Kwa Nini Muhammad Alikuwa na Wake Wengi Sana?


Toleo la Juni 2006

Utangulizi
Wake wa Muhammad
1. Khadija/Khadijah
2. Sauda/Sawda binti Zam'a/Zam'ah
3. 'A'isha
Watumwa wa A'isha
A'isha na Vita vya Ngamia
4. 'Umm Salama
5. Hafsa/Hafsah
6. Zainab/Zaynab binti Jahsh
7. Juwairiya/yya/yah
8. Omm/Umm Habiba
9. Safiya/Safiyya/Saffiya
10. Maimuna/Maymuna binti Harith
11. Fatima/Fatema/Fatimah
Fatima, Binti wa Muhammad ni Tofauti
12. Hend/Hind
13. Sana bint Asma' / al-Nashat
14. Zainab/Zaynab binti Khozayma/Khuzaima
15. Habla?
16. Amtaliki Asma' binti Noman
17. Mariam Mkhufti/Mkristo
18. Rayhana/Raihana/Rayhanah binti Zaid/Zayd
19. Amtaliki Omm/Umm Sharik / Ghaziyyah binti Jabir
20. Maymuna / Maimuna
21. Zainab wa Tatu?
22. Khawla / Khawlah binti al-Hudayl
23. Amtaliki Mulaykah binti Daudi
24. Amtaliki al-Shanba' binti 'Amr
25. Amtaliki al-'Aliyyah
26. Amtalik 'Amrah binti Yazid
27. Amtaliki Mwanamke ambaye Jina Lake Halijatajwa
28. Qutaylah binti Qays (Aliyekufa Mara Moja)
29. Sana binti Sufyan
30. Sharaf binti Khalifah
31. Wanawake wa Mkono wa Kuume wa Muhammad
Muhammad Hakumuoa Mtu Yeyote Tu!
Posa Zilizokataliwa

Utangulizi

Waislam watakwambia kuwa mtu anaweza kuwa na wake hadi wanne kwa mara moja, kulingana na Sura 4:3. Ukweli ni kwamba usemi huo hauwakilishi picha kamili ya jambo hili kwani Muislam anaweza kuwa na vimada wengi tu na anaweza kutembea na "wanawake ambao mkono wake wa kuume unawamiliki" (Sura 23:5-6; 33:50,52; 4:24; Sura 70:29-30). Hata hivyo, Muhammad alinukuu aya kwenye Koran (Sura 33:50) ambayo ilimwepusha yeye binafsi na sharti hili. Kwa nini?
 
'Aisha alisema, "Inaonekana kuwa Bwana wako aliharakisha ili atimize haja yako." Sahih Muslim juzuu ya 2 kitabu cha 8 na.3453-3454 uk.748-749.
 
Kwa upande mwingine, Muislam aliniambia kuwa kila ndoa ilianzishwa kwa sababu za kiubinadamu au ushirikiano. 'Aisha na baadhi ya wake wengine walikuwa mabinti wa machifu wenye nguvu ambao Muhammad alihitaji msaada wao. Wengine walikuwa wajane "waliokuwa wanatunzwa" na Muhammad baada ya waume zao wa awali kufariki. Niliuliza kila ndoa ilikuwa na sababu fulani? Aliponijibu "ndio", ndipo niliposema "vipi kuhusu Safiyah na Zainab binti Jahsh? Kwa kuwa hakufahamu kuhusu hao, baadhi ya Waislam (pamoja na watu wasiokuwa Waislam) wanaweza wasifahamu pia. Kuhusu usahihi wa vyanzo vya taarifa zangu, zinatoka ama kwenye Koran yenyewe ama hadithi zenye kuaminika za Waislam wa Sun.

Wake wa Muhammad

Ifuatayo ni orodha ya wake wa Muhammad iliyoandaliwa na mwanazuoni wa kiislam Ali Dashti. Huenda alitegemea sana orodha ya awali iliyo kwenye historia ya al-Tabari juzuu ya 9 uk.126-241. Ni vema ikafahamika kuwa wanazuoni na Hadithi hawakubaliani kikamilifu juu ya wake wa Muhammad. Kwa mfano, baadhi ya hadithi (mbali ya Bukhari or Sahih Muslim) zinaelezea wake kadhaa wa Muhammad aliowataliki, na hawa hawakuonyeshwa hapa. Hata hivyo, Orodha ya Ali Dashti, ingawa inaweza isikubaliwe kikamilifu kuwa pana kiasi cha kutisha, inaonyesha wengi wa wake wake. Ufuatao ni ushahidi wa mahusiano hayo toka kwenye hadithi usiomtegemea Ali Dashti.
 
1. Khadija/Khadijah binti Khuwailid/Khywaylid - alikufa kwanza
2. Sawda/Sauda binti Zam'a
3. 'Aisha/Aesha/'A'ishah - umri wa miaka 8 hadi 9, mke wa pili
4. Omm/'Umm Salama/Salamah
5. Hafsa/Hafsah
6. Zaynab/Zainab wa Jahsh
7. Jowayriya/Juwairiyya binti Harith
8. Omm Habiba
9. Safiya/Safiyya binti Huyai/Huyayy binti Akhtab
10. Maymuna/Maimuna wa Hareth
11. Fatima/Fatema/Fatimah
12. Hend/Hind
13. Asma wa Saba
14. Zaynab wa Khozayma
15. Habla?
16. Asma owaNoman / binti al-Nu'man
¾ watumwa/vimada ¾
17. Mariam Mkristo/Mkhufti
18. Rayhana/Raihana/Rayhanah binti Zayd/Zaid
¾ mahusiano ambayo hayana uhakika ¾
19. Omm Sharik
20. Maymuna/Maimuna (mjakazi?)
21. Zaynab/Zainab wa tatu?
22. Khawla / Khawlah
¾ Ali Dashti huenda akawa ameacha si chini ya wake tisa.
 
Muhammad alioa wanawake 15 na alikamilisha ndoa kwa tendo la ndoa na wanawake 13 (al-Tabari juzuu ya 9 uk.126-127).
 
Bukhari
juzuu ya 1 kitabu cha 5 sura ya 25 na.282 uk.172-173 ilisema kuwa [wakati fulani] Muhammad alikuwa na wake tisa.

 
Yafuatayo ni maelezo mafupi ya hadithi na wanahistoria wa awali wa kiislam kuhusu wake wa Muhammad.

1. Khadija/Khadijah

(Linatamkwa ka-DI-ja) binti Khuwailid/Khuwaylid Sahih Muslim juzuu ya 4 kitabu cha 29 na.5971-5972 uk.1297 alifariki miaka mitatu kabla Muhammad hajamuoa 'A'isha. Khadija ameelezewa kwenye Bukhari juzuu ya 5 kitabu cha 58 na.164,165 uk.103.
 
Jina kamili la mke wa Muhammad lilikuwa Khadijah, binti wa Khuwaylid mtoto wa Asad bin 'Abd al-'Uzza bin Qusayy. al-Tabari juzuu ya 39 uk.3
 
Muhammad alikuwa na miaka 20 alipomuoa Khadijah, mjane wa al-Tabari juzuu ya 9 uk.127.
 
'Aisha anasema kwamba Khadija alimpeleka Muhammad kwa muumini mpya wa kikristo aliyezoea kusoma vitabu vya injili vya kiarabu. Bukhari juzuu ya 4 kitabu cha 55 sura ya 17 na.605 uk.395.
 
A'isha alikuwa na wivu kwa Khadija. "Katika hilo, Mtume alikumbuka jinsi Khadija alivyokuwa anaomba ruhusa, na kwamba jambo hilo lilikuwa linamuudhi. Alisema, 'O Mungu! Hala!' Kwa hiyo mimi [A'isha] nilikuwa na wivu na alisema, 'Ni kitu gani kinachokufanya umkumbuke mwanamke mzee miongoni mwa wanawake wa Quraish, mwanamke mzee (asiye na memo mdomoni) mwenye fizi nyekundu aliyekufa muda mrefu uliopita, na ambaye badala yake Mungu amekupa mtu mwingine bora kuliko yeye?'" Bukhari juzuu ya 5 kitabu cha 58 na.168 uk.105.

2. Sauda/Sawda binti Zam'a/Zam'ah

Sahih Muslim juzuu ya 2 kitabu cha 8 na.3451 uk.747; Bukhari juzuu ya 3 kitabu cha 34 sura ya 4 na.269 uk.154; juzuu ya 3 na.853 uk.29; Sahih Muslim juzuu ya 2 kitabu cha 7 na.2958 uk.651; Sahih Muslim juzuu ya 2 rejeo chini ya ukurasa 1918 uk.748 inasema kuwa huenda 'Aisha aliolewa na Muhammad kabla ya Sauda, lakini 'Aisha hakuingia kwenye nyumba ya Muhammad mpaka wakati Sauda alipoolewa na Muhammad.
 
Hakuna maafikiano kama Muhammad aliikamilisha ndoa yake na Sauda kwa ngono kwanza na au A'isha, lakini al-Tabari juzuu ya 9 uk.128-129 inasema alikuwa Sauda.
 
Mume wa zamani wa Sauda, al-Sakran bin 'Amr bin 'Abd Shams alikuja kuwa mkristo huko Abyssinia na alifia hukohuko. al-Tabari juzuu ya 9 uk.128
 
Kimwili, 'Aisha alimwita Sauda "mwanamke mnene mkubwa". Bukhari juzuu ya 6 kitabu cha 60 sura ya 241 na.318 uk.300
 
Sauda alipokuwa mzee alioogopa kuwa Muhammad atamtaliki, kwa hiyo alitoa zamu yake kwa 'A'isha. Abu Dawud juzuu ya 2 na.2130 uk.572
 
Sauda ameelezewa pia kwenye al-Tabari juzuu ya 39 uk.169.

3. 'A'isha

A'isha alikuwa binti wa Abu Bakr. Mama yake aliitwa Umm Ruman kwa mujibu wa al-Tabari juzuu ya 9 uk. 129. Aliolewa na Muhammad alipokuwa na miaka sita (6) na alikwenda kwenye nyumba yake [Muhammad] akiwa na miaka tisa (9). Bukhari juzuu ya 7 kitabu cha 62 sura ya 60 na.88 uk.65; Sahih Muslim juzuu ya 2 kitabu cha 8 na.3309, 3310, 3311 uk.715, 716.
 
Kinyume na ndoa yake kuwa muhimu kwa sababu za kisiasa, Abu Bakr alikuwa mtu wa kwanza kubadili dini na kuwa muislam.
 
Mke huyu wa Muhammad ameelezwa sehemu mbalimbali, ikiwa ni pamoja na Sahih Muslim juzuu ya 1 kitabu cha 4 na.1694 uk.372; Abu Dawud juzuu ya 1 na.1176 uk.305; juzuu ya 1 na.1268 uk.335; juzuu ya 1 na.1330 uk.350; Abu Dawud juzuu ya 1 na.1336 uk.351; juzuu ya 1 na.1419 uk.373; juzuu ya 2 na.2382 uk.654.
 
'Aisha alichezea wanasesele mbele ya Muhammad. Sahih Muslim juzuu ya 4 kitabu cha 29 na.5981 uk.1299.

'Aisha alikuwa na miaka sita (6) alipoolewa, na ndoa yake ilikamilishwa kwa ngono alipokuwa na miaka tisa (9). al-Tabari juzuu ya 9 uk.130, 131.
 
A'isha alikuwa na miaka sita (6) alipoolewa na miaka tisa (9) alipoenda kwenye nyumba ya Muhammad. Ibn-i-Majah juzuu ya 3 na.1876 uk.133.
 
A'isha alikuwa na miaka saba alipoolewa, miaka tisa alipoanza kuishi na Muhammad, na miaka kumi na nane alipokufa. (siyo Sahih) Ibn-i-Majah juzuu ya 3 na.1877 uk.134.
 
Mantiki ya kujaribu kueleza kwa nini Muhammad alimwoa msichana mdogo kiasi hicho imo kwenye Sahih Muslim juzuu ya 2 rejeo chini ya ukurasa 1859 uk.715. Linasema kwamba "Ilikuwa ni mazingira pekee hata Hadrat 'A'isha aliolewa na Nabii. Jambo la pili kuangalia ni kwamba uislam haujaweka kizuizi cha umri wa kubarehe kwa sababu unatofautiana baina ya nchi na rangi ya ngozi tokana na hali ya hewa, urithi, hali za kimwili na kijamii." Pia wanaeleza kuungwa kwao mkono na ripoti isiyoaminika ya Kinsey inayohusu Tabia za Kingono kwa Wanawake.
 

Muhammad mwenyewe alimgonga 'Aisha kwa kukusudia "kwenye kifua kitu ambacho kilimsababishia maumivu", kwa mujibu wa Sahih Muslim juzuu ya 2 kitabu cha 4 sura ya 352 na.2127 uk.462.

 
Paliluwa na kutoelewana pia. Tukio moja, lililoanzishwa na A'isha lilikuwa baya sana, Muhammad alijitenga na wake zake kwa muda wa mwezi mmoja na siku 29. Ibn-i-Majah juzuu ya 3 na.2060 uk.241. Ibn-i-Majah juzuu ya 3 na.2063 uk.243. Haya ni mandhari ya Sura 50:1.

Watumwa wa A'isha

'A'isha alikuwa na angalau mtumwa mmoja aliyekuwa anampikia wakati wa uwakilishi kutoka Banu'l Muntafiq. Abu Dawud juzuu ya 1 na.142 uk.34.

A'isha alikuwa na mtumwa mwanaume muislam aliyeitwa Abu Yunus ambaye alimwacha huru baadaye. Sunan Nasa'i juzuu ya 1 uk.475 uk.340.
 
A'isha alikuwa na mjakazi. Abu Dawud juzuu ya 1 na.371 uk.96.
 
Barirah alikuwa mjakazi wa A'isha ambaye baadaye aliachiwa huru. Abu Dawud juzuu ya 2 na.2223 na rejeo chini ya ukurasa 1548 uk.601.
 
A'isha alikuwa mwepesi wa hasira pia, aligonganisha mikono ya mtumwa wake na kuvunja bakuli la chakula toka kwa mke mwingine wa Muhammad. Abu Dawud juzuu ya.2 na.3560-3561 uk.1011.
 
'A'isha alikuwa na sauti nzito na kubwa. al-Tabari juzuu ya 17 uk.65.
 
'Aisha aliwaacha huru watumwa wengi kwa shingo upande tokana na kuvunja kiapo. " [Ibn Az-Subair] alimtumia ['Aisha] watumwa kumi ambao aliwaacha huru kama fidia ya ya (kutotimiza) kiapo chake. 'Aisha aliwaacha huru watumwa wengine kumi zaidi kwa sababu hiyo hiyo mpaka aliwaweka huru watumwa arobaini. Alisema, "Ningejua ningesema bayana kitu cha kufanya endapo ningeshindwa kutimiza kiapo changu wakati nilipokuwa naapa, ili kwamba niweze kukitimiza kiurahisi." (1) Rejeo chini ya ukurasa (1) linasema "'Aisha hakuwa amesema kitu cha kufanya endapo asingetimiza ahadi yake, hii ndio sababu aliwaachia huru watumwa wengi sana ili aweze kujifurahisha kwa utoshelevu wa fidia yake." Bukhari juzuu ya 4 kitabu cha 56 sura ya 2 na.708 uk.465.
 
Je 'Aisha alikuwa na watumwa wangapi? Au alikuwa na hela kiasi gani hata aweze kununua watumwa arobaini? Hadithi hazisemi kitu. Madokezo pekee mawili niliyoyapata ni:
1) Wake wa Muhammad walikuwa na uwezo wa kuamuru mahema yafungwe. Ibn-i-Majah juzuu ya 3 na.1771 uk.67.
2) Sehemu moja ya tano ya nyara zilikwenda kwenye hazina ya kiislam, na Muhammad alikuwa na uwezo wa kucuhukua toka humo kwa ajili yake yeye mwenyewe na wake zake. Sahih Muslim juzuu ya 2 na.2347, 2348; juzuu ya 2 rejeo chini ya ukurasa 1463 uk.519; Bukhari juzuu ya 4 kitabu cha 51 sura ya 80 na.153 uk.99; juzuu ya 6 kitabu cha 60 sura ya 297 na.407 uk.379.

A'isha na Vita vya Ngamia

Mwanzoni, 'Aisha aliwaunga mkono watu waliokuwa wanataka kumuua 'Uthman. Alidai kuwa 'Uthman ameacha kuwa muumini. Hata hivyo, baada ya mauaji ya 'Uthman alibadilisha mawazo yake na kutaka kulipiza kisasi kwa wauaji wa 'Uthman.' Muislam mwingine alimuwajibisha kwa ajili ya jambo hilo. al-Tabari juzuu ya 17 uk.52-53.
 
Baada ya hapo, Mu'awiyah alimsababisha Muhammad bin Abu Bakr auawe kwa kumuua 'Uthman, kisha aliweka mwili wake kwenye mzoga wa punda, na kisha akamchoma punda mwaka wa 38 baada ya Hija (A.H). A'isha ailomwombolezea sana kaka yake wa kambo na kumfanyia maombi ya ziada al-Tabari juzuu ya 17 uk.158.

4. 'Umm Salama

'Umm Salama binti Abi Umayyah (akiongelea mambo ya mapenzi na mtume) Sahih Muslim juzuu ya 2 na.2455 uk.540.
 
Jina halisi la Umm Salamah lilikuwa Hind binti Abi Umayyah bin al-Mughirah bin 'Abdallah bin 'Umar bin Makhzum. al-Tabari juzuu ya 9; uk.133; juzuu ya 39 uk.175.
 
Um/Umm Salaim/Salama (ambaye haelezwi kuwa mkewe) Sahih Muslim juzuu ya 2 na.2992 uk.656; juzuu ya 2 na.3445 uk.746; mke Bukhari juzuu ya 4 kitabu cha 53 sura ya 4 na.333 uk.216; Bukhari juzuu ya 7 kitabu cha 62 sura ya 34 na.56 uk.40. Ibn-i-Majah juzuu ya 2 na.1634 uk.473; Abu Dawud juzuu ya 1 na.383 uk.99. Muhammad alimuoa Umm Salama, mjane wa Abu Salama (aliyefia Abyssinia mwaka wa 4 A.H.) Al-Tabari juzuu ya 39 uk.175. Umm Salama alikufa mwaka 59 A. H. alipokuwa na miaka 84. Sahih Muslim juzuu ya 2 rejeo chini ya ukurasa 1218 uk.435. Umm Salama alikuwa mjamzito alipoolewa na Muhammad, na binti yake alikuwa Zainab binti Abu Salama (Sahih Muslim juzuu ya 2 na. 3539-3544 uk.776-777. (Huyu ni binti yule yule Zainab binti Umm Salama)
 
Mke huyu wa Muhammad ameelezewa kwenye Abu Dawud juzuu ya 1 na.274 uk.68; juzuu ya 3 na.4742 uk.1332; juzuu ya 2 na.2382 uk.654; Sunan Nasa'i juzuu ya 1 na.240 uk.228; Ibn-i-Majah juzuu ya 3 na.1779 uk.72; al-Tabari juzuu ya 17 uk.207; al-Tabari juzuu ya 39 uk.80.
 
'Umm Salamah alikuwa na mtoto wa kiume kabla hajaolewa na Muhammad. Mtoto wake alikwenda na A'isha, al-Zubayr, na Talhah. al-Tabari juzuu ya 17 uk.42.
 
Wateja wa Umm Salamah walikuwa Nabhan (=Abu Yahya) na Ma'in bin Ujayl(=Abu Qudamah) al-Tabari juzuu ya 39 uk.320.

5. Hafsa/Hafsah

Binti wa 'Umar bin Khattab ameelezewa kwenye Sahih Muslim juzuu ya 2 na.2642 uk.576; juzuu ya 2 na.2833 uk.625; juzuu ya 2 na.3497 uk.761; Abu Dawud juzuu ya 2 na.2448 uk.675; juzuu ya 3 na.5027 uk.1402. Alikuwa binti wa 'Umar bin al-Khattab. Alikuwa mjane wa miaka 18 wa Khunais alipoolewa na Muhammad mwaka 625 B.K. Alizaliwa mwaka 607 B.K., na alikufa ama mwaka 647/648, 661/662, au 665 B.K. Pia ameelezewa kuwa mke kwenye Ibn-i-Majah juzuu ya 3 na.2086 uk.258.
 
Baada ya mume wa Hafsa kufa tokana na majeraha akiyoyapata Uhud, baba wa Hafsa alifikiri kuwa angeolewa na 'Uthman, lakini 'Uthman alikataa kwa sababu alijua kuwa Muhammad alitaka kumuoa. Walioana mwaka wa 3 A.H. Alikuwa na miaka mine zaidi ya 'A'isha. Sunan Nasa'i juzuu ya 1 na. 32 uk.117. Kwa hiyo Muhammad hakumuoa ili ampatie mahitaji yake. Badala yake alimwoa mtu ambaye angeweza kuolewa na mtu mwingine.
 
Kutopatana: 'Umar alimwambia binti yake Hafsa kutokupotoshwa na 'Aisha ambaye alikuwa anajivunia uzuri wake na upendo ambao Muhammad alikuwa nao kwake. Bukhari juzuu ya 7 kitabu cha 62 sura ya 106 na.145 uk.108. Hafsa alimwambia 'Aisha "Sijawahi kupata kitu chochote kizuri toka kwako!" Bukhari juzuu 9 kitabu cha 92 sura 5 na.406 uk.299-300.
 
'Umar alimwambia Muhammad alimtaliki Hafsah (talaka rejea) na kisha akamrudisha tena. Abu Dawud juzuu ya 2 na.2276 uk.619. Kwa mujibu wa Ibn Ishaq, Muhammad alimtaliki Hafsa lakini kisha akamrejesha tena. al-Tabari juzuu ya 9 rejeo chini ya ukurasa 884 uk.131.
 
"Yahya ... kutoka Malik kutoka kwa Muhammad ibn Abd ar-Rahman ...kwamba alisikia kuwa Hafsa ... alimuua mmoja wa wajakazi wake aliyewahi kutumia uchawi dhidi yake. Alikuwa mudabbara. Hafsa alitoa amri, na aliuawa." Muwatta Malik 42.19.14.
 
Hafsa, mke wa Muhammad, alikufa akiwa na miaka 60. al-Tabari juzuu ya 39 uk.174.

6. Zainab/Zaynab binti Jahsh

Sahih Muslim juzuu ya 2 na.2347 uk.519; juzuu ya 2 na.3330 uk.723,724; juzuu ya 2 na.3332 uk.725; juzuu ya 2 na.3494 uk.760. Bukhari juzuu ya 3 kitabu cha 33 sura ya 6 na.249 uk.138; juzuu ya 3 na.829 uk.512; juzuu ya 4 na.6883 uk.1493; Jina la awali la Zainab lilikuwa "Barrah", lakini Muhammad alilibadilisha kuwa Zainab Bukhari juzuu ya 8 kitabu cha 72 sura ya 108 na.212 uk.137; Abu Dawud juzuu ya 3 na.4935 uk.1377-1378. Abu Dawud juzuu ya 1 na.1498 inasema jina la Juwairyiha lilikuwa Barrah.
 
Sura 33:36-38 kwenye Koran inasema, "Si kwa muumini yoyote, mwanaume au mwanamke, wakati Mungu na Mjumbe wake wanapopanga jambo, kufanya uchaguzi kuhusiana na jambo. Mtu yoyote anayekosa kumtii Mungu na Mjumbe wake anakuwa amepotoka na kwenda kwenye makosa dhahiri. Ulipomwambia huyu ambaye Mungu amembariki na wewe umependelea kwamba, 'Baki na mke wako, na mche Mungu', na ulikuwa unaficha kitu ambacho Mungu angekiweka wazi, kwa ajili ya kuhofia watu wengine; na Mungu ana haki zaidi ya kuabudiwa na wewe. Kwa hiyo Zaid alipokamilisha kile alichokitaka kwake [Zainab], ndipo tulipomtoa aolewe na wewe, ili kwamba kusiwe na kosa lolote miongoni mwa waumini, kugusa wake wa watoto wao waliowaasili, wanapokuwa wamekamilisha yale ambayo walipenda kuyafanya kwao; na amri ya Mungu lazima itimizwe. Hakuna makosa kwa upande wa nabii, kugusa kitu ambacho Mungu amemweka tokea mwanzo."
 
Zainab binti Jahsh alikuwa ametolewa na mtoto wa kuasiliwa wa Muhammad, mpaka wakati Muhammad alipoisema Sura kwamba Zainab anatakiwa amtaliki mtoto wa Muhammad na kuolewa naye [Muhammad]. Zainab "alikuwa anawaringia wake wengine wa Nabii na alikuwa anasema, 'Mungu ameniozesha (kwa Nabii) mbinguni.'" Bukhari juzuu ya 9 kitabu cha 93 sura ya 22 na.517 uk.382. Pia juzuu ya 9 kitabu cha 92 sura ya 22 na.516, 518 uk.381-383; al-Tabari juzuu ya 9 uk.133. Kwa maneno mengine, kwa mujibu wa Koran ya milele isiyoumbwa mbinguni, ndoa ya Zainab ilielezewa.
 
Zainab wa Jahsh alikuwa na kaka aliyekufa kabla yake. Abu Dawud juzuu ya 2 na.2292 uk.624.
 
Usemi unaodaiwa kuwa Zaid alimtaliki mke wake Zainab kwanza ili kwamba Muhammad aweze kumuoa. al-Tabari juzuu ya 39 uk.180-182.
 
Zainab binti Jahsh alifariki alipokuwa na miaka 53. al-Tabari juzuu ya 39 uk.182.
 
Zainab (bila kubainishwa) Sahih Muslim juzuu ya 2 na.2641, 2642 uk.575, 576.
 
Zainab binti Jahsh asichanganywe na Zainab aliyekuwa mke wa Abu Sa'id al-Khudri. Ibn-i-Majah juzuu ya 3 na.2031 uk.223.
 
Zainab alimtukana A'ishah, kwa hiyo Muhammad akamwabia A'ishah amtukane. "...Mtume wa Mungu (amani na iwe kwake) alikuja kwangu [A'ishah] wakati Zainab binti wa Jahsh akiwa nasi. [Mtume] alianza kufanya kitu kwa mkono wake. Nilimwashiria hata akaelewa kuwa ni kuhusu Zainab. Kwa hiyo akaacha. Zainab akaja na kuanza kumtukana 'A'ishah. 'A'ishah alimzuia lakini hakuacha. Kwa hiyo (Nabii) akamwambia 'A'ishah: Mtukane. Kisha 'A'ishah akamtukana na kumtawala. Ndipo Zainab alipoenda kwa 'Ali na kusema: 'A'ishah amekutukana na kufanya (hiki na kile). Kisha Fatimah akaja (kwa Nabii) na akamwambia: Yeye ni kipenzi cha baba yako, kwa Bwana wa Ka'bah! Kisha akarudi na akawaambia: Nimwambie hivi na hivi, naye ameniambia hivi na hivi. Kisha 'Ali alikuja kwa Nabii (amani na iwe kwake) na kumweleza kuhusu jambo hilo." Abu Dawud juzuu ya 3 na.4880 uk.1364-1365.
 
Kwenye Biblia, Malaki sura ya 2 msitari wa 16 Mungu anasema kuwa anachukia talaka.

7. Juwairiya/yya/yah

Juwairiya binti Harith/al-Harith alikuwa mateka. Bukhari juzuu ya 3 kitabu cha 46 sura ya 13 na.717 uk.431-432. Sahih Muslim juzuu ya 2 na.2349 uk.520 inasema kuwa Muhammad alilivamia kabila la Bani Mustaliq bila onyo lolote walipokuwa wanachunga mifugo yao kizembe. Juwairiya alikuwa binti wa chifu. Sahih Muslim juzuu ya 3 na.4292 uk.942 na Abu Dawud juzuu ya 2 na.227 uk.728 na al-Tabari juzuu ya 39 uk.182-183 pia zinasema kuwa Juwairiya/Juwairiyyah alitekwa kwenye uvamizi wa kabila la Banu Mustaliq. Alikuwa ameolewa na Musafi' bin Safwan, ambaye aliuawa kwenye mapambano.
 
Jawairyiyah, mke wa Muhammad, alikuwa anaitwa Barrah. Abu Dawud juzuu ya 1 na.1498 uk.392. Hata hivyo, Bukhari juzuu ya 8 kitabu cha 72 sura ya 107 na.212 uk.137; Abu Dawud juzuu ya 3 na.4935 uk.1377-1378 inasema jina la Zainab lilikuwa Barrah.
 
Juwayriyyah binti al-Harith bin Abi Birar bin Habib, kitukuu wa Jadhimah al-Mustaliq wa kundi la Khuza'ah, alitekwa wakati waislam walipovamia kabila la al-Mustaliq. Mume wake, Musafi' bin Safwan Dhu al-Shuir bin Abi Asrb bin Malik bin Jadhimah aliuawa kwenye mapambano. Alikuwa mfungwa wa kivita aliyekubali kuolewa na Muhammad. al-Tabari juzuu ya 39 uk.182-183; al-Tabari juzuu ya 9 uk.133.
 
Juwayriyyah alitekwa nyara kwenye mapambano ya al-Muraysi [dhidi ya Banu Mustaliq]. al-Tabari juzuu ya 39 uk.183.
 
Juwayriyya aliolew na Muhammad alipokuwa na miaka 20. al-Tabari juzuu ya 39 uk.184.

8. Omm/Umm Habiba

Umm Habiba alikwa binti wa Abu Sufyan al-Tabari juzuu ya 9 uk.133; Sahih Muslim juzuu ya 2 na.3413 uk.739; juzuu ya 2 na.2963 uk.652; Sahih Muslim juzuu ya 2 na.1581 uk.352; juzuu ya 2 na.3539 uk.776 Ibn-i-Majah juzuu ya 5 na.3974 uk.302; al-Tabari juzuu ya17 uk.88.
 
Umm Habiba alikuwa mdogo kwa Muhammad kwa miaka 23. Sunan Nasa'i juzuu ya 1 #60 uk.127.
 
Umm Habiba na mume wake wa kwanza 'Ubaydallah walikuwa waislam waliokwenda Abyssinia. 'Ubaydallah alibadili dini na kuwa mkristo. al-Tabari juzuu ya 39 uk.177
Anamwelezea Zainab binti Jahsh. al-Tabari juzuu ya 39 uk.180-182.
 
Umm Habiba, mke wa Muhammad asichanganywe na mwanamke mwingine ambaye naye pia aliitwa Umm Habiba. Alikuwwa binti wa Jahsh, mke wa 'Abd al-Rahman na shemeji wa Muhammad, kwani Zainab wa Jahsh alikuwa mke wake. Abu Dawud juzuu ya 1 na.288 uk.73.

9. Safiya/Safiyya/Saffiya

Safiya binti Huyai/Huyayy alikuwa mateka aliyeolewa na Muhammad baada ya kuwauwa baba, kaka na mume wake na watu pale Khaibar, kwa mujibu wa Bukhari juzuu ya 2 kitabu cha 14 sura ya 5 na. 68 uk.35; juzuu ya 4 kitabu cha 52 sura ya 74 na.143 uk.92; juzuu ya 4 kitabu cha 52 sura ya 168 na.280 uk.175 na al-Tabari juzuu ya 39 uk.185.

Mume wa Safiyah aliitwa Sallam bin Mishkam bin al-Hakam bin Harithah bin al-Khazraj bin Ka'b bin Khazraj. al-Tabari juzuu ya 9 uk.134-135.
 
Safiyyah aliitwa Safi, kwa sababu mgao wa kwanza wa mateka uliokwenda kwa Muhammad. Abu Dawud juzuu ya 2 na.2988 uk.848; Abu Dawud juzuu ya 2 na.2985-2989 na rejeo chini ya ukurasa 2406 uk.846-849.
 
Safiyya alinunuliwa na Muhammad kwa bei ya watumwa saba. Ibn-i-Majah juzuu ya 3 na.2272 uk.357. Alikuwa na miaka 17 alipoolewa na Muhammad. al-Tabari juzuu ya 39 uk.184.
 
Muhammad alimhurumia Safiyya. "Kama Safiyyah asingeomboleza, ningemwacha [mume wake ambaye Muhammad alimuua] hadi ndege na wanyama wakali wangemla, na angefufuka toka katika matumbo yao." Abu Dawud juzuu ya 2 na.3130-3131 uk.893.
 
Kiumbo, Safiyyah alikuwa mfupi. Abu Dawud juzuu ya 3 na.4857 uk.1359.
 
Kulikuwa na kutokuelewana miongoni mwa wake. Zainab hakupenda kumwazimisha Safiyya ngamia Muhammad alipomwomba afanye hivyo. Zainab alimwita Safiyya "Mwanamke wa Kiyahudi" Abu Dawud juzuu ya 3 na.4588 uk.1293.
 
Wakati Fulani Muhammad alikuwa na wake tisa, akiwemo Safiyya binti Huyayy, na baadaye hakumpa "zamu." Sahih Muslim juzuu ya 2 na.3455-3456 uk.749.
 
Mke huyu wa Muhammad ameelezewa pia kwenye Sahih Muslim juzuu ya 2 na.3325; juzuu ya 2 na.2783 uk.605; juzuu ya 2 na.3118 uk.678; juzuu ya 2 na.3497 uk.761; Bukhari juzuu ya 3 kitabu cha 33 sura ya 8-13 na.251-255 uk.139-143; juzuu ya 2 kitabu cha 21 sura ya 22 na.255 uk.143; Ibn-i-Majah juzuu ya 3 na.1779 uk.72; Abu Dawud juzuu ya 2 na.2464 uk.681; al-Tabari juzuu ya 39 uk.169.
 
Safiya binti Abi 'Ubaid mke wa Muhammad kwenye Bukhari juzuu ya 4 kitabu cha 52 sura ya 136 na.244 uk.151 anaweza kuwa ni mtu yule yule.

10. Maimuna/Maymuna bint Harith

Sahih Muslim juzuu ya 1 na.1671, 1674, 1675 uk.368-369; juzuu ya 2 na.1672 uk.369.
 
Muhammad alimwoa Maymunah binti Al-Harith mwaka wa 7 A.H. wakati Muhammad alipokuwa kwenye hali ya utakaso wa kidini akielekea Maka. al-Tabari juzuu ya 8 uk.136; al-Tabari juzuu ya 9 uk.135
 
Maymuna alikuwa ameachika mara moja na kufiwa kabla ya kuolewa na Muhammad. al-Tabari juzuu ya 39 uk.185. Maymuna alikuwa na miaka 80/81 alipokufa . al-Tabari juzuu ya 39 uk.186.
 
Maimuna alikuwa na miaka 30 alipoolewa na Muhammad mwenye miaka 53. Muhammad alikufa miaka mine baadaye. Sunan Nasa'i juzuu ya 1 #43 uk.120.
 
Maimuna, mke wa Muhammad, alimsitiri Muhammad Bukhari juzuu ya 1 kitabu cha 5 sura ya 22 na.279 uk.170-171. Watu walisitiriwa walipokuwa wanaoga au wanaenda haja. Jambo hili halikuwa baya kwa sababu alikuwa mke wake.
 
'Ata bin Yasar alikuwa mteja wa Maymunah. al-Tabari juzuu ya 39 uk.317.
 
Watumwa:
Mjakazi wa Maimuna aliewekwa huru alipewa kondoo ambaye baadaye alikufa. Ibn-i-Majah juzuu ya 5 na.3610 uk.93.
 
Mke huyu pia ameelezewa kwenye Ibn-i-Majah juzuu ya 3 na.2408 uk.435; Sunan Nasa'i juzuu ya 1 na.809 uk.492; juzuu ya 2 na.1124 uk.108; Abu Dawud juzuu ya 1 na.1351 uk.356; juzuu ya 1 na.1359, 1360, 1362 uk..357; Sunan Nasa'i juzuu ya 1 na.243 uk.229.

11. Fatima/Fatema/Fatimah

Fatima alielezewa na 'Ali Dashti. al-Tabari juzuu ya 9 uk.39 inasema kuwa Muhammad alomwoa kwa muda mfupi Fatimah binti al-Dahhak bin Sufyan (pia anaitwa al-Kilabiyyah).
 
Muhammad alimwoa Fatimah binti Shurayh/Sara'. al-Tabari juzuu 9 uk.139. Haieleweki endapo Shuray na al-Dahhak walikuwa watu wawili tofauti, jambo linalofanya kuwa na kina Fatima wawili, au yalikuwa majina tofauti kwa baba huyo huyo mmoja.
 
Kuelezwa kwa Fatimah bin al-Dahhabi, Aliya binti Zahyah, Sana binti Sufyan al-Tabari juzuu ya 39 uk.186. Muhammad alikamilisha ndoa yake kwa tendo la ndoa na "Kilabiyyah". Huyu atakuwa Fatimah binti al-Dahhak bin Sufyan aur 'Aliyah binti Zabyan bin 'Amr bin 'Awf au Sana binti Sufyan bin 'Awf. al-Tabari juzuu ya 39 uk.187.

Fatima, binti wa Muhammad ni tofauti

Mwanamke afuataye angeweza kuwa mke wa Muhammad lakini yaelekea alikuwa binti yake. Katika mwaka wa kuiteka Maka, Fatima alimsitiri Muhammad. Ibn-i-Majah juzuu ya 1 na.465 uk.255 na Sunan Nasa'i juzuu ya 1 na.228 uk.224; juzuu ya 1 noa417 uk.307.
 
Fatima alimsitiri Muhammad wakati Nabii alipokuwa anaoga kwenye Bukhari juzuu ya 1 kitabu cha 5 sura ya 22 na.278 uk.170-171. Hata hivyo, Muhammad alikuwa anaoga na alisitiriwa na binti yake kwenye Bukhari juzuu ya 4 kitabu cha 53 sura ya 29 na.396 p.263. Fatima alikuwa binti wa Muhammad na mke wa 'Ali kwenye Bukhari juzuu ya 3 kitabu 34 sura ya 29 na.302 uk.171; Bukhari juzuu ya 4 kitabu cha 53 sura ya 1 na.325 uk.208.
 
Muhammad hakupenda 'Ali amuoe mtu mwingine yeyote isipokuwa binti yake Fatima. Ibn-i-Majah juzuu ya 3 na.1998-1999 uk.202-204. Hata hivyo, 'Ali baadaye alikuwa na mjakazi, binti wa Rab'iah, ambaye alimzalia binti aliyeitwa Umm Ruqayyah. al-Tabari juzuu ya 11 uk.66.
 
Mtumwa aliyetakiwa:
Wakati Muhammad alipompa A'isha watumwa wengi, Fatima alifikiri kuwa hakupat mgao mzuri. Fatima, binti wa Muhammad alilalamika kwa Muhammad kuhusu kutumia jiwe la kusagia na aliomba kupewa mtumwa (mfungwa wa vita). Muhammad hakumpa hilo bali alisema kuwa alimpa kitu kingine kizuri zaidi. Alimwambia aseme utukufu kwa Mungu mara 33, sifa kwa Mungu mara 34, na Mungu ni mkubwa zaidi mara 34. Abu Dawud juzuu ya 3 na.5044-5045 uk.1405.

12. Hend/Hind

Hend/Hind alikuwa ameolewa na Abu Sufyan, ambaye alikuwa ni mtu mchoyo sana, kwa mujibu wa Sahih Muslim juzuu ya 3 na.4251-4254 uk.928-929.

13. Sana bint Asma' / al-Nashat

Muhammad alimwoa al-Nashat bint Rifa'ah wa Banu Kilab bin Rabi'ah, washirika wa Qurayzah. Watu wengine wa walipaita hapa Sana binti Asma' bin al-Salt al-Sulamiyyah; wakati wengine wanasema Sana bint Asma' bin al-Salt wa Banu Harm. Hata hivyo, al-Nashat alikufa kabla Mtume hajakamilisha ndoa naye kwa tendo la ndoa. Jina linguine la al-Nashat lilikuwa Sana. al-Tabari juzuu ya 9 uk.135-136. al-Tabari juzuu ya 39 uk.166 inasema kitu hicho hicho kuhusu Sana binti al-Salt.

14. Zainab/Zaynab binti Khozayma/Khuzaima

Zainab alikuwa mwanamke wa kabila la Banu Hilal. Alikuwa ametalikiwa na Muislam aliyeitwa Tufayl, kisha akaolewa na kaka yake 'Ubaydah, ambaye aliuawa huko Badr. Baadaye aliolewa na Muhammad. Alizaliwa mwaka 595 BK na kufa mwaka 626 BK akiwa na miaka 31. Tazama al-Tabari juzuu ya 7 uk.150 marejeo chini ya ukurasa 215, 216 na al-Tabari juzuu ya 39 uk.163-164 kwa habari zaidi.
 
al-Tabari
juzuu ya 9 uk.138 pia inasema alikufa Muhammad akiwa hai.
 
Muhammad alimwoa Zainab binti Khuzaima, lakini alikufa kabla ya Mtume. Sunan Nasa'i juzuu ya 1 #64 uk.129.

15. Habla?

Habla yumo kwenye orodha ya Ali Dashti's, lakini sijaweza kuthibitisha jambo hili kwa kutumia vyanzo vingine.

16. Alimtalik Asma' binti Noman

Asma binti Noman, au Asma binti al-Nu'man bin Abi Al-Jawn, wa kabila la Kindah, aliolewa na Muhammad, lakini ndoa hii haikukamilishwa na tendo la ndoa. al-Tabari juzuu ya 10 uk.185 na rejeo chini ya ukurasa 1131 uk.185.
 
Binti wa Al-Jaun/Jahal aliolewa na Muhammad kwa muda mfupi sana. Bukhari juzuu ya 7 kitabu cha 63 na.181 uk.131, 132.
 
Kwa upande mwingine, al-Tabari juzuu ya 10 uk.190 anasema kuwa Al-Nu'man al-Jawn alimpa Muhammad binti yake, lakini Muhammad alimkataa. Neno "alikataa" huenda likawa linamaanisha kuwa alimtaliki kabla ya kulala naye.
 
Muhammad alimwoa Asma binti al-Nu'man bin al-Aswad bin Sharahil. Hata hivyo, alikuwa na ukoma na kumfanya Muhammad ampe hela na kumtaliki. al-Tabari juzuu ya 9 uk.137. Kwa nini alimfanyia namna hiyo mwanamke aliyempenda?
 
'Asma binti al-Nu'man alikuwa mjane aliyeolewa na Muhammad. Ama Hafsa au A'isha alimhadaa 'Asma kwa kumwambia Muhammad angefurahi endao angekimbilia kwa Mungu toka kwa Muhammad. al-Tabari juzuu ya 39 uk.188-190.
 
Maelezo mafupi ya 'Asma binti Nu'man kwenye al-Tabari juzuu ya 39 uk.190.
 
Muhammad alimtaliki mwanamke mmoja kwa sababu alikimbilia kwa Mungu toka kwa Muhammad. Alimtaliki mwingine kwa sababu alikuwa na ukoma. Kuna mchanganyiko wa jina lipi linahusika na kisa kipi kwenye al-Tabari juzuu ya 39 uk.187.

17. Mariam/Mariya Mkhufti/Mkristo

Mariam alikuwa mke [kimada] wa Muhammad kwa mujibu wa al-Tabari juzuu ya 9 uk.141; Sahih Muslim juzuu ya 4 rejeo chini ya ukurasa 2835. uk.1351; Maiam Mkhufti alimzalia Ibrahim mtoto wa Muhammad kwenye al-Tabari juzuu ya 9 uk.39. Alikufa alipokuwa na miaka miwili. Mjumbe wa kiislam Hatib bin Abi Balta'ah alirudi toka al-Muqawqis [Misri] na Mariam [Mariam Mkhufti], dada yake Sirin, nyumbu jike, seti ya nguo, na towashi. Hatib aliwaalika kuwa waislam, na wanawake hawa wawili walifanya hivyo [kwa mujibu wa Tabari]. Mariam alikuwa mzuri, na Muhammad alimtuma dada yake Sirin kwa Hassan bin Thabit. Sirin na Hassan walikuwa wazazi wa 'Abd al-Rahman bin Hassan. al-Tabari juzuu ya 8 uk.66,131.
 
Muislam anaweza kusema kuwa Muhammad alilazimika kumuoa kwa sababu alikuwa ni zawadi kutoka Misri, lakini dada yake Sirin alikuwa ni zawadi pia, na hakumuoa. Mariam alikuwa ni zawadi toka kwa gavana wa Alexandria. al-Tabari juzuu ya 39 uk.193.
 
Inadaiwa kuwa Mariam alikuja kuwa Muislam, lakini Muhammad bado alimtunza kama mtumwa badala ya mke wa kawaida. al-Tabari juzuu ya 39 uk.194.
 
Muhammad "alifanya naye [Mariam] tendo la ndoa kwa kigezo cha kuwa mali yake." al-Tabari juzuu ya 39 uk.194. Rejeo chini ya ukurasa 845 linaeleza, "Yaani, Mariam aliamriwa kujitanda shela kama walivyofanya wake wengine wa Nabii, lakini hakumuoa."
 
Mariam Mkhufti alikufa mwaka 637/638 B.K. al-Tabari juzuu ya 39 uk.22.

18. Rayhana/Raihana/Rayhanah binti Zaid/Zayd

Rayhana alikuwa ni mateka wa Kiyahudi kutoka kwenye kabila la Quraiza. Muhammad alipendekeza kumfanya kuwa mke badala ya mtumwa, lakini alikataa na kubaki kuwa Myahudi kwa mujibu wa al-Tabari juzuu ya 8 uk.39. Tazama pia al-Tabari juzuu ya 9 uk.137, 141. Hata hivyo, chanzo kimoja kwenye al-Tabari juzuu ya 39 uk.164-165 kinasema kuwa Muhammad alimwacha huru na kisha alimuoa.
 
Muhammad alikuwa na vimada wawili: Mariam binti Sham'un Mkhufti, na Rayhanah binti Zayd al-Quraziyyah wa Banu al-Nadir. al-Tabari juzuu ya 9 uk.141. Mariam alikuwa um walid wa Muhammad kwa mujibu wa al-Tabari juzuu ya 13 uk.58.

19. Alimtaliki Omm/Umm Sharik / Ghaziyyah binti Jabir

Omm/Umm Sharik ni mtu huyo huyo anayefahamika kama Ghaziyyah binti Jabir kwenye al-Tabari juzuu ya 9 uk.139. Aliitwa "Umm Sharik" kwa sababu alikuwa ni mama wa mtoto wa kiume aliyeitwa Sharik toka kwenye ndoa iliyotangulia.
 
"Wakati Nabii alimtembelea alimkuta kuwa ni mwanamke mzee, kwa ajili hiyo alimtaliki." al-Tabari juzuu ya 9 uk.139. Hata hivyo, rejeo chini ya ukurasa 922 linasema Ibn Sa'd kwenye Tabaqat, 8 uk.110-112 "anatoa maelezo tofauti na anamworodhesha miongoni mwa wanawake ambao Nabii aliwaposa lakini hakuwaoa. Ni yeye [Mariam] aliyejitoa mwenyewe aolewe na Nabii na mstari wa Koran 33:50 unamtaja."

20. Maymuna/Maimuna

Maimuna alikuwa ni mwanamke aliyejitoa mwenyewe alolewe na Muhammad kwa mujibu wa Sahih Muslim juzuu ya 2 rejeo chini ya ukurasa 1919. Anaweza kuwa ni Mariam huyo huyo wa 10, au tofauti. Aliolewa mwaka 7 A.H.
 
Mwanamke ambaye jina lake halijatajwa alisema kuwa alijitoa mwenyewe aolewe na Muhammad. Muhammad hakumkubali, bali alimpa muislam maskini. Kitu pekee ambacho muislam maskini aliweza kutoa kama mahari ni kukariri sura ya Koran. Muwatta' Malik 28.3.8

21. Zainab wa Tatu?

Ali Dashti anamworodhesha mke huyu, lakini sijaweza kupata ushahidi wa jambo hili kutoka vyanzo vingine.

22. Khawla/Khawlah binti al-Hudayl

Inasemekana kuwa Muhammad alimuoa Khawlah binti al-Hudayl. al-Tabari juzuu ya 9 uk.139. Alikuwa ni mke wa Muhammad kwa mujibu wa al-Tabari juzuu ya 39 uk.166.

23. Alimtaliki Mulaykah binti Daudi

Muhammad alimuoa ('alimuoa' ni neno lililopo kwenye maneno halisi ya mwandishi) Mulaykah binti Daudi al-Laythiyyah, lakini alipoambiwa kuwa Muhammad ndie aliyefanya baba yake auawe, alikimbilia kwa Mungu toka kwa Muhammad. Kwa hiyo Muhammad alijitenga naye. al-Tabari juzuu ya 8 uk.189. Jambo hili hili limezungumziwa kuhusu Mulaykah binti Ka'b (ambaye anaweza kuwa ni mtu yule yule) kwenye al-Tabari juzuu ya 39 uk.165.
 
Mulaykah binti Ka'b aliolewa kwa muda mfupi na Muhammad. A'isha alimwuliza endapo alipenda kuolewa na mtu aliyemuua mume wake. "Alikimbilia kwa Mungu" toka kwa Muhammad, kwa hiyo Muhammad alimtaliki. al-Tabari juzuu ya 39 uk.165.

24. Alimtaliki al-Shanba' binti 'Amr

Muhammad alimuoa al-Shanba' binti 'Amr al-Ghifariyyah; watu wake walikuwa washiriki wa banu Qurayza. Ibrahim alipokufa, al-Shanba' alisema kuwa kama angekuwa nabii wa kweli mtoto wake asingekufa. Muhammad alimtaliki kabla ya kukamilisha ndoa naye kwa tendo la ndoa. al-Tabari juzuu ya 9 uk.136.

25. Alimtaliki al-'Aliyyah

Muhammad aliishi na 'Aliyyah binti Zabyan bin 'Amr bin 'Awf bin Ka'b, kisha akamtaliki. al-Tabari juzuu ya 39 uk.188.
 
Muhammad alimuoa al-'Aliyyah, lakini baadaye alimtaliki. Alikufa wakati wa uhai wa Muhammad al-Tabari juzuu ya 9 uk.138.

26. Alimtaliki 'Amrah binti Yazid

Muhammad alimtaliki 'Amrah binti Yazid kwa sababu alikuwa na ukoma. al-Tabari juzuu ya 39 uk.188.
 
Muhammad alimuoa 'Amrah binti Yazid (hakuna maelezo yaliyotolewa kuhusu talaka) al-Tabari juzuu ya 9 uk.139.
 
Muhammad alimtaliki 'Amra. Ibn-i-Majah juzuu ya 3 na.2054 uk.233 juzuu ya 3 na.2030 uk.226 (daif [dhaifu], sio Sahih).
 
Muhammad alimtaliki mwanamke huyu kwa sababu alikuwa na ukoma. al-Tabari juzuu ya 39 uk.187.

27. Alimtaliki Mwanamke ambaye Jina Lake Halijatajwa

Muhammad alimtaliki mwanamke ambaye jina lake halijatajwa kwa sababu alikuwa anawachungulia watu waliokuwa wanaondoka msikitini. al-Tabari juzuu ya 39 uk.187.

28. Qutaylah binti Qays (alikufa wakati huo huo)

Muhammad alomuoa Qutaylah bint Qays lakini alikufa kabla hawajakamilisha ndoa yao kwa tendo la ndoa. Katika upekuzi, inasemekana pia kuwa yeye na kaka yake waliuasi uislam. Kwa ajili hiyo inaonekana kuwa aliuasi uislam baada ya ndoa yake na kabla ya kifo chake? al-Tabari juzuu ya 9 uk.138-139.

29. Sana binti Sufyan

Maelezo yametolewa kwa ufupi juu ya ndoa ya Muhammad na Sana binti Sufyan. al-Tabari juzuu ya 39 uk.188.

30. Sharaf binti Khalifah

Muhammad alimuoa Sharaf binti Khalifah, dada ya Dihyah bin Lhalifah al-Kalbi, lakini alikufa Muhammad angali hai. al-Tabari juzuu ya 9 uk.138.

31. Wanawake wa Mkono wa Kuume wa Muhammad

"...jiepushe na ngono, isipokuwa na watu waliounganishwa nao kwenye kifungo cha ndoa, au (watumwa) ambao mikono yao ya kuume inawamiliki - kwa sababu (kwa upande wao) hawawezi kulaumiwa", Sura 23:5-6. Tazama pia Sura 4:24.
 
"[Muhammad] alijibu, 'Ficha sehemu zako za siri isipokuwa kwa mke wako na kwa yule ambaye mkono wako wa kuume unammiliki (vijakazi).'" Abu Dawud juzuu ya 3 na.4006 p.1123.
 
Abu Dawud
juzuu ya 3 na.4443-4445 uk.1244 inaonyesha kuwa mtu atadaiwa fidia kwa kufanya tendo la ndoa na kijakazi, lakini atapigwa viboko kwa kufanya tendo la ndoa na kijakazi wa mke wake.
 
Kama ilivyokuwa kawaida ya wanaume Waarabu waliokuwa matajiri, Muhammad alihitaji vijakazi kadhaa pia. Tazama Bukhari juzuu ya 7 kitabu cha 64 sura ya 6 na.274 uk. 210.
 
Salmah alikuwa kijakazi wa Muhammad. Abu Dawud juzuu ya 3 na.3849 uk.1084.
 
Maimuna alikuwa kijakazi wa Muhammad aliyewekwa huru. Ibn-i-Majah juzuu ya 3 na.2531 uk.514; Abu Dawud juzuu ya 1 na.457 uk.118.
 
Muhammad alikuwa na mateka "mrembo sana" kwa muda kabla hajampa Mahmiyah bin Jaz' al-Zubaydi. al-Tabari juzuu ya 8 uk.151.
 
Moja ya vijakazi wa nyumba ya Muhammad alizini na mtu mwingine. Shida ilikuwa kwamba huyu alikuwa ni "mtu mwingine." Abu Dawud juzuu ya 3 na.4458 uk.1249.
 
Muhammad alimwita kijakazi mwafrika kuja na kumsitiri Abu Dharr nyuma ya pazia alipokuwa anaoga. Abu Dawud juzuu ya 1 na.332 uk.87.
 
Umm Ayman (=Barakah) ameelezewa kama mteja (kijakazi) wa Nabii. al-Tabari juzuu ya 39 uk.287.
 
Kwa hakika Muhammad alikuwa mcheshi. Umm Ayman, mteja wa Nabii [yaani mtumwa ambaye Mtume aliruhusiwa kuwa pamoja naye usiku]. Kwa mujibu wa al-Husayn ... Umm Ayman: usiku [mmoja] Nabii aliamka na kukojoa kwenye chombo cha udongo kilichokuwa kwenye kona ya nyumba. Usiku huo niliamka, na kwa ajili ya kuwa na kiu, nilikunywa kitu kilichokuwemo kwenye chombo, bila kujua [chochote]. Mtume alipoamka asubuhi alisema 'O Umm Ayman, chukua chombo cha udongo na mwaga kile kilichokuwemo ndani yake.' Nabii alicheka mpaka magego yake yakaonekana, kisha alisema 'Baada ya jambo hili hutapatwa na maumivu ya tumbo tena.'" al-Tabari juzuu ya 39 uk.199.
 
Kwa ujumla, Abu Dawud juzuu ya 3 na.4443-4445 uk.1244 unafundisha kuwa mwanaume anaruhusiwa kufanya ngono na kijakazi, lakini mwanaume atachapwa viboko kwa kufanya ngono na kijakazi wa mke wake.
 
Lakini, kufanya ngono na kijakazi wa mkewe kunaruhusiwa endapo mke atamhalalisha kijakazi kwa mumewe. Kumbuka kuwa mwanaume hakuhitaji kumuoa kijakazi. Ibn-i-Majah juzuu ya 4 na.2551 uk.12.

Muhammad Hakuoa Mtu Yeyote Tu!

A'isha alikuwa na wivu kwa wanawake ambao walijitoa wenyewe ili waolewe na Muhammad. Sahih Muslim juzuu ya 2 na.3453 uk.748. Lakini ilikuwa sahihi kwa mwanamke kujitoa ili aolewe na Muhammad. Ibn-i-Majah juzuu ya 3 na.2000-2001 uk.304-305
 
Wengine walidhani Muhammad alimuoa al-Ash'ath, lakini al-Tabari anasema kuwa si kweli kwa mujibu wa al-Tabari juzuu ya 9 uk.190i. (Kwa ujumla, al-Tabari alifanya kazi nzuri sana ya kuchukuliana na wake wa Muhammad.)

Posa Zilizokataliwa

Muhammad alimwomba amuoe Ghaziyyah kwa sababu ya uzuri wake, lakini alikataliwa. Tabari anadai kuwa [Ghaziyyah] hakuwa mwaminifu lakini hatoi ushahidi. al-Tabari juzuu ya 9 uk.136. Hakuna ushahidi kuwa [Ghaziyyah] hakuwa mwaminifu na kwamba Muhammad hakuwa makini kwa kutokumwadhibu, au kwamba hakuwa mwaminifu na Muhammad alimwadhibu.
 
Layla aligusa bega la Muhammad tokea nyuma na kumuomba amuoe. Muhammad alikubali. Ndugu za Layla walisema, "Ni jambo baya kiasi gani ulilolifanya! Wewe u mwanamke anayejiheshimu, lakini Nabii ni mpenda wanawake. Tafuta kujitengua toka kwake." Layla alikwenda kwa Nabii na kumuomba aikane ndoa hiyo na aliafikianana na hilo [ombi]." al-Tabari juzuu ya 9 uk.139.
 
Kutoka al-Tabari juzuu ya 9 uk.140-141, Muhammad alimposa lakini aliishia kutokumuoa:
1) Umm Hani' bin Abi Talib [Hind] kwa sababu alikuwa na mtoto.
2) Duba'ah binti 'Amir lakini alikuwa mzee sana.
3) Inaripotiwa kuwa alimposa Saffiyah binti Bashshamah, mateka. Alitakiwa achague mmoja kati ya Muhammad na mume wake, na alimchagua mume wake.
4) Umm Habib bint al-'Abbas lakini kwa kuwa al-'Abbas alikuwa kaka wa kulelewa pamoja naye kwa hiyo isingeruhusiwa kisheria kwa hiyo Muhammad aliamua kujiondoa.
5) Jamrah binti Al-Harith. Baba yake alida isivyo sahihi kuwa alikuwa anasumbuliwa na kitu Fulani. Aliporudi, alikuta ameisha kumbwa na ukoma.
 
Haielezwi kwa kauri moja endapo Umm Hani' alikuwa muislam kabla au baada ya Muhammad kumwomba amuoe. al-Tabari juzuu ya 39 uk.197 na rejeo chini ya ukurasa 857 uk.197.

For more info contact www.MuslimHope.com