo vya Mungu. Yesu hakusema bayana vitu vilivyo vya Kaisari, na wao hawakumuuliza.

 

S: Kwenye Mak 12:19 na Luk 20:27, kwa ufupi, tunajua kitu gani kuhusu Masadukayo?

J: Josephus anasema Masadukayo, Mafarisayo, na Waesene walikuwa madhehebu/vyama vya kidini vya Uyahudi. Dhehebu la Masadukayo lilianzishwa na Yohana Hyrcanus I (mwaka 135-104 KK) na lilikufa wakati hekalu la Yerusalemu lilipobomolewa mwaka 70 BK.

Masadukayo walikataa uwepo wa malaika na kufufuliwa kwa mwili. Walikataa vitabu vyote vya Mishna (mkusanyiko rasmi wa tafsiri za mapokeo yasiyoandikwa ya sheria ya Kiyahudi yenye kufanya sehemu ya kwanza ya Talmud), Talmud (sheria za kijamii na kidini na mapokeo yasiyothibitishwa vya Kiyahudi yenye kuhusisha Mishna na Gemara), na mapokeo mengine ya Mafarisayo. Kwa mujibu wa Josephus, Masadukayo hawakuona haja ya kukishika kitu chochote ambacho hakijaandikwa kwenye Torati, na kwa mujibu wa waandisho wa awali wa kikristo, Masadukayo walilikataa Agano la Kale lote isipokuwa vitabu vya Sheria (Torati). Kuhusu vitabu vya Sheria, Mafarisayo waliandika mifano ya jinsi walivyopishana katika mambo madogo.

 

S: Kwenye Mak 12:19 na Luk 20:27, je kuna ushahidi gani wa kibiblia na ule usio wa kibiblia kuhusu Masadukayo?

J: Yafuatayo ni karibu mambo yote tunayoyajua kuhusu Masadukayo.

1. 1 na 2 Maccabees vinatoa historia ya kina ya mivutano ya ndani na nje wakati madhehebu ya Mafarisayo na Masadukayo yalipokuwa yanaanzishwa.

2. Josephus anaongelea kuhusu Masadukayo kwenye vifungu vinne. Nukuu hizi zimetolewa toka kwenye Josephus: Complete Works.

Wars of the Jews 2.8.2,14 (2a) "Kwa sababu kuna madhehebu matatu ya kifilosofia miongoni mwa Wayahudo. Wafuasi wa dhehebu la kwanza ambao ni Mafarisayo; la pili ni Masadukayo; na dhehebu la tatu, wale wanaojifanya kuwa na nidhamu kali, wanaitwa Waesene." (14f) [Waesene ni namna jina hili linavyoandikwa kwenye kitabu] "Lakini Masadukayo ni wale ambao walioko kwenye chama cha pili, na wanayakana kabisa majaliwa, na wanachukulia kwamba Mungu hajali kufanya kwetu mambo mabaya au mazuri; na wanasema wamba kufanya vibaya au vizuri ni uchaguzi wa mtu mwenyewe, na kwamba jambo moja (kati ya haya mawili) na jingine ni ya watu wote nao wanaweza kutenda kadri wapendavyo. Masadukayo pia hukana imani kuwa nafsi za wanadamu hudumu umilele, na adhabu na malipo ya kuzimu. Zaidi ya hayo, Mafarisayo wanarafikiana sana miongoni mwao wao wenyewe, na wanapenda kuleta makubaliano na heshima kwa umma. Lakini mwenendo wa Masadukayo mmoja kwa mwingine ulikuwa kwa kiasi fulani usiostaarbika; na maongezi yao na watu wa dhehebu lao yalikuwa ya kikatili kana kwamba walikuwa wageni kwao . . ." (Baadaye kwenye Antiquities of the Jews 18.1.6 Josephus analitaja dhehebu la nne, ambalo ni kama Mafarisayo isipokuwa wafuasi wake wanapigania uhuru. Anawaongelea Wazeloti).

Antiquities of the Jews 13.5.9 Tofauti na Masadukayo, Mafarisayo walikuwa na desturi ya kutoa adhabu kali.

Antiquities of the Jews 13.10.6 Hii ni mara ya kwanza Masadukayo wanatajwa katika historia, chini ya utawala wa John Hyrcanus I akiwa mfalme na kuhani mkuu (mwaka 135-104 KK)

Antiquities of the Jews 18.1.4 "Lakini mafundisho ya Masadukayo ni haya: Kwamba nafsi zinakufa wakati mmoja na miili; pia hawakishiki jambo lolote zaidi ya yale ambayo vitabu vya Sheria [Torati?] vimewaagiza; kwa sababu wanaona kuwa ni nafasi nzuri kupingana na waalimu wa filisofia waliokuwa wanapingana nao mara kwa mara; lakini mafundisho haya yanapokelwa na wachache, ingawa ni watu wenye heshima kubwa zaidi; lakini hawawezi kufanya kitu chochote wao wenyewe; kwani wanapokuwa mahakimu, kama ambavyo hawapendi na wakati mwingine wanalazimishwa kuwa, wanajilevya fikra za Mafarisayo, kwa sababu umma usingeweza kukubaliana nao." (Josephus aliandika Antiquities of the Jews mwaka 93-94 BK)

3. Mishnah inalinganisha mafundisho ya Masadukayo nay ale ya Mafarisayo kwenye vifungu visivyopungua tisa. (Mishna za awali kabisa ziliandikwa karibu mwaka 200 BK). Yafuatayo ni baadhi ya mafundisho yaliyotolewa na Masadukayo, angalau kwa mtazamo wa Mafarisayo. Hivyo, tofauti zinatokana na mtazamo wa kitu kilichokuwa muhimu kwa Mafarisayo, maelezo machache ya sheria, na si mambo ambayo hayakuwa muhimu kwa Masadukayo.

Baba Batra 115b – Mtu anapokufa bila kuwa na mtoto wa kiume aliye hai, Mafarisayo walisema kuwa ni mjukuu wa kike tu na si binti ndio ambaye angeweza kumrithi, wakati ambapo Masadukayo walisema kuwa mabinti na wajukuu wa kike wanaweza kurithi kama hakuna watoto wa kiume.

Baba Kamma 84a – Katika kuitumia amri ya "jicho kwa jicho", Mafarisayo mara nyingi walikubali fidia ya kifedha, wakati ambapo Masadukayo hawakukubali.

Megillah Ta'anit 1 – Wakati ambapo Mafarisayo walitaka matoleo yalipwe kwa kutumia hazina, wapinzani wa Mafarisayo walitaka gharama ilipwe kwa kutumia sadaka ya hiari.

Megillah Ta'anit 4 – Vilevile kama Baba Kamma 84a.

Makkot 1:5-8 – Mafarisayo walitaka mashahidi wote wa uongo wauawe, wakati Masadukayo waliwaua mashahidi wa uongo endapo tu ushahidi wao umesababisha kifo cha mtu aliyeshtakiwa kwa uongo.

Tosefta Parah chapter 3 and Parah – Masadukayo hawakuwa wananawa mara nyingi kama Mafarisayo, lakini walishika kwa udhati zaidi usafi wa ng'ombe mke mwekundu ambaye bado hajazaa aliyetumika kujitakasa baada ya kugusa maiti.

Tosefta Sanhedrin 6:6 – Mafarisayo walitaka mashahidi wa uongo wote wauawe, wakati ambapo Masadukayo waliwaua mashahidi wa uongo endapo tu ushahidi wao ulisababisha kifo kwa mtu aliyeshtakiwa kwa uongo.

Yadaim 4:7 – Mafarisayo walifundisha kuwa mwenye shamba awajibike kwa hasara ambayo mtumwa wake amesababisha, kama ambavyo anawajibika kwa hasara ambayo mnyama wake anaisababisha. Mafarisayo walifundisha kuwa mtumwa anawajibika sawa na bwana wake, ili kwamba mtumwa anayekuwa amekasirika asitafute kumtia bwana wake matatizoni.

Yerushalmi Yevamot 1:6 – Ndoa ya kaka/mdogo wa mume (ambayo kaka/mdogo wa mtu aliyekufa bila kuwa na mtoto analazimika kumuoa mjane wa marehemu). Ndoa hii ilifanyika pale ambapo mke alikuwa ameposwa, si yule aliyeolewa.

4. Mapokeo ya Kirabi (Abot Rabbi Natan 5) anasema Zadok, mwanafunzi wa Antigonus wa Soko, ambaye alianzisha Masadukayo.

5. Agano Jipya linatuambia kuhusu Masadukayo kwa ufupi sana.

Mat 3:7f – Yohana Mbatizaji aliwaona Masadukayo na Mafarisayo.

Sio Mat 15:1 – Baadhi ya Mafarisayo na waandishi walikwenda kwa Yesu. Kwa kuwa watu hawa walisikitishwa na wanafunzi wa Yesu kutokuosha mikono yao, yaelekea kuwa hapakuwa na Masadukayo miongoni mwao.

Mat 16:1-6 – Mafarisayo na Masadukayo walimwomba Yesu awape ishara kutoka mbinguni.

Mat16:11-12 – Yesu anaagiza kuwa waangalifu na mafundisho ya Masadukayo na Mafarisayo. Ni dhahiri walifundisha vitu tofauti kwa sababu walikuwa madhehebu tofauti, lakini Yesu hakuelezea imani za lolote kati ya makundi hayo kwenye aya hii.

Mat 22:23-34; Mak 12:18-27; Luk 20:27-39, Masadukayo walimuuliza Yesu kuhusu kufufuka. Mishna kwenye Yerushalmi Yevamot 1:6 inaonyesha kuwa vile ndoa ya kaka/mdogo wa mume ilihusika tu na mwanamke aliyeposwa kwa Masadukayo, mwanamke huyu anayetajwa kwenye swali hili alikuwa ameolewa na mume wa saba tu.

Mdo 4:1-2 – Mafarisayo, makuhani, na Masadukayo waliungana katika kuwapinga mitume wa Yesu.

Mdo 5:17-18 – Kifungu hiki kinarekodi kuwa kuhani mkuu kwa wakati huo alikuwa Msadukayo. (Josephus pia anasema kuwa Kuhani Mkuu Anania mdogo alikuwa Msadukayo).

Mdo 23:6-8 – Masadukayo hawakuamini kufufuliwa, au malaika au roho.

6. Maandiko ya Kanisa

Hippolytus (mwaka 222-235/6 BK) kwenye The Refutation of All Heresies kitabu cha 9 sura ya 22, uk.136-137 ana sura nzima kuhusu Masadukayo. Kama Josephus anavyosema, wanasema kuwa Mungu haingilii mambo ya hapa duniani. Wanakana kufufuliwa kwa mwili, na wanasema kuwa nafsi haiendelei kusihi baada ya kifo.Anatoa pia maelezo mengine ambayo yanapatikana kwa Josephus. Zaidi ya maelezo ya, Hippolytus pia anasema kuwa Masadukayo walikuwa wengi sana. "Hata hivyo hawatoi uzito kwa manabii, lakini hawafanyi hivyo kwa watu wengine wenye hekima pia, isipokuwa Sheria ya Musa tu, ambayo, hata hivyo, hawaundi tafsiri mpya."

Tertullian (mwaka 198-220 BK) kwenye On the Resurrection of the Flesh sura ya 2, anawalinganisha wazushi wa kikristo wanaokataa kufufuliwa kwa mwili sawa na Masadukayo kitu ambacho Yesu alipingana nao.

Origen na Jerome, pia wanaonekana kusema kuwa Masadukayo waliifuata Torati tu, kwa mujibu wa The New International Dictionary of the Bible, uk.884-885.

Epiphanius of Salamis (mwaka 390 BK) kwenye Heresies 1,14 anadai kuwa neno "Masadukayo" limetokana na neno la Kiebrania sadiq, linalomaanisha "mwenye haki." Hata hivyo, Wycliffe Bible Dictionary, uk.1500 inasema kuna tatizo katika kuelezea jinsi ambavyo voweli ilibadilika kutoka i (carot) kwenye sadiq kuwa u (carot) kwenye seduqim.

Angalia swali linalofuata kwa maelezo zaidi kuhusu jambo hili.

 

S: Kwenye Ma 12:19 na Luk 20:27, je Masadukayo walilikataa kabisa Agano la Kale isipokuwa Torati, walizikubali sehemu nyingine za Agano la Kale lakini kuwa zina mamlaka ndogo kuliko Torati, au walikubali kila kitu kama Mafarisayo walivyofanya?

J: Ufuatao hapa ni ushahidi. Waandishi toka kanisa la kale Hippolytus, Tertullian, Origen, na Jerome walisema Masadukayo waliamini Torati tu. Hata hivyo, walikosea kwa sababu:

1) Josephus haelezi jambo hili

2) Kwenye Talmud Masadukayo wanatetea hoja zao kwa kutumia vitabu vingine vya Agano la Kale

3) Kuna uwezekano kuwa wasingeruhusiwa kuwemo kwenye baraza kuu la Wayahudi (Sanhedrin) kama wasingekuwa wanavitambua vitabu vingine vya Agano la Kale kuwa ni sehemu ya Maandiko.

Hata hivyo, kuna hoja nyingine tatu zenye kupinga maoni haya:

1r) Josephus aliandika kuhusu Masadukayo, ". . . pia hawafuati kitu chochot zaidi ya vile vinavyofundishwa kwenye vitabu vya Sheria . . ." kwenye Antiquities of the Jews 18.1.4 (karibu mwaka 93-94 BK).

2r) Isitoshe, hata kama Masadukayo hawakuzikataa kabisa sehemu zilizobaki za Agano la Kale, huenda walizikubali sehemu nyingine za Agano la Kale kuwa zina mamlaka kidogo. Maoni haya yanafanana nay a baadhi ya Wakristo kuwa vitabu vya kubuniwa vya kidini (Apokrifa) ni vya kiungu vilivyo sehemu ya Maandiko, lakini vina mamlaka ndogo kuliko sehemu nyingine za Agano la Kale. Huenda Masadukayo hawakuwa wamesema kibayana juu ya kiasi cha mamlaka kilichokwemo kwenye vitabu vya sehemu nyingine za Agano la Kale mbali ya Torati.

3r) Kwa mujibu wa Josephus, Anania (mdogo) alikuwa Msadukayo aliyechaguliwa kuwa kuhani mkuu na Warumi. Kama kuhani mkuu angeondolewa mamlaka ya baraza kuu la Wayahudi (Sanhedrin) ingepunguzwa uthamani wake. Pia, Josephus aliandika kwenye Antiquities of the Jews 18.1.4, kwamba wakati Masadukayo walipokuwa mahakimu, walishikilia mambo ambayo Mafarisayo waliyasema, kwa sababu vinginevyo umma wa watu usingewavumilia. Jambo hili linafanana na wachungaji wengi "Wakristo" wa leo wenye kutilia shaka/kutoafiki msimamo wa asili, asilia au mapokeo (liberal) wanapokataa kuwa Yesu alikufa ili kulipa deni la dhambi zetu wachungaji wengi "Wakristo" wa leo wenye kutilia shaka/kutoafiki msimamo wa asili, asilia au mapokeo (liberal) wanapokataa kuwa Yesu alikufa ili kulipa deni la dhambi zetu, lakini bado wanashiriki meza ya Bwana kila mwezi, wakirudia maneno "Hii ndiyo damu yangu ya agano imwagikayo kwa ajili ya wengi kwa ondoleo la dhambi", ingawa wanasema kuwa hawaamini maneno hayo, kwa sababu vinginevyo washirika wa kanisa wasingewakubali kuwa wachungaji.

Je waandishi toka kanisa la awali walipata wapi habari hizi walizoandika? Kwa kuwa Masadukayo walitoweka karibu mwaka 70 BK, hawakupata toka kwa Masadukayo wenyewe. Huenda walipata habari hizi toka maandiko mengi ya awali ambayo hatunayo leo. Kwa mfano, Papias, mwanafunzi wa Yohana Mtume na mtu wa kwanza nje ya Biblia kufundisha "Premillennialism" kuwa Yesu atarudi duniani kimwili na kuwachukua watu waliomwamini na kwenda nao mbinguni kabla ya miaka elfu moja ya utawala wa Yesu hapa duniani, aliyeandika juzuu nyingi ambazo zimepotea.

Kwa hiyo, ingawa hakuna kitu cha kuthibitisha kuwa waandishi toka kanisa la awali hawakuwa sahihi, kuna hoja toka pande zote mbili za mjadala kuwa ama Masadukayo walizikataa kabisa sehemu nyingine za Agano la Kale, ama walizikubali lakini waliziona kuwa zina mamlaka kidogo kuliko vitabu vya Sheria.

 

S: Kwenye Mak 12:24, kwa nini Yesu aliwaambia Masadukayo kuwa hawakuyajua Maandiko na nguvu za Mungu?

J: Yesu alikuwa sahihi katika mtazamo wa jumla na mtazamo bayana kama alivyoonyesha kwao.

Mtazamo wa jumla: Masadukayo hawakuamini kuwa kuna maisha baada ya kufa au kufufuka. Kwa mujibu wa waandishi toka kanisa la awali, Masadukayo hawakulikubali Agano la Kale isipokuwa vitabu vitano vya kwanza ti. Tazama maswali yaliyotangulia kwa maelezo zaidi.

Mtazamo bayana: Kama Yesu alivyoonyesha, hata vitabu ambavyo walivikubali kuwa ni sehemu ya Maandiko (vitabu vya Sheria au Torati) hawakuamini kikamilifuwa kuwa Mungu bado alikuwa Mungu wa Ibrahim, Isaka, na Yakobo.

 

S: Kwenye Mak 12:24, nini maana ya kutokuwa mbali na ufalme wa Mungu?

J: Haimaanishi kuwa mtu anaweza kuokolewa kwa sehemu, na haihakikishi kuwa mtu aliyeokolewa kwa sehemu atakuja kuokolewa. Yesu alimaanisha kuwa mtu huyu alikuwa karibu sana kumwamini Yesu.

 

S: Kwenye Mak 12:30, wakati Yesu alipoongelea Kum 6:4 kuhusu kumpenda Mungu, kwa nini aliongeza jambo la nne "akili?"

J: Majibu mawili yanayokamilishana.

1. Ingawa neno la Kiebrania "nafsi" lilimaanisha maisha yote ya mtu, zikiwemo akili, Yesu, ambaye alikuwa akiongea Kiaramu na/au Kigiriki hapa, amezitaja akili kiwazi kabia kusistiza ukamilifu wa maana ya nafsi.

2. Pia, tokana na kuja kwa Yesu, waamini wamepata ufahamu mkamilifu zaidi wa wa Mungu kuliko ule waliokuwa nao kwenye Agano la Kale, kama Mat 13:10-16; Mak 4:11 na Luk 8:20 zinavyoonyesha. Kwa maelezo zaidi juu ya fumbo la Yesu lililofunuliwa, tazama Efe 3:4-6,9; 6:19; Kol 1:26-27; 2:2; 4:3; Rum 16:25-26; 1 Pet 1:10-12. Tazama pia maelezo ya Kum 6:4.

 

S: Kwenye Mak 12:30, je tunapaswa kujaribu kuachana na akili ili tuwe watu wa kiroho kama baadhi ya waalimu wa Word-Faith wanavyomaanisha?

J: Sivyo kabisa. Imani huenda mbali zaidi ya akili lakini si kinyume chake. Mak 12:30 inasema kuwa tunapaswa kumpenda Mungu kwa akili zetu zote pia. Jambo la kujiuliza hapa ni kwamba kama neno la Mungu linasema kitu kimoja, na kwa akili zetu tunafikiri kitu kingine tofauti, je tunaliamini neno la Mungu kwanza au akili zetu? Kufikiria vitu kimantiki si kitu cha kututawala, wala hakupaswi kupuuzwa kama kitu kisichokuwa na thamani, lakini ni zawadi inayotakiwa kutumiwa kumtumikia Mungu kwa upendo. Isitoshe, Mungu hatumii tu akili zetu bali anaweza kuzibadilisha kwa kuzigeuza nia zetu kwenye 1 Kor 2:12. Lakini kubadilika huku si lazima kuje peke yake. Rum 12:2 inatuamuru "mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu." Kwa hiyo tunao wajibu wa kufanya kitu ambacho hatuwezi kukifanya. Tunaweza kufanya kitu ambacho sisi wenyewe hatuwezi kukifanya sisi wenyewe kwa kumuomba Mungu kufanya kazi kupitia kwetu, yaani unapaswa kuomba kwa Mungu afanye kazi ya kukubadilisha. Je unaweza kumshukuru kwa kazi ya utakaso ambayo tayari ameishaifanya, na kumuomba akufanya kuwa mwepesi kuongozwa katika kubadilika mawazo, moyo, nafsi na nguvu vyako anakokufanya?

 

S: Kwenye Mak 12:42-44, kwa kuwa waandishi walikula kwenye nyumba za wajane, kwa nini Yesu hakumzuia mjane kutia senti zake mbili kwenye sanduku la hazina?

J: Mjane huyu alisifiwa kwa ukarimu na imani vyake katika kutoa. Waandishi walikaripiwa sit u kwa kutokutoa bali hata kwa kuchukua kwa nguvu kutoka kwa maskini.

 

S: Kwenye Mak 13:34-37, kwa nini Yesu alisistiza sana kuwa wawe macho?

J: Ingawa watu wengine walikukosa kuja kwa kwanza, muktadha hapa ni hotuba kwa wanafunzi tu kuhusu kurudi kwa Yesu kwa mara ya pili. Wanafunzi hawakutakiwa kuanza kuwa macho muda wowote maalum, kwa sababu Yesu ameishawaambia kuwa hakuna mtu aijuaye saa. Badala yake wanatakiwa kuwa macho wakati wote. Kuwa macho hapa kunamaanisha kuwa na maisha matakatifu, na kuwa karibu na Mungu.

 

S: Kwenye Mak 14:4-8, kwa nini Yesu alipenda manukatano ya bei kubwa yamwagwe kwake kuliko kupewa maskini?

J: Yesu alifundisha kwenye Mak 12:29-31 kuwa kumpenda Bwana Mungu wako ndio amri kubwa zaidi, na kumpenda jirani yako kama nafsi yako ni amri inayofuta kwa ukubwa, siyo vinginevyo. Wakristo waliweza kuwasaidia maskini wakati wote, lakini wangeweza kumhudumia Yesu kwa njia hii wakati alipokuwa duniani.

 

S: Kwenye Mak 14:21, ni kwa namna gani ingekuwa bora kwa Yuda kama asingezaliwa?

J: Ingekuwa bora kwa Yuda kutokuwepo kabisa kuliko kufanya hayo aliyoyafanya na kupata adhabu ya haki kwa ajili hiyo. Baadhi ya madhehebu yanayochukuliwa na Wakristo walio wengi kuwa yana mafundisho mapotofu yanatumia aya hii kujaribu kusema kuwa jehanamu ni kama maisha ya mtu kabla ya kuzaliwa, hivyo jehanamu haipo. Hata hivyo, kwa kuwa Yesu alisema kuwa adhabu ya Yuda ni mbaya zaidi kuliko kutokuzaliwa, basi jehanamu hakuhusisha kuangamiza kabisa.

 

S: Je Mak 14:24 inaonyesha kuwa Kristo alikufa kwa ajili ya watu wote?

J: Ndiyo. Hata John Calvin anasema kuwa neno "wengi" linamaanisha "wanadamu wote." Hivi ndivyo John Calvin alivyosema kwenye Calvin's Commentaries juzuu ya 3, uk.138-139 "Marko 14:24. Hii ndiyo damu yangu. Nimekwisha kuonya, damu inaposemekana kumwagwa (kama kwenye Mathayo) kwa ondoleo la dhambi, je tunaelekezwaje kwenye kafara ya kifo cha Kristo kupitia maneno haya, na kuyapuuzia mawazo haya kunafanya ushiriki mkamilifu wa meza ya Bwana usiwezekane. Hakuna njia nyingine ambayo kwayo nafsi za wenye haki zinaweza kutoshelezwa, ikiwa hawataamini kuwa Mungu anafurahishwa nao. Neno "wengi" halimaanishi sehemu tu ya ulimwengi bali wanadamu wote: anatofautisha wengi na mmoja, kana kwamba anasema kuwa hatakuwa Mkombozi wa mtu mmoja, lakini atakutana na kifo ili kuwakomboa wengi toka kwenye hatia yao iliyolaaniwa." (Maandishi ya mlazo yapo kwenye tafsiri ya Kiingereza). Angalia kuwa Calvin anasema neno "wengi halimaanishi sehemu tu ya ulimwengu, bali wanadamu wote."

 

S: Kwenye Mak 14:27 je wanafunzi wangewezaje kukwazwa na Yesu kwa sababu hakujitetea?

J: Imani yao ingeangamizwa wakati Yesu, pamoja na nguvu zake zote, alijitoa kwa hiari yake, kukamatwa, kuteswa, na kufa. Masihi mwenye nguvu alitegemewa kujilinda na kuwashinda Warumi, na siyo kusalimu amri kwao.

 

S: Kwenye Mak 14:42-52, je kifungu hiki kinaonyesha kuwa Yesu, aliyekuwa chini ya mamlaka yao tofauti na Injili nyingine zinazoonyesha kuwa Yesu alikuwa na mamlaka juu yao, kama baadhi ya wanazuoni wenye kutilia shaka/kutoafiki msimamo wa asili wanavyosema?

J: Huku ni kurahisisha mno kunakoleta hata kupoteza maana. Tokea nyakati za awali, Wakristo walitambua kuwa Mathayo anasistiza kuwa Yesu ni Mfalme aliyehidiwa, ambaye alitimiza nabii za Agano la Kale. Marko anasistiza kuwa Yesu ni mtumwa anayeteswa na matendo yake. Luka anasistiza kuwa Yesu ni mwanadamu, na ameandika mambo mengi zaidi yanayohusu utoto wa Yesu. Yohana anasistiza kuwa Yesu ni Mungu, na huenda Injili hii iliandikwa kwa kuchukulia kuwa wasomaji wake waliishasoma Injili nyingine.

 

S: Kwenye Mak 14:51-52, ni kijana gani "aliyejitanda nguo za kitani" aliyekimbia bila nguo?

J: Ingawa Maandiko hayasemi, mapokeo yanasema kuwa alikuwa Yohana Marko, mwandishi wa Injili ya Marko. Mwinjilisti Marko anaweza kuwa alishindwa kujizuia kusema uwepo wake kwenye tukio muhimu la habari hii ya Yesu."

 

S: Kwenye Mak 14:53-55, ni kwa jinsi gani baraza kuu la Wayahudi lilivunja sheria ya Kiyahudi hapa?

J: Walivunja sheria yao wenyewe mara zisizopungua tano.

1) Hawakupaswa kufanya kesi usiku

2) Ulikuwa ni wajibu wa jaji kusimama upande wa mshtakiwa

3) Hawakuwa na mashahidi wawili walitoa ushahidi wenye kuthibitisha dhidi ya Yesu

4) Kwenye sheria za Kiyahudi mtu hakuweza kutiwa hatiani kwa ushahidi wa mshtaki tu

5) Walipaswa kusuburi masaa 24 kabla ya kutangaza kuwa mshtakiwa ana hatia

(Kutoka kwenye mahubiri ya Tim Hawks yaliyotolewa Hill Country Bible Church, Cedar Park, Texas 10/24/1997).

 

S: Kwenye Mak 14:62, je Yesu alisema kuwa Yeye ni Masihi hapa?

J: Ndiyo. Fikiri jinsi ambavyo kuhani mkorofi alivyijisikia wakati Yesu amenukuu Dan 7:13-14 kuhusu kuja kwake na mawingi ya mbinugni. Itikio lao la kumtukana na kutaka auawe kwenye Mak 14:63-65 lilikuwa ni pigo la mwisho la viongozi wa dini ya Kiyahudi.

 

S: Kwenye Mak 14:62, kwa kuwa Yesu ataketi mkono wa kuume wa Mungu Baba, anawezaje tena kuwa anakuja, jambo ambalo linamaanisha mwendo?

J: Mambo matatu ya kuyazingatia katika kujibu swali hili.

Wakati wote, "kuketi mkono wa kuume" si kuwepo mahali fulani, bali ni nafasi ya heshima.

Nyakati tofauti, Yesu anaweza kuketi, kusimama, na kutembea.

Ni kweli, mtu hawezi kukaa na kuwa anakuja kama amepanda farasi mweupe, kama ambavyo Yesu atakuwa kwenye Ufu 19:11.

 

S: Kwenye Mak 14:62, Yesu alimwambia kuhani mkuu kuwa atamwona Mwana wa Adamu akija na mawingu ya mbinguni. Lakini kuhani mkuu alikufa kabla Yesu hajarudi, jambo ambalo linathibitisha kuwa jibu la Yesu halikuwa sahihi. Vivyo hivyo kwenye Luka Yesu anasema, "Lakini tangu sasa Mwana wa Adamu atakuwa ameketi upande wa kuume wa Mungu Mwenyezi" (Luk 22:69).

J: Kwaza, kitu gani si jibu, kisha jibu.

Siyo jibu: Mat 26:64 inasema nyinyi, hivyo si kuhani mkuu tu. Hata hivyo, ni swali la kinadharia tu, kwani wajumbe wote wa baraza la Wayahudi walikufa kabla ya kurudi kwa Yesu.

Jibu: Jambo hili lina vipingamizi viwili ndani ya kimoja. Kipingamizi cha kwanza ni kwamba kuhani mkuu (na baraza zima la Wayahudi) walikufa kabla ya kurudi kwa Yesu. Jibu la swali hili ni kwamba baraza zima, pamoja na kuhani mkuu, watamuona Yesu atakaporudi. Ufu 1:7 inaahidi kuwa kila jicho litamwona Yesu atakapokuwa anarudi, hata wale wataliochoma mkuki. Watu waliokufa wakiwa wanamkataa hawataepuka kukutana na Yesu tena.

Pingamizi la pili ni kwamba Injili ya Luka, iliyoandikwa baada ya Injili ya Marko inaonekana kuwa inabadilisha kutoka "utamwona" na kueleza tu kuwa Yesu atarudi. Wazo kuu la hoja hii linadhoofishwa na tofauti ya matini kwenye hati za kale zenye kifungu hiki. Clement wa Alexandria (mwaka 193-217/220 BK) alinukuu Mak 14:62 yenye neno "mtamwona" kwenye Stromata kitabu cha 6 sura ya 52. Tunafahamu kuwa hii ni Injili ya Marko na si Injili nyingine ambayo Clement anainukuu kwa sababu anasema wazi kuwa ni Marko.

 

S: Kwenye Mak 14:65, kwa nini baadhi ya watu walimuuliza Yesu kubashiri ni nani aliyempiga hapa?

J: Askari wa Kirumi walikuwa na mchezo wa kikatili waliocheza na wafungwa uliitwa "ngumi-tatu." Askari watatu wataweka moja ya ngumi zao chini ya kidevu cha mfungwa na kumpiga. Mfungwa arejewapo na fahamu zake walimuuliza ni askari yupi aliyempiga. Ikiwa mfungwa atakosea, askari aliyekuwa amempiga atakuwa mshindi (na mfungwa atakuwa ameshindwa). Ikiwa mfungwa atapata, askari aliyempiga atakuwa ameshindwa. Inaonekana kuwa mar azote wafungwa walikuwa wanashindwa.

 

S: Kwenye Mak 15:14, kwa nini Marko anaonekana kutaka kuwalaumu Wayahudi, kama mtu mmoja mwenye kutilia shaka/kutoafiki msimamo wa asili au mapokeo alivyodai?

J: Kwanza kabisa, wataalamu wa elimukale wamevumbua ua ambao wanafikiri umati wa watu ulikuwepo, na haukuweza kuchukua zaidi ya watu 400. Hivyo, umati hapa haukuwa wa wakazi wote na wageni wa Yerusalemu, bali sehemu ndogo sana ya watu ambao makuhani waliwachagua.

Yuda, viongozi wa Kiyahudi, Wayahudi, Warumi, na hata Yesu ambaye hakukimbia, wote walikuwa na sehemu ya mapenzi ya Mungu yaliyokusudiwa kabla (Mdo 2:23). Ifuatayo ni orodha ya majukumu ya kila mmoja wao. Kama unavyoweza kuona, Marko si mkali sana kwa Wayahudi kama waandishi wengine wa Injili.

Yuda: Mat 26:14-16, 49-50; Mak 14:17-21, 42, 44-45; Luk 22:3-6, 47-48; Yoh 13:18, 21,27; 18:2

Viongozi wa Kiyahudi: Mat 26:57-58; 27:20; Mak 14:43, 46, 53-65; 15:1, 3, 10-11, 31; Luk 22:2, 52; 22:66-23:2; Yoh 18:3, 12-14, 19-24, 30

Wayahudi: Mat 27:20-23, 25; Mak 15:11-15; Luk 23:18, 21, 23

Warumi: Mat 27:11-31; Mak 15:15-20; 16:24; Luk 23:24; Yoh 18:33-19:3; 19:16

Yesu kutokukimbia: Mat 26:39-46, 53-54; Mak 14:35-42; Luk 22:39-46; Yoh 18:4-11

 

S: Kwenye Mak 15:17, kulikuwa na umuhimu gani kumvika Yesu nguo yenye rangi ya zambarau?

J: Nguo za zambarau zilikuwa ghali kwa vile zilitiwa rangi iliyo ngumu kupatikana itokanayo na magamba ya makonokono ya kwenye miamba (murex). Kwenye ufalme wa Rumu, ni mfalme tu na familia yake ndio waliotakiwa kuvaa nguo za rangi ya zambarau, ingawa mfalme, kwa upendeleo, angeweza kugawa nguo zake za zamani kwa watu wengine. Joho la rangi ya zambarau lilikuwa linadhiki maneno ya Yesu kuwa Yeye ni mfalme.

 

S: Kwenye Mak 15:32, tunaambiwa kuwa Yesu alitundikwa "msalabani" ili asulubiwe: Kristo mfalme wa Israeli na ashuke sasa msalabani tupate kuona na kuamini. Hata wale waliosulubiwa pamoja naye wakamfyolea.

Neno "msalaba" hapa kwa Kigiriki ni stauros, ambalo James Strong analifafanua kuwa:

(4716) kutoka kwenye msingi wa 2476; nguzo au mhimili (uliosimamishwa), yaani (maalumu) nguzo au msalaba (kama chombo cha kutekelezea adhabu ya kifo); kwa lugha ya picha, kuweka kwenye hatari ya kifo, yaani, kujikana mwenyewe; kwa kudokeza, kifo cha Kristo kwa ajili ya dhambi za wanadamu: --msalaba.[1]

Hata hivyo, kwenye 1Pet 2:24, tunaambiwa kuwa Yesu alisulubiwa kwenye "mti": Yeye mwenyewe alizichukua dhambi zetu katika mwili wake juu ya mti, tukiwa wafu kwa mambo ya dhambi, tuwe hai kwa mambo ya haki; na kwa kupigwa kwake mliponywa.

Neno "mti" kwa Kigiriki ni xulon, na limefafanuliwa na Strong kama:

(3586) kutoka kwenye msingi mwingine wa 3582; mbao (kama nishati au mali ghafi); kwa kudokezea, fimbo, rungu au mti au kifaa kingine cha mti au kitu: --fimbo, gongo, mti, mbao.[2]

Kosa hapa ni dhahiri. Neno la Kigiriki stauros linamaanisha bayana kabisa "msalaba." Hakuna maana mbili zilizotumiwa katika neno hili. Ingawa neno xulon linaweza kutafsiriwa kwa kubadilishana kama "mbao", "gongo", "mti", n.k., lakini kwenye 1 Pet 2:24, limetafsiriwa kama "mti." Sasa tunahitaji kujiuliza kwa nini neno xulon lilitumiwa wakati palikuwa na neno la hakika zaidi, stauros, kama aya ilikusudia kumaanisha "msalaba?"

Kwa hiyo ni dhahiri kuwa neno xulon limetumiwa kumaanisha "mti" kwenye 1 2:24, na, kwa ajili hiyo, kuna ukinzani na Mak 15: 32.

Rejea

[1] James Strong, The New Strong's Exhaustive Concordance of the Bible (Thomas Nelson, 1996)

[2] James Strong, Op. Cit. (A Muslim Asked This)

J: Yesu aliangikwa kwenye msalaba wa mbao, uliotokana na mti. Warumi, Wakarthaginia, na Waajemi walitumia vigingi vya mbao vyenye vipande vilivyopishana, siyo miti ulio hai. Kutumia maneno mawili yenye kumaanisha kitu kilekile (kama vile staurus na xulon) si shida, sawa na kutumia majina mawili ya Mungu kwenye Kurani.

Petro anasema Yesu aliangikwa mtini (Mdo 5:30; 10:39), lakini pia Petro anasema Yesu alipigiliwa misumari msalabani (Mdo 2:23).

Paulo anasema Yesu aliangikwa mtini (Gal 3:13; Mdo 13:29), lakini pia Paulo anataja msalaba wa Yesu kwenye Gal 5:11; 6:12, 14; 1 Kor 1:17, 18.

"Mti" na "msalaba" ni maneno ambayo yametumiwa kwa kufanana; mwandishi huyohuyo anayatumia maneno yote mawili. Yesu alipigiliwa misumari mtini; lakini Biblia haisemi kuwa mti ulikuwa hai.

Mafundisho ya kweli ya Kiislamu pia yanafundisha kuwa "kuonekana kwa Yesu" kulisulubiwa pia. Sasa kuna jambo la muhimu kuhusiana na huku kusulubiwa. Ama:
a) Ni Yesy kweli aliyesulubiwa, au
b) "Mabadiliko makubwa hasa ya ulaghai" Allah sit u kwamba aliwadanganya Wayahudi na Warumi kufikiri kuwa Yesu alisulubiwa wakati ukweli ni kwamba hakufanya hivyo, Allah pia alidandanya mama wa Yesu, wanafunzi wa Yesu na Wakristo wote wa awali, ambao walimhubiri Kristo aliyesulubiwa. Tuna maandishi ya Ignatius na Polycarp, wanafunzi wa Yohana Mtume, na watu wengine walioamini kuwa Yesu alisulubiwa na kufufuliwa kutoka kwa wafu. Hata kama u Muislamu huwezi kuwalaumu Wakristo kwa kuamini kuwa Yesu alisulubiwa, kama unadhani kuwa Allah aliwadanganya wafuasi wake mwenyewe. "Allah ni mdanganyifu mkubwa kuliko wote" (Sura 3:54). Kama Allah huyu amwadanganya Wakristo, na huna shida na jambo hilo, je Allah huyu anaweza kuwadanganya Waislamu pia?

 

S: Kwenye Mak 15:42, je hii ni siku ya maandalizi ya sabato, au siku ya maandalizi ya Pasaka?

J: Kuna majibu tofauti mawili yanayowezekana.

Siku ya sabato inayoweza kuwa ilienda pamoja na sikukuu ya Pasaka mwaka ule: Usisahau kuwa Sikukuu ya Pasaka na siku ya sabato vilienda pamoja miaka fulani. Hakuna uhakika mkamilifu kuhusu starehe hasa wakati ule, lakini watu wengi wanafikir kuwa sikukuu ya Pasaka na siku ya sabato zilienda pamoja mwaka 30 BK au 33 BK.

Sabato kuu: Kila jumamosi ilikuwa ni siku ya sabato, lakini si kila siku ya sabato ilikuwa jumamosi, kama Law 23:39 inavyothibitisha. Kwa mfano, siku za kwanza na ya nane ya mwezi wa saba ziwe "Sabato ya kupumzika." "Hapakuwa na kufanya" kazi katika siku hizo kila mwaka, lakini siku hizo hazikuwa jumamosi mara nyingi. Sikukuu ya Pasaka ilikuwa ni siku ya kwanza ya Mikate isyotiwa chachu, na siku za kwanza na saba za sikukuu hiyo zilikuwa "siku za mapumziko" kwa mujibu wa Kut 12:16.

Yoh 19:31 ingeweza kutoa jibu kuwa lipi kati ya majibu mawili hapo juu ni sahihi, isipokuwa ingetumika kuunga mkon majibu yote. Inasema, ". . . maana sabato ile ilikuwa ni siku kubwa." Lakini kwa kuwa ilikuwa ni siku kubwa, haikuwa lazima kuwa jumamosi.

 

S: Kwenye Mak 15:44, kwa nini Pilato alishangaa kuwa Yesu alikuwa tayari amekwisha kufa?

J: Ama Pilato alikuwa amesahau muda tu, au watu wengi waliokuwa wanasulubiwa walichukua muda mrefu kabla ya kufa. Yesu alipigwa mijeledi na viboko kabla ya kusulubiwa.

 

S: Kwenye Marko 16, je kuna mambo gani ambayo yameandikwa pia kwenye Injili nyingine na Matendo ya Mitume?

J: Yafuatayo ni mambo yaliyoandikwa kwenye Marko 16 na vitabu vingine vya Biblia

Yesu alifufuka mapema sana asubuhi (Mak 16:2, 9 Mat 28:1; Luk 24:1; Yoh 20:1)

Yesu alifufuka siku ya kwanza ya juma (Mak 16:2, 9; Mat 28:1; Luk 24:1; Yoh 20:1)

Mapepo saba yalitolewa kwa Mariamu Magdalena (Mak 16:9; Luk 8:2)

Mariamu Magdalena/wanawakw walikwenda kaburini (Mat 28:1-8; Mak 16:9-10; Yoh 20:1; Luk 24:1-10)

Watu wengine hawakuamini mara moja waliposikia kufufuka kwa Yesu (Mat 28:17; Mak 16:11; Luk 24:11)

Yesu anawatokea wanafunzi wake wawili (Mak 16:12; Luk 24:13-35)

Bado hawakuamini (Mak 16:13; Luk 24:36)

Yesu awakemea wanafunzi wake 11 kwa ajili ya kutoamini kwao (Mak 16:14; Luk 24:38-41)

Yesu awaagiza wanafunzi wake kuhubiri injili kwa watu wote (Mak 16:15; Luk 24:47-48)

Aaminiye na kubarizwa ataokoka, asiyeamini atahukumiwa (Mak 16:16; Mdo 2:38-39)

Ishara (Mak 16:17, 22; Matendo yote)

Kutoa mapepo (Mak 16:17 na kwenye Matendo)

Kunena kwa lugha (Mak 16:17; Mdo 2:2-13)

Kuumwa na nyoka bila kudhurika (Mak 16:17; Luk 10:19; Mdo 28:3-6)

Kunywa vitu vya kufisha bila kudhurika (Mak 16:18 – hakuna sehemu nyingine)

Yesu apaa mbinguni (Mak 16:19; Luk 24:51; Mdo 1:9-11)

Yesu ameketi mkono wa kuume wa Mungu (Mak 16:19; Mdo 7:56)

Walihubiri kila mahali (Mak 16:20; Mdo 1:8)

Hitimisho, kunywa kitu cha kufisha (chenye sumu inayoua) bila kudhurika ni jambo pekee kwenye mwisho wa Injili ya Mark ambalo halijaongelewa sehemu nyingine ya Biblia.

 

S: Kwenye Mak 16:1, kwa nini wanawake walichukua manukato ili kwenda kuupata mwili wa Yesu?

J: Yesu aliwekwa kaburini kwa haraka kabla ya sabato kuanza jua lilipokuwa linazama. Wanawake walichukua manukanto ili kuuhifadhi mwili wa Yesu kwa kuuweka dawa.

 

S: Kwenye Mak 16:4, je jiwe lilikuwa limeviringishwa?

J: Hapana. Neno la Kigiriki linaweza kutafsiriwa vizuri zaidi kwa kusema "lilivurumishwa" kuliko kuviringishwa. Kama jiwe lilikuwa na uzito wa tani kadhaa, ingehitajika malaika kulivurumisha.

 

S: Kwenye Mak 16:8, kwa kuwa wanawake hawakusema kitu chochote kwa mtu yeyote, je waliwaambia wanafunzi?

J: Ingawa hawakumwambia mtu yeyote walipokuwa njia kutoka kaburini, mwishoni walimwambia kila mtu, na wanafunzi walikuwa wa kwanza kuambiwa. Ingawa kutokumwambia mtu yeyote kunaweza kumaanisha kuwa hawakuwaambia hata wanafunzi mpaka baada ya muda fulani, kuna uwezekano mkubwa zaidi kuwa usemi huu unamaanisha kwamba waliwaambia wanafunzi tu na si mtu mwingine yeyote mbali ya kundi lao dogo.

 

S: Kwenye Mak 16:12, je Yesu alitokea vipi kwa namna nyingine?

J: Usemi huu unamaanisha tu kuwa watu hao wawili hawakumtambua Yesu wakati walipokuwa wanatembea naye. Huenda Yesu alikuwa amevaa nguo tofauti, na kwa jinsi hiyo angeonekana tofauti na alivyokuwa amevaa alipokuwa amekufa. Yesu alifufuka kwa mwili kutoka mauti akiwa na mwili halisi ulio na utukufu. Haitakuwa sahihi kutumia ayah ii kusema kuwa Yesu alikuwa na miili tofauti, kwa sababu kutokumtambua kwao hakuonyeshi mwili tofauti.

 

S: Kwenye Mak 16:16, vipi kuhusu watu ambao wameamini lakini hawajawahi kubatizwa?

J: Ingawa Mak 16:16 haisema bayana, Yoh 3:36 na aya nyingine nyingi zinasema kuwa yeyota aaminye ameokolew. Mwizi alikuwa mkono wa kuume wa Yesu aliamini na alikwenda paradiso bila kubatizwa, na kabla ya mwizi pale msalabani, wanafunzi wa Yesu walibatiza (Yoh 3:26; 4:2) na Yohana Mbatizaji alibatiza kwa ajili ya ondoleo la dhambi (Mak 1:4; Luk 1:77; 3:3b). Mstari huu hausemi kiwazi kabisa lakini kuna hali nne tofauti.

Wameamini na kubatizwa: Wameokolewa

Wameamini ila bado kubatizwa, wameokolewa. Ayah ii haisemi, lakini Mdo 10:45-47 inaonyesha watu walioamini, na waliokolewa kama ilivyodhihirishwa na kunena kwao kwa kweli kwa lugha mpya, kabla ya kubatizwa kwa maji.

Hawajaamini ila wamebatizwa: hawajaokolewa

Hawajaamini na hawajabatizwa: hawajaokolewa, isipokuwa Mungu anaweza kuwapa neema ya pekee watoto wachanga wanaokufa, watu wanaokuwa na utindio mkali wa ubongo, n.k.

Sababu ya kutoelezwa kwenye hali ya pili inawezakuwa kwamba ni mapenzi ya Mungu kuwa waamini wote wanatakiwa kuwa watiifu kwa Mungu na kubatizwa kwa maji.

Isitoshe, muktadha wa aya hii unaonekana kuwa watu wanaoweza kuamini. Watoto wachanga, watu wenye utindio mkali wa ubongo, huenda na wengine ambao hawajawahi kumkana Yesu lakini hawajaamini hawaongelewi kwenye aya hii.

Huu hapa ni mfano. Kama binti yangu jikoni ananiomba chanji ya hela, na namwambia nipe hela na chupa ya maji nami nitakupa chenji. Kama binti yangu atanipa vyote hela na chupa ya maji nitampa chenji. Kama hatanipa hela basi sitampa chenji. Lakini vipi kama binti yangu atanipa hela bila kunipa chupa ya maji. Hapo itategemeana. Kama atasema, nimetafuta lakini sikuweza kupata chupa ya maji basi nitampa chenji. Lakini kama ataongea bila heshima, na atakataa kunipa chupa ya maji ambayo anaweza kuipata basi sitampa chenji.

Mshiriki wa Kanisa la Kristo alitoa mfano kuwa "Ukila chakula na kukisaga utaishi, usipokula utakufa." Kusaga chakula kumedokezwa. Hata hivyo, kuutumia mfano huu wa kitendo cha mwili kisichotegemea hiari yetu kwenye amri ya Mungu ya Mak 16:16 ambayo tunatakiwa kuitii kwa hiari yetu kunapingana na neno la Mungu, lenye kuahidi wokovu kwa watu wote wanaoamini kwenye vifungu vifuatavyo: Yoh 3:16, 18, 36; 5:24; 6:47; 11:25-26; Mdo 10:43-48; Rum 9:33; Joel 2:32a; Mdo 2:21; Rum 10:9-10; 10:13; 1 Yoh 5:1, 10-13.

Muhtasari: Kama unaamini, nenda ukabatizwe. Hata hivyo, ubatizo haufaidii kitu kama huamini.

 

S: Kwenye Mak 16:18, je kwa kusema kuwa watashika nyoka kunahalalisha watu wa Appalachia wanaodhani kuwa kuna watu wanaopaswa kushika nyoka wakati wa ibada?

J: Hapana. Hata bila aya hii, Biblia inaonyesha kuwa Mungu anawapa Wakristo ulinzi wanaohitaji, na Mungu atafanya miujiza, na si tu wa kinga dhidi ya kuumwa na nyoka, pale panapokuwa na hitaji. Hata hivyo, hata katika mstari huu, Biblia inasema kuwa hatupaswi kumjaribu Mungu kwa kujiweka kwenye hali yeyote ile kwa lengo la kutaka kuonekana.

Kut 17:2-7; Hes 14:22; Kum 6:16, Zab 78:17-18, 40-41, 56-57; 95:8-9. Ahaz hakufuata kawaida na hivyo anathibitisha kanuni. Ingawa Ahaz alifahamu suala la kumjaribu Mungu kwenye Isa 7:12, kutoa jibu wakati nabii wa Mungu anakuuliza swali siyo kumjaribu Mungu.

 

S: Je Mak 16:9-20 iliandikwa na Marko?

J: Wakristo wa kweli hawakubali kuwa Mak 16:9-20 ilikuwepo kwenye matini ya awali ya Injili hii.

Ushahidi wa nje unaoafiki kuwepo kwa kifungu hiki

Mwaka 182-188 BK

Irenaeus Against Heresies kitabu cha 3 sura ya 10 mst. 5. (Irenaeus alikuwa mwanafunzi wa Polycarp, mwanafunzi wa Yohana Mtume)"Pia, mwisho mwa Injili yake, Marko anasema: "Basi Bwana Yesu, baada ya kusema nao, akachukuliwa juu mbinguni, akaketi mkono wa kuume wa Mungu" (nukuu kutoka Mak 16:19)

Karibu mwaka 170 BK

Tatian's Diatessaron

Sura ya 55, ananukuu Mak 16:15-20

Mwaka 200 BK

Tertullian Treatise on the Soul

"si wa mmoja tu, kama ilivyokuwa pepo la Socrates mwenyewe; lakini wa mapepo saba kama ilivyokuwa kwa of the Magdalena." (Hata hivyo, habari hii hapa kuwa mapepo saba yalitolewa toka kwa Mariamu Magdalena, ipo pia kwenye Luk 8:2.)

Mwaka 198-220 BK

Tertullian On the Resurrection of the Flesh sura ya 51, uk.584 pia Against Praxeas sura ya 2, uk598; sura ya 30, uk.627

Maneno "Yesu akiketi mkono wa kuume wa Baba" yanatoka Mak 16:19, lakini yapo pia kwenye aya nyingine (Mat 26:64; Mak 14:62; Luk 22:69; Mdo 2:34; Kol 3:1; Ebr 1:3,13; 8:1), kwa hiyo hii si kumbukumbu pekee. Tertullian hakuwa ananukuu Maandiko mara nyingi lakini anayadokezea mara nyingi. Kwa hiyo Tertullian hawezi kutumiwa kuthibitisha kuwa Mak 16:19 ilikuwemo kwenye Injili ya Marko, lakini hatoi ushahidi dhidi ya kuwepo kwake.

Mwaka 198-220 BK

Tertullian Scorpiace sura ya 15, uk.648

"Imeandikwa, Msujudie Bwana Mungu wako, umwabudu yeye peke yake.' Lakini hata sasa ni sahihi kuwa asikie, kwa vile muda mrefu baadaye, alimwaga hizi sumu, ambazo hata sasa zinadhuru kwa haraka yeyote aliye mnyonge, kama mtu yeyote atakunywa kwa imani, kabla ya kudhurika, au hata muda mfupi baada ya hapo, huu ukame wetu." (dokezo la kistari la kunywa sumu bila kudhurika)

Mwaka 120-150 BK

The Didache

 

Karne ya 3au 4

Tafsiri ya Kisiria cha Kuretoni

 

Constitutions of the Holy Apostles kitabu cha 6 sehemu ya 3 sura ya 15 (sehemu za mwisho zaidi karibu mwaka 380 BK)

Kwa kuwa Bwana anasema . . . ‘Aaminiye na kubatizwa ataokoka; lakini asiyeamini atahukumiwa'" (ananukuu Mak 16:16)

Constitutions of the Holy Apostles (karibu mwaka 380BK) kitabu cha 7 sehemu ya 1 sura ya 1 (linganisha na kitabu cha 5 na 8)

Ananukuu Mak 16:17-18 maneno yenyewe hasa kama ya Yesu Kristo

Karibu mwaka 450 BK

Alexandrinus

 

Karne ya 3 hadi 4

Kimisri cha Kibohairi

 

Karne ya 3 hadi 4

Kimisri cha Kisahidi

 

Karne ya 5

th century

Freer Gospels

 

Mwaka 400-500 BK

Hati ya kale yenye maandiko

Ephraemi Rescriptus

 

Mwaka 400-600 BK

Hati ya kale yenye maandiko

Codex Bezae

 

Karibu mwaka 700 BK

Matini kubwa ya jamii ya

Byzantine

 

Matini za Biblia za miaka ya baadaye (angalau matini 38)

Kisiria cha Kfilokeni,

Kisiria cha Kiharkle, Kisiria cha Kipalestina,

Kiethiopia, aina kadhaa za Kijojia (kutoka karne ya tano), Kislavoniki, Kitaliki, Biblia ya Kilatini (Vulgate), Kimisri cha cha Kifayumi

 

Fyi, injili yenye kutiliwa shaka ya Nicodemus I na II inaongelea kunena kwa lugha mpya, nyoka, na sumu, lakini kitabu hiki kinaweza kuwa kiliandikwa miaka ya baadaye.

Ushahidi wa ndani unaoafikiana na kuwepo kwa kifungu hiki: Hakuna.

Ushahidi wan je usioafikiana na kuwepo kwa kifungu hiki

Karibu mwaka 360 BK Eusebius Questions to Marianus I

Mwka 325-350 BK Vaticanus: Nafasi wazi sehemu hii. Vaticanus haina nafasi nyingine zozote wazi kama hii kwenye hati nzima.

Mwaka 340-350 BK Sinaiticus: Nafasi wazi sehemu hii. Hata hivyo, kwa mujibu wa www.LogosResourcePages.org/uncials.htm, unaweza kuona mahali ambapo maandhishi haya yalikuwepo kwenye Sinaiticus, lakini yalifutwa kwa fuwawe.

Kumbuka kuwa kwenye Sinaiticus na Vaticanus Injili ya Marko inaishia na neno "kwa sababu" (gar kwenye Kigiriki). Hakuna kitabu miongoni mwa maandiko ya Kigiriki ambacho kimewahi kupatikana chenye kuishia na neno "kwa sababu." Kwa upande mwingine, kuna mifano mingi ya sentensi za Kigiriki na vifungu vyenye kuishia na neno hili.

Mwaka 193-217/220 BK Clement wa Alexandria

Mwaka 225-254 BK Origen

Mwaka 407 BK Jerome, Epistle 120

Hati zenye maandiko

zisizopungua 6

Kisiria cha Sinai

Mwaka 900-1000 BK Hati ya kale ya Kiamenia inasema kifungu hiki kiliongezwa na Aristion, anayetajwa na Papias

Hati kadhaa za Kijojia (zilizoandikwa karne ya tano)

Ushahidi wa ndani usioafiki kuwepo kwa kifungu hiki

Mabadiliko ya ghafla ya pronomini kutka aya ya 8 kwenda aya ya 9. Mhusika wa aya ya 8 ni wanawake, wakati pronomino kwenye aya ya 9, anastas, ni ya kiume. Hata hivyo, sehemu nyingine zina mabadiliko ya ghafla ya pronomino pia, kama vile yeye (mwanaume) = Yusufu wa Arimatao kwenye Mak 15:46; yeye (mwanaume) = Yesu kwenye Mak 15:47 na wao = Mariamu na Salome kwenye Mak 16:1.

Misamiati: Theluthi ya maneno muhimu ya Kigiriki hayajatumiwa au yametumiwa tofauti kwenye sehemu nyingine za Marko. Kuna maneno 166 kwa jumla, maneno tofauti 101. Ukiachilia mbali majina, kibainishi "the", n.k. kuna maneno makubwa muhim 75 yaliyo ya tofauti. Kati ya hayo15, (yakiwemo apistia (kutokuamini) na sklerokardia (ugumu wa mioyo) yametumiwa sehemu nyingine kwenye Injili ya Marko. Maneno mengine 11 yametumiwa kwa maana nyingine.

Ukweli mkavu: unaonekana kukosa maelezo yenye uhai yaliyo kwenye sehemu nyingine za Marko.

Mambo yanayofanana kwenye Injili zingine: Mathayo na Luka wanaongelea mambo yanayofanana na Marko hadi mwisho wa mstari wa 8.

Ushahidi wa nje unaosema kuwa haieleweki vizuri: Zaidi ya hati za maandiko 8 za kale hazina sura nzima ya Marko 16. Hizi ni pamoja na p45 (Mak 12:29 na kuendelea haipo)

2386 – haina ukurasa mzima

1420 – haina ukurasa mzima

16 – imeharibika na haina Mak 16:6 yote na kuendelea

304 – ina maandishi na maoni

Mwisho mfupi wa Marko

Kimisri cha Kibohairi [Boh] 3karne ya 3 au 4

Kiethiopia [Eth] kutoka karibu mwaka 500 BK

Katalogi ya hati za kale za Injili ya Marko

P45 Papyrus 45 (225) ~ imeharibika

B Vaticanus (325-350) ~ hakipo

À Sinaiticus (340-350)~ hakipo

A Alexandrinus (c.450) ~ kipo

C Ephraemi (450) ~ kipo

D Bezae (500?) ~ kipo

L Regius (750) ~ kipo mara mbili

M Campianus (850) ~ kipo

N Purpureus Petropolitanus (550) ~

imeharibika

U Nanianus (900) ~ kipo

W Washington (400) ~ kipo pamoja na

Freer Logion

D Sangellensis (900)~ kipo

Q Koridethi (800?) ~ kipo

P Petropolitanus (850) ~ imeharibika/kipo

(haina 16:18-20)

S Rossanensis (550) ~ imeharibika/kipo

(hakina 16:14-20)

F Beratinus (550) ~ imeharibika

Y Laurensis (850) ~ kipo mara mbili (mfano na mwisho mfupi ukiwa umedokezwa)

Hati ndogo sana za f1 (1, 118, 131, 209, 1582) ~ kipo pamoja na maelezo au sigla

Hati ndogo za f13 (13, 346, 543, 826, 828, 69, 124, 788, 983, 1689) ~ kipo

28 (miaka ya 1100 BK) ~ kipo

33 (mwaka 1000 BK) ~ kipo

157 (mwaka 1100 BK) ~ kipo

565 (miaka ya 800 BK) ~ kipo

579 (miaka ya 1200 BK) kipo mara mbili

700 (miaka ya 1100BK) ~ kipo

892 (mwaka 950 BK) ~ kipo

1071 (miaka ya 1100 BK) ~ kipo

1342 (miaka ya 1000 BK) ~ kipo

1424 (miaka ya 800 BK) ~ kipo

Maelezo haya yamechukuliwa kutoka Mark 16:9-20, a Study of the External Evidence, kilichotungwa na Jim Snapp II (2003).

Mambo yaliyopo kwenye Mak 16:9-20 tu

Mafundisho yote na dhana zote kwenye mwisho mrefu wa Injili ya Marko vinapatikana pia sehemu nyingine za Biblia isipokuwa mambo manne:

1. Yesu alikuwa ameyatoa mapepo saba toka kwa Mariamu Magdalena

2. Ishara zitakazofuatana na waamini:

[Wakilazimika], wataweza kushika nyoka kwa mikono yao. (Luk 10:19 inasema wanafunzi wangeweza kukanyaga nyoka na nge, jambo ambalo linafanana na Mako 16). Pia mfano umetolewa kwenye Mdo 28:3-6 wa Paulo akiumwa na nyoka mweny sumu kali bila kudhurika.

3. [Wakilazimika], wataweza kunywa sumu mbaya.

4. Hili karipio kubwa sana lililoandikwa ambalo Yesu alilitoa kwa wanafunzi wake.

Mambo yasiyokuwemo: Mak 14:28, 16:7 hazielezei kutokea kwa Yesu Galilaya.

Hitimisho: Kama Mak 16:9-20 iliaongezwa kwa makosa kwenye baadhi ya hati, iliongezwa kabla ya mwaka 150 BK. Kama ilitolewa kwa makosa basi ilitolewa kabla ya mwaka 217 BK.

 

S: Je Mak 16:9-20 inafaa kuchukuliwa kuwa Maandiko kama sehemu nyingine za Injili ya Marko?

J: Inafaa kama Marko aliiandika. Hata hivyo, kuna Wakristo wanaosema kuwa kwa sababu ya kuwepo kwake, kuenea na kukubalika kwake mapema sana, bado ni sehemu ya Maandiko, hata kama iliandikwa na mwandishi au mtu mwingine yeyote yule mbali ya (Yohana) Marko. Bruce Metzger anaonekana kuwa na maoni haya.

 

S: Kuna ushahidi gani kwenye Injili ya Marko kuwa (Yohana) Marko ndiye aliyeandika kitabu hiki?

J: Kanisa la awali liliitambua Injili hii kuwa iliandikwa na Marko. Papias, mwanafunzi wa Yohana Mtume,alisema kuwa (Yohana) Marko aliyekuwa anafuatana na Petro Mtume ndiye aliyeandika Injili hii.

 

S: Kwenye Marko, kwa kuwa (Yohana) Marko hakuwa mmoja wa mitume wa Yesu, kwa nini Injili hii inakuwa sehemu ya Biblia?

J: Marko alitambuliwa kuwa mkalimani wa Petro. Huu hapa ni ushahidi wa jambo hili.

Papias (mwaka 130-150 BK): "Mingoni mwa hawa yeye [Papias] anasema kuwa kutakuwa na milenia baada ya kufufuka kwa wafu, wakati ambapo utawala wa Kristo utaanzishwa hapa duniani. [Papias] anasimulia vitu vingine, kwenye maandiko yake, vilivyoelezwa hapo awali na Aristion kuhusu maneno ya Bwana, na mapokeo ya Mzee John. Kwa maelezo zaidi kuhusu jambo hili, tunachoweza kufanya ni kuwaelekeza wasomaji wetu kwenye vitabu vyenyewe; lakini sasa, kuhusu dondoo zilizokwisha fanywa, tutaongeza, kama suala la umuhimu mkubwa, mapokeo yanayomhusu Marko, aliyeandika Injili, ambayo yeye [Papias] amezitoa kwenye maneno yafuatayo: Na Mzee alisema hivi, Marko, baada ya kuwa makalimani wa Petro, aliandika kwa usahihi mambo yeyote aliyokumbuka. Hata hivyo hakusimulia maneno au matendo ya kristo kwa mfuatano halisi wa jinsi yalivyotokea (Eusebius' Ecclesiastical History 3:39 juzuu ya 1, uk.154).

Clement wa Alexandria (mwaka 193-217/220 BK): ". . . Marko, ambaye anachukuliwa kuwa ndiye mwandishi wa Injili, akiwa mshirika wa Petro . . ." (Kipande cha Clement wa Alexandria kwenye Eusebius' Ecclesiastical History kitabu cha 2 sura ya 15).

Tertullian (mwaka 198-220 BK) "Mamlaka ileile ya makanisa la kimitume yatatoa ushahidi kuhusu Injili nyingine pia, ambazo zimetufikia mikononi mwetu kupitia kwao, na kwa mujibu wa matumizi yao – Ninamaanisha Injili za Yohana na Mathayo – wakati ile ambayo Marko aliiandika inaweza kuthibitishwa kuwa ya Petro ambaye Marko alikwa mkalimani wake. Kwani hata aina ya Injili ya Luka watu waichukulia kuwa imeandikwa na Paulo. Na inawezekana kuwa kazi ambazo wafuasi waliziandika ni mali ya viongozi wao" (Tertullian Against Marcion kitabu cha 4 sura ya 5, uk.350).

 

S: Je Injili ya Marko iliandikwa lini?

J: Utangulizi wa anti-Marcionite kuhusu Marko unasema pia "Baada ya kifo cha Petro mwenyewe, yeye [Marko] alindika Injili hiyohiyo . . ." (imechukuliwa kutoka The Bible Knowledge Commentary : New Testament uk.99). Irenaeus kwenye Against Heresies kitabu cha 3 sura ya 1.1, uk.414 (mwaka 182-188 BK) anasema Marko alindika baada ya "kuondoka" kwa Petro na Paulo, ambako kunaweza kuwa muda mfupi baada ya karibu mwaka 64-65 BK. Hata hivyo, The Expositor's Bible Commentary juzuu ya 8, uk. 608 inasema Irenaeus pia aliandika kuwa Injili ya Mathayo iliandikwa wakati Petro na Paulo wakiwa bado hai, na tuna unhakika kuwa jambo hili lina uwezekano mkubwa wa kutokuwa sahihi.

Hata hivyo, kwa mujibu wa kazi ya Eusebius Ecclesiastical History 6:14.5-7, Clement wa Alexandria iliandikwa wakati Petro alikuwa yupo Rumi karibu mwaka 45-64 BK. Origen pia alifikiri kuwa Petro alikuwa hai wkati Injili ya Marko ilipokuwa inaandikwa.

Harnack alifikiri kuwa iliandikwa kabla ya mwaka 62 BK.

The Bible Knowledge Commentary: New Testament, uk.98 inasema kuwa ni vigumu kutambua muda ambao Injili ya Marko iliandikwa, na kwamba vipindi vyenye uwezekano mkubwa zaidi ni ama mwaka 67-69 BK, au mwaka 64-68 BK.

Kwenye New International Bible Commentary, uk.1157, Stephen S. Short anasema ilikuwa karibu mwaka 65 BK. Kwenye uk.1183 Laurence E. Porter anasema kuwa ni dhahiri kuwa Injili ya Marko iliandikwa kabla ya Injili ya Luka, na Luka huenda iliandikwa kwenye nusu ya kwanza ya miaka ya 60.

The Expositor's Bible Commentary juzuu ya 8, uk.608 inasema kadirio zuri zaidi ni mwaka 65-70 BK, kati ya moto mkubwa wa Rumi na kubomolewa kwa Hekalu la Yerusalemu. Jose O'Callaghan alilikuta karatasi la mafunjo kwenye pango la 7 huko Qumran ambalo linaweza kuwa ni vipande vya Injili ya Marko, lililoandikwa karibu mwaka 50 BK. Hata hivyo, The Expositor's Bible Commentary juzuu ya 8, uk.608 inasema kuwa wazo hili "limepingwa vikali sana na wanazuoni wa Agano Jipya (linganisha na EBC 1:420-421, rejeo la 1). Ushahidi ambao O'Callaghan anatoa haujamakilika kabisa hata inakuwa vigumu kuaminika."

The New Geneva Study Bible, uk.1558 inasema kuwa Injili ya Marko ilitakiwa kuwa imeandikwa kabla ya mwaka 70 BK. Hata hivyo, kitabu hiki kinaendelea kusema kuwa kama Luka na Matendo ya Mitume vilikamilika karibu na mwaka 62 BK, basi Injili ya Marko ilikamilika hata kabla ya mwaka 62 BK.

The NIV Study Bible, uk.1490 inasema kuwa inaweza kuwa miaka ya 50 au 60' au muda mfupi tu kabla ya kuteketezwa kwa Yerusalem mwaka 70 BK.

The New International Dictionary of the Bible, uk.622 inasema ilikuwa mwaka 65-70 BK, ingawa baadhi ya watu wenye kushikilia msimamo wa kale wanasema kuwa ni kwenye miaka ya 50.

The Wycliffe Bible Dictionary, uk.1078 inasema kuwa ingawa watafsiri wengi wanasema kuwa Injili ya Marko iliadikwa mwaka 65-70 BK, muda ambao una uwezekano mkubwa zaidi ni mwaka 67-70 BK.

Believer's Bible Commentary, uk.1318 inasema kuwa ingawa baadhi ya watu wanasema kuwa Injili ya Marko ilindikwa mapema zaidi kiasi cha miaka ya 50 BK, miaka ya 57-60 BK inaonekana kuwa na uwezekano mkubwa zaidi.

Dictionary of Jesus and the Gospels, uk.528 inasema kuwa iliandikwa kwenye mwishoni mwa miaka ya 60, kama 68-70 BK.

Mwandishi mwenye kushuku Asimov's Guide to the Bible, uk.903 kinasema Injili ya Marko huenda iliandikwa muda mfupi baada ya mwala 64 BK. Huenda haikuandikwa hadi baada ya mwaka 66 BK, lakini haiwezi kuwa iliandikwa muda mrefu baada ya mwaka 70 BK, akijenga hoja yake kwenye mawazo kuwa Injili za Mathayo na Luka ziliumia taarifa toka kwenye Injili ya Marko.

 

S: Kwenye Marko, tunajuaje kuwa Maandiko leo hii yamehifadhi kwa uaminifu mambo yaliyoandikwa mwanzoni?

J: Kuna sababu nzuri zisizopungua tatu.

1. Mungu aliahidi kulitunza neno lake kwenye Isa 55:10-11; 59:21; 40:6-8; 1 Pet 1:24-25 na Mat 24:35.

2. Ushahidi wa kanisa la awali. Waandishi waliiongelea Injili ya Marko.

1 Clement sura ya 15, uk.9 ananukuu Mak 15:8 na Isa 29:13.

Barua ya Barnaba (mwaka 100-150 BK) sura ya 5, uk.139 inanukuu Mak 2:17b, ambayo pia ni Mat 9:13b na Luk 5:32. (½ nukuu)

Papias (mwaka 130-150 BK) anavitaja kwa majina vitabu vya Marko, Mathayo, Waraka wa Kwanza wa Yohana na Waraka wa Petro. Kipande cha 6 kutoka Eusebius' Ecclesiastical History kitabu cha 3 sura ya 39. Eusebius anaandika na anatilia shaka Waraka wa Pili wa Petro, kwa hiyo Waraka wa Petro hapa unamaanisha Waraka wa Kwanza wa Petro.

Polycarp (karibu mwaka 150 BK) ananukuu nusu ya mstari: Mak 14:38b. Polycarp's Letter to the Philippians, sura ya 7, uk.34-35.

Justin Martyr (karibu mwaka 38-165 BK) ananukuu toka kwenye mistari miwili ya Mak 2:17 na 12:25. Kwenye mistari hii yote anasema kuwa ni maneno ya Mwokozi.

Mzushi Tatian (aliyekufa mwaka 177 BK) aliandika mlinganisho wa Injili nne ulioitwa Diatessaron. Ndani mwake anaongelea mistari 402 ya Injili ya Marko. Hii ni 59% ya Injili yote.

Melito wa Sardis (mwaka 170-180 BK) anazitaja Luka na Marko kama "Injili." Anaitaja 1 Kor kama kitabu kilichoandikwa na mtume. Kuna nukuu toka Waraka wa Waebrania. Oration on the Lord's Passion sura ya 9, uk.760-761.

Mnostia mzushi Ptolemy (kabla ya 188 BK) anaongelea Mak 15:34 kwa nujibu wa Irenaeus.

Irenaeus (mwaka 182-188 BK) ananukuu sehemu zote za mistari 18 kwenye Marko. Kwenye Irenaeus Against Heresies kitabu cha 3 sura ya 10.5, uk.425 anamtaja Marko, mkalimani na mfuasi wa Petro, kwenye masimulizi yake ya Injili, na ananukuu Mak 1:2a. Kwenye sura kumi na mbili za kwanza za Marko, Irenaeus ananukuu au kufafanua Mak 1:1,2,24; 3:27; 4:28; 5:31; 9:23; 10:38; 13:32; 14:21b; 16:19.

Irenaeus anadokezea Mak 6:41,44; 9:2; 10:17; 13:33.

Irenaeus anamwelezea Yesu akitoa mamlaka ya kukanyaga nyoka na nge, ambayo ni nukuu ya Luk 10:19, lakini pia yanaweza kuwa yananukuu Mak 16:17, 18.

The Muratorian Canon (karibu mwaka 170 BK) inaitaja Marko pamoja na Injli nyingine.

Clement wa Alexandria (mwaka 193-217/220 BK) inafafanua Mak 10:17-31 ikisema "Mambo haya yameandikwa kwenye Injili ya Marko" Who is the Rich Man That Shall be Saved? sura ya 5, uk.592.

Tertullian (mwaka 198-220 BK) anasistizia uandishi wa Mathayo, marko, Luka, Yohana, Ufunuo, na nyingi ya Nyaraka za Paulo kwenye Five Books Against Marcion kitabu cha 4 sura ya 5, uk.350.

Hippolytus (mwaka 225-235/6 BK) anaandika, "kwamba si Paulo mtume wala Marko, mmoja wa waliolemazwa kidole, alitaja (mafundisho) kama haya. Kwa kuwa hakuna yeyote kati ya (mafundisho) haya yaliyoandikwa kwenye Injili ya Marko." Refutation of All Heresies book 7 sura ya 18, uk.112. Hippolytus pia ananukuu ½ ya Mak 10:38 Refutation of All Heresies kitabu cha 5 sura ya 3, uk.53.

Hippolytus anaongelea Mat 19:17; Mak 10:18 na Luk 18:19 akisema kuwa "ni maneno ya Mwokozi" kwenye Refutation of All Heresies kitabu cha 5, sura ya 2, uk.50.

Commodianus (mwaka 240 BK) ana mahali pamoja ambapo anadokeza Mak 12:42 naLuk 21:2.

Origen (mwaka 225-254 BK) ananukuu Injili ya Marko mara nyingi sana ikiwa ni pamoja na Mak 1:1-2. Pia ameandika maelezo ya Injili yote y Marko.

Origen anazitaja Injili za Mathayo, Marko, Luka na Yohana. Origen Against Celsus kitabu cha 5 sura ya 56, uk.568. Pia akinukuu Mat 18:1 kwenye Origen's Commentary on Matthew kitabu cha 13 sura ya 14, uk.482.

Anonymous Treatise on Rebaptism (karibu mwaka 250-258 BK) sura ya 17, uk.677 "Pia kwa mujibu wa Marko alisema, kwa lengo lilelile, kwa wana wa Zebedayo." Pia inaitaja Mak 16:8.

Cyprian wa Carthage (mwaka 246-258 BK) "Pia kwa mujibu wa Marko: ‘Dhambi zangu zitasamehewa, na makufuru, kwa wanadamu; lakini yeyote atakaye mkufuru Roho Mtakatifu, haitasamehewa, lakini atahesabiwaa hatia ya dhambi ya milele'" (Mak 3:28-29) Treatises of Cyprian Makala ya 3 sura ya 28, uk.542.

Firmilian wa Caesarea kwa Cyprian (mwaka 256 BK) ananukuu Mak 13:6 kama maneno ya "Bwana mwenyewe" (Barua ya 74 sura ya 9, uk.392).

Dionysius wa Alexandria (mwaka 246-265 BK) "Ilikuwa ‘mwishoni mwa sabato,' kama Mathayo alivyosema; ilikuwa ‘mapema, kungali bado giza,' kama Yohana anvyoandika; ilikuwa ‘asubuhi na mapema,' kama Luka anavyoeleza; na ilikwa ‘asubuhi na mapema, jua lilipokuwa linachomoza,' kama Marko anavyotuambia. Hivyo, hakuna mtu aliyetuonesha muda kamili alipofufuka." Letter 5 to the bishop Basilides, uk.94.

Archelaus (mwaka 262-278 BK) ananukuu Mak 2:9 kama maneno ya Yesu kwenye moja ya hotuba zake kwenye Disputation with Manes sura ya 42, uk.217.

Theonas wa Alexandria (karibu mwaka 300 BK) anaongelea Mak 11:25: "kama mpendavyo kuwa awasamehe dhambi zenu, wasameheni pia dhambi zao;" Letter the Lucianus, the Chief Chamberlain sura ya 9 (juzuu ya 6), uk.160.

Adamantius (karibu mwaka 300 BK) "Je utakubali endapo nitakunyesha kwenye Injili kuwa si uzushi?" . . . "Wanafunzi wa Kristo waliyaandika: Yohana na Mathayo; Marko na Luka. Dialogue on the True Faith Sehemu ya kwanza "b 5" uk.41.

Victorinus of Petau (aliyeuawa mwaka 304 BK) anazitaja Injili za Mathayo, Marko na Luka kwenye Commentary on the Apocalypse of the Blessed John, uk.348.

Methodius (mwaka 260-312 BK) (nusu ya nukuu) ananukuu Mak 11:9b, ambayo pia ni Zab 118:26a; Mat 21:9b; Luk 19:38a na Yoh 12:13b. "Badala ya mavazi yetu, natutapanye mioyo yetu mbele yake. Kwa zaburi na nyimbo, natumwinulie kelele za shukrani; na tuseme bila kukoma, ‘Amebarikiwa Yeye ajaye kwa jina la Bwana'" Oration on the Psalms sura ya 1, uk.394.

Athanasius (karibu mwaka 318 BK) ananukuu sehemu ya Mak 12:29 kama "Bwana na Mwokozi wetu Yesu anasema" kwenye Against the Heathen sura ya 6, uk.7.

Amphilochius anaongelea Injili ya Marko

Lactantius (karibu mwaka 303 hadi karibu mwaka 325 BK) anadokezea Mathayo 14; Marko 6, Luka 9, na Yohana 6 wakati anasimulia tukio la mikate mitano na samaki wawili. The Divine Institutes kitabu cha 4 sura ya 15, uk.115.

Lactantius (karibu mwaka 303 hadi karibu mwaka 325 BK) anadokezea Mathayo 8, Marko 4, na Luka 8 wakati anaposema kuhusu "maandiko matakatifu" yakifundisha kuwa Yesu "aliziamuru pepo kumtii, bahari kumtumikia, magonjwa kuondoka, wafu kunyeyekea." The Divine Institutes kitabu cha 4 sura ya 15, uk.116.

Baada ya baraza la kanisa la Nikea

Eusebius' Ecclesiastical History (mwaka 323-326 BK) kitabu cha 3 sura ya 24, uk.152 kinaelezea Injili nne, Mathayo, Marko, Luka na Yohana. Nicene and Post-Nicene Fathers Second Series juzuu ya 1, uk.152.

Juvencus (mwaka 329 BK) aliandika maelezo ya Injili nne.

Hilary wa Poitiers (kabla ya mwaka 367 BK)

Athanasius (mwaka 367 BK) aliorodhesha vitabu vya Agano Jipya kwenye Festal Letter 39, uk.552.

Basil wa Cappadocia (mwaka 357-378/379 BK)

Ambrosiaster (baada ya 384 BK)

Cyril wa Yerusalem (karibu mwaka 349-386 BK) anaongelea Mak 1:1, 4 kama Injili kwenye Lecture 3.6, uk.15.

Apostolic Constitutions (muda wa kuandikwa kwake hauna uhakika)

Ambrose wa Milan (mwaka 370-390 BK)

Arian mzushi Eunomius wa Cyzicus (karibu mwala 360 hadi karibu mwaka 394 BK) anadokeza Mak 10:18 (Mungu pekee ni mwema) Apologetic Letter sura ya 21, uk.61.

Didymus Kipofu (mwaka 398 BK)

Asterius wa Emesa (karibu mwaka 400 BK)

Severian (aliyevuma mwaka 400-408 BK)

Epiphanius wa Salamis (mwaka 360-403 BK) anaongelea Injili ya Marko. The Panarion sehemu ya 3 sura ya 44, uk.345.

Jerome (mwaka 373-420 BK)

John Chrysostom (aliyeuawa mwaka 406 BK) anaitaja Injili ya Marko kwenye Homily 4, uk.20 (juzuu ya 10).

Chromatius (aliyekufa mwaka 407/407 BK)

Orosius/Hosius of Braga (mwaka 414-418 BK) anadokezea Mat 26:47-50; Mak 14:43-46; Luk 22:47-48; Yoh 18:3-9. Defense Against the Pelagians sura ya 8, uk.124.

John Cassian (mwaka 419-430 BK) Mak 9:23 inasemekana kutoka kwenye Injili kwenye Conference of the Abbot Paphnutius sura ya 16, uk.327.

Augustine wa Hippo (mwaka 354-430 BK)

Marcus wa Eremita (baada ya mwaka 430 BK)

Polychronius wa Apamea (aliyevuma mwaka 428-431 BK) anaongelea Mak 13:2.

Theodoret wa Cyrus, askofu na mwanahistoria (mwaka 423-458 BK)

Hesychius (hadi mwaka 450 BK)

Speculum (karne ya tano)

Nestorius' Bazaar of Heracleides (mwaka 451/452 BK)

Proclus (mwaka 412-485 BK) anaongelea Mak 14:5

3. Hati za kale zaidi tulizokuwa nazo zinaonyesha kuwa kuna tofauti ndogo ya matini na tofauti moja kubwa, lakini hakuna makosa ya msingi ya kitheolojia. Mwisho wa Injili ya Marko ina maandishi yanayopishana kwa kiasi kikubwa zaidi kwenye Agano Jipya lote.

p45 Chester Beatty I, Injili zote nne na Matendo ya Mitume (mwaka100-150 BK) (awali ilidhaniwa kuwa iliandikwa mwishoni mwa karne ya pili au mwanzoni mwa karne ya tatu BK (Mak 4:36-5:2; 5:16-26; 5:38-6:3; barua 2 za 6:15; 6:16-25, 36-50; 7:3-15; 7:25-8:1; 8:10-26; 8:34-9:8; barua 4 za 9:9; 9:18-31; 11:27-12:1; 12:5-8, 13-19, 24-28 [mistari 147]). Nakala hii ilikuwa ni ufafanuzi huru, wakati mwandishi alikuwa anajaribu kuweka wazi maana ya kila msemo. Hati ya kwanza ya kukunja inasemekana kuwa ilikuwa karibu makaratasi 220, kati ya haya tunayo makaratasi 30. Sita kati ya haya yanatoka kwenye Injili ya Marko.

Karne ya tatu - 1968 - The Text of the New Testament

Karne ya tatu - 1975 - Aland na wengine. Toleo la tatu

Karne ya tatu - 1998 - Aland na wengine.

Toleo ta nne

Mwisho wa karne ya pili au mwanzoni mwa karne ya tatu - 1999 - The Complete Text of the Earliest New Testament Manuscripts.

p84 Mak 2:2-5, 8-9; 6:30-31, 33-34; 36-37, 39-41 pia Yoh 5:5; 17:3, 7-8 (karne ya 6)

p88 Mak 2:1-26 (karne ya 4)

Vaticanus [B] (mwaka 325-350 BK), Sinaiticus [Si] (mwaka 340-350 BK), na Alexandrinus [A] (karibu mwaka wa 450 BK) zina Injili yote ya Marko.

Washington Codex (karne ya 4 au 5) ina Injili nzima ya Marko isipokuwa Mak 15:13-38.

Kwenye pano la 7 kule Qumran, Jose O'Callaghan aliyakuta makaratasi ya mafunjo iliyoandikwa mwaka 50 BK, ambayo inaweza kuwa ni vipande vya Injili ya Marko. Hata hivyo, The Expositor's Bible Commentary juzuu ya 8, uk.608 inasema wazo hili "limekataliwa sana na wanazuoni wa Agano Jipya (linganisha na EBC 1:420-421, rejeo la 1). Ushahidi ambao O'Callaghan anauwakilisha haujakamilika kabisa kiasi cha kuweza kuaminiwa."

Carston Thiede anadai kuwa Mak 6:52-53 ilihifadhiwa kwenye pango la 7 kule Qumran kama hati ya kukunja 7Q5. Hata hivyo, jambo hili bado linabishaniwa, huku wengi wa wanazuoni wenye kushika msimamo wa kale wakiwa hawalikubali. Wakati hata wapinzani wake wanadai kuwa 7Q5 inaweza kuwa Mak 6:52-53, kipande hicho kinasumbua sana kukisoma hata wanazuoni walio wengi wanasema kuwa hakuna mtu anayeweza kufanya uamuzi wowote ule iwe kuafiki au kupinga.

Kimisri cha Kibohairi [Boh] karne ya 3 au 4

Kimisri cha Kisahidi [Sah] karne ya 3 au 4

Kiarmenia [Arm] kutoka karne ya 5

Kijojia [Geo] kutoka karne ya 5

Kiethiopia [Eth] kutoka karibu mwaka 500 BK

Kisiria cha Kiharkle [Syr H]

 

Tazama www.BibleQuery.org/mkMss.html kwa maelezo zaidi kuhusu hati za kale zilizo na Injili ya Marko.